|
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul (aliyebeba begi mngongoni) akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mhe. Kisare Makore alipowasili katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA)
tarehe 29 Februari, 2024. Mhe. Keul yuko nchini kwa ziara ya kikazi ya
Siku Nne.
|
|
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul (aliyebeba begi mngongoni) akisalimiana na Balozi wa Tanzania
nchini Ujerumani Mhe. Hassan Mwamweta alipowasili katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA)
tarehe 29 Februari, 2024. |
|
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul (aliyebeba begi mngongoni) akisalimiana na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya America na Ulaya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Naomi Zegezege alipowasili katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA)
tarehe 29 Februari, 2024. |
|
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Mkuu wa
Wilaya ya Moshi Mhe. Kisare Makore (kuli) akizungumza na Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul alipowasili katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA) tarehe 29 Februari, 2024. |
|
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul akizungumza na Katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro Bw. Tixon Nzunda (wa pili) kulia na Balozi wa Tanzania
nchini Ujerumani Mhe. Hassan Mwamweta ( wa pili kushoto) alipowasili katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA)
tarehe 29 Februari, 2024 |
|
Mazungumzo yakiendelea katika chumba cha kupumzikia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)
|
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul amewasili nchini tarehe 29 Februari, 2024. Mhe. Keul yuko nchini kwa ziara ya kikazi ya Siku Nne.
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA) Mhe. Keul amelakiwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Kisare Makore, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Hassan Mwamweta na viongozi wengine wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Akiwa nchini Mhe. Keul atatembelea Hospitali ya KCMC, kuzuru kaburi la Mangi Meli na kutembelea Parish ya kidia ambako atahudhuria sherehe za kukumbuka maisha ya kazi za mwandishi wa Ujerumani mchungaji Bruno Gutmann aliyeishi eneo hilo kwa miaka 28 na kuzindua kitabu cha maisha ya kiutamaduni ya wachaga kilichoandikwa kwa lugha ya kiswahili.
Mhe. Keul pia anatarajiwa kukutana na kuzungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Angellah Kairuki na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro.
Ziara ya Mhe. Keul pamoja na kujionea shughuli mbalimbali za maendeleo zinazofadhiliwa na Serikali ya Ujerumani katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha pia inalenga kuendelea kuimarisha Uhusiano na ushirikiano Kati ya Tanzania na Ujerumani.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.