Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax
ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 25 wa Kawaida wa Kamati ya
Mawaziri wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa
Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (MCO) unaofanyika jijini Windhoek, Namibia
tarehe 20 na 21 Julai, 2023.
Mkutano
huo ambao ulitanguliwa na Mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Asasi
ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC
uliofanyika kuanzia tarehe 17 hadi 19 Julai 2023, pamoja na mambo mengine
umepokea na kujadili agenda mbalimbali zilizowasilishwa ikiwemo Mapitio ya Utekelezaji wa Maamuzi ya Mkutano wa 24 wa MCO na Wakuu wa Nchi
na Serikali wa SADC; Hali ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Kanda; na Uimarishaji wa Demokrasia katika Kanda.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Naibu
Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia, Mhe. Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah
amezipongeza nchi wanachama kwa ushirikiano katika kuendelea kuimarisha amani,
usalama na utulivu katika Kanda ambavyo amevitaja kama msingi wa maendeleo endelevu.
Amesema kuwa kwa ujumla hali ya usalama katika kanda
inaridhisha na kwamba Jumuiya ya SADC itaendelea na jitihada mbalimbali katika
kuhakikisha amani ya kudumu inapatikana katika maeneo yenye changamoto za usalama
ikiwemo eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na lile la
Kaskazini mwa Jimbo la Cabo Delgado nchini Msumbiji.
Ameongeza kusema nchi wanachama zinaendelea kuunga mkono
jitihada mbalimbali zinazofanyika katika kutafuta suluhu ya kudumu kwa ya hali
ya usalama mashariki mwa Congo ili hatimaye eneo hilo lifikie hali ya utulivu
na amani ya kudumu.
Akizungumzia
hali ya usalama Kaskazini mwa Jimbo la Cabo Delgado la nchini Msumbiji, Mhe.
Nandi-Ndaitwah amesema hali kwa kiasi kikubwa ni shwari na vitendo vya ugaidi
vimedhibitiwa huku maisha ya wananchi hususan wale waliokimbia makazi yao
yakirejea katika hali ya kawaida.
Kadhalika
ametoa wito kwa nchi wanachama kuendelea na jitihada za pamoja katika
kukabiliana na biashara haramu ya usafirishaji binadamu kwa kuimarisha masuala
ya sheria, kuwajengea uwezo wataalam na
kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu suala hili.
Kadhalika
ametoa rai nchi wanachama ambazo hazijasaini au kuridhia Itifaki ya Uhuru wa raia
wa Kanda ya SADC kutembea kwenye nchi za Jumuiya hiyo ya mwaka 2005 kufanya
hivyo ili kuwawezesha wananchi kunufaika kikamilifu na agenda ya Mtangamano wa SADC.
“Nazihamasisha nchi ambazo hazijasaini au
kuridhia Itifaki ya Uhuru wa Raia katika Kanda Kutembea ya mwaka 2005 kufanya
hivyo. Itifaki hii ikianza kutekelezwa itaimarisha utalii miongoni mwetu na
kuwawezesha raia kufanya biashara na uwekezaji katika kanda kwa uhuru zaidi,
alisisitiza Mhe. Nandi-Ndaitwah.
Awali akizungumza, Katibu Mtendaji wa SADC, Bw. Elias Mpedi
Magosi amesema kuwa Sekretarieti ya SADC itaendelea kushirikiana na Nchi
Wanachama hususan katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo katika
kanda zikiwemo za kiusalama, kijamii na kiuchumi ili hatimaye kuwa na Kanda
tulivu kwa ajili ya maendeleo endelevu.
Pia alimpongeza Mwenyekiti wa Kamati ya Mawaziri anayemaliza
muda wake Mhe. Nandi-Ndaitwa kwa kazi nzuri aliyofanya katika kipindi chote na
kumkaribisha na kumwahidi ushirikiano Mwenyekiti mpya ambaye ni Waziri wa Mambo
ya Nje wa Zambia.
Pia alitumia fursa hiyo kumtambulisha kwa Mawaziri
Mkurugenzi mpya wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC, Prof. Kula
Ishmael Theletsane kutoka Afrika Kusini.
Mbali na Mhe. Dkt. Tax, Ujumbe wa Tanzania ulimjumuisha pia
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Innocent Bashungwa, Mwakilishi wa Mkuu wa
Majeshi ya Ulinzi na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi, Lt. Jenerali Salum Othman, Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Faraji Mnyepe, Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Kaspar Mmuya, Naibu katibu Mkuu
wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma
Mohammed Rajab na Balozi wa Tanzania nchini Namibia,
Mhe. Dkt. Modestus Kipilimba.
|
Mwenyekiti wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa
Mambo ya Nje wa Namibia, Mhe. Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah akifungua rasmi Mkutano wa Kamati hiyo unaofanyika jijini Windhoek, Namibia tarehe 20 na 21 Julai 2023
| |
|
Mhe. Nandi-Ndaitwah akiwa na wajumbe wa meza kuu wakati wa ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Kawaida wa 25 wa Kamati Mawaziri wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama
wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (MCO) unaofanyika jijini Windhoek, Namibia tarehe 20 na 21 Julai 2023
|
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Kawaida wa 25 wa Kamati Mawaziri wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama
wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (MCO) unaofanyika jijini Windhoek, Namibia tarehe 20 na 21 Julai 2023.
|
|
Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, Mhe. Elias Mpedi Magosi akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Kawaida wa 25 wa Kamati Mawaziri wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama
wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (MCO) unaofanyika jijini Windhoek, Namibia tarehe 20 na 21 Julai 2023 |
|
Mhe. Dkt. Tax akishiriki taratibu za ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Kawaida wa 25 wa Kamati Mawaziri wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama
wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (MCO) unaofanyika jijini Windhoek, Namibia tarehe 20 na 21 Julai 2023. Wengine katika picha ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, mhe. Innocent Bashungwa (kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Faraji Mnyepe na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Mohammed Rajab.
|
|
Ufunguzi ukiendelea
|
|
Mhe. Bashungwa akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Wizara yake, Dkt. Mnyepe. Kulia ni Balozi Fatma
|
|
Mkutano ukiendelea
|
|
Mkutano ukiendelea
|
|
Sehemu ya Sekretarieti ya SADC wakati wa mkutano
|
|
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi, Lt.
Jenerali Salum Othma akibadilisha mawazo na mmoja wa wajumbe wanaoshiriki Mkutano wa Kamati ya
Mawaziri
wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama
wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (MCO), unaofanyika nchini
Namibia kuaniza tarehe 20 hadi 21 Julai 2023 |
|
|
Sehemu
ya ujumbe wa Tanzania wakifuatilia hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa
Kawaida wa 25 wa Kamati Mawaziri wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala
ya Siasa, Ulinzi na Usalama
wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (MCO) unaofanyika jijini
Windhoek, Namibia tarehe 20 na 21 Julai 2023 |
|
Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania wakati wa Mkutano
|
|
Kikundi cha Utamaduni kutoka Windhoek kikitoa burudani kwa Mawaziri wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kawaida wa 25 wa Kamati Mawaziri wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama
wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (MCO) unaofanyika jijini Windhoek, Namibia tarehe 20 na 21 Julai 2023 |
|
Picha ya pamoaja
|
|
Mhe. Dkt. Tax akizungumza na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa
Mambo ya Nje wa Namibia ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mawaziri
wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama
wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (MCO), Mhe. Dkt. Netumbo
Nandi-Ndaitwah kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Kamati hiyo
|
|
Mhe. Dkt. Tax akizungumza na Waziri wa
Mambo ya Nje wa Afrika Kusini, Mhe. Dkt. Naledi Pandor walipokutana jijini Windhoek Namibia wakati wa Mkutano wa Kamati ya Mawaziri
wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama
wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (MCO), unaofanyika nchini Namibia kuaniza tarehe 20 hadi 21 Julai 2023
|
|
Mhe. Dkt. Tax akizungumza na Waziri wa
Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) walipokutana
jijini Windhoek Namibia wakati wa Mkutano wa Kamati ya Mawaziri
wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama
wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (MCO), unaofanyika nchini Namibia kuaniza tarehe 20 hadi 21 Julai 2023 |
|
Mhe. Dkt. Tax akizungumza na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Innocent Bashungwa, kabla ya kushiriki Mkutano wa Kamati ya Mawaziri
wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama
wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (MCO), unaofanyika nchini Namibia kuaniza tarehe 20 hadi 21 Julai 2023 |
|
Mhe. Dkt. Tax akisalimiana na Katibu Mtendaji wa SADC, Mhe. Elias Mpedi Magosi walipokutana
jijini Windhoek, Namibia wakati wa Mkutano wa Kamati ya Mawaziri
wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama
wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (MCO), unaofanyika nchini Namibia kuaniza tarehe 20 hadi 21 Julai 2023 |
|
Dkt. Mnyepe akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Kaspar Mmuya kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Kamati ya Mawaziri
wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama
wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (MCO), unaofanyika nchini Namibia kuaniza tarehe 20 hadi 21 Julai 2023 |
|
Mhe. Dkt. Tax akipokelewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Mohammed Rajab mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa mikutano kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kamati ya
Mawaziri
wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama
wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (MCO), unaofanyika nchini
Namibia kuaniza tarehe 20 hadi 21 Julai 2023 |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.