Monday, August 22, 2022

BALOZI SOKOINE AFUNGUA JPC YA 15 YA TANZANIA NA MSUMBIJI



Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine akifungua Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 22 -24 Agosti, 2022

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine (wa pili kulia) akiteta kitu na Balozi Hermenegildo Caetano kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikino wa Jamhuri ya Msumbiji wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 22 -24 Agosti, 2022

Balozi Hermenegildo Caetano kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Jamhuri ya Msumbiji akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 22 -24 Agosti, 2022

Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Naimi Aziz akizungumza  wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 22 -24 Agosti, 2022


Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi.  Mwanaasha Ngenya  akijitambulisha wakati wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanznaia na Msumbiji katika picha ya pamoja bada ya ufuinguzi wa Mkutano huo unaofanyika jijini Dar es Salam kuanzia tarehe 22 Agosti hadi 24 Agosti 2022
Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Alli Ubwa akijitambulisha wakati wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanznaia na Msumbiji katika picha ya pamoja bada ya ufuinguzi wa Mkutano huo unaofanyika jijini Dar es Salam kuanzia tarehe 22 Agosti hadi 24 Agosti 2022

Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Frank Mwega akijitambulisha wakati wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanznaia na Msumbiji katika picha ya pamoja bada ya ufuinguzi wa Mkutano huo unaofanyika jijini Dar es Salam kuanzia tarehe 22 Agosti hadi 24 Agosti 2022                                                                      
     

           

Washiriki wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanznaia na Msumbiji katika picha ya pamoja bada ya ufuinguzi wa Mkutano huo unaofanyika jijini Dar es Salam kuanzia tarehe 22 Agosti hadi 24 Agosti 2022
 Ujumbe wa Msumbiji unaoshiriki Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanznaia na Msumbiji katika picha ya pamoja bada ya ufuinguzi wa Mkutano huo unaofanyika jijini Dar es Salam kuanzia tarehe 22 Agosti hadi 24 Agosti 2022



 

 

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine amefungua Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 22 -24 Agosti, 2022.
Mkutano huo ulioanza leo tarehe 22 Agosti 2022 katika ngazi ya Wataalamu utafuatiwa na mkutano wa ngazi ya Makatibu Waku una baadaye mkutano wa ngazi ya Mawaziri utakaofanyika tarehe 24 Agosti 2022 Jijini Dar es salaam.

Akifungua mkutano huo Balozi Sokoine amewaomba watendaji kutoka Tanzania na Msumbiji kutumia mikutano ya JPC kuondoa vikwazo vya kibiashara na kuweka mazingira wezeshi ili sekta za umma na binafsi ziweze kuwekeza kwenye uchumi wa kila nchi kwa maendeleo endelevu na kuinua uchumi wa nchi zote mbili.
Balozi Sokoine pia ametumia mkutano huo kuihakikishia Msumbiji juu ya imani iliyonayo Tanzania katika uhusiano wake na Msumbiji na kwamba itaendelea kuulinda uhusiano huo na kuongeza kuwa Tanzania itaendelea kuimarisha uhusiano huo kwa manufaa ya pande zote mbili.

“Tanzania ina imani na uhusiano iliyonao na Msumbiji na itaendelea kuulinda uhusiano huo na ni dhamira yetu kuwa tutaendelea kuimarisha uhusiano wetu ambao ni wa kindugu na kihistoria kwa manufaa ya vizazi vijavyo,” alisisitiza.


Balozi Sokoine alitoa shukurani kwa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi kwa baraka na jitihada zao katika kuimarisha uhusiano baina ya nchi mbili hizi.


Tanzania na Msumbiji zinashirikiana katika sekta za Diplomasia, Ulinzi na Usalama, Fedha, Nishati, Maendeleo ya Jamii, Afya, Kazi, Ujenzi wa Miundombinu, Uchukuzi, Sayansi, Teknolojia, Habari, Elimu,Utamaduni na Sanaa, Biashara na Uwekezaji, Utalii na Wanyamapori, Kilimo, Uvuvi, Maji, Mazingira, Madini, Afya, Mifugo, Nishati na Elimu.

Tume ya Kudumu ya Pamoja (JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji ilianzishwa mwaka 1979 na tangu wakati huo jumla ya mikutano 14 imefanyika ambapo maeneo ya ushirikiano yalikuwa yanajadiliwa na kukubaliwa kwa pamoja. Maeneo hayo ni Uhusiano wa Kidiplomasia, Biashara, Mawasiliano, Uchukuzi, Uhamiaji, Ulinzi na Usalama, Kilimo, Utalii na Uvuvi.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.