Rais Mstaafu wa Tanzania na Kiongozi wa Timu ya waangalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Kenya, ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na timu yake ya wajumbe 52 kutoka taasisi na mashirika ya kiraia ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki inashuhudia zoezi la upigaji kura la uchaguzi mkuu nchini Kenya lililoanza Leo mapema asubuhi.
Kabla ya uchaguzi huo Dkt. Kikwete alikutana na wadau mbalimbali wakiwemo wagombea wa Urais kupitia chama cha Muungano wa Azimio la Umoja, Mhe. Raila Odinga na mgombea Urais wa chama cha UDA,vMhe. William Ruto.
|
Rais Mstaafu wa Tanzania na Kiongozi wa Timu ya waangalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Kenya, ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika mazungumzo na mgombea Urais wa chama cha UDA, William Ruto. Mazungumzo hayo yalifanyika hivi karibuni Jijini Nairobi |
|
Rais Mstaafu wa Tanzania na Kiongozi wa Timu ya waangalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Kenya, ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mgombea Urais wa chama cha Muungano wa Azimio la Umoja, Raila Odinga hivi karibuni Jijini Nairobi |
|
Rais Mstaafu wa Tanzania na Kiongozi wa Timu ya waangalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Kenya, ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na mgombea Urais wa chama cha Muungano wa Azimio la Umoja, Raila Odinga Jijini Nairobi |
|
Rais Mstaafu wa Tanzania na Kiongozi wa Timu ya waangalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Kenya, ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na mgombea Urais wa chama cha UDA, William Ruto Jijini Nairobi |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.