Saturday, March 9, 2024

WAZIRI GWAJIMA ATOA WITO KWA DIASPORA KUSAIDIA WENYE MAHITAJI


Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wnawake na makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ametoa wito kwa wadau mbalimbali ndani na nje ya nchi wakiwemo Diaspora kujitoa katika kusaidia makundi maalum ya watanzania wakiwemo wazaee, walemavu ili kuleta ustawi wa Jamii.



Mhe Dkt. Gwajima ametoa wito huo alipotembelea banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwenye maonesho ya wiki ya wanawake yanayofanyika katika viwanja vya mashujaa jijini Dodoma.



Amesema akiwa Waziri mwenye dhamana na ustawi wa jamii amekuwa akikutana na changamoto mbalimbali zinazowakabili watanzania hususan makundi maalum ambao ni wazee, walemavu, wajane na yatima ambao wengi wao wanahitaji chakula, mavazi, malazi na matibabu na kutoa wito kwa watanzania waliopo ndani na nje ya nchi kujitolea kusaidia makundi hayo.

 

Ameongeza kusema ana imani wapo Diaspora wenye nia ya kusaidia watanzania wenzao wasiojiweza lakini hawajui namna ya kufikisha msaada huo. Hivyo wizara yake itaangalia namna ya kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ili kujadili mikakati ya kufanikisha suala  hilo.



"Mungu ametujalia baadhi yetu kuwa na mahitaji muhimu ya binadamu  kama chakula, mavazi na menggine na ziada. Hivyo ni vizuri kuwakumbuka wenzetu ambao Mungu kawajalia uhai lakini wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za kushindwa kujitafutia mahitaji hayo muhimu ya kila siku, naomba tujitoe kuwasaidia"  alisema Dkt. Gwajima.

 

Mhe. Dkt Gwajima ametembelea banda hilo ikiwa ni mwendelezo wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake ambapo mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na Wizara yake wameandaa maonesho ya Wiki ya wanawake yanayofanyika katika viwanja vya mashujaa jijini Dodoma kuanzia tarehe 07 hadi 11 Machi 2024.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza mara baada ya kutembelea banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwenye maonesho ya wiki ya wanawake yanayoendelea katika viwanja vya mashujaa jijini Dodoma kuanzia tarehe 07 hadi 11 Machi 2024. Maonesho hayo ni mwendelezo wa siku ya wanawake duniani
Meneja Mawasiliano kutoka Taasisi ya Mpango wa Hiari wa Afrika wa kujitathmini kwa Vigezo vya Utawala Bora (APRM) akimweleza  Mhe. Gwajima kuhusu utendaji wa taasisi hiyo ambayomipo chini ya Wizara.
Mhe. Dkt. Gwajima akimsikiliza Afisa Mambo ya Nje, Bi. Elizabeth Bukwimba akimweleza kuhusu majukumu  ya Wizara.
Bi. Elizabeth akimpatia zawadi ya jarida linaloeleza utekelezaji wa diplomasia ya uchumi katika Balozi za Tanzania nje 
Afisa Mambo ya Nje, Bi. Blandina Kasagama akimweleza mteja majukumu mbalimbali yanayotekeelzwa na Wizara ikiwemo jukumu la kutibitisha vyeti mbalimbali.












 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.