Sehemu ya Mabalozi wakifurahia jambo wakati Waziri Makamba akizungumza kwenye kikao cha maandalizi kuelekea warsha ya Mabalozi inayotarajiwa kuanza tarehe 21 Aprili 2024 mjini Kibaha, Pwani |
Saturday, April 20, 2024
MABALOZI WA TANZANIA WAJIFUNGIA KIBAHA KUTAFAKARI NA KUJIPANGA UPYA
Friday, April 19, 2024
MHE. RAIS SAMIA AWAKARIBISHA WAFANYABIASHARA WA UTURUKI KUSHIRIKI MAONESHO YA SABASABA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa mwaliko rasmi kwa Jumuiya ya Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Uturuki kushiriki Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu kama Sabasaba yanayotarajiwa kufanyika nchini mwishoni mwa mwezi Juni 2024.
Mhe. Rais Dkt. Samia ametoa mwaliko huo wakati akifungua rasmi Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Uturuki lililofanyika leo tarehe 19 Aprili 2024 jijini Istanbul na kuhudhuriwa na zaidi ya wafanyabiashara na wakezaji 150 kutoka nchi hizi mbili.
Amesema maonesho hayo ya biashara ambayo ni makubwa Afrika Mashariki hutoa fursa ya kuwakutanisha wafanyabiashara na kuwawezesha kubadilishana taarifa na uzoefu, kujua taarifa mpya za masoko na bidhaa pamoja na kuuza bidhaa zao.
Kadhalika Mhe. Rais Samia ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Uturuki kuja kuwekeza nchini na kuitaja Tanzania kama nchi yenye fursa lukuki kama vile ardhi yenye rutuba kwa ajili ya kilimo, Hifadhi za wanyama kwa ajili ya utalii, nishati, madini ikiwemo Tanzanite ambayo hupatikana nchini Tanzania pekee na fursa za biashara na uwekezaji.
Amesema Serikali yake imeendelea kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji ambapo pamoja na mambo mengine imewekeza katika kujenga miundombinu inayoiunganisha Tanzania na nchi nyingine jirani ikiwemo Reli ya Kisasa ya SGR.
Vilevile, Mhe. Rais Samia alitumia fursa hiyo kuzipongeza Wizara za Mambo ya Nje za nchi hizi mbili kwa kuandaa kwa mafanikio Kongamano hilo ambalo ni jukwaa muhimu katika kukuza ushirikiano kwenye sekta ya biashara na uwekezaji.
Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa Uturuki, Mhe. Cevdet Yilmaz ambaye alishiriki Kongamano hilo, amesema nchi yake itaendelea kuimarisha ushirikiano na Tanzania katika sekta ambazo nchi hiyo imepiga hatua ikiwemo Utalii, Usafirishaji, Biashara na Uwekezaji.
Awali akizungumza kwenye Kongamano hilo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amesisitiza umuhimu wa nchi hizi mbili kushirikiana na Sekta Binafsi katika kufikia malengo ya kukuza uchumi kwa manufaa ya wananchi wa mataifa haya.
Kadhalika ametoa rai kwa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Tanzania kuunga mkono juhudu nyingi zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na mataifa mbalimbali ikiwemo Uturuki ili kutengeneza mazingira wezeshi ya ufanyaji biashara za kuvuka mipaka kwa Watanzania.
Mhe. Rais Samia yupo nchini Uturuki kwa ziara ya kitaifa kufuatia mwaliko wa Rais wa nchi hiyo, Mhe. Recep Tayyip Erdogan.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji akizunumza wakati wa Kongamano la Baishara kati ya Tanzania na Uturuki |
Makamu wa Rais wa Uturuki, Mhe. Cevdet Yilmaz akizungumza wakati wa Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Uturuki |
Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Uturuki likiendelea |
Kongamano likiendelea |
Sehemu ya Wafanyabiasha na wawekezaji wa Uturuki wakishiriki Kongamano |
Mhe. Waziri Makamba akibadilishana mawazo na mmoja wa wageni waalikwa walioshiriki Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Uturuki |
Kongamano likiendelea |
Sehemu ya washiriki wa Kongamano |
Mhe. Rais Samia na Viongozi wengine wakishiriki sehemu ya utaratibu wa ufunguzi wa Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Uturuki |
Thursday, April 18, 2024
WIZARA YA MAMBO YA NJE YAJIVUNIA KUIMARIKA KWA DIPLOMASIA, MIAKA 60 YA MUUNGANO
MHE. RAIS SAMIA ATUNUKIWA SHAHADA YA HESHIMA YA UDAKTARI NCHINI UTURUKI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Samia Suluhu ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari (Honoris Causa) katika Uchumi na Chuo Kikuu cha Ankara cha nchini Uturuki ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wake katika kuboresha maisha ya watanzania kupitia mageuzi mbalimbali pamoja na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na nchi mbaimbali duniani ikiwemo Uturuki.
“Nilipopokea taarifa kuhusu kutunukiwa shahada hii nilijiuliza, wametumia vigezo gani hadi kufikia uamuzi huu, Waziri wangu wa Mambo ya Nje alinipatia orodha yenye vigezo hivyo nikakubali, nawashukuru sana” alisema Rais Dkt. Samia
Mhe. Rais Samia amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na Uturuki katika kufikia malengo yake ya kukuza uchumi kupitia ushirikiano katika sekta mbalimbali ikiwemo biashara, kilimo, uwekezaji na ushirikiano baina ya watu wa nchi hizi mbili.
Baraza la Chuo Kikuu cha Ankara kwa kauli moja liliamua kumtunukia Mhe. Rais Dkt. Samia Shahada hiyo ya heshima, kwa kutambua Uongozi wake wa kipekee ambao umeleta mageuzi makubwa ya kijamii, kisiasa, na kiuchumi nchini Tanzania. Mageuzi hayo yameboresha ustawi wa Watanzania; na kuimarisha sifa ya Tanzania ulimwenguni; na yamekuza mahusiano ya kibiashara, kiuchumi na kisiasa kati ya Tanzania na nchi nyingine, ikiwemo Uturuki.
|
Shahada hii ni ya pili kwa Mhe. Rais Samia kutunukiwa kutoka ugenini ambapo Shahada ya kwanza ya aina hiyo alitunukiwa na Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru cha nchini India mwezi Oktoba 2023.
Taratibu mbalimbali zikiendelea kabla ya Mhe. Rais Samia kutunukiwa Shahada yake ya Udaktari. Pichani ni viongozi wakiwa wamesimama kwa heshima ya nyimbo za mataifa yao |
Mhe. Rais Dkt. Samia akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Chuo cha Ankara, Wakufunzi na Viongozi mbalimbali |