Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo anaongoza ujumbe wa Tanzania
katika Mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu wa Utatu wa Asasi mbili za Jumuiya ya
Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika Lusaka, Zambia Machi 22, 2024.
Mkutano huo ni maandalizi ya Mikutano ya ngazi ya Mawaziri
na Wakuu wa Nchi na Serikali itakayofanyika tarehe 22 na 23 Machi 2024
mutawalia.
Wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo, Mwenyekiti ambaye
ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya Zambia,
Bi. Etambuyu Anamela Gundersen alisema mwitikio mkubwa wa wajumbe kushiriki
mkutano huo ni ishara ya wazi kuwa nchi wanachama zimedhamiria kumaliza
changamoto za kiuslama katika kanda ya SADC, hususan Mashariki mwa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo na Jimbo la Cabo Delgado nchini Msumbiji.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashsriki, Mhe. January Makamba (Mb) na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga
Taifa, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) watashiriki Mkutano wa ngazi ya Mawaziri ambao
umepangwa kufanyika mchana na utakamilisha agenda zitakazojadiliwa katika
Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Philip Isdor Mpango atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
katika Mkutano huo.
Wajumbe wa Mkutano wakifuatilia hotuba ya ufunguzi ya Mkutano wa Makatibu Wakuu wa Utatu wa Asasi mbili za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika unaofanyika Lusaka, Zambia |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.