Sunday, February 19, 2023

MKUTANO WA KAWAIDA WA 43 WA BARAZA LA MAWAZIRI WA EAC KUFANYIKA BURUNDI


Mkutano wa Kawaida wa 43 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unatarajiwa kufanyika jijini Bujumbura, Burundi tarehe 23 Februari 2023.

 

Mkutano huo ambao umeanza kwa Ngazi ya Wataalam tarehe19 hadi 20 Februari 2023 utafuatiwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu utakaofanyika tarehe 21 na 22 Februari 2023 na kuhitimishwa na Mkutano wa Mawaziri utakaofanyika tarehe 23 Februari 2023.

 

Mkutano wa Wataalam utapitia na kujadili agenda mbalimbali muhimu kuhusu masuala ya mtangamano wa Jumuiya hiyo ambazo baadaye zitawasilishwa kwenye Mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu utakaofanyika tarehe 21 na 22 Februari 2023 kwa majadiliano na hatimaye agenda hizo zitawasilishwa kwenye Mkutano ngazi ya  Mawaziri unaotarajiwa kufanyika jijini hapa tarehe 23 Februari 2023.

 

Miongoni mwa agenda hizo ni pamoja na Taarifa ya Utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa kwenye vikao vilivyopita katika maeneo mbalimbali ikiwemo biashara na forodha, miundombinu, ulinzi na usalama, sheria, utalii, ajira na utawala na fedha; Kupokea taarifa ya mwaka ya Ukaguzi wa Hesabu za Jumuiya kwa mwaka wa fedha ulioishia mwezi Juni 2022; Taarifa ya Ofisi ya Katibu Mkuu wa Jumuiya; Taarifa kuhusu Taasisi za Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na kupitia na kupitisha ratiba ya shughuli za Jumuiya kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Juni 2023.

 

Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Ngazi ya Wataalam unaongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi. Ujumbe huo pia unajumuisha Wajumbe kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Wizara ya Fedha na Mipango na Wizara ya Katiba na Sheria.

 

Kadhalika Mkutano huo umehudhuriwa na Wajumbe kutoka nchi zote wanachama ambazo ni Burundi ambaye ni mwenyeji wa mkutano, Kenya, Uganda, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Sudan Kusini ambao wameshiriki kwa njia ya mtandao.

Mwenyekiti wa Mkutano wa majadiliano kwa ngazi ya wataalam kutoka Burundi (kushoto) akiongoza kikao hicho kilichofanyika jijini Bujumbura, Burundi tarehe 19 Februari 2023 kwa ajili ya kuandaa Mkutano wa Kawaida wa 43 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Masahriki unaotarajiwa kufanyika tarehe 23 Februari 2023. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Mipango na Utawala, Mhandisi Steven Mlote.
Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa majadiliano kwa ngazi ya wataalam uliofanyika jijini Bujumbura, Burundi tarehe 19 Februari 2023 kwa ajili ya kuandaa Mkutano wa Kawaida wa 43 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Masahriki unaotarajiwa kufanyika tarehe 23 Februari 2023. Mkutano kwa ngazi ya wataalam unafanyika kuanzia tarehe 19 hadi 20 Februari 2023 na utafuatiwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu tarehe 21 na 22 Februari 2023. Kulia ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Haji Janabi

Ujumbe wa Burundi ukishiriki Mkutano wa Ngazi ya Wataalam unaofanyika jijjini Bujumbura, Burundi kwa ajili ya kuandaa Mkutano wa Kawaida wa 43 wa Baraza la Mawaziri wa EAC. Burundi ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Kiongozi wa Ujumbe wa Rwanda akishiriki Mkutano wa Wataalam
Ujumbe wa Uganda ukishiriki Mkutano huo
Ujumbe wa Kenya nao ukiwa katika Mkutano
Kiongozi wa Ujumbe wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo nae akishiriki mkutano wa wataalam
Wajumbe kutoka Taasisi za Jumuiya ya Afrika wakishiriki mkutano wamaandalizi ya mkutano wa 43 wa Baraza la Mawaziri wa EAC

Wajumbe kutoka Sekreatarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wakishiriki Mkutano wa Wataalam jijini Bujumbura
Mkurugenzi wa Uendelezaji wa Sera, Ofisi ya Rais, Menejementi ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi Agnes Meena akishiriki Mkutano wa Wataalam
Mkurugenzi wa Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw.  Bernard Haule akishiriki mkutano wa wataalam

Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania wakishiriki Mkutano wa Wataalam
Sehemu ya Wajumbe wa Sekretarieti ya EAC wakifuatilia mkutano
Mkutano ukiendelea
Wajumbe kutoka Tanzania katika mkutano
Mkutano ukiendelea



















 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.