Mkurugenzi
wa Forodha na Ushuru wa bidhaa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) anayesimamia
majimbo ya Haut Katanga, Lualaba, Tanganyika na Lomami, Bw. René Kalala
Masimango na ujumbe wake upo nchini kwa ziara ya kikazi ambapo tarehe 04 Mei
2023 ulikutana na Uongozi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) jijini Dar Es
Salaam.
Akizungumzia
kuhusu ziara hiyo, Balozi wa Tanzania nchini DRC, Mhe. Said Mshana alisema
ubalozi wake umeiandaa kwa lengo la kuwakutanisha wadau wa Tanzania na DRC ili wajadili
na kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazokwamisha biashara kati ya nchi hizo
mbili.
Wakati
wa kikao na uongozi wa TPA, Bw. Masimango alisema Bandari ya Dar es Salaam ni
muhimu sana kwa mizigo ya Congo na inahudumia mizigo mingi, hivyo ziara yake ni
kujionea utendaji kazi wa Bandari na ameridhika kuwa kazi zinazofanywa na
mamlaka hiyo ni nzuri na zimepangiliwa vizuri.
Kwa upande
wake, Mkurugenzi Mkuu wa TPA Bw. Plasduce Mkeli Mbossa ameahidi kuwa
Menejimenti yake ipo tayari kutatua changamoto zozote zitakazojitokeza katika
kuhudumia shehena ya mizigo inayoenda na kutoka Congo kupitia Bandari za Tanzania
kwa lengo la kulinda uhusiano mzuri na wa muda mrefu wa kidiplomasia na
biashara kati ya nchi hizi mbili.
“Menejimenti
ya TPA itaendelea kuzifanyia kazi changamoto zozote katika kuhudumia shehena ya
Congo na kuimarisha uhusiano ili shughuli zinazofanywa na TPA katika bandari
zake ziwe na manufaa kwa DRC.” Alisema Bw. Mbossa.
Naye
Balozi wa DRC nchini Tanzania, Mhe. Jean Pierre Massala amesema ziara hiyo ni
muhimu kwa uhusiano kati ya DRC na Tanzania na muhimu ni kufanya kazi kwa
pamoja kwa faida ya nchi hizi mbili.
Ujumbe
huo wa DRC unaendelea na ziara yake nchini na leo tarehe 05 Mei 2023 umepanga
kutembelea Bandari Kavu ya Kwala na Reli ya Kisasa ya SGR.
|
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Bw. Plasduce Mkeli Mbossa akitoa maelezo kwa ujumbe wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ukiongozwa na Mkurugenzi wa Forodha na
Ushuru wa bidhaa anayesimamia
majimbo ya Haut Katanga, Lualaba, Tanganyika na Lomami, Bw. René Kalala
Masimango ulipotembelea bandari ya Dar Es Salaam |
|
Balozi wa Tanzania nchini
DRC, Mhe. Said Mshana (kushoto) akizungumza wakati wa kikao baina ya ujumbe wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ukiongozwa na Mkurugenzi wa Forodha na Ushuru wa bidhaa anayesimamia majimbo ya Haut Katanga, Lualaba, Tanganyika na Lomami, Bw. René Kalala Masimango na uongozi wa TPA. |
|
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Bw. Plasduce Mkeli Mbossa (wa nne kulia) na Balozi wa Tanzania nchini DRC, Mhe. Said Mshana (katikati) katika picha ya pamoja na ujumbe wa DRC uliotembelea Bandari ya Dar Es Salaam. |
|
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Bw. Plasduce Mkeli Mbossa akiwapitisha maeneo mbalimbali ya Bandari ya Dar Es Salaam ujumbe wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ukiongozwa na Mkurugenzi wa Forodha na Ushuru wa bidhaa anayesimamia majimbo ya Haut Katanga, Lualaba, Tanganyika na Lomami, Bw. René Kalala Masimango ulipotembelea bandari hiyo |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.