Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Said Shaibu Mussa ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Kikao cha Kamati ya
Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)
kinachofanyika jijini Luanda, Angola tarehe 4 – 5 Machi, 2024.
Kikao
hicho kitafuatiwa na kikao cha Kamati ya Fedha tarehe 6 Machi, 2024 ambapo kwa
pamoja vikao hivyo ni maandalizi ya Baraza la Mawaziri litakalofanyika tarehe
10 - 11 Machi, 2024 jijini Luanda, Angola.
Aidha,
pamoja na mambo mengine vikao hivi vya awali vitapokea na kujadili taarifa
zifuatazo: Tathmini ya utekelezaji wa maamuzi ya Mikutano iliyopita, Hatua
iliyofikiwa katika kugharamia utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Maendeleo wa
SADC wa 2020–2030, Taarifa ya Kamati ya
Fedha, Taarifa ya Kamati ya Rasilimali Watu na Utawala, Hatua iliyofikiwa
katika kutafsiri nyaraka muhimu za SADC kwa lugha ya Kiswahili na nyinginezo.
Kauli mbiu ya Baraza la Mawaziri la mwaka huu ni ‘’Rasilimali Watu na Fedha: Nyenzo muhimu kwa ukuaji Endelevu wa Viwanda katika Kanda ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)”.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.