Wednesday, January 11, 2023

TANZANIA YAAINISHA VIPAUMBELE VYAKE KWA MABALOZI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) akizungumza na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam hawapo pichani
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) akizungumza na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam wanaonekana mbele katika picha
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab akizungumza na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Sehemu ya Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (hayupo pichani) katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika picha ya pamoja na  waheshimiwa Mabalozi kutoka nchi za Ulaya na Amerika wanaoziwakilisha nchi  zao hapa nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika picha ya pamoja na wajumbe wa menejimenti wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na baadhi ya waheshimiwa Mabalozi na wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeanisha vipaumbele vyake vya mwaka 2023 kwa Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa wanaoziwakilisha nchi zao nchini.

Vipaombele hivyo vimeainishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) alipokutana na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Januari, 2023.

“Misimamo ya Tanzania ni kuwa hatufungamani na upande wowote lakini pia Tanzania ni muumini wa uendelezaji wa ushirikiano wa kimataifa na kikanda. Tumeelezana vipaumbele vya Serikali hususani utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi na kuona ni jinsi gani mabalozi wanaweza kushirikiana na Tanzania katika utekelezaji wa diplomasia ya uchumi kwa manufaa ya pande zote,” alisema Dkt. Tax

Dkt. Tax aliongeza kuwa amesisitiza umuhimu wa maboresho yanayofanywa na Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini ili kuboresha shughuli za kiuchumi, ambapo Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa na wameridhika na maboresho yanayofanywa na Serikali na kuahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta za kipaumbele zaidi ambazo Tanzania imeziainisha.

Kwa upande wake kiongozi wa Mabalozi nchini ambaye pia ni Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini, Mhe. Dkt. Ahmada El Badaoui Mohamed ameishukuru Serikali kwa kuainisha vipaumbele vyake kwa mwaka 2023 na kuahidi kuwa wataendelea kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha kuwa inafika malengo yake iliyojiwekea kwa mwaka 2023.

“Kwa niaba ya Mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya Kimataifa, napenda kuahidi kuwa tutaendelea kushirikiana na wizara na Serikali kwa ujumla katika kuhakikisha inafikia viapombele na malengo yake iliyojiwekea kwa mwaka 2023,” alisema Balozi El Badaoui Mohamed

Mkutano huo ulilenga kufahamiana, kukumbushana na kutoa mwelekeo wa Serikali ya Tanzania katika masuala ya Diplomasia na mahusiano yake na nchi na taasisi mbalimbali kwa wana jumuiya hao wa kidiplomasia wanaowakilisha hapa nchini.

DKT. TAX AKUTANA NA BALOZI WA INDIA, DPRK NA MWAKILISHI WA HUAWEI-TANZANIA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax amekutana kwa mazungumzo kwa nyakati tofauti na wageni kadhaa waliomtembelea ofisini kwake Mtumba  jijini Dodoma.

Wageni hao ni Balozi wa India nchini, Mhe Binaya Pradhan, Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea, Mhe. Kim Young Su na Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Huawei Tanzania Bw. Tao Mian.

Akizungumza na Balozi wa India nchini Mhe. Dkt. Tax amemshukuru Balozi huyo kwa kutenga muda wa kumtembelea kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe kwenye wadhifa huo na kueleza kwamba ziara hiyo itamwezesha kuelewa kwa kina hatua mbalimbali zilizofikiwa katika ushirikiano kati ya Tanzania na India na pia kubadilishana  mawazo ya namna ya kufanikisha masuala mbalimbali yaliyokubalika katika ushirikiano baina ya nchi hizi mbili.

Amesema Tanzania na India zinashirikiana katika Sekta mbalimbali zenye umuhimu kwa  wananchi ikiwemo Sekta ya maji, elimu, teknolojia na  afya na kwamba ni wakati sasa kwa nchi hizi mbili kuendelea kutekeleza kwa kasi makubaliano mbalimbali ambayo tayari yamefikiwa ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

 “Ushirikiano wetu unaenda vizuri na mambo tunayokubaliana kushirikiana na kufanyia kazi kwa pamoja yanaenda, zaidi tuongeze kasi kuyatekeleza. Niwahakikishie kuwa tutaaendelea kushirikiana ili kuendeleza uhusiano wetu ambao ni wa kidugu na kihistoria, ambao umekuwepo kwa miaka mingi,” amesema Dkt. Tax.

Naye Balozi wa India Mhe. Binaya Pradhan  ameeleza kuridhishwa kwake na ushirikiano anaoupata nchini katika kutekeleza majukumu yake na kueleza kwamba Serikali ya India kupitia Hospitali ya Apolo wamekubali kushirikiana na Hospitali ya Muhimbili kupitia Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Hospitali ya Bugando ya jijini Mwanza na Taasisi ya Saratani ya Ocean  Road ya jijini Dar es Salaam katika kutoa huduma na kuwajengea uwezo watumishi katika hospitali hizo ili kusaidia wananchi wa Tanzania.

Kuhusu sekta ya elimu,  Balozi huyo amesema wamekuwa wakishirikiana na Chuo cha Teknolojia cha Dar es Salaam (DIT) katika kukiboresha ili kukiwezesha kuwa Kituo bora cha utoaji wa huduma za teknolojia ya habari na mawasiliano nchini.

Akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea Mhe. Dkt. Tax amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi hiyo katika sekta kama kilimo, elimu afya na teknolojia ya habari na mawasiliano.

Kwa upande wake, Balozi Kim Young Su amempongeza Mhe. Dkt. Tax kwa kuteuliwa kwenye wadhifa huo ikiwa ni mara yake ya kwanza kukutana naye na kumwahidi ushirikiano. Pia amesema kuwa, Nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta mbalimbali.

Akizungumza na Naibu Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huawei Tanzania Mhe. Tax ameipongeza kampuni hiyo kwa uwekezaji wao katika masuala ya Teknolojia hususan kupitia mradi wao wa kusambaza huduma za kidigitali vijijini.

“ Huawei ni Kampuni kubwa na tunathamini uwepo wenu hapa nchini. Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ni mingoni mwa vipaumbele vya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hivyo tutaendelea kushirikiana nanyi hususan kwenye kusambaza huduma za kidigitali vijijini na vyuoni ili hatimaye tuweze kufikia ndoto yetu ya kuwa kitovu cha kidigitali,” alisema Mhe. Dkt. Tax.

Kwa upande wake, Bw. Tao Mian alieleza kwamba hapa nchini Kampuni hiyo imetengeneza ajira zaidi ya 1000 ambapo zaidi ya asilimia 70 ya ajira ni za watanzania.Kadhalika Kampuni hiyo inashirikiana na  zaidi ya kampuni 70 za ndani, Wahandisi wa TEHAMA zaidi ya 2000 nchi nzima pamoja na vyuo zaidi ya 19 nchini. Aidha, Kampuni hiyo inaendesha mafunzo ya TEHAMA kwa zaidi ya wanafunzi 2000, kuhudumia zaidi ya asilimia 75 ya watanzania na kwamba imekuwa mchangiaji mkubwa wa ujenzi wa miundombinu ya TEHAMA nchini.

“Tunaridhishwa na uungwaji mkono wa Kampuni yetu hapa Tanzania na tunaahidi kuendelea kuchapa kazi ili kuhakikisha huduma za kidigitali zinawafikia wananchi wengi kwa wakati mmoja hususan wale wa vijijini” alisema Bw. Mian.

Pia alimueleza Mhe. Dkt Tax juu ya Mpango kabambe wa kuboresha mawasiliano ya TEHAMA vijijini ambao ni sehemu ya Mkataba wa ushirikiano uliosainiwa baina ya Tanzania na China ambao unatarajiwa kutekelezwa na Kampuni hiyo. Katika mradi huo kutakuwa na jumla ya miradi 19 ya kipaumbele, uboreshaji wa mawasiliano vijijini, usambazaji wa umeme Kaskazini Mashariki mwa Tanzania pamoja na miradi 9 ya msaada ambayo itatekelezwa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Stadi (VETA) na Hospitali ya Zanzibar.

Kampuni ya Huawei Tanzania ambayo imewekeza kwa zaidi miaka 15 nchini, inashirikiana na Kampuni ya Mawasiliano ya Simu Tanzania (TTCL) kusambaza Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ili kuwezesha huduma za kidigitali kupatikana kwa urahisi nchi nzima ambapo hadi sasa mkongo huo umesambaa kwa zaidi ya kilomita 15,000 nchi nzima.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Balozi wa India nchini Mhe Binaya Pradhan, alipomtembelea ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma hivi karibuni.

Mhe. Dkt. Tax akimsikiliza Balozi Mhe Binaya Pradhan wakati wa mazungumzo kati yao yaliyofanyika ofisini kwake jijini Dodoma. Kushoto ni Kaimu mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Halmenshi Lunyumbu.

Mhe Binaya Pradhan, Balozi wa India nchini (kulia) akiwa na Naibu Balozi wa Ubalozi huo wakati wa mazungumzo kati yake na Mhe. Dkt. Tax

Mhe Binaya Pradhan, Balozi wa India nchini akimkabidhi Mhe. Dkt. Tax zawadi ya kasha la kuhifadhia vitu.
Mhe. Dkt. Tax akiagana na Balozi Mhe Binaya Pradhan mara baada ya kukamilisha mazungumzo yao
Mhe. Dkt. Tax na Mhe. Balozi Mhe Binaya Pradhan wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe walioshiriki mazungumzo yao 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea nchini, Mhe.  Kim Young Su alipomtembelea ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma hivi karibuni

Mhe. Dkt. Tax akiwa katika mazungumzo na Mhe. Balozi Kim Young Su 

Mhe. Dkt. Tax akiagana na Mhe. Kim Young Su mara baada ya kukamilisha mazungumzo yao

Picha ya pamoja
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Huawei Tanzania Bw. Tao Mian alipomtembelea ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma tarehe hivi karibuni

Mhe. Dkt. Tax akiendelea na mazungumzo na  Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Huawei Tanzania Bw. Tao Mian. Walioketi kushoto kwa Mhe. Waziri ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Magabilo Murobi na Afisa katika Idara hiyo, Bw. Herman Berege.

Picha ya pamoja
Mhe. Dkt. Tax akiagana na Bw. Tao Mian mara baada ya kukamilisha mazungumzo yao

VACANCY ANNOUNCEMENT AT THE SOUTHERN AFRICAN DEVELOPMENT COMMUNITY

Tuesday, January 10, 2023

DKT. TAX AKUTANA NA BALOZI WA INDIA, DPRK NA MWAKILISHI WA HUAWEI-TANZANIA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax amekutana kwa mazungumzo kwa nyakati tofauti na wageni kadhaa waliomtembelea ofisini kwake Mtumba  jijini Dodoma.

Wageni hao ni Balozi wa India nchini, Mhe Binaya Pradhan, Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea, Mhe. Kim Young Su na Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Huawei Tanzania Bw. Tao Mian.

Akizungumza na Balozi wa India nchini Mhe. Dkt. Tax amemshukuru Balozi huyo kwa kutenga muda wa kumtembelea kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe kwenye wadhifa huo na kueleza kwamba ziara hiyo itamwezesha kuelewa kwa kina hatua mbalimbali zilizofikiwa katika ushirikiano kati ya Tanzania na India na pia kubadilishana  mawazo ya namna ya kufanikisha masuala mbalimbali yaliyokubalika katika ushirikiano baina ya nchi hizi mbili.

Amesema Tanzania na India zinashirikiana katika Sekta mbalimbali zenye umuhimu kwa  wananchi ikiwemo Sekta ya maji, elimu, teknolojia na  afya na kwamba ni wakati sasa kwa nchi hizi mbili kuendelea kutekeleza kwa kasi makubaliano mbalimbali ambayo tayari yamefikiwa ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

 “Ushirikiano wetu unaenda vizuri na mambo tunayokubaliana kushirikiana na kufanyia kazi kwa pamoja yanaenda, zaidi tuongeze kasi kuyatekeleza. Niwahakikishie kuwa tutaaendelea kushirikiana ili kuendeleza uhusiano wetu ambao ni wa kidugu na kihistoria, ambao umekuwepo kwa miaka mingi,” amesema Dkt. Tax.

Naye Balozi wa India Mhe. Binaya Pradhan  ameeleza kuridhishwa kwake na ushirikiano anaoupata nchini katika kutekeleza majukumu yake na kueleza kwamba Serikali ya India kupitia Hospitali ya Apolo wamekubali kushirikiana na Hospitali ya Muhimbili kupitia Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Hospitali ya Bugando ya jijini Mwanza na Taasisi ya Saratani ya Ocean  Road ya jijini Dar es Salaam katika kutoa huduma na kuwajengea uwezo watumishi katika hospitali hizo ili kusaidia wananchi wa Tanzania.

Kuhusu sekta ya elimu,  Balozi huyo amesema wamekuwa wakishirikiana na Chuo cha Teknolojia cha Dar es Salaam (DIT) katika kukiboresha ili kukiwezesha kuwa Kituo bora cha utoaji wa huduma za teknolojia ya habari na mawasiliano nchini.

Akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea Mhe. Dkt. Tax amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi hiyo katika sekta mbalimbali ambazo tayari nchi hizi mbili zinashirikiana ikiwemo kilimo, elimu afya na teknolojia ya habari na mawasiliano na utamaduni.

Kwa upande wake, Balozi Kim Young Su amempongeza Mhe. Dkt. Tax kwa kuteuliwa kwenye wadhifa huo ikiwa ni mara yake ya kwanza kukutana naye na kumwahidi ushirikiano. Pia amesema kuwa, Nchi yake itaendelea kushirkiana na  Tanzania katika sekta mbalimbali na kwamba ushirikiano wa kihistoria uliopo ambao umejengwa katika misingi iliyoachwa na waasisi wa mataifa mataifa haya utaendelezwa.

Akizungumza na Naibu Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huawei Tanzania Mhe. Tax ameipongeza kampuni hiyo kwa uwekezaji wao katika masuala ya Teknolojia hususan kupitia mradi wao wa kusambaza huduma za kidigitali vijijini.

“ Huawei ni Kampuni kubwa na tunathamini uwepo wenu hapa nchini. Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ni mingoni mwa vipaumbele vya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hivyo tutaendelea kushirikiana nanyi hususan kwenye kusambaza huduma za kidigitali vijijini na vyuoni ili hatimaye tuweze kufikia ndoto yetu ya kuwa kitovu cha kidigitali,” alisema Mhe. Dkt. Tax.

Kwa upande wake, Bw. Tao Mian alieleza kwamba hapa nchini Kampuni hiyo imetengeneza ajira zaidi ya 1000 ambapo zaidi ya asilimia 70 ya ajira ni za watanzania.Kadhalika Kampuni hiyo inashirikiana na  zaidi ya kampuni 70 za ndani, Wahandisi wa TEHAMA zaidi ya 2000 nchi nzima pamoja na vyuo zaidi ya 19 nchini. Aidha, Kampuni hiyo inaendesha mafunzo ya TEHAMA kwa zaidi ya wanafunzi 2000, kuhudumia zaidi ya asilimia 75 ya watanzania na kwamba imekuwa mchangiaji mkubwa wa ujenzi wa miundombinu ya TEHAMA nchini.

“Tunaridhishwa na uungwaji mkono wa Kampuni yetu hapa Tanzania na tunaahidi kuendelea kuchapa kazi ili kuhakikisha huduma za kidigitali zinawafikia wananchi wengi kwa wakati mmoja hususan wale wa vijijini” alisema Bw. Mian.

Pia alimueleza Mhe. Dkt Tax juu ya Mpango kabambe wa kuboresha mawasiliano ya TEHAMA vijijini ambao ni sehemu ya Mkataba wa ushirikiano uliosainiwa baina ya Tanzania na China ambao unatarajiwa kutekelezwa na Kampuni hiyo. Katika mradi huo kutakuwa na jumla ya miradi 19 ya kipaumbele, uboreshaji wa mawasiliano vijijini, usambazaji wa umeme Kaskazini Mashariki mwa Tanzania pamoja na miradi 9 ya msaada ambayo itatekelezwa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Stadi (VETA) na Hospitali ya Zanzibar.

Kampuni ya Huawei Tanzania ambayo imewekeza kwa zaidi miaka 15 nchini, inashirikiana na Kampuni ya Mawasiliano ya Simu Tanzania (TTCL) kusambaza Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ili kuwezesha huduma za kidigitali kupatikana kwa urahisi nchi nzima ambapo hadi sasa mkongo huo umesambaa kwa zaidi ya kilomita 15,000 nchi nzima.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Balozi wa India nchini Mhe Binaya Pradhan, alipomtembelea ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma tarehe 10 Januari 2023
Mhe. Dkt. Tax akimsikiliza Balozi Mhe Binaya Pradhan wakati wa mazungumzo kati yao yaliyofanyika ofisini kwake jijini Dodoma. Kushoto ni Kaimu mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Halmenshi Lunyumbu.
Mhe Binaya Pradhan, Balozi wa India nchini (kulia) akiwa na Naibu Balozi wa Ubalozi huo wakati wa mazungumzo kati yake na Mhe. Dkt. Tax
Mhe Binaya Pradhan, Balozi wa India nchini akimkabidhi Mhe. Dkt. Tax zawadi ya kasha la kuhifadhia vitu.
Mhe. Dkt. Tax akiagana na Balozi Mhe Binaya Pradhan mara baada ya kukamilisha mazungumzo yao 
Mhe. Dkt. Tax na Mhe. Balozi Mhe Binaya Pradhan wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe walioshiriki mazungumzo yao 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea nchini, Mhe.  Kim Young Su alipomtembelea ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma tarehe 10 Januari 2023
Mhe. Dkt. Tax akiwa katika mazungumzo na Mhe. Balozi Kim Young Su 
Mazungumzo yakiendelea
Mhe. Dkt. Tax akiagana na Mhe. Kim Young Su mara baada ya kukamilisha mazungumzo yao
Picha ya pamoja
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Huawei Tanzania Bw. Tao Mian alipomtembelea ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma tarehe 10 Januari 2023
Mhe. Dkt. Tax akiendelea na mazungumzo na  Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Huawei Tanzania Bw. Tao Mian. Walioketi kushoto kwa Mhe. Waziri ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Magabilo Murobi na Afisa katika Idara hiyo, Bw. Herman Berege.
Picha ya pamoja
Mhe. Dkt. Tax akiagana na Bw. Tao Mian mar abaada ya kukamilisha mazungumzo yao

VACANCY ANNOUNCEMENT AT THE AFRICAN UNION COMMISSION

Monday, January 9, 2023

DKT. TAX AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UFARANSA NA WAWAKILISHI WA MASHIRIKA YA KIMATAIFA YALIYOPO NCHINI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax   leo tarehe 09 Januari 2023 amekutana kwa mazungumzo kwa nyakati tofauti na wageni mbalimbali waliomtembelea ofisini kwake Mtumba  jijini Dodoma

Wageni hao ni Balozi wa Ufaransa nchini,  Mhe. Nabil Hajlaoui; Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Bi. Mahoua Parums; Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Bianadamu na Watu, Mhe. Jaji Iman Aboud na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF), Bi. Shalini Bahuguna.

Akizungumza na Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Dkt. Tax amempongeza Mhe. Balozi Nabil Hajlaoui kwa hatua ya Ubalozi huo kufungua ofisi jijini Dodoma ikiwa ni ishara ya Ufaransa katika kuuunga mkono harakati za Serikali ya Tanzania za kuimarisha makao makuu ya nchi Dodoma.

“Mhe. Balozi nchi zetu zimekuwa na uhusiano wa kirafiki uliodumu tangu Tanzania ilipopata uhuru wake, na tumeendelea kuungana mkono katika ngazi ya nchi na hata kimataifa, na kwa hili mnalolifanya hapa Dodoma linadhihirisha kuimarika kwa ushirikiano wetu,” alisema Dkt. Tax

Akizungumza katika kikao hicho Balozi wa Ufaransa alisema nchi yake imeamua kufungua ofisi ya ubalozi jijini Dodoma kama njia mojawapo ya kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Ufaransa pamoja kuunga mkono hatua ya Serikali ya kuhamishia makao makuu yake jijini humo.

Ameongeza kusema mwezi Juni 2023 Ufaransa inatarajia kuanzisha safari za ndege za moja kwa moja kutoka Paris hadi Dar es Salaam kupitia Zanzibar. Itakumbukwa kuwa mwaka 2021 Shirika hilo lilianzisha safari zake Zanzibar kupitia Nairobi, Kenya.

Amesema kuanzishwa kwa safari hizo za moja kwa moja zitawawezesha watalii kutoka Ufaransa kuja moja kwa moja nchini na hivyo kupunguza urefu wa safari na hivyo kufanya watalii na wafanybiashara wengi kuja kuangalia fursa na kutembelea vivutio vya utalii nchini kwa urahisi.

Mhe. Balozi pia amesema Ubalozi pia utaendeloea kutoa mafunzo ya lugha ya kifaransa kwa watumishi wa umma ambapo ikwa kuanzia wanaendelea na mafunzo hayo kwa watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Ulinzi na katika Chuo cha Idara ya Uhamiaji mjini Moshi.

Mhe. Balozi pia ameongelea nia ya nchi yake kuunganisha nguvu na Tanzania katika sekta ya nishati mbadala ili kuiwezesha Tanzania kujitosheleza na nishati hiyo nchini na hivyo kukuza uchumi wake.

Katika mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Bi. Mahoua Parums, Mhe. Dkt. Tax amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na Shirika hilo katika zoezi linaloendelea la kuwarejesha kwa hiari wakimbizi kwenye nchi zao za asili.

Kwa upande wake, Bi. Parums ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuhifadhi wakimbizi licha ya changamoto mbalimbali zilizopo. Amesema Shirika lake linathamini mchango huo wa kibinadamu wa Tanzania kwa wakimbizi hao na kwamba litaendelea kushirikiana na Serikali katika kuwarejesha kwa hiari wakimbizi wa Burundi.

Akizungumza na Mhe. Jaji Iman wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Bianadamu na Watu, Mhe. Dkt. Tax amesema Serikali ya Tanzania kama mwenyeji wa Mahakama hiyo iliyopo Arusha itaendelea kutekeleza makubaliano ya mkataba wa uenyeji kama ulivyoainisha.

Naye Jaji Iman amemhakikishia ushirikiano Dkt. Tax na kwamba wanaipongeza Serikali kwa kuendelea kutekeleza makubaliano ya mkataba wa uenyeji ambapo  hadi sasa Mahakama hiyo imepatiwa eneo la ukubwa wa ekari 25 kwa ajili ya kujenga ofisi zake za kudumu jijini Arusha.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa UNICEF nchini ameipongeza Tanzania kwa kuendelea kusimamia na kutekeleza kikamilifu mikataba mbalimbali ya Kimataifa inayohusu masuala ya haki za watoto ikiwemo afya, elimu na kuwalinda dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Waziri wa Mambo ya  Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Balozi wa Ufaransa nchini, Mhe. Nabil Hajlaoui alipomtembelea ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma tarehe 09 Januari 2023
Waziri wa Mambo ya  Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Ufaransa nchini, Mhe. Nabil Hajlaoui pamoja na wajumbe walioambatana nao kwenye mazungumzo kati yao yaliyofanyika ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma tarehe 09 Januari 2023
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Bi. Bi. Mahoua Parums alipomtembelea ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma tarehe 09 Januari 2023
Mhe. Dkt. Tax akipokea zawadi ya machapisho mbalimbali kutoka kwa Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Bi. Bi. Mahoua Parums alipomtembelea ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma tarehe 09 Januari 2023
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Bianadamu na Watu, Mhe. Jaji Iman Aboud alipomtembelea ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma tarehe 09 Januari 2023
Mhe. Dkt. Tax akiwa katika mazungumzo na Mhe. Jaji Iman
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF), Bi. Shalini Bahuguna alipomtembelea ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma tarehe 09 Januari 2023
Sehemu ya ujumbe wa Mhe. Dkt. Tax ukifuatilia mazungumzo kati yake na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF), Bi. Shalini Bahuguna
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF), Bi. Shalini Bahuguna akimpatia Mhe. Dkt. Tax maelezo ya zawadi ya picha kabla ya kumkabidhi 

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF), Bi. Shalini Bahuguna akimkabidhi Mhe. Dkt. Tax zawadi ya picha ya watoto kama ishara ya kuonesha mchango wa shirika hilo katika kuwahudumia watoto hapa nchini

VACANCY ANNOUNCEMENT AT THE COMMONWEALTH SECRETARIAT

NAFASI ZA MASOMO NCHINI JAPAN