Friday, July 21, 2023

NCHI WANACHAMA WA SADC ZARIDHIA KUMUUNGA MKONO DKT. TULIA NAFASI YA URAIS UMOJA WA MABUNGE DUNIANI

Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (MCO) imeridhia kwa kauli moja kumuunga mkono mgombea wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb.), Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kama mgombea wa Kanda katika nafasi ya Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Luanda, Angola mwezi Oktoba 2023.

 

Hatua hiyo imefikiwa wakati wa Mkutano wa 25 wa Kamati hiyo uliofanyika jijini Windhoek, Namibia tarehe 20 na 21 Julai 2023, baada ya Kamati hiyo kupokea na kuridhia ombi la Serikali ya Tanzania la kumuunga mkono Mhe. Dkt. Tulia lililowasilishwa kwao na Kiongozi wa Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano huo ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax.

 

Aidha, wakati wa Mkutano huo, Jamhuri ya Zimbabwe ilitangaza kuwa imemuondoa kwenye kinyang’anyiro hicho mgombea wake ambaye ni Spika wa Bunge la nchi hiyo, Mhe. Jacob Mudenda ili kumuunga mkono mgombea wa Tanzania kuwania nafasi hiyo.

 

Akizungumza mara baada ya hatua hiyo, Mhe. Dkt. Tax ameishukuru Jamhuri ya Zimbabwe na Kanda kwa ujumla kwa kumuunga mkono mgombea wa Tanzania na kueleza kuwa Kanda itawezesha mgombea huyo huyo kushinda nafasi hiyo.

 

Vile vile, Mhe. Dkt. Tax ameieleza Kamati hiyo kwamba Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb) tayari ameungwa mkono na Umoja wa Afrika (AU), Bunge la Afrika (PAP), Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya Afrika Mashariki na Jukwaa la Mabunge ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC PF) katika kugombea nafasi hiyo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa 25 wa Kawaida wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika ambao umefanyika jijini Windhoek, Namibia  tarehe 20 na 21 Julai, 2023. Wengine wanaoishiriki ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Innocent Bashungwa, kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Faraji Mnyepe, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Kaspar Mmuya na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Mohammed Rajab
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Innocent Bashungwa (kushoto) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Mnyepe (katikati), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Kaspar Mmuya (mwenye vifaa vya kusikilizia) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma (kulia)
Mwenyekiti wa  Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika  ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia, Mhe. Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah akifunga Mkutano wa Kamati hiyo uliofanyika jijini Windhoek, Namibia tarehe 20 na 21 Julai 2023
Meza Kuu
Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini, Mhe. Dkt. Naledi Pandor naye ni miongoni mwa Mawaziri walioshiriki Mkutano wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika
Taratibu za kufunga rasmi Mkutano wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika zikiendelea ambapo wimbo wa Taila la Namibia na Wimbo wa SADC ziliimbwa
Hafla ya kufunga mkutano ikiendelea
Mhe. Dkt. Tax  (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Bashungwa (wa tatu kushoto) mara baada ya kushiriki Mkutanoi wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika uliofanyika Windhoek tarehe 20 na 21 Julai 2023. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu wa Ulizni na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Mnyepe (wa tatu kulia), Katibu Mku wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mmuya (wa pili kushoto) na Naibu katibu mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma (kushoto)
Picha ya pamoja

Picha ya pamoja


















 

Thursday, July 20, 2023

DKT. TAX AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA MKUTANO WA 25 WA KAMATI YA MAWAZIRI WA ASASI YA SADC YA SIASA, ULINZI NA USALAMA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 25 wa Kawaida wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (MCO) unaofanyika jijini Windhoek, Namibia tarehe 20 na 21 Julai, 2023.

 

Mkutano huo ambao ulitanguliwa na Mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC uliofanyika kuanzia tarehe 17 hadi 19 Julai 2023, pamoja na mambo mengine umepokea na kujadili agenda mbalimbali zilizowasilishwa ikiwemo Mapitio ya Utekelezaji wa Maamuzi ya Mkutano wa 24 wa MCO na Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC; Hali ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Kanda; na Uimarishaji wa Demokrasia katika Kanda.

 

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia, Mhe. Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah amezipongeza nchi wanachama kwa ushirikiano katika kuendelea kuimarisha amani, usalama na utulivu katika Kanda ambavyo amevitaja kama msingi  wa maendeleo endelevu.

 

Amesema kuwa kwa ujumla hali ya usalama katika kanda inaridhisha na kwamba Jumuiya ya SADC itaendelea na jitihada mbalimbali katika kuhakikisha amani ya kudumu inapatikana katika maeneo yenye changamoto za usalama ikiwemo eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na lile la Kaskazini mwa Jimbo la Cabo Delgado nchini Msumbiji.

 

Ameongeza kusema nchi wanachama zinaendelea kuunga mkono jitihada mbalimbali zinazofanyika katika kutafuta suluhu ya kudumu kwa ya hali ya usalama mashariki mwa Congo ili hatimaye eneo hilo lifikie hali ya utulivu na amani ya kudumu.

 

Akizungumzia hali ya usalama Kaskazini mwa Jimbo la Cabo Delgado la nchini Msumbiji, Mhe. Nandi-Ndaitwah amesema hali kwa kiasi kikubwa ni shwari na vitendo vya ugaidi vimedhibitiwa huku maisha ya wananchi hususan wale waliokimbia makazi yao yakirejea katika hali ya kawaida.

 

Kadhalika ametoa wito kwa nchi wanachama kuendelea na jitihada za pamoja katika kukabiliana na biashara haramu ya usafirishaji binadamu kwa kuimarisha masuala ya sheria, kuwajengea uwezo wataalam  na kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu suala hili.

 

Kadhalika ametoa rai nchi wanachama ambazo hazijasaini au kuridhia Itifaki ya Uhuru wa raia wa Kanda ya SADC kutembea kwenye nchi za Jumuiya hiyo ya mwaka 2005 kufanya hivyo ili kuwawezesha wananchi kunufaika kikamilifu na  agenda ya Mtangamano wa SADC.

 

 “Nazihamasisha nchi ambazo hazijasaini au kuridhia Itifaki ya Uhuru wa Raia katika Kanda Kutembea ya mwaka 2005 kufanya hivyo. Itifaki hii ikianza kutekelezwa itaimarisha utalii miongoni mwetu na kuwawezesha raia kufanya biashara na uwekezaji katika kanda kwa uhuru zaidi, alisisitiza Mhe. Nandi-Ndaitwah.

 

Awali akizungumza, Katibu Mtendaji wa SADC, Bw. Elias Mpedi Magosi amesema kuwa Sekretarieti ya SADC itaendelea kushirikiana na Nchi Wanachama hususan katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo katika kanda zikiwemo za kiusalama, kijamii na kiuchumi ili hatimaye kuwa na Kanda tulivu kwa ajili ya maendeleo endelevu.

 

Pia alimpongeza Mwenyekiti wa Kamati ya Mawaziri anayemaliza muda wake Mhe. Nandi-Ndaitwa kwa kazi nzuri aliyofanya katika kipindi chote na kumkaribisha na kumwahidi ushirikiano Mwenyekiti mpya ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Zambia.

 

Pia alitumia fursa hiyo kumtambulisha kwa Mawaziri Mkurugenzi mpya wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC, Prof. Kula Ishmael Theletsane kutoka Afrika Kusini.

 

Mbali na Mhe. Dkt. Tax, Ujumbe wa Tanzania ulimjumuisha pia Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Innocent Bashungwa, Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi, Lt. Jenerali Salum Othman, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Faraji Mnyepe, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Kaspar Mmuya, Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Mohammed Rajab na Balozi wa Tanzania nchini Namibia, Mhe. Dkt. Modestus Kipilimba.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia, Mhe. Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah akifungua rasmi Mkutano wa Kamati hiyo unaofanyika jijini Windhoek, Namibia tarehe 20 na 21 Julai 2023
 

Mhe. Nandi-Ndaitwah akiwa na wajumbe wa meza kuu wakati wa ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Kawaida wa 25 wa Kamati Mawaziri wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (MCO) unaofanyika jijini Windhoek, Namibia tarehe 20 na 21 Julai 2023
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Kawaida wa 25 wa Kamati Mawaziri wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (MCO) unaofanyika jijini Windhoek, Namibia tarehe 20 na 21 Julai 2023. 
Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, Mhe. Elias Mpedi Magosi akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Kawaida wa 25 wa Kamati Mawaziri wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (MCO) unaofanyika jijini Windhoek, Namibia tarehe 20 na 21 Julai 2023
Mhe. Dkt. Tax akishiriki taratibu za ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Kawaida wa 25 wa Kamati Mawaziri wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (MCO) unaofanyika jijini Windhoek, Namibia tarehe 20 na 21 Julai 2023. Wengine katika picha ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, mhe. Innocent Bashungwa (kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Faraji Mnyepe na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Mohammed Rajab.
Ufunguzi ukiendelea
Mhe. Bashungwa akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Wizara yake, Dkt. Mnyepe. Kulia ni Balozi Fatma
Mkutano ukiendelea
Mkutano ukiendelea
Sehemu ya Sekretarieti ya SADC wakati wa mkutano
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi, Lt. Jenerali Salum Othma akibadilisha mawazo na mmoja wa wajumbe wanaoshiriki Mkutano wa  Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (MCO), unaofanyika nchini Namibia  kuaniza tarehe 20 hadi 21 Julai 2023
Sehemu ya ujumbe wa Tanzania wakifuatilia hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Kawaida wa 25 wa Kamati Mawaziri wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (MCO) unaofanyika jijini Windhoek, Namibia tarehe 20 na 21 Julai 2023
Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania wakati wa Mkutano
Kikundi cha Utamaduni kutoka Windhoek kikitoa burudani kwa Mawaziri wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kawaida wa 25 wa Kamati Mawaziri wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (MCO) unaofanyika jijini Windhoek, Namibia tarehe 20 na 21 Julai 2023
Picha ya pamoaja
Mhe. Dkt. Tax akizungumza  na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (MCO), Mhe. Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Kamati hiyo
Mhe. Dkt. Tax akizungumza  na  Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini, Mhe. Dkt. Naledi Pandor  walipokutana jijini Windhoek Namibia wakati wa Mkutano wa  Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (MCO), unaofanyika nchini Namibia  kuaniza tarehe 20 hadi 21 Julai 2023
Mhe. Dkt. Tax akizungumza  na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) walipokutana jijini Windhoek Namibia wakati wa Mkutano wa  Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (MCO), unaofanyika nchini Namibia  kuaniza tarehe 20 hadi 21 Julai 2023
Mhe. Dkt. Tax akizungumza  na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Innocent Bashungwa, kabla ya kushiriki Mkutano wa  Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (MCO), unaofanyika nchini Namibia  kuaniza tarehe 20 hadi 21 Julai 2023
Mhe. Dkt. Tax akisalimiana  na  Katibu Mtendaji wa SADC, Mhe. Elias Mpedi Magosi walipokutana jijini Windhoek, Namibia wakati wa Mkutano wa  Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (MCO), unaofanyika nchini Namibia  kuaniza tarehe 20 hadi 21 Julai 2023


Dkt. Mnyepe akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Kaspar Mmuya kabla ya kuanza kwa Mkutano wa  Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (MCO), unaofanyika nchini Namibia  kuaniza tarehe 20 hadi 21 Julai 2023
Mhe. Dkt. Tax akipokelewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Mohammed Rajab mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa mikutano kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa  Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (MCO), unaofanyika nchini Namibia  kuaniza tarehe 20 hadi 21 Julai 2023
































 

Wednesday, July 19, 2023

WAZIRI WA MAENDELEO YA KIMATAIFA WA CANADA AWASILI NCHINI

Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada anayeshughulikia Maendeleo ya Kiuchumi ya Pasific, Mhe. Harjit Sajjan amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tano kuanzia tarehe 19 – 23 Julai, 2023. 

Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Mhe. Sajjan alipokelewa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo.

Akiwa nchini, Mhe. Sajjan pamoja na ujumbe wake anatarajia kukutana na viongozi mbalimbali wa Serikali na kujadiliana nao masuala ya ushirikiano kati ya Tanzania na Canada.

Aidha, Waziri Sajjan anatarajia kukutana kwa mazungumzo na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Waziri wa Afya pamoja na kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo inayofadhiliwa na Serikali ya Canada.

Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada anayeshughulikia Maendeleo ya Kiuchumi ya Pasific, Mhe. Harjit Sajjan akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam na kupokelewa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo



Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada anayeshughulikia Maendeleo ya Kiuchumi ya Pasific, Mhe. Harjit Sajjan akisalimiana na viongozi mbalimbali baada ya kuwasilis katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada anayeshughulikia Maendeleo ya Kiuchumi ya Pasific, Mhe. Harjit Sajjan akisalimiana naKatibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada anayeshughulikia Maendeleo ya Kiuchumi ya Pasific, Mhe. Harjit Sajjan akimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada anayeshughulikia Maendeleo ya Kiuchumi ya Pasific, Mhe. Harjit Sajjan akizungumza na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam


Tuesday, July 18, 2023

TANZANIA NA HUNGARY ZAAINISHA MAENEO YA KUSHIRIKIANA





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) Ikulu Jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza mazungumzo na mgeni wake Rais wa Hungary Mheshimiwa Katalin Novák

Rais wa Hungary Mheshimiwa Katalin Novák akizungumza na Waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) Ikulu Jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza mazungumzo na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na mgeni wake Rais wa Hungary, Mheshimiwa Katalin Novák wakizungumza na Waandishi wa Habari Ikulu Jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza mazungumzo yao 

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknoloji Prof. Adolf Mkenda akipongezana na Waziri wa Nchi wa Hungary Azbej Tristan  baada ya kusaini Hati ya Makubaliano (MoU) 




Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) akiteta jambo na Waziri wa Elimu, Prof. Adolf Mkenda pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo Ikulu Jijini Dar es Salaam 

Rais wa Hungary Mheshimiwa Katalin Novák akipokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) kwenye makazi ya Mwakilishi wa Heshima wa Hungary nchini Tanzania, Bw. Solomon Kimaro Jijini Dar es Salaam 

Rais wa Hungary Mheshimiwa Katalin Novák akisalimiana na  Mwakilishi wa Heshima wa Hungary nchini Tanzania, Bw. Solomon Kimaro kwenye makazi yake Jijini Dar es Salaam 

 

Monday, July 17, 2023

RAIS WA HUNGARY AWASILI TANZANIA

Rais wa Hungary Mheshimwa Katalin Novák, amewasili leo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku nne itakayomalizika tarehe 20, Julai 2023.

Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Mheshimiwa, Novák amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) 

Akiwa nchini, tarehe 18 Julai 2023 Mheshimiwa Novák anatarajia kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na kufanya mazungumzo rasmi na baadae viongozi hao kuzungumza na Waandishi wa Habari.

Mheshimiwa Novák ni Rais wa kwanza mwanamke kuongoza Hungary ambapo alichaguliwa mwezi Mei, 2022. Aidha, ni Rais wa kwanza kutoka Hungary kufanya ziara ya kikazi nchini Tanzania.

Ziara hiyo ni matokeo ya jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na Mataifa mbalimbali duniani.

Tanzania na Hungary zimekuwa zikishirikiana katika sekta za biashara, elimu, utalii, kilimo, utangazaji na viwanda.

Viongozi wengine walioambatana na Dkt. Tax kumpokea Rais wa Hungary ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Muliro Jumanne, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani anayeiwakilisha pia Tanzania nchini Hungary, Mhe. Abdallah Possi, Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Swahiba Mndeme pamoja na Viongozi mbalimbali waandamizi wa Serikali.