Thursday, December 4, 2014

Hon. Membe, Kinana on special mission over South Sudan

H.E. Uhuru Kenyatta (Centre), President of Kenya in a group photo with Hon. Bernard K. Membe (2nd from left), Minister for Foreign Affairs and International Cooperation of Tanzania, Hon. Amina Mohammed (left), Kenyan Minister for Foreign Affairs, Mr. Abdulrahman Kinana (2nd from right), Secretary General of CCM, and Amb. Batilda S. Burian (right),   Tanzanian ambassador to Kenya. The Tanzania Special Envoys are on a mission to reassure IGAD leaders that the Arusha initiative to resolve the South Sudan crisis is not in conflict with the separate peace negotiations in Addis Ababa spearheaded by the regional grouping.


Membe, Kinana on special mission over South Sudan
Sudan and Kenya have endorsed Tanzania’s efforts to reunite factions of the Sudan People’s Liberation Movement (SPLM), whose antagonism is central to the civil war in South Sudan.
Presidents Omar Al-Bashir and Uhuru Kenyatta said separatey during meetings with Special envoys of President Kikwete-- the Minister for Foreign Affairs and International Cooperation, Hon. Bernard Membe, and CCM Secretary General Abdulrahman Kinana, that the CCM-brokered mediation in Arusha had great potential to resolve the South Sudan crisis.
“It will be a difficult process, but if Arusha does not succeed there may be no peace in South Sudan,” declared President Al-Bashir, when the Special envoys called on him at the State House in Khartoum on Tuesday evening.
But the two leaders emphasized that the Arusha dialogue should be complementary to the South Sudan peace talks being conducted by the Inter-Governmental Authority for Development (IGAD). 
Hon. Membe and the CCM Secretary General are on a mission to reassure IGAD leaders that the Arusha initiative, which was requested by South Sudan President Salva Kiir last September, is not in conflict with the separate peace negotiations in Addis Ababa spearheaded by the regional grouping.
Mr. Kinana reassured the Sudan and Kenya leaders that the Arusha mediation conducted October 12-20 and set to resume next week, was not competing against the IGAD process. 
Hon. Membe told reporters in Khartoum that while the peace talks under IGAD conducted at the AU Headquarters in Addis Ababa involved 10 parties to the conflict in South Sudan, Arusha was focused on the SPLM factions led by President Kiir, his fired deputy Riek Machar and Ex-detainees. The bloody conflict has seen thousands of people killed and hundreds others displaced.
During the meeting with President Kenyatta at the State House in Nairobi yesterday, the Kenyan leader told the Special Envoys that the warring parties in South Sudan must not take advantage of the new initiative in Arusha to ignore the decisions reached at IGAD.
One of the decisions is that the killing of civilians should stop immediately. “They must not hide under the Arusha dialogue and continue the killings,” President Kenyatta warned. 
The two leaders agreed that CCM could use its experience spanning  over 50 years to reconcile the warring factions in SPLM, seen as the core of the conflict in Juba. Tanzania hosted the liberation movements of Angola, Mozambique, Namibia, Zimbabwe and South Africa.
The Special Envoys yesterday held talks with South Sudan President Kiir in Juba. The President reaffirmed his commitment to the dialogue in Arusha and assured CCM and the Tanzania government that he will respect and fully implement the decisions to be taken.
The Special Envoys are scheduled to wind up their mission today after consulting Uganda President Yoweri Museveni in Entebbe.
Ends

Makala ya Rais ya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Nchini Vietnam Oktoba 2014

Wednesday, December 3, 2014

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar afanya ziara nchini Comoro

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Seif Sharif Hamad akilakiwa mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Prince Said Ibrahim Hahaya nchini Comoro kwa ziara binafsi uanzia tarehe 1 hadi 4 Desemba, 2014.
Mhe. Hamad akisalimiana na Mhe. Muhammad Ali Soilihi, Makamu wa Rais wa Comoro. Kushoto ni Mhe. Chabaka Kilumanga, Balozi wa Tanzania nchini Comoro na kulia Dkt. Ahamada Albadaoui Fakih, Balozi wa Comoro nchini Tanzania.
Mhe. Hamad akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar, Balozi Silima Haji
Mhe. Hamad akiwa na baadhi ya Masheikh na Viongozi aliofutana nao
================================================



Mhe. Seif Sharif Hamad, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amefanya ziara binafsi visiwani Comoro kuanzia tarehe 1 hadi tarehe 4 Desemba 2014. Madhumuni ya ziara hii yalikuwa ni kushiriki katika maadhimisho ya miaka arobaini (40) tangu kufariki kwa Marehemu Sheikh Alhabib Omar bin Sumeti, mwanazuoni mashuhuri katika eneo la 
Bahari ya Hindi, ambaye aliwahi kuishi, kujifunza na kutoa elimu Visiwani Zanzibar.

Akiwa nchini Comoro, Mhe. Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar alipata pia fursa ya kuonana na Mhe. Dkt. Ikililou Dhoinine, Rais wa Muungano wa Visiwa vya Comoro, na Mhe. Muhammad Ali Soilihi, Makamu wa Rais wa Comoro. Katika mazungumzo yake na viongozi hao, Mhe. Makamu wa Rais alisifia juhudi zinazochukuliwa kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Comoro. Alibainisha kuwa zipo fursa nyingi za ushirikiano ambazo endapo zitafanyiwa kazi, zitazinufaisha zaidi pande hizi mbili. Aidha, Mhe. Seif Sharif Hamad alikutana na Jumuiya ya Watanzania wanaishi Nchini Comoro na kuzungumza nao.


Monday, December 1, 2014

Waziri wa Mambo ya Nje amuaga Balozi wa Australia


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Kamilius Membe (Mb.) ameagana na Balozi wa Australia nchini Tanzania Mhe Geoffrey Tooth ambaye amemaliza muda wake wa uwakilishi nchini. 
 Waziri Membe akizungumza na Balozi Tooth na kumweleza kuwa wakati wa kipindi chake cha uwakilishi, uhusiano baina ya nchi hizi mbili umeimarika. Mhe. Membe pia amemshukuiru Balozi Tooth kwa ushirikiano mzuri alioutoa katika kipindi chote na kusisitiza kuwa Tanzania ni nyumbani kwake sasa na asisite kurudi nchini kutembea au kwa mapumziko mara apatapo fursa ya kufanya hivyo.
Mazungumzo yakiendelea kushoto wa kwanza ni Katibu wa Tatu wa Ubalozi huo Bi. Freya Carlton.
Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairuki akizungumza na Balozi wa Australia ambaye amemaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini.



Picha na Reginald Philip
==========================================

Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa leo ameagana na Mhe.Geoffrey Tooth Balozi wa Australia nchini Tanzania ambaye amemaliza muda wake wa uwakilishi nchini. Katika mazungumzo yao. Waziri Membe alimueleza Balozi Tooth kuwa wakati wa kipindi chake cha uwakilishi, uhusiano baina ya nchi hizi mbili umeimarika. Mhe. Membe pia amemshukuiru Balozi Tooth kwa ushirikiano mzuri alioutoa katika kipindi chote na kusisitiza kuwa Tanzania ni nyumbani kwake sasa na asisite kurudi nchini kutembea au kwa mapumziko mara apatapo fursa ya kufanya hivyo.

Kwa upande wake, Balozi Tooth ambaye amekuwa akiiwakilisha nchi yake hapa Tanzania kutokea Nairobi Kenya, kuanzia Desemba 2010 amemshukuru Mhe. Membe, uongozi wa Wizara na wafanyakazi wote kwa ushirikiano mzuri alioupata wakati wote. Alisifu hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali katika kuleta maendeleo na kukuza mahusiano baina ya Tanzania na nchi nyingine.

Balozi Tooth aliyeongozana na Bi. Freya Carlton, Katibu wa Tatu wa Ubalozi huo, anatarajiwa kuondoka nchini wiki hii kurejea Australia ambapo atakuwa mshauri wa Serikali kwenye masuala ya mazingira na mabadiliko wa tabia nchi. 

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA 3 WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI (EAC) KUHUSU MIUNDOMBINU JIJINI NAIROBI, KENYA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza katika mkutano wa 3 
tatu wa wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu miundombinu, uliofanyika katika ukumbi wa KICC jijini Nairobi jana 
Novemba 29, 2014
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wa tatu kutoka (kushoto) Makamu wa Rais 

wa Kenya, William Ruto, (kushoto kwake) Makamu wa Rais kwanza wa Burundi, (kulia kwake) wakijumuika kwa pamoja na viongozi 


wengine wakionyesha Taarifa ya pamoja waliyoisaini kuhusu majadiliano ya kuimarisha Miundombinu kwa nchi wanachama wa 
Jumuiya ya Afrika Mashariki, katika mkutano wa 3 wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Miundombinu, uliofanyika 
kwenye Ukumbi wa KICC, jijini Nairobi jana Novemba 29, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya viongozi wakati 

wakitoka kwenye Ukumbi wa mikutano wa KICC, baada ya kushiriki katika mkutano wa 3 wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki 
(EAC) kuhusu Miundombinu 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi 

wengine walioshiriki katika mkutano huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia jambo na Makamu wa Rais wa 

Kenya William Ruto na Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, wakati wakiondoka katika viwanja vya Ukumbi wa mikutano wa 

KICC, baada ya kushiriki kwenye mkutano wa 3 wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Miundombinu, uliofanyika 

jijini Nairobi, Kenya jana Novemba 29, 2014.
 (Picha na OMR)

==========================================

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MHESHIMIWA MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI (EAC) KUHUSU MIUNDOMBINU JIJINI NAIROBI, KENYA
Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal jana Novemba 29, 2014 aliiwakilisha Tanzania katika mkutano wa siku moja wa Wakuu wa Nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Nairobi, Kenya. Mkutano huo, kwa mujibu wa utaratibu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, unafanyika kila baada ya miaka miwili na lengo lake kuu ni kufanya tathmini juu ya miradi ya miundombinu inayoshirikisha nchi washirika, sambamba na kutazama fursa ya kutanua miundombinu mipya katika nchi hizi kwa lengo la kukuza uchumi wa pamoja kwa nchi za Afrika Mashariki.
Tathmini hii ya Miundombinu inafanyika kwa kuwa mataifa ya Afrika Mashariki yanatambua umuhimu wa kuwa na miundombinu bora katika nchi hizi ili kuharakisha ukuaji wa uchumi, sambamba na kutanua mtengamano wa nchi hizi na hivyo kuwafanya wananchi wanaoishi ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuzidi kuwa wamoja.
Mkutano wa jana uliongozwa na Kaimu Rais wa Kenya Mheshimiwa William Ruto na kuhudhuriwa na Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Bilal, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Burundi, Waziri Mkuu wa Rwanda pamoja na Waziri wa Afrika Mashariki wa Uganda. Viongozi wengine waliopata nafasi ya kuhudhuria mkutano huo ni pamoja na Mheshimiwa Balozi Richard Sezibera, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Waziri wa Wizara hiyo kutoka Tanzania, Mheshimkiwa Samwel Sitta, Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Dkt. Donald Kaberuka, Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Ukanda wa Afrika, Bwana Makhtar Diop, Katibu Mtendaji wa UNCTAD, Dkt. Mukhisa Kituyi na Baalozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Balozi Filiberto Sebregondi. Pia mkutano huo ulihudhuriwa na wawakilishi wa nchi za China, Marekani, Japan na nyinginezo ambazo ni wadau wakubwa wa ujenzi wa miundombinu katika nchi za Afrika Mashariki.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Kaimu Rais wa Kenya, William Ruto alifafanua juu ya umuhimu wa kuhakikisha Afrika Mashariki inaunganishwa kwa miundombinu imara ili kukuza uchumi na akapongeza jitihada mbalimbali zinazofanyika katika kufanikisha azma hiyo huku pia akiomba nchi wanachama wa Afrika Mashariki kuendelea kuungana katika kutekeleza miradi ya miundombinu na kujitahidi kutafuta fedha kwa ajili ya kukamilisha miradi hiyo.
Mkutano huu pia uliambatana na kupokea ripoti ya utekelezaji wa maagizo ya Wakuu wa Nchi za EAC kuhusu Miundombinu kutoka kwa Mawaziri wa Nchi za Jumuiya.  Wakuu wa Nchi katika Mkutano huu walipokea taarifa ya utekelezaji wa maagizo waliyoyatoa katika mkutano wa pili uliofanyika mwezi Novemba, 2012 na kuidhinisha miradi 72 ya miundombinu ya kipaumbele ya Barabara, Reli, Nishati na Bandari.
Kwa upande wa utekelezaji; miradi 16 imekamilika, 39 inaendelea kutekelezwa na 17 ipo katika hatua za awali za kutafutiwa fedha kwa ajili ya utekelezaji wake.
Kwa upande wa Tanzania miradi minne imekamilika ambayo ni Umeme katika mji wa Kibondo, mradi wa barabara ya Mbezi-Shule-Tangibovu-Makutano ya Nelson Mandela na barabara ya Tabata. Barabara nyingine iliyokamilika ni Nyangunge – Musoma – Sirari na sehemu ya Simiyu - Musoma inayounganisha Kenya na Tanzania huko ujenzi unaendelea.
Akizungumza katika Mkutano huo Makamu wa Rais amezitaka nchi wanachama kuharakisha utekelezaji wa miradi ya Miundombinu ili kusaidia utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja, ambayo inalenga kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na abiria. “Tusiishie kubakiza mipango hii katika karatasi, tusiishie kuzungumza tu bali huu ni wakati wa kuhakikisha tunarahisisha ufanyaji biashara katika nchi zetu na kupunguza vikwazo visivyo vya lazima,” alisema Mheshimiwa Makamu wa Rais.
Katika mkutano huo, Mheshimiwa Makamu wa Rais pia aliambatana na Mheshimiwa Dkt. Mahadhi J. Maalim, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara wa Zanzibar, Mheshimiwa Nassor Ahmed Mazrui. Mheshimiwa Makamu wa Rais na msafara wake tayari wamerejea nyumbani Tanzania ambapo kesho anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, maadhimisho yanayofanyika Kitaifa Mkoani Njombe.
Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
Novemba 30, 2014


Konseli Mkuu wa Tanzania Dubai afanya mazungumzo na Konseli Mkuu wa Saudi Arabia Dubai

Konseli Mkuu wa Tanzania, Dubai, Bw. Omar Mjenga amekutana na Konseli Mkuu wa Saudi Arabia, Dubai, ambaye pia ndio Mkuu wa Makonseli Wakuu waliopo Dubai (Dean of Diplomatic Corps), Bw. Emad A. Madani katika ofisi za Koseli Kuu wa Saudi Arabia.
Konseli Mkuu Bw. Omar Mjenga akiwa katika picha ya pamoja na Konseli Mkuu  wa Saudi Arabia Dubai Bw. Bw. Emad A. Madani


Konseli Mkuu wa Tanzania, Dubai, Bw. Omar Mjenga amekutana na Konseli Mkuu wa Saudi Arabia, Dubai, ambaye pia ndio Mkuu Makonseli Wakuu waliopo Dubai (Dean of Diplomatic Corps), Mhe. Emad A. Madani katika ofisi za Koseli Kuu ya Saudi Arabia.

Bw. Mjenga alienda kumtembelea ili kuomba ushiriki wake pamoja na Makonseli Wakuu wote kwenye kongamano la uwekezaji kwenye sekta ya Utalii nchini Tanzania, litakalofanyika tarehe 17 Disemba 2014.

Bw. Emad Madani amesema atashiriki vikamlifu kwenye kongamano hilo huku akisema kuwa Tanzania na Saudi Arabia ni nchi rafiki wa siku nyingi, na hivyo basi wapo tayari kuomba taasisi ya utalii ya Saudi Arabia kushiriki pia.

Aliahidi kuwaomba Makonseli Wakuu wote washiriki.
Kongamano hilo limeandaliwa na Koseli Kuu ya Tanzania uliopo Dubai kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).

Wednesday, November 26, 2014

Watanzania kupata punguzo la asilimia 40 kwa matibabu katika Hospitali ya Irani iliyoko Dubai


Konseli Mkuu, Bw. Omar Mjenga wa Konseli Kuu ya Dubai kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Irani iliyopo Dubai (Iranian Hospital Dubai),  wakiweka saini makubaliano ya pamoja ambayo yatatoa punguzo la asilimia 40 ya matibabu kwa Mtanzania yeyote yule atakayetibiwa katika hospitali hiyo.  Makubaliano hayo yamewekwa saini katika hospitali ya Irani iliyopo Dubai, maeneo ya Jumeirah. 
Konseli Mkuu Omar Mjenga wa Tanzania, Dubai pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Irani, Dubai wakionyesha makubaliano mara baada ya kumaliza kutiliana saini.

Tuesday, November 25, 2014

Rais Kikwete apokea salamu za kheri toka kwa Rais Obama

Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mh. Liberata Mulamula akiwasilisha kwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete salamu za kumtakia afya njema kutoka kwa Rais wa Marekani Barack Obama leo jijini Baltimore, Maryland, Marekani.

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea kwa furaha na ujumbe kutoka Ubalozi wa Tanzania ulioko jijini Washington DC uliomtembelea kumjulia hali na kuwasilisha salamu maalumu za pole za Rais Barack Obama jijini Baltimore, Maryland.  
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Balozi Liberata Mulamula na ujumbe wake wa maafosa waandamizi wa ubalozi wa Tanzania nchini Marekani baada ya kupokea salamu maalumu za kumtakia kheri ya afya njema kutoka kwa Rais Barack Obama wa Marekani leo jijini Baltimore, Maryland, Marekani.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Balozi Liberata Mulamula na ujumbe wake wa maafosa waandamizi wa ubalozi wa Tanzania nchini Marekani baada ya kupokea salamu maalumu za kumtakia kheri ya afya njema kutoka kwa Rais Barack Obama wa Marekani leo jijini Baltimore, Maryland, Marekani.
Rais Prof. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mulamula na Maafisa Waandamizi wa Ubalozi Tanzania, nchini Marekani (Picha na Freddy Maro)

Friday, November 21, 2014

Waziri Membe azindua Chama cha Urafiki wa Tanzania na China

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akitoa hotuba ya uzinduzi wa  Chama cha Urafiki wa Tanzania na China. Hafla ya uzinduzi huo ilifanyika Jijini Dar es Salaam na kuhuduhuriwa na Mwenyekiti wa Chama hicho ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Dkt. Salim Ahmed Salim, Balozi wa China nchini, Mhe. Lu Yongqing na Viongozi wengine.
Mhe. Membe akihutubia.
Balozi wa China nchini, Mhe. Lu Yongqing akihutubia wakati wa hafla hiyo. 
Mwenyekiti wa Chama hicho Mhe. Salim nae akizungumza wakati wa hafla hiyo
Mhe. Membe kwa kushirikiana na Balozi Lu Yongqing wakizindua Chama hicho kwa mara nyingine.
Waziri Membe, Balozi Lu na Dkt. Salim pamoja na wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo.
Waziri Membe pamoja na Wageni waalikwa wakiinua glasi juu kutakiana heri

Waziri Membe akijadiliana jambo na Dkt. Salim
Hafla ikiendelea

WAZIRI MEMBE AWAASA WAHITIMU WA KIU KUTII SHERIA ZA NCHI

 Brass Band ya Jeshi la Magereza ikiwaongoza Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU), Kampasi ya Dar es Salaam , Rais Mstaafu, Mhe. Ali Hassan Mwinyi, mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe, Maafisa, Wahadhiri,Wahitimu pamoja na Wageni Waalikwa kuingia katika Viwanja vya Chuo Kikuu  hicho katika sherehe za Mahafali ya Kumi na Moja ya chuo hicho yaliyofanyika tarehe 21.11.2014.
  Mhe. Membe (mwenye joho la bluu) akiongozana na baadhi ya Wahadhiri kuingia katika viwanja yalikofanyika mahafali ya kumi na moja ya chuo kikuu cha Kimataifa cha Kampala Kampasi Dar es Salaam huko Gongo la Mboto.
 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Mhe. Ally Hassan Mwinyi  (mwenye kofia ya njano) akiwa pamoja na mgeni rasmi  Mhe. Membe (wa pili kutoka kushoto) wakiwa wamesimama kwa heshima ya Wimbo wa Taifa kama ishara ya kuanza kwa mahafali hayo ya kumi na moja.
 Shekhe Dr.Badruh H.Sseguja akifungua kwa sala Mahafali ya Kumi na Moja ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam tarehe 21.11.2014
  Mchungaji Ogah Ogbole akifungua kwa sala mahafali ya kumi na moja ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam tarehe 21.11.2014
 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala Profesa Mohamed Ndaula akitoa hotuba ya ufunguzi wa  mahafali hayo ya kumi na moja ya chuo hicho Jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wahitimu wa fani mbalimbali wa chuo kikuu cha kimataifa cha Kampala Kampasi ya Dar es Salaam wakiwa wamekaa kwa utulivu tayari kabisa kwa ajili ya sherehe za mahafali ya kumi na moja ya chuo hicho ambapo jumla ya wanafunzi 902 walihitimu masomo yao.
 Baadhi ya wakuu wa idara mbalimbali za Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala wakiingia katika viwanja vya chuo hicho Kampasi ya Dar es Salaam tayari kwa mahafali ya kumi na moja ya chuo hicho.
 Mkuu wa chuo kikuu cha kimataifa cha Kampala Mheshimiwa Ally Hassan Mwinyi akiwahutubia wahitimu wa mahafali hayo ya kumi na moja.
   Mgeni rasmi, Mhe. Bernard Membe akiwahutubia wahitimu wa mahafali hayo ya kumi na moja ambapo aliwaasa kwenda kufanya kazi kwa bidii na kutii sheria za nchi.
 Baadhi ya wahitimu wa chuo kikuu cha kimataifa cha Kampala wakinyanyua kofia zao juu mara baada ya kutunukiwa shahada zao katika mahafali yao ya kumi na moja ya chuo hicho.
 Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria mahafali hayo wakifuatilia hatua kwa hatua kile kinachoendelea katika sherehe hizo.
 Mkuu wa chuo kikuu cha kimataifa cha Kampala akitunuku shahada kwa wahitimu wa mahafali hayo.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Pili, Mhe. Ally Hassan Mwinyi ( mwenye joho la njano) akiwa pamoja na mgeni rasmi, Mhe. Membe pamoja na meza kuu wakiwa wamesimama kwa heshima ya wimbo wa taifa kama ishara ya kufunga mahafali hayo ya kumi na moja.


 Mgeni rasmi akizungumza na waandishi wa habari baada ya mahafali hayo.

PICHA NA Reuben Mchome
======================================

Membe Mgeni Rasmi Mahafali KIU

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe, amesema elimu imekomboa wanawake nchini Tanzania kwa kuwapa uwezo wa kushiriki sawa sawa na wanaume kwenye fursa za kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Mhe. Membe, ambaye alikuwa akihutubia kwenye mahafali ya 11 ya Chuo Kikuu cha Kampala (KIU), Jijini Dar es Salaam leo, aliwataka wanawake kutumia kikamilifu fursa za elimu ya juu ili wajitegemee kiuchumi na kuondokana kabisa na unyanyasaji wa kijinsia.

Alielezea kuridhishwa na uwezo ulioonyeshwa na wahitimu wa kike katika chuo hicho. Kati ya wahitimu 902 waliotunukiwa Shahada na Stashahada na Mkuu wa Chuo Kikuu hicho, Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, 423 ni wanawake.

Mhe. Membe aliwataka wahitimu hao watumie elimu yao vizuri katika kuiendeleza jamii na taifa, kufanya kazi kwa bidii na kutii sheria za nchi.