|
Mwakilishi
wa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Balozi James Bwana (wa pili kulia) na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Bw. Ibrahim Maftah (wa pili kushoto) wakiwa na wanasheria wao wakisaini makubaliano ya
kuipatia Wizara
Shilingi Milioni 50 kwa ajili ya kufadhili utengenezaji wa Mfumo wa
Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, (Diaspora Digital Hub)
iliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam. |
|
Mwakilishi
wa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Balozi James Bwana (kulia) na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Bw. Ibrahim Maftah wakipongezana baada ya kusaini makubaliano ya
kuipatia Wizara
Shilingi Milioni 50 kwa ajili ya kufadhili utengenezaji wa Mfumo wa
Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, (Diaspora Digital Hub)
iliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam. |
|
Mwakilishi
wa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Balozi James Bwana (wa pili kulia) na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Bw. Ibrahim Maftah (wa pili kushoto) na wanasheria wao wakionesha kabrasha lenye makubaliano ya
kuipatia Wizara
Shilingi Milioni 50 kwa ajili ya kufadhili utengenezaji wa Mfumo wa
Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, (Diaspora Digital Hub)
iliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam. |
|
Mwakilishi
wa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Balozi James Bwana akizungumza katika hafla ya utiaji saini makubaliano ya
kuipatia Wizara
Shilingi Milioni 50 kwa ajili ya kufadhili utengenezaji wa Mfumo wa
Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, (Diaspora Digital Hub)
iliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam. |
|
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Bw. Ibrahim Maftah akizungumza baada ya hafla ya utiaji, saini makubaliano ya
kuipatia Wizara
Shilingi Milioni 50 kwa ajili ya kufadhili utengenezaji wa Mfumo wa
Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, (Diaspora Digital Hub)
iliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam, aliyekaa kushoto ni Mkurugenzi wa Diaspora Wizarani Balozi James Bwana akimsikiliza. |
|
Mwakilishi
wa Mkurugenzi wa Kitengo cha Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Semeni Nandonde akizungumza katika hafla ya utiaji saini makubaliano ya
kuipatia Wizara
Shilingi Milioni 50 kwa ajili ya kufadhili utengenezaji wa Mfumo wa
Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, (Diaspora Digital Hub)
iliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam. |
|
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki katika picha ya pamoja na
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Bw. Ibrahim Maftah baada ya kutia saini makubaliano ya
kuipatia Wizara
Shilingi Milioni 50 kwa ajili ya kufadhili utengenezaji wa Mfumo wa
Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, (Diaspora Digital Hub)
iliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam. |
|
Watumishi wa Mfuko
wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) katika picha ya pamoja na Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi James Bwana baada ya kutia saini makubaliano ya
kuipatia Wizara
Shilingi Milioni 50 kwa ajili ya kufadhili utengenezaji wa Mfumo wa
Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, (Diaspora Digital Hub)
iliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam. |
|
Watumishi wa Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Watumishi wa Mfuko
wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) katika picha ya pamoja katika hafla ya kutia saini makubaliano ya kuipatia Wizara
Shilingi Milioni 50 kwa ajili ya kufadhili utengenezaji wa Mfumo wa
Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, (Diaspora Digital Hub) iliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam. |
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umesaini makubaliano na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ya kuipatia Wizara Shilingi Milioni 50 kwa ajili ya kufadhili utengenezaji wa Mfumo wa Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, (Diaspora Digital Hub).
Makubaliano hayo yamesainiwa leo kati ya Mkurugenzi wa Kitengo cha Diaspora Balozi James Bwana kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mkurugenzi wa Uthaminishaji, Takwimu na Usimamizi wa Hadhari, Bw. Ibrahim Maftah kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NSSF katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa makubaliano hayo, Balozi Bwana amesema kukamilika kwa mfumo huo wa kidigitali kutaiwezesha Serikali kuwasajili, kuwatambua na kurahisisha shughuli za kuwaratibu Diaspora na kuwawezesha kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya Taifa.
“Leo hii tumeshuhudia utiaji saini wa makubaliano ambayo yataiwezesha NSSF kutoa Shilingi Milioni 50 ambazo zitaiwezesha Wizara kutengeneza Mfumo wa Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, kitendo hiki ni mwanzo wa ushirikiano wa muda mrefu ambao Wizara umekuwa nao na NSSF, ni matarajio ya Wizara kuwa NSSF itahuisha program yao ya Diaspora na kubuni programu mpya ili kutoa huduma kwa Diaspora wetu na wao kunufaika zaidi na programu hizo,” alisema Balozi Bwana.
Balozi Bwana aliongeza kuwa Diaspora ni eneo muhimu la uwekezaji kwa maendeleo ya taifa hasa ikizingatiwa kuwa kwa mwaka 2021 Diaspora waliwekeza jumla ya Shilingi Bilioni 3.9 katika mpango wa UTT Amis na kutuma nchini Shilingi Milioni 569.3 kwa ndugu na jamaa zao hapa nchini.
“Serikali inategemea mfumo utakaowatambua, kuwasajili na kuwawezesha Diaspora wa Tanzania Duniani kote kupata huduma nyingi na muhimu wanazohitaji na kushiriki kidijitali katika shughuli mbalimbali za maendeleo biashara, uchumi na uwekezaji hapa nchini,” aliongeza Balozi Bwana.
Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Ibrahim Maftah ameipongeza Wizara kwa kuja na wazo la kuanzisha mfumo huo na kuihakikishia Wizara kuwa NSSF itaendelea kushirikiana na Wizara kuhakikisha mfumo wa kidigitali wa Diaspora Digital Hub unakamilika na kutumika katika maeneo yote yenye tija kwao na kwa taifa kwa ujumla.
“Kitendo cha NSSF kusaini makubaliano hayo kinaonesha utayari na muelekeo wetu katika kutumia fursa mbalimbali zinazopatikana katika eneo la Diaspora,” alisema Bw. Maftah.
Awali mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kitengo cha Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Semeni Nandonde amesema kukamilika kwa mfumo huo kutaiwezesha Serikali kufahamu kwa ufasaha idadi ya diaspora wake, ujuzi walionao, elimu zao .
Ameongeza kuwa mfumo huo utakapokamilika diaspora wataweza kupata huduma maalum zitakazoandaliwa kwa ajili ya mahitaji yao kama vile huduma za kibenki, hifadhi ya jamii, bima ya afya kwa wategemezi wao waliopo hapa nyumbani, taarifa za fursa za uwekezaji, biashara na masoko, masuala ya uhamiaji, vitambuklkisho vya taifa na huduma nyinginezo.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.