Monday, May 29, 2023

MKUTANO MAALUM WA MAWAZIRI WA ULINZI WA EAC WAFANYIKA JIJINI BUJUMBURA

Mkutano Maalum wa Mawaziri wa Ulinzi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kujadili hali ya Usalama katika Eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umefanyika jijini Bujumbura, Burundi tarehe 29 Mei 2023.

 

Akifungua Mkutano huo, Waziri wa Ulinzi wa Burundi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mawaziri wa Ulinzi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Alain Tribert Mutabaze, amesema jitihada za pamoja ikiwemo mikakati mipya ya namna ya kukabiliana na vikundi vya waasi katika eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo bado zinahitajika ili kuhakikisha amani ya kudumu inapatikana katika eneo hilo.

 

Amesema  pamoja na kupongeza jitihada nyingi zinazofanywa na Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki  ikiwemo kupeleka Kikosi cha Kulinda amani cha Jumuiya (EACRF),  bado ipo haja ya kufanya tathmini ya mara kwa mara ya mikakati iliyopo kama inaleta tija na kuandaa mikakati  mipya ikiwa ni pamoja na kuviwezesha Vikosi hivyo  ili viweze kutekeleza kikamilifu jukumu la  kulinda amani  katika eneo hilo.

 

“Changamoto katika eneo la Mashariki mwa Congo bado zipo. Tunatakiwa kuboresha mikakati yetu na kufanya tathmini za mara kwa mara ya maendeleo ya jitihada hizi,  kwani hali inayoendelea Mashariki mwa Congo inatuathiri sote kama jumuiya kwa namna moja au nyingine. Hivyo niwaombe Waheshimiwa Mawaziri tuje na mapendekezo yenye tija  tutakayoyawasilisha kwa Wakuu wetu wa Nchi kwa mustakabali wa eneo  hilo la Mashariki mwa Congo na sisi sote” amesema Mhe.  Mutabaze.

 

Mhe. Mutabaze pia alitumia fursa hiyo kuwakaribisha Mawaziri hao nchini Burundi na kuwaomba kutumia muda wao kujadili na kuandaa mapendekezo yatakayoleta suluhu ya kudumu nchini DRC hususan eneo la Mashariki mwa nchi hiyo.

 

Awali akizungumza kwenye mkutano huo,  Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,  Dkt. Peter Mathuki amesema  Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki itaendelea kufanya kazi bega kwa bega na Nchi Wanachama ili kuhakikisha amani na utulivu wa kudumu unapatikana katika eneo la Mashariki mwa Congo.

 

Mkutano huo umewahusisha Mawaziri wa Ulinzi kutoka nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Makatibu Wakuu  na Wakuu wa Majeshi.

 

Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano huo umeongozwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Innocent Bashungwa (Mb.) na kumshirikisha pia Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,  Dkt. Faraji Mnyepe, Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Mhe. Jilly Maleko, Mkurugenzi wa Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi pamoja na Maafisa wengine waandamizi kutoka Serikalini.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Innocent Bashungwa (kulia) ambaye pia anaongoza Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano Maalum wa Mawaziri wa Ulinzi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu hali ya Usalama katika Eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo   akizungumza wakati wa mkutano huo uliofanyika Bujumbura, Burundi tarehe 29 Mei 2023. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Faraji Mnyepe na Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Mhe. Jilly Maleko.
Waziri wa Ulinzi wa Burundi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mawaziri wa Ulinzi wa Jumuiya ya Afrika Masahriki, Mhe. Alain Tribert Mutabaze akifungua rasmi Mkutano Maalum wa Mawaziri wa Ulinzi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu hali ya Usalama katika Eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo uliofanyika jijini Bujumbura tarehe 29 Mei 2023
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Peter Mathuki akizungumza wakati wa Mkutano Maalum wa Mawaziri wa Ulinzi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu hali ya Usalama katika Eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo uliofanyika jijini Bujumbura, Burundi tarehe 29 Mei 2023
Mkurugenzi wa Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi (kulia) akishiriki Mkutano Maalum wa Mawaziri wa Ulinzi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu hali ya Usalama katika Eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo uliofanyika jijini Bujumbura, Burundi tarehe 29 Mei 2023
Ujumbe wa Burundi katika Mkutano Maalum wa Mawaziri wa Ulinzi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu hali ya Usalama katika Eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Ujumbe wa Sudan Kusini ukishiriki Mkutano Maalum wa Mawaziri wa Ulinzi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu hali ya Usalama katika Eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Ujumbe wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika Mkutano Maalum wa Mawaziri wa Ulinzi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu hali ya Usalama katika Eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Ujumbe wa Kenya ukishiriki Mkutano Maalum wa Mawaziri wa Ulinzi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu hali ya Usalama katika Eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Mhe. Bashungwa kwa pamoja na Katibu Mkuu, Dkt. Mnyepe na Mhe. Balozi Maleko wakiimba wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa ufunguzi rasmi wa Mkutano Maalum wa Mawaziri wa Ulinzi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu hali ya Usalama katika Eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
.
Sehemu ya Ujumbe wa Rwanda ukishiriki wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa ufunguzi rasmi wa Mkutano Maalum wa Mawaziri wa Ulinzi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu hali ya Usalama katika Eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Balozi Mbundi na washiriki wengine wakiimba wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa ufunguzi rasmi wa Mkutano Maalum wa Mawaziri wa Ulinzi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu hali ya Usalama katika Eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Mnyepe akiteta jambo na Balozi Maleko kabla ya kuanza kwa Mkutano Maalum wa Mawaziri wa Ulinzi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu hali ya Usalama katika Eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo


ehemu ya ujumbe wa Tanzania wakishiriki Mkutano Maalum wa Mawaziri wa Ulinzi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu hali ya Usalama katika Eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania wakishiriki Mkutano Maalum wa Mawaziri wa Ulinzi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu hali ya Usalama katika Eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Picha ya pamoja

Picha ya pamoja





 
 
 

VACANCY ANNOUNCEMENT AT UNECA https://www.uneca.org/about/vacancies




 

Friday, May 26, 2023

WAZIRI TAX ASISITIZA UBORA WA KAZI KWA WATUMISHI WA WIZARA


Meza Kuu wakiwa katika hali ya furaha walipojumuika na Watumishi wa Wizara (hawapo pichani) kuimba wimbo wa mshikamano daima kwenye Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dodoma.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax amewasisitiza watumishi wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa kujituma na kuzingatia ubora wa kazi wanapotekeleza majukumu yao.

Waziri Tax ameyasema hayo alipokuwa akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dodoma tarehe 26 Mei, 2023.

Pia akawaeleza wajumbe wa mkutano huo kuwa wanawajibu wa kuelewa kwa ufasaha bajeti na mipango iliyowekwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2023/2024 ili kujipanga kutekeleza vipaumbele vya Wizara kikamilifu.

‘’Pamoja na kuielewa mipango ni jukumu lenu pia kupendekeza mipango na mikakati mizuri zaidi katika kutekeleza vipaumbele vya Wizara katika utekelezaji wa majukumu hususan, kufanikisha utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi na uwekezaji,” alisema Dkt. Tax.

Kwa upande wa Katibu Mkuu na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Samwel Shelukindo katika hotuba yake ya ufunguzi ameeleza kuwa baraza la wafanyakazi ni takwa la kisheria na pia linaleta fursa ya ushirikishwaji kwa watumishi hasa katika mipango ya uendeshaji wa Wizara na hivyo huchangia ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara.

"Hivyo, ni matumani yangu kuwa wajumbe wa mkutano huu mtatoa michango yenye tija ambayo itaboresha Rasimu ya Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kabla ya kusomwa Bungeni” alisema Balozi Shelukindo.


Naye Naibu Katibu Mkuu TUGHE Taifa, Bw. Samuel Nyungwa akizungumza, ameushukuru uongozi wa Wizara kwa kuendelea kuthamini umuhimu na tija ya baraza hilo pamoja na kutoa nafasi ya ushirikishwaji wa mipango ya Wizara kwa watumishi.

Lengo la Mkutano wa Baraza la wafanyakazi ni kupitia taarifa ya utekelezaji wa Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2022/2023, na makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2023/2024, bajeti ambayo inatarajiwa kuwasilishwa Bungeni tarehe 30 Mei 2023. 

Mkutano huu ulihudhuriwa pia na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Samweli Shelukindo akitoa neno la utangulizi kwenye Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dodoma.
Meza Kuu wakifuatilia Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dodoma
Sehemu ya Wakuu wa Idara na Vitengo wakifuatilia Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliokuwa ukiendelea jijini Dodoma
Meza Kuu wakishirikiana na Wajumbe wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (hawapo pichani) kuimba wimbo wa mshikamano daima
Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Bi. Chiku Kiguhe akifuatilia Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (katikati) akiwasili katika ukumbi wa St. Gapar kufungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu TUGHE Taifa, Bw. Samuel Nyungwa akizungumza kwenye Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dodoma
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mindi Kasiga akifuatilia Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliokuwa ukiendelea jijini Dodoma
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax mara baada ya kuzindua Baraza hilo jijini Dodoma.

SERIKALI YA TANZANIA YAPEWA TUZO NA DRC

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kupitia kwa Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani na Usalama, Mhe  Peter Kazadi ameikabidhi Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tuzo ya Heshima (Gardons notre amitié) - inayohusu KUDUMISHA UHUSIANO baina ya Nchi hizo mbili .Tuzo hiyo imepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini DRC, Mhe. Said J Mshana wakati wa Sherehe za Miaka 60 ya Umoja wa Afrika iliyoandaliwa kwa ajili ya Mawaziri wa SADC waliohudhuria Mkutano kuhusu Udhibiti wa Maafa.

Balozi wa Tanzania nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mhe Said J Mshana akiongea jambo baada ya kukabidhiwa Tuzo na Serikali ya DRC

Balozi wa Tanzania nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mhe Said J Mshana alimwakilisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Sera, Bunge na Uratibu katika kikao cha Mawaziri wa SADC kilichohusu udhibiti wa maafa kilichofanyika jijini Kinshasa.
Hadi kufikia tarehe 25 Mei 2023, Nchi Wanachama sita kati ya kumi na sita zilikuwa zimesaini Mkataba wa Uendeshaji wa Kituo cha Operesheni na Huduma za Kibinadamu cha SADC.
Balozi wa Tanzania nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mhe Said J Mshana katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano wa Mawaziri wa SADC uliohusu udhibiti wa maafa uliofanyika jijini Kinshasa