Serikali
za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zitaendelea kuthamini
mchango unaotolewa na sekta isiyo rasmi katika kukuza maendeleo ya nchi hizo ikiwemo ajira.
Kauli
hiyo imetolewa na Mwakilishi wa Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Brigedia
Jenerali Salum Mnumbe wakati akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Tanzania
maarufu kama Tanzania Day
yaliyofanyika jijini Bujumbura, Burundi ikiwa ni sehemu ya shughuli za Maonesho
ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
yanayoendelea jijini hapa.
Amesema
kuwa Nchi Wanachama wa Afrika Mashariki zilianzisha Maonesho hayo kwa kutambua
na kuthamini mchango unaotolewa na sekta isiyo rasmi katika maendeleo ya nchi
hizo ikiwemo kuzalisha fursa za ajira kwa wingi na kuzalisha bidhaa
zinazotumiwa zaidi na wananchi.
“Lengo
la kuanzisha maonesho hayo lilikuwa ni kuwapatia fursa wajasiriamali wa sekta
hii ili waweze kushiriki katika uzalishaji na kuwawezesha kukua na kuingia
kwenye sekta rasmi” amesema Brig. Jen. Mnumbe.
Pia
amewahamasisha Wajasiriamali hao kushirikiana na Sekretarieti ya Jumuiya ya
Afrika Mashariki kuongeza bidii katika kuzalisha bidhaa bora kwa viwango vya
kimataifa na kuzitangaza bidhaa hizo ndani na nje ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki ili kuongeza wigo wa soko.
Pia
amewataka kuendelea kushirikiana, kubadilishana mawazo na ujuzi katika uzalishaji
wa bidhaa na utengenezaji wa vifungashio na kuthaminisha.
Kadhalika
ametumia fursa hiyo kuwapongeza na kuwashukuru wajasiriamali kutoka Tanzania wanaoshiriki
maonesho hayo kwa kuandaa bidhaa zenye ubunifu, ubora wa hali ya juu na zenye
asili ya kitanzania.
Maadhimisho
ya Tanzania Day yaliambatana na shughuli mbalimbali zilizofanywa na
wajasiriamali wa Tanzania kwa kuonesha utamaduni wa Tanzania pamoja na bidhaa
mbalimbali zinazozalishwa nchini. Miongoni mwa shuguli zilizofanywa ni pamoja
na maonesho ya mavazi ya asili, ngoma za asili na muziki.
Maonesho ya 23 ambayo
yamewashirikisha wajasiriamali 1,500 kutoka nchi zote wanachama wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki, wakiwemo 259 kutoka Tanzania yanafanyika kwa mara ya tatu
nchini Burundi tangu kuanzishwa kwake mwaka 1999.
|
Mgeni Rasmi na Mwakilishi wa Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Brigedia Jenerali Salum Mnumbe akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Tanzania iliyofanyika jijini Bujumbura, Burundi ikiwa ni sehemu ya Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea jijini hapa kuanzia tarehe 05 hadi 15 Desemba 2023
|
|
Mgeni Rasmi na Mwakilishi wa Balozi wa Tanzania nchini Burundi,
Brigedia Jenerali Salum Mnumbe (kushoto) akiwa jukwaa kuu na wageni wengine waalikwa walioshiriki maadhimisho ya Siku ya
Tanzania iliyofanyika jijini Bujumbura, Burundi ikiwa ni sehemu ya
Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati kutoka Nchi Wanachama
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea jijini hapa kuanzia tarehe
05 hadi 15 Desemba 2023. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Bernard Haule na katikati ni Naibu
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Fedha na
Biashara, Bi. Annette Mutaawe. |
|
Mgeni Rasmi, Brigedia Jenerali Mnumbe akiwa jukwaa kuu na wageni waalikwa
|
|
Naibu
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Fedha na
Biashara, Bi. Annette Mutaawe akitoa salamu za Sekretarieti ya Jumuiya hiyo wakati wa maadhimisho ya Siku ya
Tanzania iliyofanyika jijini Bujumbura, Burundi |
Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati Afrika Mashariki, Bw. Josephat Rweyemamu naye akizungumza
|
Brigedia Jenerali Mnumbe akipokea zawadi ya kitabu kutoka kwa Naibu
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Fedha na
Biashara, Bi. Annette Mutaawe alipotembelea banda la Sekretariei ya Jumuiya hiyo
|
|
Mgeni Rasmi na Mwakilishi wa Balozi wa Tanzania nchini Burundi,
Brigedia Jenerali Salum Mnumbe akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika banda la Tanzania kabla ya kuanza kwa sherehe za maadhimisho ya Siku ya
Tanzania iliyofanyika jijini Bujumbura, Burundi ikiwa ni sehemu ya
Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati kutoka Nchi Wanachama
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea jijini hapa kuanzia tarehe
05 hadi 15 Desemba 2023 |
|
Mgeni
Rasmi na Mwakilishi wa Balozi wa Tanzania nchini Burundi,
Brigedia Jenerali Salum Mnumbe akipata maelezo kutoka kwa Mjasiriamali wa Tanzania alipotembelea mabanda ya wajasiriamali hao wakati wa maadhimisho ya Siku ya
Tanzania iliyofanyika jijini Bujumbura, Burundi ikiwa ni sehemu ya
Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati kutoka Nchi Wanachama
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea jijini hapa kuanzia tarehe
05 hadi 15 Desemba 2023 |
Mgeni
Rasmi na Mwakilishi wa Balozi wa Tanzania nchini Burundi,
Brigedia Jenerali Salum Mnumbe akipata maelezo kutoka kwa Mjasiriamali
wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo alipotembelea mabanda ya wajasiriamali kutoka nchi za EAC wakati wa
maadhimisho ya Siku ya
Tanzania iliyofanyika jijini Bujumbura, Burundi ikiwa ni sehemu ya
Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati kutoka Nchi Wanachama
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea jijini hapa kuanzia tarehe
05 hadi 15 Desemba 2023 |
Watanzania wakiwa na furaha wakati wa wa
maadhimisho ya Siku ya
Tanzania iliyofanyika jijini Bujumbura, Burundi ikiwa ni sehemu ya
Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati kutoka Nchi Wanachama
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea jijini hapa kuanzia tarehe
05 hadi 15 Desemba 2023 |
|
Sehemu nyingine ya Watanzania |
|
|
|
Wajasiriamali kutoka Tanzania wanaoshiriki Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati kutoka Nchi Wanachama
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea jijini Bujumbura wakionesha ubunifu wa mavazi mbalimbali wanayotengeza ikiwa ni shamrashara za kuadhimisha siku ya Tanzania |
|
Mkurugenzi wa Ajira na Ukuzaji Ujuzi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Ally Msaki (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Watanzania walioshiriki maadhimisho ya Siku ya
Tanzania iliyofanyika jijini Bujumbura, Burundi ikiwa ni sehemu ya
Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati kutoka Nchi Wanachama
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea jijini hapa kuanzia tarehe
05 hadi 15 Desemba 2023 |
|
Picha ya pamoja
|