![]() |
| Semina ya namna bora ya uzalishaji wa vifaranga vya matango bahari na ukulima bora wa zao la mwani uliofanyika katika Hoteli ya Verde mjini Zanzibar |
| Picha ya pamoja |
![]() |
| Semina ya namna bora ya uzalishaji wa vifaranga vya matango bahari na ukulima bora wa zao la mwani uliofanyika katika Hoteli ya Verde mjini Zanzibar |
| Picha ya pamoja |
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeahidi kuendelea kushirikiana na vyuo vikuu nchini ili kupanua wigo wa kutoa elimu kwa wanafunzi kuhusu fursa mbalimbali zinazotolewa na wahisani yakiwemo mashirika ya Kikanda, Kimataifa na nchi marafiki.
Ahadi hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga alipokutana na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Henry James na baadhi ya Viongozi wa Serikali za wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) jana katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Ubungo.
“Fursa za Masomo Nje ya Nchi na ajira zimekuwa zikitangazwa na kuratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje kwa kushirikiana na wadau wengine ili kuendelea kupanua wigo wa kutoa elimu kwa wanafunzi kuhusu fursa mbalimbali zinazotolewa na Wizara Kikanda na Kimataifa.,” Alisema Balozi Mindi
Naye Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Bw. Kheri James amepongeza jitihada zinazotekelezwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika kuhakikisha watanzania wanapata fursa mbalimbali za masomo na kazi Nje ya nchi kwani jambo hilo ni la kizalendo.
“Wizara ina fursa ya ziada ya kuviunganisha vyuo vikuu nchini na Vyuo Vikuu Nje ya nchi kwa ufadhili wa masomo, mahusiano kati ya vyuo vya Tanzania na vya Nje na kubadilishana wanafunzi katika taaluma mbalimbali ili kuwajengea uwezo na ufanisi katika masomo,”Alisema Bw. James.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Rais wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bw. Spencer Minja na Rais wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji Bw. Mark Makaranga ambapo pamoja na mambo mengine wanafunzi hao wameipongeza na kuiomba Wizara kuandaa Kongamano la wanafunzi wa Elimu ya Juu kuhusu Mtangamano wa Jumuiya ya Kikanda na Kimataifa.
Halmashauri ya Wilaya ya Ubungo ina vyuo vitano ambavyo ni, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Shule Kuu ya Sheria, Chuo cha Maji na Chuo cha Mtakatifu Joseph.
![]() |
| Rais wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji Bw. Mark Makaranga akieleza jambo wakati wa kikao |
![]() |
| Kikao kikiendelea |
![]() |
| Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akifungua Mkutano wa Tano wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Malawi uliofanyika jijini Dar es Salaam |
![]() |
| Waziri wa Sheria wa nchini Malawi Mhe. Titus Mvalo akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Tano wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Malawi uliofanyika jijini Dar es Salaam |
![]() |
| Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro na Waziri wa Sheria wa nchini Malawi Mhe. Titus Mvalo wakibadilishana nyaraka kwenye Mkutano wa Tano wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Malawi uliofanyika jijini Dar es Salaam |
![]() |
| Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro na Waziri wa Sheria wa nchini Malawi Mhe. Titus Mvalo wakisaini Hati za Makubaliano kwenye Mkutano wa Tano wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Malawi uliofanyika jijini Dar es Salaam |
![]() |
| Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Naimi Azizi akitoa neno la ukaribisho wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Tano wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Malawi uliofanyika jijini Dar es Salaam |
![]() |
| Balozi wa Tanzania nchini Malawi Mhe. Humphrey Polepole akifuatilia Mkutano wa Tano wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Malawi uliokuwa ukiendelea |
![]() |
| Sehemu ya Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia Mkutano wa Tano wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Malawi uliokuwa ukiendelea jijini Dar es Salaam |
![]() |
| Picha ya pamoja |
![]() |
| Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Bw. Ally S. Gugu na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Bw. Kheri Abdul Mahimbali wakibadilishana mawazo wakati wa Mkutano wa Tano wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Malawi uliokuwa ukiendelea jijini Dar es Salaam |
![]() |
| Mkutano wa Tano wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Malawi ukiendelea |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax amewasisitiza Diaspora wote Duniani kutumia huduma za kifedha kupitia kwa watoa huduma waliosajiliwa ili kuendelea kuchangia uchumi wa Tanzania.
Dkt. Tax ametoa wito huo jijini Dar es Salaam aliposhiriki uzinduzi wa huduma ya kutuma na kupokea fedha kwa baadhi ya nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) iliyoanzishwa na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom kupitia huduma ya kutuma fedha ya M-Pesa.
Amesema, upo umuhimu mkubwa kwa Diaspora kutumia huduma za kifedha zilizosajiliwa ili kuhakikisha usalama wa fedha zao na kuweka kumbukumbu sawa. Amesema kwa mujubu wa Takwimu kutoka Benki Kuu ya Tanzania Diaspora walichangia uchumi wa Taifa kwa kiasi cha Dola za Kimarekani milioni 30 mwaka 2019 na mwaka 2021 Diaspora walichangia uchumi wa Taifa kwa Dola za Kimarekani milioni 569 sawa na kuchangia asilimia 0.8 ya pato la Taifa.
Mhe. Dkt. Tax ameipongeza Kampuni ya Vodacom kwa kuwekeza katika ubunifu na kuboresha huduma zao wakati wote ili kuendana na mahitaji ya wananchi kulingana na mabadiliko ya Teknolojia.
Amesema anaipongeza Kampuni hiyo kwa kuwa mstari wa mbele katika kuiunganisha Afrika kupitia huduma zao ambapo kwa sasa wamepanua wigo kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na kuongeza ukanda wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) jambo ambalo litawawezesha Diaspora kwenye maeneo hayo kutuma na kupokea fedha pasipo kikwazo chochote.
“Sekta ya fedha ni sekta muhimu katika nchi yoyote, Serikali inaona jambo hili ni kubwa kwa sababu ya umuhimu wa sekta ya fedha lakini kwa kutambua kwa sasa dunia ipo katika uchumi wa kidigitali. Uchumi wa kidigitali unafanya kazi kidigitali hivyo nawasihi Diaspora kutumia huduma hii ili kuweza kuchangia maendeleo ya taifa kwa kuwa benki na taasisi nyingine zinazotoa huduma za kifedha zimerahisisha biashara na uwekezaji na shughuli za kiuchumi kwa ujumla,” alisema Dkt. Tax.
Kadhalika Mhe. Dkt. Tax ameipongeza Benki Kuu ya Tanzania kwa kutoa miongozo mbalimbali inayowawezesha watoa huduma za fedha nchini kuandaa huduma zenye manufaa kwa wanannchi na kuahidi Serikali kuendelea kushirikiana na Sekta Binafsi ili kutimiza lengo la kuwainua wananchi kiuchumi kupitia huduma mbalimbali.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Vodacom M-pesa, Bw. Epimack Mbeteni amesema kuzinduliwa kwa huduma ya M-Pesa katika ukanda wa SADC kumetoa fursa ya kuongeza wigo wa kutuma na kupokea pesa katika nchi nyingi zaidi barani Afrika hususan nchi za SADC.
“Wateja wetu wanaweza kupokea na kutuma fedha katika ukanda wa Sadc, sasa tumeiunganisha Afrika na M-Pesa, jambo hili litachangia ukuaji wa uchumi wa taifa letu,” amesema Bw. Mbeteni
Bw. Mbeteni ameongeza kuwa uzinduzi wa huduma hiyo utarahisisha ufanyaji wa biashara na huduma nyingine za kijamii. Uzinduzi wa huduma hiyo uliongozwa na kauli mbiu ya “Dunia Kijiji, Afrika ni M-Pesa”. Katika uzinduzi huo, Dkt. Tax aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Godwin Gondwe.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akiwasilisha hotuba ya ufunguzi aliposhiriki uzinduzi wa huduma ya kutuma na kupokea fedha kwa baadhi ya nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) iliyoanzishwa na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom kupitia huduma ya kutuma fedha ya M-Pesa
| Mkurugenzi wa Vodacom M-pesa, Bw. Epimack Mbeteni akiongea na washiriki wakati wa uzinduzi wa huduma ya kutuma na kupokea fedha kwa baadhi ya nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) |
| Washiriki wakifuatilia mkutano wa uzinduzi wa wa huduma ya kutuma na kupokea fedha kwa baadhi ya nchi za SADC |
| Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na waandishi wa habari kuhusu huduma ya kutuma na kupokea fedha kwa baadhi ya nchi za SADC |
| Washiriki wakifuatilia mkutano wa uzinduzi wa wa huduma ya kutuma na kupokea fedha kwa baadhi ya nchi za SADC |
| Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Godwin Gondwe na wafanyakazi wa Kampuni ya simu ya Vodacom |
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa Tano (5) wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Malawi katika ngazi ya Maafisa Waandamizi unaofayika jijini Dar es Salaam.
|
![]() |
| Sehemu ya ujumbe wa Malawi wakifuatilia Mkutano wa Tano (5) wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Malawi katika ngazi ya Maafisa Waandamizi uliokuwa ukiendelea jijini Dar es Salaam. |
![]() |
| Mkurugenzi wa Idara ya Afrika na Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Malawi Bw. William Kantayeni akichangia jambo kwenye Mkutano wa Tano (5) wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Malawi uliokuwa ukiendelea jijini Dar es Salaam. |
![]() |
| Balozi wa Tanzania nchini Malawi Mhe. Balozi Humphrey Polepole akifuatilia mkutano wa Tano (5) wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Malawi katika ngazi ya Maafisa Waandamizi uliokuwa ukiendelea jijini Dar es Salaam. |
![]() | |
| Meza kuu wakifuatilia Mkutano wa Tano (5) wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Malawi katika ngazi ya Maafisa Waandamizi uliokuwa ukiendelea katika ukumbi wa Mikutano wa Kamataifa wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax amepokea ujumbe maalum kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Mhe. Sameh Hassan Shoukry uliowasilishwa kwake na Mjumbe Maalum ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayeshughulikia masuala ya Afrika wa nchi hiyo, Mhe. Sherif Issa.
Akizungumza mara baada ya kupokea ujumbe huo leo tarehe 26 Oktoba 2022 jijini Dar es Salaam, Mhe. Dkt. Tax ameishukuru Serikali ya Misri kwa kuendelea kuthamini ushirikiano wa kihistoria uliopo baina yake na Tanzania hususan kwenye sekta ambazo zinagusa maisha ya wananchi moja kwa moja kama afya, elimu, maji, nishati na ujenzi wa miundombinu.
Amesema, ni kutokana na kuthamini mchango unaotolewa na Misri kwenye sekta mbalimbali za maendeleo nchini Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alifanya ziara nchini humo mwezi Novemba 2021 na maeneo mbalimbali ya ushirikiano yalijadiliwa na kukubalika.
“Ninayo furaha kukukaribisha nchini Mhe. Waziri. Nakiri kupokea ujumbe huu muhimu kutoka kwa Waziri mwenzangu. Nitaupitia na kuufanyia kazi na kuwasilisha kwenu mrejesho haraka iwezekanavyo”, amesema Mhe. Dkt. Tax.
Naye, Mhe. Issa amempongeza Mhe. Dkt. Tax kwa kuteuliwa katika wadhifa huo mpya na kumweleza utayari wa Serikali ya Misri katika kushirikiana naye.
Kadhalika amesema, Serikali ya Misri itaendelea kushirikiana na Tanzania katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutekeleza na kukamilisha miradi yote ya pamoja ambayo nchi hizo zimekubaliana ukiwemo Mradi wa Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere.
“Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere ni kwa ajili ya Watanzania. Mradi huu ni mkubwa na wa kwanza kwa Misri kuutekekeleza hapa nchini. Hivyo tutajitahidi kama Serikali kushirikiana na Tanzania ili kuhakikisha mradi wote unakamilika na kukabidhiwa”, alisisitiza Mhe. Issa.
Pia Mhe. Issa alitumia nafasi hiyo kuikaribisha Tanzania kushirki kwenye Mkutano wa 27 wa Kimataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP27) utakaofanyika mwezi Novemba 2022 katika Mji wa Sharm El Sheikh, nchini humo.
Kwa upande wake, Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba ambaye alishiriki mazungumzo hayo amesema, Mradi wa Bwawa la Kufua Umeme wa Julius Nyerere ni alama ya ushirkiano kati ya Tanzania na Misri na kwamba Wizara yake itaendelea kutoa ushirikiano wote unaohitajika kwa Serikali ya Misri na Timu ya Wataalam wa Mradi huo ili kuufanikisha.
|
Waziri wa Mambo ya Nje
na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akipokea
ujumbe maalum kutoka
kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Mhe. Sameh Hassan Shoukry
uliowasilishwa kwake
na Mjumbe Maalum ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri
anayeshughulikia
masuala ya Afrika wa nchi hiyo, Mhe. Sherif Issa.Mhe. Dkt. Tax amepokea
ujumbe huo leo tarehe 26 Oktoba, 2022 akiwa katika Ofisi Ndogo za Wizara
zilizopo jijini Dar es Salaam |
| Mhe. Dkt. Tax akiwa katika mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe. Sherif Issa |
| Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba ambaye alishiriki mazungumzo hayo naye akichangia jambo |
| Mazungumzo yakiendelea |
| Mhe. Dkt. Tax na mgeni wake wakimsikiliza Balozi wa Misri hapa nchini Mhe. Mohammed Gaber Abulwafa wakati akifafanua jambo |
| Mhe. Makamba akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Bw. Maharage Chande pamoja na wadau wengine wakaishiriki mazungumzo kati ya Mhe. Dkt. Tax na Mhe. Issa (hawapo pichani) |
| Picha ya pamoja |
| Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (kulia) akiwa na Kamishina wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia Ubia wa Kimataifa, Mhe. Jutta Urpilainen kabla ya kuanza mazungumzo yaliyofanyika jijini Dar Es Salaam |
| Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo na Kamishina wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia Ubia wa Kimataifa, Mhe. Jutta Urpilainen. Kushoto kwa Mhe. Waziri ni Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji na katika Umoja wa Ulaya, Mhe. Jestas Nyamanga. |
| Kamishina wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia Ubia wa Kimataifa, Mhe. Jutta Urpilainen (katikati) na ujumbe wake wakisikiliza jambo kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax wakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika jijini Dar Es Salaam |
| Kamishina wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia Ubia wa Kimataifa, Mhe. Jutta Urpilainen akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax |
| Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji na katika Umoja wa Ulaya, Mhe. Jestas Nyamanga akisalimiana na .Kamishina wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia Ubia wa Kimataifa, Mhe. Jutta Urpilainen alipowasili kwenye ofisi za Wizara kwa ajili ya mazungumzo |
| Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba akisalimiana na Kamishina wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia Ubia wa Kimataifa, Mhe. Jutta Urpilainen alipowasili kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere kwa ajili ya kufanya mazungumzo |
| Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba na ujumbe wake wakiwa katika mazungumzo na Kamishina wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia Ubia wa Kimataifa, Mhe. Jutta Urpilainen yaliyofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere |