Wednesday, February 22, 2023

MAKATIBU WAKUU WAKAMILISHA MAANDALIZI YA MKUTANO WA 43 WA BARAZA LA MAWAZIRI WA EAC

Mkutano wa Makatibu Wakuu kukamilisha maandalizi ya Mkutano wa 43 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki umefanyika  jijini Bujumbura, Burundi.

 

Mkutano huo ambao umetanguliwa na mkutano wa Wataalam uliofanyika kuanzia tarehe 19 hadi 21 Februari 2023 umepokea na kupitia taarifa, agenda na mapendekezo yaliyotokana na Mkutano wa wataalam hao kuhusu masuala mbalimbali ya Jumuiya ambazo hatimaye zitawasilishwa kwenye Mkutano wa Baraza la Mawaziri tarehe 23 Februari 2023.

 

Taarifa zilizowasilishwa ni pamoja na  taarifa ya utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa kwenye vikao vilivyopita katika maeneo mbalimbali ya  biashara na forodha, miundombinu, ulinzi na usalama, sheria, utalii, ajira na utawala na fedha. Pia mkutano umepokea taarifa ya mwaka ya Ukaguzi wa Hesabu za Jumuiya kwa mwaka wa fedha ulioishia mwezi Juni 2022; Taarifa ya Ofisi ya Katibu Mkuu wa Jumuiya; Taarifa kuhusu Taasisi za Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na kupitia na kupitisha ratiba ya shughuli za Jumuiya kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Juni 2023.

 

Kadhalika masuala mengine yaliyojadiliwa ni pamoja na umuhimu wa kukitangaza Kiswahili kwa kuanzisha vituo vya utamaduni wa lugha hiyo katika Balozi za Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki; na kutoa mwelekeo wa kuanza kutumika kwa lugha ya Kifaransa na Kiswahili katika uendeshaji wa shughuli  rasmi za Jumuiya. 

 

Katika Mkutano huo ujumbe wa Tanzania umeongozwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine.

 

Viongozi wengine walioambatana naye ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi,  Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba na Sheria, Dkt. Khatibu Kazungu, Naibu  Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Yamungu Kayandabila na Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Mhe. Dkt. Jilly Maleko.

 

Wengine waliombatana naye ni Balozi Stephen  Mbundi, Mkurugenzi wa Siasa, Ulinzi na Usalama, Bw. Bernard Haule Mkurugenzi Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji, Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Bw. Haji Janabi wote wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na Maafisa kutoka Wizara mbalimbali. 

 

Mkutano huo ambao umefanyika chini ya uenyekiti wa Burundi, umehudhuriwa na nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki huku Sudan Kusini wakishiriki kwa njia ya mtandao

Mwenyekiti wa Mkutano wa Makatibu Wakuu ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Burundi, Bw. Severin Mbarubukeye (katikati) akiongoza Mkutano wa Makatibu Wakuu uliofanyika jijini Bujumbura tarehe 22 Februari 2023 kwa ajili ya kuandaa Mkutano wa 43 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika jijini hapa tarehe 23 Februari 2023. Mkutano huo pamoja na mambo mengine umejadili na kupitisha agenda mbalimbali zitakazowasilishwa kwenye Mkutano wa Mawaziri. Kushoto ni Naibu katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhandisi Steven Mlote

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine (kulia) akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Makatibu Wakuu uliofanyika jijini Bujumbura tarehe 22 Februari 2023 kwa ajili ya kukamilisha maandalizi ya Mkutano wa 43 wa Baraza la Mawaziri la  Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika jijini hapa tarehe 23 Fevruari 2023. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bibi. Amina Khamis Shaaban na katikati ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akichangia jambo wakati wa Mkutano wa makatibu Wakuu uliofanyika Bujumbura kuandaa Mkutano wa 43 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
Mkutano ukiendelea
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akisaini Ripoti itakayowasilishwa kwenye Mkutano wa 43 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
Mwenyekiti kutoka Burundi nae akisaini Ripoti hiyo
Mjumbe kutoka Rwanda nae akisaini Ripoti
Mjumbe kutoka Uganda akisaini Ripoti

Mjumbe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo akisaini ripoti

Mjumbe kutoka Kenya akisaini ripoti

Balozi Sokoine akibadilisha kwa pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Kenya, Bw. Abdi Dubat na Mjumbe kutoka Uganda wakibadilishana mawazo wakati wa mkutano wa Makatibu Wakuu

Awali Timu ya maandalizi ya Mkutano wa 43 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Ngazi ya Wataalam wakisaini ripoti iliyowasilishwa kwenye Mkutano wa Makatibu Wakuu. Ujumbe  Tanzania uliongozwa na Mkurugenzi wa Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi (wa pili kushoto)

Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Mhe. Dkt. Jilly Maleko (kushoto) akishiriki moja ya vikao vya maandalizi
Wajumbe wengine kutoka Tanzania katika vikao vya maandalizi

Wajumbe wakifuatilia mikutano ya maandalizi ya Mkutano wa 43 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya  ya Afrika Mashariki

Mkutano ukiendelea


VACANCY ANNOUNCEMENT AT COMMONWEALTH SECRETARIAT


 

Tuesday, February 21, 2023

MAANDALIZI YA MKUTANO WA KAWAIDA WA 43 WA BARAZA LA MAWAZIRI WA EAC YAENDELEA BUJUMBURA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akipokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Mhe. Dkt. Jilly Maleko mara baada ya kuwasili Ubalozini hapo kwa ajili ya kupokea taarifa ya nchi kuhusu  maandalizi ya Mkutano wa 43 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaotarajiwa kufanyika jijini Bujumbura tarehe 23 Februari 2023. Balozi Sokoine ataongoza Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Makatibu Wakuu wa Jumuiya hiyo utakaofanyika tarehe 22 Februari 2022
Mhe. Balozi Maleko akimkaribisha Ubalozini, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban
B
Balozi Sokoine akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Ubalozi wa Tanzania nchini Burundi huku Balozi Dkt. Maleko akishuhudia.
 
Balozi Sokoine akimsikiliza Kiongozi wa Ujumbe wa Tanzania kweynye Mkutano wa EAC, Ngazi ya Wataalam, Balozi Stephen Mbundi wakati akitoa taarifa kuhusu maandalizi ya agenda mbalimbali za mkutano zilizojadiliwa katika kikao cha wataalam kilichofanyika kuanzaia tarehe 19 hadi 21 Februari 2023.


Sehemu ya viongozi watakaoshiriki Mkutano wa Makatibu Wakuu wakiwemo Naibu Makatibu Wakuu na Naibu Gavana kikao cha kupokea taarifa ya nchi ya maandalizi ya Mkutano wa 43 wa Baraza la Mawaziri wa EAC kutoka kwa wataalam
Sehemu nyingine ya viongozi kwenye kikao hicho
 
Sehemu ya Wakurugenzi kutoka Wizara mbalimbali walioshiriki mkutano wa wataalam wakiwa katika kikao na kiongozi wa ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano wa makatibu wakuu utakaofanyika tarehe 22 Februari 2023
Kikao kikiendelea


Sehemu nyingine ya Wakurugenzi
Kikao kikiendelea

Kikao kikiendelea

Kikao kikiendelea

Wajumbe wakiwa katika kikao

Kikao kikiendelea









Tanzania showcased tourism attraction in Israel

 

Tanzania showcased tourism attraction in Israel

The Embassy of the United Republic of Tanzania to Israel in collaboration with African Queen Adventures ltd, Ona safaris ltd, Land Africa ltd, Masai Land ltd, Sun Tour and Travel ltd, Endito Nagoi Adventures ltd, Zagas Explorer ltd, African Escape Safari ltd and other key players in the tourism sector participated in the International Mediterranean Tourism Market (IMTM) held in Tel Aviv, Israel from 14th to 15th February 2023.

During the official opening of the IMTM 2023, The Ambassador of the United Republic of Tanzania to Israel, H.E Alex Gabriel Kallua said the exhibition was an opportunity for Tanzania to showcase her abundant tourism attractions to such unique platform that attract reputable tourism companies available in the world. Tanzania’s participation in IMTM 2023 would strengthen the relationship with the Israel not only in tourism industry but also in other sectors, He added.

International Mediterranean Tourism Market (IMTM) is a global networking and industry event designed to connect professionals from all levels of business and service in tourism and travel, offering the opportunity to exhibit an in-person exhibition at the Tel Aviv Expo Centre- Israel.

Tanzania Booth at the International Mediterranean Tourism Market (IMTM) held in Tel Aviv, Israel from 14th to 15th February 2023

Showcasing Tanzania's tourism attractions at the International Mediterranean Tourism Market (IMTM) in Israel



Sunday, February 19, 2023

MKUTANO WA KAWAIDA WA 43 WA BARAZA LA MAWAZIRI WA EAC KUFANYIKA BURUNDI


Mkutano wa Kawaida wa 43 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unatarajiwa kufanyika jijini Bujumbura, Burundi tarehe 23 Februari 2023.

 

Mkutano huo ambao umeanza kwa Ngazi ya Wataalam tarehe19 hadi 20 Februari 2023 utafuatiwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu utakaofanyika tarehe 21 na 22 Februari 2023 na kuhitimishwa na Mkutano wa Mawaziri utakaofanyika tarehe 23 Februari 2023.

 

Mkutano wa Wataalam utapitia na kujadili agenda mbalimbali muhimu kuhusu masuala ya mtangamano wa Jumuiya hiyo ambazo baadaye zitawasilishwa kwenye Mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu utakaofanyika tarehe 21 na 22 Februari 2023 kwa majadiliano na hatimaye agenda hizo zitawasilishwa kwenye Mkutano ngazi ya  Mawaziri unaotarajiwa kufanyika jijini hapa tarehe 23 Februari 2023.

 

Miongoni mwa agenda hizo ni pamoja na Taarifa ya Utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa kwenye vikao vilivyopita katika maeneo mbalimbali ikiwemo biashara na forodha, miundombinu, ulinzi na usalama, sheria, utalii, ajira na utawala na fedha; Kupokea taarifa ya mwaka ya Ukaguzi wa Hesabu za Jumuiya kwa mwaka wa fedha ulioishia mwezi Juni 2022; Taarifa ya Ofisi ya Katibu Mkuu wa Jumuiya; Taarifa kuhusu Taasisi za Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na kupitia na kupitisha ratiba ya shughuli za Jumuiya kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Juni 2023.

 

Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Ngazi ya Wataalam unaongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi. Ujumbe huo pia unajumuisha Wajumbe kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Wizara ya Fedha na Mipango na Wizara ya Katiba na Sheria.

 

Kadhalika Mkutano huo umehudhuriwa na Wajumbe kutoka nchi zote wanachama ambazo ni Burundi ambaye ni mwenyeji wa mkutano, Kenya, Uganda, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Sudan Kusini ambao wameshiriki kwa njia ya mtandao.

Mwenyekiti wa Mkutano wa majadiliano kwa ngazi ya wataalam kutoka Burundi (kushoto) akiongoza kikao hicho kilichofanyika jijini Bujumbura, Burundi tarehe 19 Februari 2023 kwa ajili ya kuandaa Mkutano wa Kawaida wa 43 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Masahriki unaotarajiwa kufanyika tarehe 23 Februari 2023. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Mipango na Utawala, Mhandisi Steven Mlote.
Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa majadiliano kwa ngazi ya wataalam uliofanyika jijini Bujumbura, Burundi tarehe 19 Februari 2023 kwa ajili ya kuandaa Mkutano wa Kawaida wa 43 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Masahriki unaotarajiwa kufanyika tarehe 23 Februari 2023. Mkutano kwa ngazi ya wataalam unafanyika kuanzia tarehe 19 hadi 20 Februari 2023 na utafuatiwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu tarehe 21 na 22 Februari 2023. Kulia ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Haji Janabi

Ujumbe wa Burundi ukishiriki Mkutano wa Ngazi ya Wataalam unaofanyika jijjini Bujumbura, Burundi kwa ajili ya kuandaa Mkutano wa Kawaida wa 43 wa Baraza la Mawaziri wa EAC. Burundi ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Kiongozi wa Ujumbe wa Rwanda akishiriki Mkutano wa Wataalam
Ujumbe wa Uganda ukishiriki Mkutano huo
Ujumbe wa Kenya nao ukiwa katika Mkutano
Kiongozi wa Ujumbe wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo nae akishiriki mkutano wa wataalam
Wajumbe kutoka Taasisi za Jumuiya ya Afrika wakishiriki mkutano wamaandalizi ya mkutano wa 43 wa Baraza la Mawaziri wa EAC

Wajumbe kutoka Sekreatarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wakishiriki Mkutano wa Wataalam jijini Bujumbura
Mkurugenzi wa Uendelezaji wa Sera, Ofisi ya Rais, Menejementi ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi Agnes Meena akishiriki Mkutano wa Wataalam
Mkurugenzi wa Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw.  Bernard Haule akishiriki mkutano wa wataalam

Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania wakishiriki Mkutano wa Wataalam
Sehemu ya Wajumbe wa Sekretarieti ya EAC wakifuatilia mkutano
Mkutano ukiendelea
Wajumbe kutoka Tanzania katika mkutano
Mkutano ukiendelea



















 

Thursday, February 16, 2023

TANZANIA, ANGOLA ZASAINI HATI ZA MAKUBALIANO

Serikali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Angola zimesaini Hati mbili za Makubaliano (MoU) kuanzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja (JPC) na Ushirikiano kati ya Chuo Cha Diplomasia cha Tanzania (CFR) na Chuo cha Venancio de Moura cha Angola.

Makubaliano hayo yamesainiwa leo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola, Mhe. Balozi Téte António katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, Addis Ababa nchini Ethiopia.

Mara baada ya kusaini Hati hizo za Makubaliano, Dkt. Tax alisema Tanzania na Angola zimekuwa zikishirikiana kwa muda mrefu, na Tanzania ilikuwa mstari wa mbele kuzisaidia nchi za Kusini mwa Bara la Afrika kujikomboa na tangu wakati huo imeendelea kushirikiana katika maeneo mbalimbali.

“Leo tumeona ni vyema turasimishe ushirikiano wetu kwa sababu dunia inakwenda mbele na kuna mambo mengi ya kufanya pamoja na hivyo tumesaini Hati mbili za Makubaliano ya kuanzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja itakayotuwezesha kukutana na kujadili masuala mbalimbali yenye manufaa kwa pande zote mbili.

………lakini sisi kwa kuwa ni wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Umoja wa Afrika (AU) tutaweza kujadili yanayojiri katika Kanda zetu na Kimataifa na kuona tunavyoweza kufanyia kazi kwa pamoja kwani umoja ni nguvu,” alisema Dkt. Tax

Kuhusu Makubaliano ya Ushirikiano wa Vyuo vya Diplomasia kati ya Tanzania na Angola, Waziri Tax alisema kupitia makubaliano hayo vyuo hivyo vitaweza kubadilishana uzoefu, utaalamu na wanafunzi ili kuboresha taasisi hizo za diplomasia.

“Kupitia makubaliano tuliyosaini leo, vyuo vyetu vya Dioplomasia vitabadilishana uzoefu, utaalamu na wanafunzi ili kuboresha zaidi taasisi zetu hizi za diplomasia,” alisema Waziri Tax.

Kwa Upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola, Mhe. Balozi Téte António amesema Angola imefurahishwa na uamuzi wa Serikali ya Tanzania kukubali kuanzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja (JPC) na kuelezea utayari wake wa kushirikiana katika nyanja mbalimbali kwa maslahi ya pande zote mbili.

“Tanzania na Angola ni marafiki wa siku nyingi, kupiti makubaliano tuliyosaini leo tumefungua ukurasa mpya wa ushirikiano baina ya mataifa yetu, tunayo mengi ya kushirikiana.

Kadhalika, kuhusu ushirikiano wa vyuo vyetu Waangola tumekuwa tukija kujifunza masuala mbalimbali ya kidiplomasia katika Chuo cha Diplomasia (CFR) na kuwa wanadiplomasia, hivyo kupitia makubaliano ya leo tutaweza kubadilishana uzoefu wa kidiplomasia na kuwanoa wanadiplomasia wengi zaidi,” alisema Balozi António.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola, Mhe. Balozi Téte António wakisaini Hati za Makubaliano (MoUs) za kuanzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja (JPC) na Hati ya Ushirikiano kati ya Chuo Cha Diplomasia cha Tanzania (CFR) na Chuo cha Venancio de Moura cha Angola. Hafla ya utiaji saini imefanyika katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 16 Februari 2023.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola, Mhe. Balozi Téte António wakibadilishana Hati za Makubaliano (MoUs) za kuanzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja (JPC) na Hati ya Ushirikiano kati ya Chuo Cha Diplomasia cha Tanzania (CFR) na Chuo cha Venancio de Moura cha Angola baada ya kuzisaini katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 16 Februari 2023.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akieleza jambo baada ya kusaini Hati za Makubaliano (MoUs) za kuanzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja (JPC) na Hati ya Ushirikiano kati ya Chuo Cha Diplomasia cha Tanzania (CFR) na Chuo cha Venancio de Moura cha Angola katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 16 Februari 2023.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola, Mhe. Balozi Téte António baada ya kusaini Hati za Makubaliano (MoUs) katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 16 Februari 2023.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika na Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola, Mhe. Balozi Téte António kwenye picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa serikali za Tanzania na Angola katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 16 Februari 2023


UBALOZI AUSTRIA WAFANIKISHA UWEKAJI SAINI HATI YA MAKUBALIANO SEKTA YA AFYA

Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika (wa pili kushoto); Naibu Mkuu wa Chuo cha Tiba cha Vienna, Dkt. Michaela Fritz na Mkurugenzi wa Idara ya Urolojia katika Hospitali Kuu ya Vienna, Prof. Shahrokh Shariat wakiweka saini Hati ya Makubaliano kuhusu kushirikiana katika masuala ya tiba za kibingwa. Kulia ni Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Austria, Bi. Elizabeth Rwitunga.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika (wa pili kushoto); Naibu Mkuu wa Chuo cha Tiba cha Vienna, Dkt. Michaela Fritz na Mkurugenzi wa Idara ya Urolojia katika Hospitali Kuu ya Vienna, Prof. Shahrokh Shariat wakibadilishana Hati ya Makubaliano kuhusu kushirikiana katika masuala ya tiba za kibingwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Hosiptali ya Benjamin Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika akifanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kimataifa ya Open Medical Institute yenye makao makuu Austria, Prof. Wolfgang Aulitzky.