Thursday, December 10, 2020
TANZANIA NA HUNGARY ZATILIANA MKATABA MKATABA WA UFADHILI WA MASOMO KWA WANAFUNZI 30 WA KITANZNIA KWA MWAKA 2021 - 2023
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE, MHE. OLE NASHA ALIVYOPOKELEWA WIZARANI
Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akisalimiana na Mkurugenzi wa Kitengo cha Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Anisa Mbega wakati wa mapokezi yake alipowasili Wizarani |
Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Caesar Waitara wakati wa mapokezi yake alipowasili Wizarani |
Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bibi Agnes Kayola wakati wa mapokezi yake alipowasili Wizarani |
Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akisalimiana na Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Swalehe Chondoma wakati wa mapokezi yake alipowasili Wizarani |
Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Ugavi na Ununuzi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Salifius Mligo wakati wa mapokezi yake alipowasili Wizarani. |
Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akisalimiana na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Japhary Kachenje wakati wa mapokezi yake alipowasili Wizarani |
Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bibi Agnela Nyoni wakati wa mapokezi yake alipowasili Wizarani |
Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bibi Caroline Chipeta wakati wa mapokezi yake alipowasili Wizarani |
Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Masoud Balozi wakati wa mapokezi yake alipowasili Wizarani |
Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Macocha Tembele wakati wa mapokezi yake alipowasili Wizarani |
Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Aman Mwatonoka wakati wa mapokezi yake alipowasili Wizarani |
Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akisalimiana na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Emmanuel Buhohela wakati wa mapokezi yake alipowasili Wizarani |
Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Gwamaka Lazarous wakati wa mapokezi yake alipowasili Wizarani |
Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Isaac Kalumuna wakati wa mapokezi yake alipowasili Wizarani |
Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akisalimiana na mmoja wa Watumishi wa Wizara waliofika kumpokea alipowasili Wizarani
|
aibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akizungumza na Viongozi na Watumishi wa Wizara mara baada ya Wizarani baada ya kuapishwa |
Mhe. Prof. Kabudi akiwa na Mhe. Ole Nasha wakizungumza na Watumishi wa Wizara |
Picha ya pamoja kati Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (wa tatu kushoto mstari wa kwanza) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. William Tate Ole Nasha (wa nne kulia mstari wa kwanza) pamoja na Watumishi wa Wizara walioshiriki mapokezi ya Mhe. Ole Nasha alipowasili Wizarani baada ya kuapishwa ========================================== Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. William Tate Ole Nasha ameahidi ushirikiano kwa Watumishi wa Wizara katika kuhakikisha Wizara inakuwa na matokeo chanya yenye tija kwa jamii na Taifa kwa ujumla katika utekelezaji wa majukumu yake. Mhe. Ole Nasha ameyasema hayo aliwapowasili Wizarani mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika hafla iliyofanyika Ikulu, Chamwino jijini Dodoma tarehe 9 Desemba 2020. Mhe. Ole Nasha ambaye alipokelewa na Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amesema kuwa yupo tayari kujifunza kutoka kwa Watumishi wote ili kuiwezesha Wizara kufikia malengo yaliyokusudiwa. Kwa upande wake. Prof. Kabudi alimhakikishia Mhe. Ole Nasha ushirikiano wake binafsi na kutoka kwa Watumishi wote na kwamba uwepo wake utaongeza nguvu za kuifikisha Wizara katika viwango vya juu kiutendaji. |
Tuesday, December 8, 2020
HABARI KATIKA PICHA MAHAFALI YA 50 YA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John
Kabudi (Mb) akimkabidhi zawadi ya vitabu Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Namibia ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia, Mhe. Netumbo Ndaitwah
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John
Kabudi (Mb) akiwasilisha salamu za Serikali kwenye mahafali ya 50 ya chuo hicho
yaliyofanyika jijini Dar es Salaam
Mkuu
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete akimkabidhi moja kati ya zawadi Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Namibia ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia, Mhe. Netumbo Ndaitwah
Mkuu
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete akimtunuku shahada ya heshima Naibu Waziri Mkuu Wa Jamhuri ya
Namibia ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia, Mhe. Netumbo Ndaitwah
Baadhi
ya wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakiwa ukumbini tayari kwa ajili ya
kutunukiwa shahada
Baadhi
ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa Nchini wakifuatilia sherehe za
mahafali ya 50 ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es Salaam
Mkuu
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) katika mahafali ya 50 ya chuo
hicho yaliyofanyika jijini Dar es Salaam
Monday, December 7, 2020
WAKURUGENZI NA WAKUU WA IDARA WA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI WAPIGWA MSASA KUHUSU MANUNUZI YA UMMA
TANZANIA, NAMIBIA ZAKUBALIANA KUIMARISHA SEKTA ZA UVUVI NA MIFUGO
Katika jitihada za kuendeleza Diplomasia ya Uchumi, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekubaliana na Jamhuri ya Namibia kuimarisha sekta za uvuvi na mifugo.
Makubaliano
hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam ambapo Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi (Mb) amekubaliana na Naibu
Waziri Mkuu Wa Jamhuri ya Namibia ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia, Netumbo Ndaitwah kuimarisha
ushirikiano katika sekta ya Uvuvi pamoja na Sekta ya Mifugo.
"Tumekubalina kuimarisha ushirikiano katika
enao la uvuvi wa bahari kuu lakini pia kuwahamasisha wadau wa sekta binafsi
kutoka Tanzania na Namibia kuwekeza katika eneo hilo. Kwa upande wa mifugo na
uuzaji wa nyama nchi za nje Namibia wamepiga hatua kubwa sana na sasa wanauza
nyama Ulaya na Asia," Amesema Prof. Kabudi
Aidha, Prof. Kabudi ameongeza kuwa wamekubaliana
pia kuhamasisha sekta binafsi kutoka Namibia kuja kuwekeza katika machinjio na
viwanda vya kusindika nyama hapa nchini (Tanzania) kwa ajili ya kuuza nyama
hiyo nje ya Tanzania na kuendeleza sekta za uvuvi na mifugo.
Pamoja na mambo mengine, kikao cha leo kimepitia
makubaliano ya miaka miwili iliyopita ambapo Tanzania na Namibia zimekubaliana
kutumia fursa zilizopo kati yao kuendeleza sekta za uwekezaji, uvuvi, kilimo na
mifugo kwa maslahi mapana ya pande zote mbili.
Kwa upande wake Naibu
Waziri Mkuu Wa Jamhuri Ya Namibia ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia, Netumbo Ndaitwah amesema
kuwa wamekubaliana kuimarisha sekta mbili ambazo ni Uvuvi na mifugo pamoja na
kilimo kwa ujumla kwa kuzingatia mazingira bora ya uwekezaji na biashara ndani
ya Umoja wa Afrika (AU).
"Kuna maeneo mbalimbali ambayo kwa pamoja
tumekubaliana kuyaimarisha ikiwemo uvuvi, mifugo na kilimo kwa ujumla, kupitia
kikao cha leo tunaamini kuwa wawekezaji kutoka Namibia watakuja kuwekeza
Tanzania na vilevile wawekezaji kutoka Tanzania watawekeza Namibia,"
Amesema
Ameeleza kuwa Namibia itaendelea kufanya kazi kwa
karibu na Tanzania katika kuhakikisha kuwa wanakuza uchumi wa nchi zetu zote
mbili na Afrika kwa ujumla kwa kuzingatia misingi ya biashara na uwekezaji
iliyopo ndani ya Umoja wa Afrika (AU).
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi (Mb) akimuelezea jambo Naibu Waziri Mkuu Wa Jamhuri ya Namibia ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia, Netumbo Ndaitwah walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam |
Naibu Waziri Mkuu Wa Jamhuri ya Namibia ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia, Netumbo Ndaitwah akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi (Mb) wakati walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam |
Naibu
Waziri Mkuu Wa Jamhuri ya Namibia ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia, Netumbo Ndaitwah na Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi
katika picha ya pamoja. Kushoto mwa Mhe. Ndaitwah ni Balozi wa Namibia hapa nchini, Mhe. Theresia Samaria
ambaye amamaliza muda wake wa utumishi, na Kulia mwa Prof. Kabudi ni Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Afrika, Bw. Frank Mwega. |
Naibu
Waziri Mkuu Wa Jamhuri ya Namibia ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia, Netumbo Ndaitwah akimkabidhi
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba
Kabudi zawadi za vitabu |