Thursday, August 25, 2022

WIZARA NA BENKI YA NMB WASAINI HATI YA MAKUBALIANO

Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi James Bwana akizungumza katika hafla ya utiaji saini hati za makubaliano ya kutengeneza Mfumo wa Kanzi Data wa Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, (Diaspora Digital Hub) kati ya Wizara na Benki ya NMB PLC  katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es salaam


Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kitengo cha Diaspora Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Semeni Nandonde (aliyesimama kukulia) akizungumza wakati wa hafla ya kusaini  hati za makubaliano ya kutengeneza Mfumo wa Kanzi Data wa Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, (Diaspora Digital Hub) kati ya Wizara na Benki ya NMB katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es salaam .




Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi James Bwana (kulia) na Mwakalishi wa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bw. Alfred Shao (kushoto) wakisaini hati za makubaliano ya kutengeneza Mfumo wa Kanzi Data wa Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, (Diaspora Digital Hub) walizosaini katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es salaam .


Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi James Bwana (kulia) na Mwakalishi wa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bw. Alfred Shao (kushoto) wakionesha hati za makubaliano walizosaini ya kutengeneza Mfumo wa Kanzi Data wa Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, (Diaspora Digital Hub) walizosaini katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es salaam .

Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bw. Alfred Shao akizungumza katika hafla ya kusaini Hati ya Makubaliano ya kutengeneza Mfumo wa Kanzi Data wa Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, (Diaspora Digital Hub) na Benki ya NMB PLC.



 
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika picha ya pamoja baada ya kusaini Hati ya Makubaliano ya kutengeneza Mfumo wa Kanzi Data wa Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, (Diaspora Digital Hub) na Benki ya NMB PLC.

Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Watumishi wa Benki ya NMB Plc katika picha ya pamoja baada ya kusaini Hati ya Makubaliano ya kutengeneza Mfumo wa Kanzi Data wa Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, (Diaspora Digital Hub).

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Benki ya NMB Plc wamesaini Hati ya Makubaliano ya kutengeneza Mfumo wa Kanzi Data wa Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, (Diaspora Digital Hub).

Makubaliano hayo yamesainiwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Kitengo cha Diaspora Balozi James Bwana kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine  na Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB, Bw. Alfred Shao kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Akiongea katika hafla ya utiaji saini wa makubaliano hayo Balozi Bwana amesema mfumo huo wa kidigitali utaisaidia Serikali kuwatambua, kuwasajili na kuwawezesha Diaspora wa Tanzania waliopo sehemu mbalimbali ulimwenguni kupata huduma mbalimbali na kushiriki kidigitali katika shughuli mbalimbali za maendeleo, biashara, uchumi na uwekezaji nchini.

“Ushirikiano wa Wizara na Benki ya NMB Plc ni wa muda mrefu na wenye mafanikio mengi katika kuendelea kusukuma gurudumu la maendeleo ya Tanzania. Wizara ina imani kuwa kupitia udhamini huu wa shilingi milioni 100 kutoka Benki ya NMB, fedha hizo zitawezesha kukamilisha matengenezo ya mfumo wa Diaspora Digital Hub na hivyo kuboresha huduma zenye kukidhi mahitaji ya Diaspora wote ulimwenguni,” amesema Balozi Bwana

Balozi Bwana ameongeza kuwa, mfumo huo pamoja na mambo mengine, utafungua uwezekano wa fursa zaidi za ushirikiano kati ya Wizara na Benki hiyo utawezesha utunzaji wa taarifa mbalimbali za Diaspora wa Tanzania popote walipo ulimwenguni na hivyo kurahisisha kazi ya uratibu wa Diaspora.

Balozi Bwana amesema Serikali inategemea kuwa kukamilika kwa  mfumo huo kutaweza kuwatambua, kuwasajili na kuwawezesha Diaspora wa Tanzania Duniani kote kupata huduma nyingi na muhimu wanazohitaji na kushiriki kidijitali katika shughuli mbalimbali za maendeleo biashara, uchumi na uwekezaji hapa nchini.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bw. Alfred Shao  amesema benki yao inaamini kuwa kukamilika kwa mfumo huo kutawawezesha Diaspora wa Tanzania kuungana, kutambulika na kuiwezesha Serikali kuwa na Kanzi Data ya uhakika na kuwafikia diaspora wengi kwa wakati mmoja na hivyo kuleta mafanikio makubwa kwa Taifa na Mtanzania mmoja mmoja anayeishi nje ya nchi.

"Sisi NMB tunaamini kuwa mfumo huu, utawaunganisha, utawatambua na kuiwezesha Serikali kuwa na Kanzidata ya Diaspora wake, ni wazi kuwa mfumo huu utaleta maendeleo makubwa kwa Taifa na Mtanzania mmoja mmoja wanaoishi nje ya nchi," alisema Bw. Shao

Aliahidi kuwa NMB itaendelea kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika kuhakikisha mfumo wa kidigitali wa Diaspora Digital Hub unakamilika kwa wakati.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kitengo cha Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Semeni Nandonde amesema makubaliano yaliyoingiwa kati ya Wizara na Benki ya NMB yanaashiria utayari wao katika kulifadhili na kuliwezesha wazo la Wizara la kuwa na mfumo wa kutunza taarifa za Diaspora na kuwawezesha dispora kunufaika na huduma mbalimbali pindi mfumo huo utakapokamilika.



 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.