Naibu Waziri Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu kinachoelezea maisha na tamaduni za kabila la wachaga kilichoandikwa kwa lugha ya Kiswahili |
Naibu Waziri Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul akiweka shada la maua katika kaburi la Mangi Meli aliyeuawa na wakoloni wa kijerumani wakati wa utawala wao |
wananchi wa kabila la Kichaga wakicheza ngoma za asili wakati wa hafla ya uzinduzi wa kitabu kinachoelezea maisha na tamaduni za kabila la wachaga kilichoandikwa kwa lugha ya Kiswahili |
Naibu Waziri Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul ameshiriki uzinduzi wa kitabu kinachoelezea maisha na tamaduni za kabila la kichaga kilichoandikwa kwa lugha ya Kiswahili.
Wakati wa uzinduzi ambao umefanyika katika kigango cha Kidia, Old Moshi, imeelezwa kuwa kitabu hicho ambacho kimetafsiri kazi ya mwandishi mchungaji Bruno Gutmann, kinalenga kutambua utumishi wa mchungaji huyo raia wa Ujerumani ambaye aliishi eneo hilo kwa miaka 28 na kushirikiana na wananchi wa maeneo hayo huku akieneza injili.
Kitabu hicho ni miongoni mwa vitabu 400 vilivyoandikwa kwa lugha ya Kijerumani na mchungaji huyo ambapo mpaka sasa vitabu vitano vimeandikwa kwa lugha nyingine ikiwemo kichaga na kiswahili.
Uzinduzi huo pia umeshuhudiwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Kısare Makore, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Mhe. Hassan Mwamweta na Mkurugenzi wa Utamaduni kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Resani Mnata.
Naibu Waziri Keul yuko nchini kwa ziara ya siku nne ya kikazi kuanzia tarehe 29 Februari hadi Machi 4 2024.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.