Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Balozi Fatma Rajab amekutana kwa mazungumzo na Ujumbe wa Serikali ya
Oman leo tarehe 26 Julai 2022 katika ofisi za Wizara jijini
Dodoma.
Mazungumzo
yao yalijikita katika kuimarisha ushirikiano wa kihistoria uliopo baina ya
Tanzania na Oman kwakuwa nchi hizo zinashirikiana katika sekta za
biashara, kilimo, uwekezaji, utalii, afya, elimu, ujenzi wa miundombinu,madini
na uvuvi.
Ujumbe huo
upo nchini kwa ziara ya siku 6 na unaongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya
Mambo ya Nje wa Oman, Mhe. Mohammed Bin Nasser Al Wahaibi ambaye ameambana na
viongozi wengine wa Serikali ya Oman.
Pamoja na
Balozi Fatma Rajab, ujumbe huo pia umefanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma, Mhe. Antony Mtaka pamoja na uongozi wa jiji la Dodoma ambapo, ulipata
wasaa wa kutembelea kiwanja kilichotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwa ajili ya kujenga ofisi za Ubalozi wa Oman.
Aidha,
tarehe 24 Julai 2022 ujumbe huo ulikutana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
ambapo ulifanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Ziara ya
ujumbe huu ni matokeo ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Samia Suluhu Hassan nchini Oman.
Hivyo,
ujumbe huu upo nchini kufanya ufuatiliaji wa masuala ya utekelezaji katika
maeneo mbalimbali ya ushirikiano yaliyokubaliwa wakati wa ziara hiyo na
kuangalia namna ya kuhuisha mikutano ya Tume ya Pamoja ya Ushirikiano baina ya
nchi hizo mbili.
=====================================
Kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Abdallah Kilima, mjumbe kutoka Serikali ya Oman na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mashariki ya Kati, Bw. Leonce Bilauri wakifuatilia mazungumzo. |
Ujumbe uliombatana na Mhe. Wahaibi ukifuatilia mazungumzo. |
Picha ya pamoja. |
Balozi Fatma Rajab akimkaribisha Mhe. Wahaibi na ujumbe wake. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.