Viongozi mbalimbali kutoka Barani Afrika wameendelea kuwasili nchini kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu Rasilimali Watu utakayofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar Es Salaam, tarehe 25 - 27 Julai 2023.
Leo tarehe 24 Julai 2023, kwa nyakati tofauti viongozi mbalimbali wamewasili nchini kushiriki Mkutano huo. Viongozi waliowasili leo ni mke wa Rais wa zamani wa Msumbiji, Mama Graca Machel, Balozi wa Ivory Coast nchini Afrika Kusini, Mhe. Sakaria Kone.
Wengine ni Waziri wa Fedha wa Kenya, Mhe. Prof. Njuguna Ndug’u, Waziri wa Elimu wa Afrika Kusini, Mhe. Dr. Bonginkosi Nzimande pamoja na Waziri wa Elimu wa Togo, Mhe. Prof. Dodzi Komla Kokoroko.
Mbali ya Wakuu wa Nchi na Serikali, mkutano huo utawahusisha Mawaziri wa Fedha, Mawaziri wa Sekta nyingine zinazohusika na maendeleo ya Rasilimaliwatu, Watendaji Wakuu wa Benki ya Dunia na watu mashuhuri.
|
Mke wa Rais wa zamani wa Msumbiji, Mama Graca Machel akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Mama Machel yupo nchini kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu Rasilimali Watu utakayofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar Es Salaam, tarehe 25 - 27 Julai 2023. |
|
Mke wa Rais wa zamani wa Msumbiji, Mama Graca Machel akizunguza na Waziri wa Nchi Utawala na Utumishi wa Umma - Msumbiji, Mhe. Ana Comoane baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam |
|
Balozi wa Ivory Coast nchini Afrika Kusini, Mhe. Sakaria Kone akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu Rasilimali Watu tarehe 25 - 27 Julai 2023 |
|
Balozi wa Ivory Coast nchini Afrika Kusini, Mhe. Sakaria Kone akizungumza na mmoja kati ya wajumbe alioambatana na kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu Rasilimali Watu tarehe 25 - 27 Julai 2023 |
|
Waziri wa Elimu wa Togo, Mhe. Prof. Dodzi Komla Kokoroko akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu Rasilimali Watu tarehe 25 - 27 Julai 2023 |
|
Waziri wa Elimu wa Togo, Mhe. Prof. Dodzi Komla Kokoroko pamoja na ujumbe wake wakiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Viongozi hao wapo nchini kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu Rasilimali Watu tarehe 25 - 27 Julai 2023 |
|
Waziri wa Elimu wa Afrika Kusini, Mhe. Dr. Bonginkosi Nzimande akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu Rasilimali Watu tarehe 25 - 27 Julai 2023 |
|
Waziri wa Elimu wa Afrika Kusini, Mhe. Dr. Bonginkosi Nzimande akizungmza na Balozi wa Afrika Kusini nchini, Mhe. Noluthando Mayende-Malepe katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam |
|
Waziri wa Fedha wa Kenya, Mhe. Prof. Njuguna Ndug’u (kushoto) akizungumza na mmoja kati ya wajumbe wake katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.