Thursday, February 26, 2015

Tanzania na Zambia zadhamiria kufufua Reli ya TAZARA



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Zambia kwa ajili ya mazungumzo rasmi na Mwenyeji wake Rais Edgar Lungu ( mwenye suti ya kijivu aliyesimama mbele ya Rais Kikwete)
Rais Lungu akimkaribisha Rais Kikwete (hayupo pichani kuzungumza)
Mhe. Rais Kikwete akizungumza wakati wa mazungumzo rasmi na Rais Lungu na Ujumbe wake katika Ikulu ya Zambia. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Mebe na kulia ni Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya Salu na Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe. Grace Mujuma.
Mazungumzo yakiendelea
Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania wakati wa mazungumzo rasmi akiwemo Mhe. Charles Tizeba (wa kwanza  kulia), Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Abbas Kandoro (wa pili kulia), Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bi. Zuhura Bundala (wa tatu kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Bi. Talha Mohammed (wa kwanza kushoto), Afisa Mambo ya Nje.

Picha ya Pamoja
Mhe. Rais Lungu akiwa amefuatana na Mhe. Membe.
==============================================



Tanzania na Zambia kufufua Reli ya TAZARA

Tanzania na Zambia zimekubaliana kushirikiana na kuimarisha sekta ya miundombinu hususan kufufua Reli inayounganisha nchi hizi mbili (TAZARA) ili kukuza biashara na uwekezaji.

Makubaliano hayo yamefikiwa jana wakati wa ziara ya siku mbili ya Rais wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete nchini Zambia.

Akizungumza wakati wa mkutano rasmi kati yake na mwenyeji wake, Mhe. Edgar Lungu, Rais wa Zambia, Rais Kikwete alisema kuwa umefika wakati sasa  wa kuifufuA Reli ya TAZARA ambayo ni kiungo muhimu na alama kubwa ya ushirikiano kati ya Tanzania na Zambia.

Mhe. Rais Kikwete alifafanua kuwa umuhimu wa reli hiyo ni wa kihistoria ambao unahusisha nchi tatu za Tanzania, Zambia na Jamhuri ya Watu wa China ambao kwa kiasi kikubwa walichangia ujenzi wa reli hiyo.

“Upo umuhimu mkubwa wa kuifufua Reli ya TAZARA ili ifanye kazi kama awali kwani ni alama na kiungo muhimu cha ushirikiano wetu sisi Tanzania na Zambia”, alisema Rais Kikwete.

Aidha, aliongeza kuwa Tanzania na Zambia zimekubaliana kuwekeza zaidi katika reli hiyo ikiwemo kuboresha uendeshaji na ukarabati ili kuirejesha katika hali yake ya awali na hatimaye kukuza biashara na uwekezaji. Alifafanua kwamba hapo awali reli hiyo iliweza kusafirisha tani zaidi ya milioni 2 za bidhaa kwa mwaka wakati sasa reli hiyo inasafirisha  tani laki 2 kwa safari inayotumia hadi siku 12 kutoka Dar es Salaam hadi New Kapiri Mposhi wakati malori yanatumia siku tano pekee.

“TAZARA inapita katika kipindi kigumu sasa, hivyo tumezungumza namna ya kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili ikiwemo uendeshaji na ukarabati ili irejee katika hali yake ya awali”, alisisitiza Rais Kikwete.

Katika  hatua nyingine Mhe. Rais Kikwete alimpongeza Rais Lungu kwa kuchaguliwa hivi karibuni kuwa Rais wa Zambia na pia alitoa salamu za pole kwa Rais huyo na Wazambia wote kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Hayati Michael Satta.

Kwa upande wake, Rais Lungu alisema kuwa Tanzania na Zambia zinajivunia mafanikio ya ushirikiano yaliyopo baina ya nchi hizi mbili ambayo yamejikita katika sekta za Kilimo, Usafirishaji, Nishati na Mawasiliano.

Pia, alisema kwamba nchi yake ipo tayari kuimarisha ushirikiano wa kihistoria uliopo ambao unaanzia ngazi ya serikali, kanda, Bara  na Kimataifa na kusisitiza umuhimu wa kuitumia Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) ambayo ilianzishwa rasmi mwaka 1992 kwa ajili ya kusimamia utekelezaji wa makubaliano mbalimbali yanayofikiwa na nchi hizi mbili. Aidha, alikubaliana na hoja ya kuifufua reli ya TAZARA kwa manufaa ya nchi hizi mbili.

Rais Kikwete ambaye alikuwa nchini humo kwa mwaliko wa Rais Lungu alifuatana na Mama Salma Kikwete, Mhe. Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Saada Mkuya Salum, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Charles Tizeba, Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Abbas Kandoro, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Grace Mujuma, Balozi wa Tanzania nchini Zambia na Viongozi Waandamizi kutoka Serikalini na Mamlaka mbalimbali.

_Mwisho_


Wednesday, February 25, 2015

Rais Kikwete awasili Zambia kwa ziara ya kikazi ya siku mbili

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) kwa pamoja na mwenyeji wake Rais wa Zambia, Mhe. Edgar Lungu akisikiliza Wimbo  wa Taifa ukipigwa kwa heshima yake mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Keneth Kaunda nchini Zambia kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili.
Mhe. Rais KIkwete akikagua Gwaride la Heshima wakati wa ziara hiyo

Mama Salma Kikwete (mwenye kilemba chekundu) akiwa na  Mke wa Rais Lungu, Mama Esther pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe (mwenye tai nyekundu) wakifuatilia kwa furaha mapokezi.

Mhe. Rais Kikwete na Mhe Rais Lungu wakifurahia jambo kabla ya kuondoka uwanjani hapo baada ya mapokezi
Mhe. Rais Kikwete akiwasili katika eneo la Embassy Park Jijini Lusaka yalipo makaburi ya Viongozi Wakuu wa nchi hiyo kwa ajili ya kuweka mashada ya maua kuwakumbuka Viongozi hao akiwemo Hayati Fredrick Chiluba, Hayati Levy Mwanawasa na Hayati Michael Satta.
Mhe. Rais Kikwete kwa pamoja na Mama Salma wakiweka shada la maua kwenye moja ya kaburi la viongozi hao.
Mhe. Rais Kikwete akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuweka mashada ya maua kuwakumbuka Marais watatu wa Zambia waliozikwa kwenye eneo hilo
Waziri Membe (kulia) akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe. Grace Mujuma pamoja na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Bw. Salva Rweyemamu.
============================================
            Rais Kikwete awasili Zambia kwa ziara ya kikazi


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amewasili nchini Zambia leo tarehe 25 Februari, 2015 kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ikiwa ni mwaliko kutoka kwa Rais wa Zambia, Mhe. Edgar Lungu.

Mara baada ya kuwasili, Mhe. Rais Kikwete amepokelewa rasmi na mwenyeji wake Mhe. Rais Lungu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Keneth Kaunda ambapo alikagua Gwaride la Heshima na kupigiwa mizinga 21.

Baada ya mapokezi hayo, Mhe. Rais Kikwete alitembelea Eneo la Emmbasy Park, Jijini Lusaka ambalo ni maalum kwa maziko ya Viongozi Wakuu wa Taifa hilo na kuweka mashada ya maua kwenye makaburi ya Marais watatu ambao ni Hayati Rais Fredirick Chiluba, Hayati Rais Levy Mwanawasa na Hayati Rais Michael Satta.

Vile vile, Mhe. Rais Kikwete atafanya mazungumzo ya faragha na Rais Lungu yakifuatiwa na mazungumzo rasmi na baadaye dhifa ya Chakula cha Jioni iliyoandaliwa maalum kwa ajili yake na Rais Lungu.

Mhe. Rais Kikwete atamtembelea mwasisi wa Taifa la Zambia na Rais wa kwanza wa nchi hiyo Mhe. Keneth Kaunda tarehe 26 Februari 2015 na baadaye kukutana na Jumuiya ya Watanzania waishio Zambia.

Mhe Rais Kikwete ambaye amefuatana na Mama Salma Kikwete, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe, Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya Salum, Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Charles Tizeba, Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe. Grace Mujuma, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Abbas Kandoro na Viongozi Waandamizi kutoka Serikalini na Mamlaka mbalimbali, atarejea nchini tarehe 26 Februari, 2015.

_Mwisho-





BALOZI DORA MMARI MSECHU AKUTANA NA WATANZANIA WAISHIO DENMARK.

Balozi wa Tanzania wa nchi za Nordic na Baltic Mhe. Dora Mmari Msechu akiongea na Watanzania waishia Denmark siku ya Jumamosi Februari 21, 2015 siku alipokutana nao kwenye  Hafla iliyofanyika Radisson Blue Royal Hotel. Hammarichsgade 1, 1611 Kopenhagen..      
Balozi wa Tanzania wa nchi za Nordic na Baltic Mhe. Dora Mmari Msechu akisalimiana na  watanzania waishio nchini Denmark siku ya Jumamosi Februari 21, 2015 Hafla iliyofanyika Radisson Blue Royal Hotel. Hammarichsgade 1, 1611 Kopenhagen..
Balozi wa Tanzania wa nchi za Nordic na Baltic Mhe. Dora Mmari Msechu akiwa katika picha ya pamoja na Watanzania waishio Denmark.



Mkuu wa Mkoa wa Arusha atembelea Wizara ya Mambo ya Nje

Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Irene Kasyanju (kulia) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Filex Daud Ntibenda, walipo kutana ofisini kwa Balozi leo. Wawili hao walijadili maendeleo ya ujenzi wa miundombinu katika eneo la lakilaki jijini Arusha ambalo limetengwa kwa ajili ya ujenzi wa Taasisi za Kimataifa.
Wakwanza kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Balozi Hassan Simba Yahaya akifuatilia mazungumzo.  
Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia Balozi Mbelwa Kairuki akisikiliza mazungumzo hayo kwa makini
Afisa Mambo ya Nje Bw. Elisha Suku akifuatilia kwa umakini mazungumzo kati ya Balozi Kasianju na Mhe. Ntibenda Mkuu wa Mkoa wa Arusha



Mazungumzo yakiendelea


Picha na Reginald Kisaka

Tuesday, February 24, 2015

Naibu Balozi wa Misri amtembelea Naibu Waziri wa Mambo ya Nje ofisini kwake jijini Dar es Salaam

 Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb) akimsikiliza Naibu Balozi wa Misri hapa Nchini, Bw. Ahmed Elsayed Abdelrahim alipomtembelea ofisini kwake leo. Wawili hao pamoja na mambo mengine walijadiliana kwa kina namna ya kuimarisha mahusiano ya kidplomasia kati ya nchi hizi mbili.
Mazungumzo yakiendelea ofisini kwa Naibu waziri huku Naibu Balozi wa Misri hapa Nchini Bw.Ahmed Elsayed Abdelrahim akimsikiliza kwa makini Naibu Waziri Mhe. Mahadhi.
Maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Celestine Kakere (kulia) na Bw. Adam Issara wakifuatilia mazungumzo hayo. 
=============
Picha na Reuben Mchome.

Monday, February 23, 2015

Rais Kikwete amkabidhi Mtukufu Aga Khan Hati ya Utambulisho wa Chuo Kikuu cha Aga Khan Nchini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Kiongozi wa Madhehebu ya Ismailia Duniani, Mtukufu Karim Aga Khan alipowasili Ikulu, Mtukufu Aga Khan amefanya mazungumzo na Mhe. Rais na kukabidhiwa Hati ya Chuo Kikuu cha Aga Khan (Aga Khan University) kilichopo Jijini Dar es Salaam.
Mhe. Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mtukufu Aga Khan
Mhe. Rais Kikwete pamoja na Mtukufu Aga Khan wakifurahia jambo wakati wa mazungumzo yao.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mhe. Shukuru Kawambwa (Mb.) akizungumza na kumkaribisha Mhe. Rais Kikwete kwa ajili ya kumkabidhi Mtukufu Aga Khan Hati ya Utambulisho wa Chuo Kikuu cha Aga Khan nchini.
Wajumbe walioambatana na Mtukufu Aga Khan wakifuatilia mazungumzo hayo kwa makini
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete, akimkabidhi Mtukufu Aga Khani Hati ya Chuo Kikuu cha Aga Khan nchini.
Sehemu ya Ujumbe wa Tanzania wakifuatilia mazungumzo kati ya  Mhe. Rais Kikwete, Mtukufu Aga Khan  na Waandishi wa Habari (hawapo pichani). Wa kwanza mstari wa pili ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga.
Mtukufu Aga Khani akizungumza wakati wa  mkutano kati yao na waandishi habari (hawapo pichani) huku Rais Jakaya Kikwete akimsikiliza
Mkutano na Waandishi wa Habari ukiendelea
Picha ya pamoja baada ya Mkutano


Picha na Reginald Philip

Friday, February 20, 2015

Waziri Membe ampokea Mtukufu Karim Aga khan

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb.) akimpokea Mwanzilishi wa Taasisi ya Maendeleo ya Aga khan Duniani,  Mtukufu Karim Aga Khan mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Mtukufu Aga Khan yupo nchini kwa ziara binafsi ya siku nne, ambapo pia atatumia fursa hiyo kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo ya taasisi hiyo hapa nchini.


 


Mtukufu Aga Khan akisalimiana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Nchini  Dkt. Shukuru Kawambwa mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
 
Mtukufu Aga Khan akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bi. Mindi Kasiga mara baada ya kupokelewa kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Ijumaa tarehe 20.02.2015
Mtukufu Aga Khan akisalimiana na Afisa Mambo ya Nje Hassan Mwamweta baada ya kuwasili jijini Dar es salaam kwa ziara ya siku nne nchini Tanzania. 
Waziri Membe akizungumza jambo na Mtukufu Aga Khan mara baada ya sherehe fupi ya mapokezi baada ya kuwasili nchini.  


Picha na Reginald Philip

Balozi wa Tanzania Nchini Canada awasilisha Hati za utambulisho

Balozi mpya wa Tanzania nchini Canada Mhe. Jack Mugendi Zoka akiwakilisha hati ya utambulisho kwa Gavana Mkuu wa Canada Mhe. David Johnson siku ya Jumatano Februari 18, 2015
Balozi mpya wa Tanzania nchini Canada Mhe. Jack Mugendi Zoka akiwa katika picha ya pamoja na Gavana Mkuu wa Canada Mhe. David Johnson.
Balozi mpya wa Tanzania nchini Canada Mhe. Jack Mugendi Zoka na mke wake Bi. Esther Zoka wakiwa katika picha ya pamoja na Gavana mkuu wa Canada Mhe. David Johnson.
Balozi mpya wa Tanzania nchini Canada Mhe. Jack Mugendi Zoka na mke wake Bi. Esther Zoka na baadhi ya Watanzania waliohudhuria uwakilishi hati ya utambulisho wakiwa katika picha ya pamoja na Gavana mkuu wa Canada Mhe. David Johnson.

WAZIRI CHIKAWE AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WAKUPAMBANA NA VURUGU NA UGAIDI, WASHINGTON MAREKANI

Rais wa Marekani, Barack Obama akitoa hotuba yake katika Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani uliofanyika katika Ukumbi wa Loy Henderson, Wizara ya Mambo ya Nje, jijini Washington DC nchini humo leo. Mkutano huo uliowashirikisha Mawaziri wanaoshughulika na masuala ya usalama kutoka mataifa mbalimbali duniani, Maafisa Waandamizi wa Umoja wa Mataifa (UN), Vyama vya Kiraia na Sekta Binafsi ulijadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupambana na ugaidi pamoja na vurugu mbalimbali dunaini. Katika hotuba yake, Obama alisema mapambano dhidi ya watu wenye msimamo mkali hayawezi kulinganishwa na mapambano dhidi ya waislamu. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe aliiwakilisha Tanzania katika mkutano huo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akimsikiliza kwa makini Rais Barack Obama (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba yake katika Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani uliofanyika katika Ukumbi wa Loy Henderson wa Wizara ya Mambo ya Nje, jijini Washington DC nchini humo leo. Mkutano huo uliowashirikisha Mawaziri wanaoshughulika na masuala ya usalama kutoka mataifa mbalimbali duniani, Maafisa Waandamizi wa Umoja wa Mataifa (UN), Vyama vya Kiraia na Sekta Binafsi ulijadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupambana na vurugu na ugaidi dunaini. Katika hotuba yake, Obama alisema mapambano dhidi ya watu wenye msimamo mkali hayawezi kulinganishwa na mapambano dhidi ya waislamu, hivyo hakuna dini yoyote inayowajibika kwa ugaidi, isipokuwa watu ndio wanaowajibika kwa vurugu na ugaidi.

Rais wa Marekani, Barack Obama akitoa hotuba yake katika Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani uliofanyika katika Ukumbi wa Loy Henderson, Wizara ya Mambo ya Nje, jijini Washington DC nchini humo leo. Mkutano huo uliowashirikisha Mawaziri wanaoshughulika na masuala ya usalama kutoka mataifa mbalimbali duniani, Maafisa Waandamizi wa Umoja wa Mataifa (UN), Vyama vya Kiraia na Sekta Binafsi ulijadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupambana na ugaidi pamoja na vurugu mbalimbali dunaini. Katika hotuba yake, Obama alisema mapambano dhidi ya watu wenye msimamo mkali hayawezi kulinganishwa na mapambano dhidi ya waislamu. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe aliiwakilisha Tanzania katika mkutano huo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kushoto-mstari wa pili), Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula (nyuma ya waziri) wakimsikiliza kwa makini Rais Barack Obama (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba yake katika Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani uliofanyika katika Ukumbi wa Loy Henderson wa Wizara ya Mambo ya Nje, jijini Washington DC nchini humo leo. Mkutano huo uliowashirikisha Mawaziri wanaoshughulika na masuala ya usalama kutoka mataifa mbalimbali duniani, Maafisa Waandamizi wa Umoja wa Mataifa (UN), Vyama vya Kiraia na Sekta Binafsi ulijadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupambana na vurugu na ugaidi dunaini. Katika hotuba yake, Obama alisema mapambano dhidi ya watu wenye msimamo mkali hayawezi kulinganishwa na mapambano dhidi ya waislamu, hivyo hakuna dini yoyote inayowajibika kwa ugaidi, isipokuwa watu ndio wanaowajibika kwa vurugu na ugaidi. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.