Tanzania na Morocco zimeahidi kuendelea kuimarisha ushirikiano katika sekta za biashara na uwekezaji kwa maslahi mapana ya pande zote mbili.
Ahadi hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) alipokutana kwa mazungumzo na Balozi wa Morocco nchini, Mhe. Zakaria El Guomiri katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Waziri Makamba amesema kuwa Tanzania na Morocco zimekuwa na uhusiano wa kidiplomasia wa imara na wa muda mrefu, hivyo ni vyema kwa mataifa hayo kujikita zaidi kuimarisha ushirikiano katika sekta za biashara na uwekezaji ili kukuza uchumi wa pande zote mbili.
Naye Balozi wa Morocco nchini, Mhe. Zakaria El Koumiri amesema kuwa Morocco itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuimarisha sekta ya biashara na uwekezaji kwa manufaa ya pande zote mbili.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba akimkaribisha Balozi wa Morocco nchini, Mhe. Zakaria El Guomiri katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba akizungumza na Balozi wa Morocco nchini, Mhe. Zakaria El Guomiri katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.