Friday, May 26, 2023

WAZIRI TAX ASISITIZA UBORA WA KAZI KWA WATUMISHI WA WIZARA


Meza Kuu wakiwa katika hali ya furaha walipojumuika na Watumishi wa Wizara (hawapo pichani) kuimba wimbo wa mshikamano daima kwenye Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dodoma.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax amewasisitiza watumishi wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa kujituma na kuzingatia ubora wa kazi wanapotekeleza majukumu yao.

Waziri Tax ameyasema hayo alipokuwa akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dodoma tarehe 26 Mei, 2023.

Pia akawaeleza wajumbe wa mkutano huo kuwa wanawajibu wa kuelewa kwa ufasaha bajeti na mipango iliyowekwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2023/2024 ili kujipanga kutekeleza vipaumbele vya Wizara kikamilifu.

‘’Pamoja na kuielewa mipango ni jukumu lenu pia kupendekeza mipango na mikakati mizuri zaidi katika kutekeleza vipaumbele vya Wizara katika utekelezaji wa majukumu hususan, kufanikisha utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi na uwekezaji,” alisema Dkt. Tax.

Kwa upande wa Katibu Mkuu na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Samwel Shelukindo katika hotuba yake ya ufunguzi ameeleza kuwa baraza la wafanyakazi ni takwa la kisheria na pia linaleta fursa ya ushirikishwaji kwa watumishi hasa katika mipango ya uendeshaji wa Wizara na hivyo huchangia ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara.

"Hivyo, ni matumani yangu kuwa wajumbe wa mkutano huu mtatoa michango yenye tija ambayo itaboresha Rasimu ya Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kabla ya kusomwa Bungeni” alisema Balozi Shelukindo.


Naye Naibu Katibu Mkuu TUGHE Taifa, Bw. Samuel Nyungwa akizungumza, ameushukuru uongozi wa Wizara kwa kuendelea kuthamini umuhimu na tija ya baraza hilo pamoja na kutoa nafasi ya ushirikishwaji wa mipango ya Wizara kwa watumishi.

Lengo la Mkutano wa Baraza la wafanyakazi ni kupitia taarifa ya utekelezaji wa Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2022/2023, na makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2023/2024, bajeti ambayo inatarajiwa kuwasilishwa Bungeni tarehe 30 Mei 2023. 

Mkutano huu ulihudhuriwa pia na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Samweli Shelukindo akitoa neno la utangulizi kwenye Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dodoma.
Meza Kuu wakifuatilia Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dodoma
Sehemu ya Wakuu wa Idara na Vitengo wakifuatilia Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliokuwa ukiendelea jijini Dodoma
Meza Kuu wakishirikiana na Wajumbe wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (hawapo pichani) kuimba wimbo wa mshikamano daima
Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Bi. Chiku Kiguhe akifuatilia Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (katikati) akiwasili katika ukumbi wa St. Gapar kufungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu TUGHE Taifa, Bw. Samuel Nyungwa akizungumza kwenye Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dodoma
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mindi Kasiga akifuatilia Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliokuwa ukiendelea jijini Dodoma
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax mara baada ya kuzindua Baraza hilo jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.