|
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashiriki
Balozi Joseph Sokoine akifuatilia utambulisho wa washiriki wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu
(JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe
22 -24 Agosti, 2022 wakifuatilia mkutano huo wakati wa ufunguzi wake. |
|
Mkurugenzi wa Idara ya
Afrika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Naimi Aziz akifuatilia utambulisho wa washiriki wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu
(JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe
22 -24 Agosti, 2022 wakifuatilia mkutano huo wakati wa ufunguzi wake. |
|
Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji Mhe. Faustine Kasike akishiriki katika Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu
(JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji kutoka nchini Msumbiji
akijitambulisha wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo unaofanyika jijini Dar
es salaam kuanzia tarehe
22 -24 Agosti, 2022 |
|
Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia Tanzania Bw. Felix Wandwe akijitambulisha wakati wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu
(JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji kutoka nchini Msumbiji
akijitambulisha wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo unaofanyika jijini Dar
es salaam kuanzia tarehe
22 -24 Agosti, 2022 |
|
Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji Mhe. Faustine Kasike (wa
kwanza kushoto) akiwa na Balozi Naimi Aziz-Mkurugenzi wa Idara ya
Afrika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja
na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashiriki
Balozi Joseph Sokoine wakifuatilia utambulisho wa washiriki wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu
(JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe
22 -24 Agosti, 2022 wakifuatilia mkutano huo wakati wa ufunguzi wake. |
|
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu
(JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe
22 -24 Agosti, 2022 wakifuatilia mkutano huo wakati wa ufunguzi wake.
|
|
Mshiriki kutoka Msumbiji katika Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu
(JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji kutoka nchini Msumbiji akijitambulisha wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo unaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe
22 -24 Agosti, 2022
|
|
|
Baadhi ya washiriki wa Tanzania katika Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu
(JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe
22 -24 Agosti, 2022 katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa mkutano huo. |
|
Baadhi ya washiriki wa Msumbiji katika Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu
(JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe
22 -24 Agosti, 2022 katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa mkutano huo. |
|
Washiriki wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu
(JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe
22 -24 Agosti, 2022 katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa mkutano huo. |
Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu kati ya Tanzania na Msumbiji umeanza leo tarehe 22 Agosti, 2022 katika ngazi ya Wataalamu Jijini Dar es salaam.
Mkutano huu wa awali pamoja na mambo mengine utajadili masuala ya ushirikiano yaliyokubaliwa baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Msumbiji. Mkutano huu utafuatiwa na mkutano katika ngazi ya Makatibu Wakuu na ngazi ya Mawaziri utakaofanyika tarehe 24 Agosti, 2022.
Mkutano wa Tume ya Kudumu ya Pamoja unalenga kujadili na kutathmini hatua za utekelezaji zilizofikiwa katika masuala mbalimbali ya ushirikiano yaliyokubaliwa kwenye mkutano wa 14 uliofanyika mwaka 2006.
Mkutano huu pia utajadili kuanzisha maeneo mapya ya ushirikiano kwenye sekta za Elimu, Sayansi na Teknolojia, Maji na Umwagiliaji, Nishati, Madini, Afya, Ujenzi na Uchukuzi, Mifugo, Uvuvi, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Maliasili na Utalii.
Tanzania na Msumbiji zimekuwa zikishirikiana katika maeneo ya Uhusiano wa Kidiplomasia, Ulinzi na Usalama, Fedha, Nishati, Maendeleo ya Jamii, Afya, Kazi, Ujenzi wa Miundombinu, Uchukuzi, Sayansi, Teknolojia, Habari, Elimu,Utamaduni na Sanaa, Biashara na Uwekezaji, Utalii na Wanyamapori, Kilimo, Uvuvi, Maji, Mazingira, Madini, Afya, Mifugo, Nishati na Elimu.
Tume ya Kudumu ya Pamoja (JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji ilianzishwa
mwaka 1979 na tangu wakati huo jumla ya mikutano 14 imefanyika ambapo maeneo
ya ushirikiano yalikuwa yanajadiliwa na kukubaliwa kwa pamoja. Maeneo hayo ni
Uhusiano wa Kidiplomasia, Biashara, Mawasiliano, Uchukuzi, Uhamiaji, Ulinzi na Usalama,
Kilimo, Utalii na Uvuvi.