Mkutano wa 25 wa Kawaida wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (MCO) utafanyika jijini Windhoek, Namibia kuanzia tarehe 17 hadi 21 Julai, 2023
Mkutano huo umetanguliwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu unaofanyika tarehe 17 na 18 Julai 2023 ambapo ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Kamati hii unaongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt Faraji Mnyepe.
Akifungua Mkutano huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Namibia na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC, Balozi Penda Naanda amewakaribisha Wajumbe nchini Namibia na kuwaomba kujadili agenda zilizopo mezani kwa umakini ili hatimaye kuziwasilisha kwa Kamati ya Mawaziri kwa hatua zinazofuata.
Ameongeza kusema kuwa, vikao vya Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC ni muhimu kwani huzikutanisha nchi wanachama kwa ajili ya kujadili na kutathmini hali ya siasa, ulinzi na usalama ya kanda, demokrasia na utawala bora kwa maslahi mapana ya nchi wanachama.
“Nawakaribisha jijini Windhoek na katika kikao chetu hiki ili kwa pamoja tupokee na kujadili taarifa mbalimbali za vikao vilivyotangulia ili kutathimini hatua zilizofikiwa na kutoa mapendekezo yetu ya namna ya kuendeleza mtangamano wa Jumuiya yetu kupitia vikao hivi” alisema Balozi Naanda.
Akichangia hoja wakati wa Mkutano huo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Mohammed Rajab ambaye amemwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Dkt. Samwel Shelukindo amesema ni matarajio ya Tanzania kuwa, vikao hivyo ambavyo hufanyika kila mwaka vitaendelea kutoa mchango chanya katika kukuza na kuimarisha masuala mbalimbali ya Jumuiya ikiwemo demokrasia katika Kanda; hali ya Siasa, ulinzi na usalama; mapambano dhidi ya uhalifu wa kupangwa, rushwa na usafirishaji haramu wa binadamu.
Aidha, ametoa rai kwa Jumuiya ya SADC kuendelea kutilia maanani changamoto ya ongezeko la vitendo vya usafirishaji haramu wa binadamu na wimbi la utekaji nyara Watoto kwa kuwa ni changamoto ambazo kwa kiasi kikubwa zinaathiri vijana ambao ndio nguvu kazi ya Kanda.
“Ni vyema Kanda yetu ikaendelea kujiwekea mikakati madhubuti ya kudhibiti changamoto hizi ikiwemo kutafuta fedha za kuwasafirisha wahamiaji haramu wanapomaliza vifungo vyao, manunuzi ya magari na vifaa kwa ajili ya kufanyia doria za pamoja za udhibiti wa mipaka na utoaji wa mafunzo kwa taasisi husika” alisisitiza Balozi Fatma.
Kuhusu athari zitokanazo na migogoro ya ndani na nje ya Afrika ikiwemo mgogoro wa Urusi na Ukraine ambao umeathiri usalama wa chakula, Balozi Fatma ameziomba nchi wanachama kuchukua hatua mbalimbali za kujitegemea kwa kuhakikisha zinazalisha chakula cha kutosha, kuimarisha mifumo ya ubora wa mazao, kuwa na soko la Kanda la kuuziana mazao na kuuza nje ya nchi kwa ajili ya kuongeza upatikanaji wa fedha za kigeni.
Mkutano wa 25 unalenga pamoja na mambo mengine kupokea na kujadili agenda mbalimbali zikiwemo mapitio ya utekelezaji wa maamuzi ya Mkutano wa 24 wa MCO na Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC; Hali ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya kanda; masuala ya demokrasia; mapambano dhidi ya uhalifu wa kupangwa, rushwa na usafirishaji haramu wa binadamu.
Nchi Wanachama 16 za SADC zimeshiriki Mkutano huo wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC.
Mjumbe wa Angola akishirki Mkutano wa Kamati ya Kudumu ya
Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC, |
Mjumbe wa Botswana akishirki Mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC, |
Mjumbe wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) akishirki Mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC, |
Mjumbe wa Lesotho akishirki Mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC, |
Mjumbe wa Namibia akishirki Mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC, |
Mjumbe wa Afrika Kusini akishirki Mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC, |
Mjumbe wa Zimbabwe akishirki Mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC, |
Wajumbe wa Sekretarieti ya SADC wakishirki Mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC, |
Sehemu ya Washiriki wakati wa Mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC, |
Mkutano ukiendelea |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.