|
Mtendaji
Mkuu wa
Makumbusho ya Taifa ya Oman Mheshimiwa Jamal al-Moosawi (kushoto)
akisikiliza maelezo kutoka kwa mtalamu wa Makumbusho alipotembelea Makumbusho ya Taifa Dar es Salaam |
|
Mtendaji
Mkuu wa
Makumbusho ya Taifa ya Oman Mheshimiwa Jamal al-Moosawi (kushoto)
akiangalia kitabu kilichowekwa mezani na mtaalamu wa Makumbusho alipotembelea Makumbusho ya Taifa Dar es Salaam |
|
Mtendaji
Mkuu wa
Makumbusho ya Taifa ya Oman Mheshimiwa Jamal al-Moosawi (aliyeshika koti)
akizungumza kitu alipotembelea Makumbusho ya Taifa Dar es Salaam |
|
Mtendaji
Mkuu wa
Makumbusho ya Taifa ya Oman Mheshimiwa Jamal al-Moosawi (mwenye tai)
akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt. Noel Luoga
alipotembelea Makumbusho ya Taifa Dar es Salaam |
|
Mtendaji
Mkuu wa
Makumbusho ya Taifa ya Oman Mheshimiwa Jamal al-Moosawi (kushoto)
akisikiliza maelezo kutoka kwa mtalamu wa Makumbusho alipotembelea Makumbusho ya Taifa Dar es Salaam |
Ujumbe wa watu sita kutoka Makumbusho ya
Taifa ya Oman umetembelea Makumbusho ya Taifa Dar es Salam kwa ajili ya
kujifunza na kujionea historia ya Tanzania.
Ujumbe huo unaongozwa na Mtendaji Mkuu wa
Makumbusho ya Taifa ya Oman Mheshimiwa Jamal al-Moosawi. Pamoja na mambo mengine, ujumbe huo
unatarajia pia kutembelea Kijiji cha Makumbusho
Kijitonyama, Jumba la Atiman na Jengo la Boma la zamani yaliyoko katika
Mtaa wa Sokoine ambapo majengo hayo yaliyojengwa na kukaliwa na Sultan wa
Zanzibar miaka ya 1860’s.
Ujumbe huo kutoka Makumbusho ya Taifa ya
Oman unatarajia kutembelea visiwa vya Zanzibar ambapo watakutana na kuzungumza
na uongozi wa watendaji wa Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale iliyochini ya
Wizara ya Utalii na Urithi Zanzibar.
Ukiwa Zanzibar Ujumbe huo utatembelea Mji
Mkongwe, Makumbusho ya amani na historia ya Mnazi Mmoja, Jumba la Kibweni na
Magofu ya Mtoni. Ujumbe huo pia utatembelea Pango la Kuumbi la Jambiani,
Makumbusho ya Unguja Kuu na Mji Mkongwe
kwa ajili ya kujifunza na kujionea historia iliyosheheni ya Zanzibar.
Ujumbe huo kutoka nchini Oman uliwasili
nchini tarehe 05 Oktoba, 2023 ambapo pamoja na mambo mengine, una shiriki
Mkutano wa Kwanza wa Pamoja wa Wataalamu kati ya Tanzania na Oman unaofanyika
jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo unalenga kuendeleza uhusiano
kati ya Tanzania na Oman kupitia Makumbusho ya Taifa ya Tanzania na Makumbusho
ya Taifa ya Oman.
Mkutano huo wa Kwanza wa Pamoja wa
Wataalamu kati ya Makumbusho ya Taifa ya Tanzania na Makumbusho ya Taifa ya
Oman ni moja ya mbinu na nyenzo za kuimarisha Uhusiano kati ya Tanzania na
Oman.
Kufanyika kwa Mkutano huo ni utekelezaji wa
makubaliano yaliyosainiwa kati ya Wizara ya Maliasili na Utalii na Makumbusho
ya Taifa ya Oman mwezi Juni ,2022.
Ujumbe huo unatarajiwa kuondoka nchini
tarehe 12 Oktoba 2023 kupitia Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani
Karume Zanzibar.