Viongozi kutoka mataifa mbalimbali Barani Afrika wameendelea kuwasili nchini kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu Rasilimali Watu kuanzia tarehe 25 - 26 Julai, 2023.
Viongozi waliowasili alfajiri ya Leo tarehe 25 Julai 2023, ni Makamu wa Rais wa Zambia, Mhe. W.K. Mutale Nalumango, Makamu wa Rais wa Benin, Mhe. Madam Mariam Chabi Talata, Waziri Mkuu wa Eswatini, Mhe. Cleopas Sipho Dlamin, Waziri Mkuu wa Somalia, Mhe. Hamze Abdi Barre.
Wengine ni Waziri wa Elimu wa Misri, Mhe. Reda Hegazy, Waziri wa Fedha wa Djibouti, Mhe. Ilyas Moussa Dawaleh pamoja na Waziri Ofisi ya Rais - Namibia, Mhe. Christine Hoebes.
|
Makamu wa Rais wa Zambia, Mhe. W.K. Mutale Nalumango akisalimiana na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mbarawa baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu Rasilimali Watu kuanzia tarehe 25 - 26 Julai, 2023 |
|
Makamu wa Rais wa Zambia, Mhe. W.K. Mutale Nalumango akizungumza na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mbarawa baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu Rasilimali Watu kuanzia tarehe 25 - 26 Julai, 2023 |
|
Makamu wa Rais wa Benin, Mhe. Madam Mariam Chabi Talata akipokelewa na Waziri wa Maji, Mhe. Juma Aweso baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu Rasilimali Watu kuanzia tarehe 25 - 26 Julai, 2023 |
|
Makamu wa Rais wa Benin, Mhe. Madam Mariam Chabi Talata katika mazungumzo na Waziri wa Maji, Mhe. Juma Aweso baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu Rasilimali Watu kuanzia tarehe 25 - 26 Julai, 2023 |
|
Waziri Mkuu wa Eswatini, Mhe. Cleopas Sipho Dlamin akizungumza na Waziri wa nchi Afisi ya Rais Ikulu - Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Jamal Kassim Ali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu Rasilimali Watu kuanzia tarehe 25 - 26 Julai, 2023 |
|
Waziri Mkuu wa Somalia, Mhe. Hamze Abdi Barre akifurahia jambo wakati wa mazungumzo yake na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega baada ya kuwasili nchini kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu Rasilimali Watu kuanzia tarehe 25 - 26 Julai, 2023 |
|
Waziri wa Elimu wa Misri, Mhe. Reda Hegazy akiwa na Balozi wa Misri nchini, Mhe. Sherif Abdelhamid Ismail baada ya kuwasili kuwasili nchini kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu Rasilimali Watu kuanzia tarehe 25 - 26 Julai, 2023 |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.