Monday, July 22, 2013

Mhe. Membe akutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa New Zealand

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza masuala mbalimbali katika kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na New Zealand alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Murray McCully tarehe 22 Julai 2013. Mhe. McCully na ujumbe wake wapo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili tarehe 21  na 22 Julai, 2013.
Mhe. McCully nae akimweleza Mhe. Membe masuala ya msisitizo katika kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizi mbili ikiwemo ushirikiano katika masuala ya biashara na kilimo.

Mhe. Membe na wajumbe kutoka Tanzania na New Zealand wakimsikiliza Mhe. McCully.

Mhe. Membe  akimkabidhi Mhe. McCully zawadi ya kinyago mara baada ya mazungumzo yao.


Mhe. Membe akiagana na mgeni wake mara baada ya mazungumzo yao.

Sunday, July 21, 2013

Tanzania yadhamiria kushirikiana na New Zealand kukuza sekta ya kilimo



Waziri wa Mambo ya Nje wa New Zealand, Mhe. Murray McCully amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kuanzia tarehe 21- 22 Julai, 2013.

 Wakati wa ziara hiyo, Mhe. McCully atafanya mazungumzo na Viongozi wa Kitaifa wa Serikali akiwemo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Peter Pinda (Mb); Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb); Wazri wa Nishati na Madini, Mhe. Prof. Sospeter Muhongo (Mb); na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. William Mgimwa (Mb). 

Mazungumzo yao yanatarajiwa kujikita katika kuimarisha maeneo ya ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na New Zealand. Tanzania ina lenga kujifunza kutoka New Zealand kutokana na nchi hiyo kupata mafanikio makubwa katika sekta ya kilimo hususan ufugaji na viwanda vya kusindika maziwa na mazao mengine.
Eneo lingine ambalo Tanzania inataka kushirikiana na New Zealand ni sekta ya nishati mbadala. Tanzania imedhamiria kukarabisha makampuni ya New Zealand kuwekeza nchini katika uzalishaji wa nishati ya nguvu ya jua na geothermal.

Kukaribishwa kwa makampuni hayo ni moja ya mikakati ya Serikali ya kufikia lengo lake la kuwapatia umeme asilimia 30 ya wananchi wa vijijini ifikapo mwaka 2015.

Waziri wa Mambo ya Nje wa New Zealand atua nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi ya siku mbili

Waziri wa Mambo ya Nje wa New Zealand, Mhe. Murray McCully (kulia) akipeana mkono na Mkurugenzi wa Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mberwa Kairuki wakati alipo wasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Mhe. McCully yupo nchini kwa ziara ya siku mbili ambapo atajadili na Viongozi wa Kitaifa wa Serikali namna ya kukuza na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na New Zealand.

Balozi Kairuki na Mhe. McCully wakielekea chumba maalum kwa ajili ya kufanya mazungumzo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa New Zealand (kushoto) akiwa katika maungumzo na Balozi Kairuki.

Saturday, July 20, 2013

Miili ya Askari waliofariki mjini Darfur yawasili nchini


Sehemu ya Masanduku yenye miili ya askari saba wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliofariki dunia hivi karibuni mjini Darfur nchini Sudan wakati wakilinda amani, yawasili nchini leo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.  

Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wanananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa wamebeba moja ya masanduku saba yenye miili ya askari wa jeshi hilo waliofariki dunia mjini Darfur wakati wakilinda amani.  

Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wanananchi wa Tanzania (JWTZ) wakipakia moja ya masanduku saba yenye miili ya askari wa jeshi hilo waliofariki dunia mjini Darfur wakati wakilinda amani.  

Askari hao waliuwawa kwa shambulio la kushtukiza na kundi la waasi wakati wakiwa kwenye kazi yao ya kulinda amani nchini Sudan.  

Jeshi la JWTZ lilioa taarifa likisema kuwa tukio hilo ni pigo kubwa kwa nchi yetu ya Tanzania ikiwa ni la kwanza kutokea tangu Tanzania ilipoanza kuchangia walinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa mwaka 2007.


Picha na maelezo kwa hisani ya www.issamichuzi.blogspot.com




Friday, July 19, 2013

Mhe. Membe akutana na Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu wa China


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza na Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali wa Jamhuri ya Watu wa China, Bw. Liu Jiayi alipofika Wizarani na Ujumbe wake kwa mazungumzo kuhusu Serikali hizi mbili kushirikiana kwa kubadilishana uzoefu katika masuala ya ukaguzi wa hesabu za serikali.
Bw. Liu Jiayi (wa kwanza kulia) na ujumbe wake akiwemo Balozi wa China hapa nchini, Mhe.Lv Youqing (wa tatu kutoka kulia) wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) wakati wa mazungumzo nae.
Bw. Liu Jiayi akimweleza jambo Mhe. Membe aliyekuwa akisikiliza kwa makini.

Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Ludovick Utoh na ujumbe wake wakimsikiliza Bw. Lui Jiayi (hayupo pichani) wakati wa mazungumzo na Mhe. Membe.

Mhe. Membe na wajumbe kutoka Tanzania na China kwa pamoja wakimsikiliza Bw. Liu Jiayi.

Mhe. Membe na Bw. Utoh wakimsikiliza Bw. Liu Jiayi alipokuwa akifafanua jambo katika moja ya taarifa za ukaguzi za nchini kwake alizomkabidhi Mhe. Membe.

Bw. Adam Isara, Afisa Mambo ya Nje akinukuu mazungumzo kati ya Mhe. Membe na Bw. Liu Jiayi.
Mhe. Membe katika picha ya pamoja na Bw. Liu Jiayi na Mhe. Balozi Lv Youqing.

Mhe. Membe akiagana na Bw. Liu Jiayi.