Saturday, March 9, 2024

WAZIRI GWAJIMA ATOA WITO KWA DIASPORA KUSAIDIA WENYE MAHITAJI


Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wnawake na makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ametoa wito kwa wadau mbalimbali ndani na nje ya nchi wakiwemo Diaspora kujitoa katika kusaidia makundi maalum ya watanzania wakiwemo wazaee, walemavu ili kuleta ustawi wa Jamii.



Mhe Dkt. Gwajima ametoa wito huo alipotembelea banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwenye maonesho ya wiki ya wanawake yanayofanyika katika viwanja vya mashujaa jijini Dodoma.



Amesema akiwa Waziri mwenye dhamana na ustawi wa jamii amekuwa akikutana na changamoto mbalimbali zinazowakabili watanzania hususan makundi maalum ambao ni wazee, walemavu, wajane na yatima ambao wengi wao wanahitaji chakula, mavazi, malazi na matibabu na kutoa wito kwa watanzania waliopo ndani na nje ya nchi kujitolea kusaidia makundi hayo.

 

Ameongeza kusema ana imani wapo Diaspora wenye nia ya kusaidia watanzania wenzao wasiojiweza lakini hawajui namna ya kufikisha msaada huo. Hivyo wizara yake itaangalia namna ya kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ili kujadili mikakati ya kufanikisha suala  hilo.



"Mungu ametujalia baadhi yetu kuwa na mahitaji muhimu ya binadamu  kama chakula, mavazi na menggine na ziada. Hivyo ni vizuri kuwakumbuka wenzetu ambao Mungu kawajalia uhai lakini wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za kushindwa kujitafutia mahitaji hayo muhimu ya kila siku, naomba tujitoe kuwasaidia"  alisema Dkt. Gwajima.

 

Mhe. Dkt Gwajima ametembelea banda hilo ikiwa ni mwendelezo wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake ambapo mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na Wizara yake wameandaa maonesho ya Wiki ya wanawake yanayofanyika katika viwanja vya mashujaa jijini Dodoma kuanzia tarehe 07 hadi 11 Machi 2024.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza mara baada ya kutembelea banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwenye maonesho ya wiki ya wanawake yanayoendelea katika viwanja vya mashujaa jijini Dodoma kuanzia tarehe 07 hadi 11 Machi 2024. Maonesho hayo ni mwendelezo wa siku ya wanawake duniani
Meneja Mawasiliano kutoka Taasisi ya Mpango wa Hiari wa Afrika wa kujitathmini kwa Vigezo vya Utawala Bora (APRM) akimweleza  Mhe. Gwajima kuhusu utendaji wa taasisi hiyo ambayomipo chini ya Wizara.
Mhe. Dkt. Gwajima akimsikiliza Afisa Mambo ya Nje, Bi. Elizabeth Bukwimba akimweleza kuhusu majukumu  ya Wizara.
Bi. Elizabeth akimpatia zawadi ya jarida linaloeleza utekelezaji wa diplomasia ya uchumi katika Balozi za Tanzania nje 
Afisa Mambo ya Nje, Bi. Blandina Kasagama akimweleza mteja majukumu mbalimbali yanayotekeelzwa na Wizara ikiwemo jukumu la kutibitisha vyeti mbalimbali.












 

Friday, March 8, 2024

WANAWAKE WA WIZARA YA MAMBO YA NJE WALIVYOADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Watumishi Wanawake wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wameungana na wanawake wengine duniani kote kuadhimisha siku ya wanawake leo Machi 8, 2024.

 

Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yamefanyika kitaifa jijini Dodoma katika Wilaya ya Chamwino ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa ambaye aliwakilishwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima.

 

Pamoja na mambo mengine, uzinduzi wa Sera wa Taifa ya Maendeleo ya Wanawake umefanyika wakati wa maadhimisho hayo yenye kaulimbiu isemayo “Wekeza kwa Wanawake kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii”.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima (wa pili kulia) akiwasalimia Watumishi Wanawake wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (hawapo pichani) walipopita mbele ya jukwaa kuu wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika Wilayani Chamwino jijini Dodoma tarehe 08 Machi 2024. Kulia kwa Mhe. Dkt. Gwajima ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule
Sehemu ya Watumishi Wanawake wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki waliopo Dodoma wakipita kwa furaha mbele ya jukwaa kuu wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani
Shamrashamra zikiendelea
Sehemu nyingine ta watumishi wanawake wa Wizara wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa maadhimisho hayo
Picha ya pamoja

Watumishi hao wakiwa na bango lenye kaulimbiu ya maadhimisho hayo

Shamrashara za maadhimisho ya siku ya waawake zikiendelea

Sehemu ya watumishi wanawake wa Wizara wakati wa maadhimisho hayo


Sehemu ya watumishi wanawake wa Wizara wakati wa maadhimisho hayo

Watumishi kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara za Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC), Mpango wa Hiari wa Afrika wa kujipima kwa Vigezo vya Utawala Bora (APRM) na Kituo cha Usiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika jijini Dodoma

...Maadhimisho katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam


Sehemu ya Watumishi Wanawake wa Wizara waliopo Ofisi Ndogo za Wizara zilizopo jijini Dar es Salaam nao hawakubaki nyuma kushiriki maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kama wanavyoonekana pichani.

Watumishi hao wakiwa katika picha ya pamoja



 

Wednesday, March 6, 2024

WIZARA YA MAMBO YA NJE KUSHIRIKI MAONESHO MAALUM KUELEKEA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inashiriki maonesho maalum ya wanawake yanayofanyika kimkoa katika viwanja vya Mashujaa jijini Dodoma kuanzia tarehe 07 hadi 11 Machi 2024 ikiwa ni maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani itakayofanyika duniani kote tarehe 08 Machi 2024.


Maonesho hayo ambayo yanaratibiwa na  Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma yatafunguliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Rosemary Senyamule tarehe 07 Machi 2024.


Huduma zitakazotolewa katika Banda la Wizara wakati wa maonesho hayo ni pamoja na uthibitishaji wa nyaraka mbalimbali ikiwemo vyeti vya taaluma, ndoa na nyaraka nyingine, zoezi ambalo litaanza rasmi tarehe 07 hadi 11 Machi, 2024.


Taarifa nyingine  ni kuhusu utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje na  mchango wa wanawake kwenye medani za kimataifa na diplomasia.

Kadhalika maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na Taasisi zilizo chini ya Wizara ambazo ni Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim zamani Chuo cha Diplomasia; Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC) na Mpango wa Hiari wa Kujipima kwa Vigezo vya Utawala Bora (APRM) yatatolewa.


Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwa mwaka 2024 yamebeba kaulimbiu isemayo "Wekeza kwa Wanawake kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii". 

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Kawina Kawina akimsikiliza Afisa Mambo ya Nje, Bi. Elizabeth Bukwimba akimweleza kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya ushiriki wa Wizara kwenye maonesho maalum yatakayofanyika katika Viwanja vya Mashujaa jijini Dodoma kuanzia tarehe 07  hadi 11 Machi 2024 ikiwa ni maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani itakayoadhimishwa duniani kote tarehe 08 Machi 2024. Bw. Kawina ametembelea banda hilo tarehe 06 Machi 2024 kukagua hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya ushiriki wa Wizara
Bw. Kawina akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Wizara kukagua maandalizi  ya ushiriki wa Wizara katika maonesho maalum kuelekea siku ya wanawake duniani yanayofanyika  katika viwanja vya mashujaa jijini Dodoma kuanzia tarehe 07 hadi 11 Machi 2024. Wanaoshuhudia ni Watumishi kutoka Taasisi za Wizara akiwemo Badriya Masoud (kulia), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa APRM, Bi. Praxeda Gaspar kutoka APRM na Bi. Susan Masawe kutoka Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim


Bw. Kawina akikagua vipeperushi vitakavyogawiwa kwa wananchi watakaotembelea banda la Wizara wakati wa maonesho maalum kuelekea siku ya wanawake duniani yanayofanyika jijini Dodoma katika viwanja vya mashujaa kuanzia tarehe 07 hadi 11 machi 2024

Afisa kutoka Taasisi ya Wizara ya Mpango wa Hiari wa Kujipima kwa Vigezo vya Utawala Bora (APRM), Bi. Praxeda Gaspar akimpatia Bw. Kawina kipeperushi kuhusu Taasisi hiyo

Bw. Kawina akipata maelezo kutoka kwa Bi. Janeth Benedict kutoka  Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC)  kuhusu vipeperushi watakavyosambaza kwa wananchi kuhusu taasisi hiyo

Mwonekano wa Banda la Wizara



 

BALOZI MUSSA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA KIKAO CHA KAMATI YA FEDHA CHA SADC

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa ameendelea kuongoza Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kikao cha Kamati ya Fedha ya Jumuiya ya Maendeleo Kusaini mwa Afrika (SADC) kinachofanyika Jijini Luanda, Angola tarehe 6 Machi, 2024.


Pamoja na masuala mengine, kikao hicho kimepokea na kujadili taarifa ya Kamati Ndogo ya Fedha ya SADC na Kamati ya Ukaguzi ambapo ajenda mbalimbali zimejadiliwa ikiwemo mpango wa bajeti ya kanda kwa kipindi cha 2024/2025 na mapendekezo yake yatawasilishwa katika Baraza la Mawaziri kwa ajili ya kuidhinishwa tarehe 10 na 11 Machi, 2024.

Kutoka kulia ni Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Rished Bade, Afisa kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Joseph Haule na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Noah Mboma wakifuatilia majadiliano katika Kikao cha Kamati ya Fedha cha SADC kinachoendelea jijini Luanda, Angola tarehe 6 Machi, 2024.

Sehemu nyingine ya ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikifuatilia majadiliano ya Kikao cha Kamati ya Fedha kinachoendelea jijini Luanda, Angola tarehe 6 Machi, 2024.

Balozi Mussa akiteta jambo na sehemu ya wajumbe wa kikao hicho kutoka Tanzania na Afrika Kusini.




 

Monday, March 4, 2024

TANZANIA, MOROCCO KUIMARISHA USHIRIKIANO SEKTA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI

Tanzania na Morocco zimeahidi kuendelea kuimarisha ushirikiano katika sekta za biashara na uwekezaji kwa maslahi mapana ya pande zote mbili.

Ahadi hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) alipokutana kwa mazungumzo na Balozi wa Morocco nchini, Mhe. Zakaria El Guomiri katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Waziri Makamba amesema kuwa Tanzania na Morocco zimekuwa na uhusiano wa kidiplomasia wa imara na wa muda mrefu, hivyo ni vyema kwa mataifa hayo kujikita zaidi kuimarisha ushirikiano katika sekta za biashara na uwekezaji ili kukuza uchumi wa pande zote mbili.

Naye Balozi wa Morocco nchini, Mhe. Zakaria El Koumiri amesema kuwa Morocco itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuimarisha sekta ya biashara na uwekezaji kwa manufaa ya pande zote mbili.

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba akimkaribisha Balozi wa Morocco nchini, Mhe. Zakaria El Guomiri katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba akizungumza na Balozi wa Morocco nchini, Mhe. Zakaria El Guomiri katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Kikao cha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba na Balozi wa Morocco nchini, Mhe. Zakaria El Guomiri  kikiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba katika picha ya pamoja na ujumbe wa Morocco ukiongozwa na Balozi wa Morocco nchini, Mhe. Zakaria El Guomiri katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam