Wednesday, June 17, 2015

Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Mambo ya Nje aagana na aliyekuwa Mkurugenzi wa UNDP nchini

Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akimkabidhi Kitabu kinachoelezea Vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo nchini Mkurugenzi wa UNDP nchini, Bw. Philippe Poinsot, alipokuja kuaga mara baada ya kupata uhamisho wa kwenda kuwa Mratibu Mkazi wa UNDP nchini Moroco
Balozi Mushy akiwa katika mazungumzo na Bw. Philippe Poinsot mara baada ya kumkabidhi kitabu.
Balozi Mushy (wa nne kulia)  akiwa katika picha ya pamoja na Bw. Poinsot (wa nne kushoto) pamoja na Maafisa Mambo ya Nje wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa
Picha na Reginald Philip 

Katibu Mkuu Balozi Mulamula apokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Qatar nchini

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akipokea Nakala ya Hati za Utambulisho kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) kutoka kwa Balozi Mteule wa Qatar nchini Tanzania,  Mhe. Abdullah Jassim Mohamed Al Maadadi leo tarehe 17 Juni 2015.
Balozi Mulamula akiwa katika mazungumzo na Balozi Al Maadadi mara baada ya Balozi huyo kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati (wa kwanza kulia) Bw. Elibariki Maleko na Afisa Mambo ya Nje Bwa. Batholomeo Jungu wakisikiliza kwa makini mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea kati ya Balozi Mulamula na Balozi Mteule Mhe. Al Maadadi (hawapo pichani). 

Saturday, June 13, 2015

Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje amuaga Balozi wa Brazil aliyemaliza muda wa kazi nchini

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula kwa pamoja na Mkuu wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini ambaye pia ni Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mhe. Juma Halfan Mpango wakimsikiliza kwa furaha Balozi wa Brazil aliyemaliza muda wake wa kazi hapa nchini, Mhe.Francisco Suarez Luz (kushoto) kabla ya kuanza kwa hafla fupi ya chakula cha mchana iliyoandaliwa kwa ajili ya kumuaga Balozi Luz. Hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam tarehe 13 Juni, 2015.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mulamula kwa pamoja na Balozi Mpango wakiendelea kumsikiliza Balozi Luz mara baada ya kuketi tayari kwa kushiriki chakula cha mchana kwa heshima ya kumuaga Balozi Luz.
Meza Kuu wakiwemo Mabalozi kutoka nchi mbalimbali zenye uwakilishi hapa nchini
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mulamula akisoma hotuba kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) kwa ajili ya kumuaga Balozi wa Brazil aliyemaliza muda wake wa kazi hapa nchini, Mhe. Francisco Suarez Luz. Katika hotuba yake alimshukuru Balozi huyo kwa kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizi mbili katika kipindi chote alichokuwepo nchini na kumuomba aendelee kuwa Balozi mzuri kwa kuitangaza Tanzania.
Balozi Luz pamoja na Mablozi wengine wakimsikiliza Balozi Mulamula ambaye haonekani pichani
Balozi Luz nae akitoa hotuba yake ambapo aliisifu Tanzania kuwa ni nchi ya amani na kwamba nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika nyanja mbalimbali za maendeleo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mulamula pamoja na Mabalozi wengine wakimsikiliza Balozi Luz (hayupo pichani)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mulamula na Balozi Luz wakigonga glasi kama ishara ya kuutakia heri ushirikiano kati ya Tanzania na Brazil 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mulamula akimkabidhi Balozi Luz zawadi ya picha ya mchoro unaoonesha Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro kama kumbukumbu ya vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania. Anayeshuhudia ni Bi. Felister Rugambwa, Afisa Mambo ya Nje.
Sehemu ya Mabalozi wakishuhudia Balozi Luz akipewa zawadi (hayupo pichani)
Maafisa Mambo ya Nje nao wakifuatilia matukio wakati wa hafla ya kumuaga aliyekuwa  Balozi wa Brazil hapa nchini. Kushoto ni Bw. Leonce Bilauri na Bi. Felister Rugambwa
Balozi wa Namibia hapa nchini akiwa pamoja na Balozi wa Cuba nchini.
Balozi wa Urusi hapa nchini Mhe. Yuri Fedorovich Popov (kushoto) akimweleza jambo mmoja wa wageni waalikwa kwenye hafla ya kumuaga Balozi wa Brazil
Sehemu nyingine ya Wageni waalikwa


Waziri Membe awaaga Mawaziri wa nchin wanachama wa Umoja wa Afrika

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimtaifa, Mhe. Bernard Membe (Mb.) akisoma Hotuba ya kuwaaga Mawaziri wenzake katika mkutano wa Mawaziri wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa (watatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Mhe. Naimi Azizi (wa Nne kulia), Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia Balozi Dkt. Mohamed Maundi, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Afrika Bi. Zuhura Bundala pamoja na ujumbe alioambatana nao



Friday, June 12, 2015

Watanzania wengine 13 warejea kutoka nchini Yemen

Kiongozi wa msafara wa Watanzania kumi na tatu waliorejea leo nchini wakitokea nchini Yemeni, Bw.Faiz Abdulsheikh Said akizungumza na Mwakilishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi.Asha Mkuja wakati wa mapokezi ya Watanzania hao walipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa Shirika la Ndege la Qatar. Serikali imefanikiwa kuwarejesha nchini zaidi ya Watanzania 100  kutoka Yemen baada ya nchi hiyo kukumbwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe. Zoezi la kuwarejesha Watanzania hao linaratibiwa na kusimamiwa na Wizara kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Oman. Watanzania wengine 15 wanatarajiwa kuwasili nchini kesho tarehe 13 Juni, 2015.
Bi. Asha Mkuja akiendelea kupata maelezo kutoka kwa mmoja wa Watanzania hao Mzee Bader Saleh Omar kuhusu hali ilivyo nchini Yemen.
 Mazungumzo yakiendelea
 Mwakilishi wa Wizara ya Mambo ya Nje Bi.Asha akimsikiliza kwa makini mzee Bader, akimpa maelezo ya hali ilivyo huko Nchini Yemen.
 Watanzania hao wakijiandaa kuondoka ndani ya Uwanja wa Ndege baada ya kukamilisha taratibu zote.

Picha na Reuben Mchome

Wednesday, June 10, 2015

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje aongoza maadhimisho ya siku ya Taifa la Sweden

Mgeni rasmi kwenye sherehe ya Siku ya Taifa la Sweden, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye makazi ya Balozi wa Sweden hapa nchini. Mhe. Lennarth Hjelmaker (hayupo pichani).
Balozi wa Sweden hapa nchini, Mhe.Balozi Lennarth Hjelmaker akifungua hafla hiyo iliyofanyika usiku wa tarehe 09/06/2015 katika Makazi ya Balozi huyo Masaki Jijini Dar es Salaam.
 Balozi Lennarth akimkaribisha Balozi Mulamula katika hafla hiyo.
 Balozi wa Umoja wa Ulaya hapa nchini, Mhe. Filberto Cerian Sebregondi akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Liberata Mulamula huku Afisa wa Wizara hiyo Bi.Asha Mkuja (kushoto mwenye kilemba).
 Mkuu wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini ambaye pia ni Balozi wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hapa nchini Mhe.Balozi Juma Halifan Mpango akisalimiana na Balozi Liberata Mulamula.
 Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Balozi Mulamula (hayupo pichani)
Katibu Mkuu Mulamula akiendelea na hotuba yake,kushoto ni Balozi wa Sweden hapa nchini Mhe.Lennarth 
 Balozi Lennarth  na Katibu Mkuu Balozi Mulamula pamoja na wageni waalikwa wakinyanyua glasi kutakiana kheri katika ushirikiano wa nchi hizi mbili.
 Balozi wa Sweden Mhe.Lennarth  akicheza kwa furaha pamoja na wafanyakazi wa Ubalozi huo hapa nchini kama ishara ya kufurahia maadhimisho ya siku ya Taifa lao la Sweden sherehe zilizofanyika katika makazi ya balozi huyo Masaki Jijini Dar es Salaam.
Kikundi cha watoto wa Maafisa wa Ubalozi wa Sweden hapa nchini walioshiriki hafla hiyo kwa wakiimba kwa ufasaha nyimbo za Mataifa ya Sweden na Tanzania.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa   Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na     Waandishi wa abari katika hafla hiyo.

                            ===================
                          Picha na Reuben Mchome.

Tuesday, June 9, 2015

Balozi Mulamula akutana kwa mazungumzo na Ujumbe wa EU hapa nchini

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akimsikiliza Kiongozi wa Ujumbe wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) hapa nchini, Balozi Filberto Cerian Sebregondi alipofika Wizarani kwa mazungumzo kuhusu ushirikiano kati ya Jumuiya  hiyo na Tanzania na pia kujitambulisha kwa Balozi Mulamula ambaye ameteuliwa hivi karibuni kuwa Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje. 
Maafisa Mambo ya Nje Waandamizi wakifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Mulamula na Balozi Sebregondi (hawapo pichani).
Balozi wa Uingereza hapa nchini Mhe. Diana Melrose kwa pamoja na Balozi wa Ubelgiji hapa nchini, Mhe Adam Koeler na Maaafisa wengine  kutoka nchi za EU  wakifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Mulamula na Balozi Sebregondi.
Balozi Mulamula na Balozi  Sebregondi wakimsikiliza Balozi Melrose akifafanua jambo
Kikao kikiendelea

Picha na Reginald Philip

Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje azungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe. Balozi Linda Thomas - Greenfield alipotembelea Wizarani na kufanya mazungumzo yaliyojikita katika kukuza mahusiano kati ya Tanzania na Marekani katika Sekta mbalimbali.
Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Mark Childress pamoja na ujumbe ulioambatana na Mhe. Thomas - Greenfield nao wakifuatilia mazungumzo.
Balozi Linda akitoa ufafanuzi wa jambo huku Balozi Mulamula akimsikiliza kwa makini. 
Balozi Mulamula (katikati) akimsikiliza Mhe. Linda alipokuwa akizungumza naye kulia ni Afisa Mambo ya Nje Bwa. Lucas Mayenga. 
Mazungumzo yakiendelea
 Balozi Liberatta Mulamula akimlaki kwa furaha Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe. Balozi Linda Thomas - Greenfield wakati alipowasili na kufanya mazungumzo yaliyojikita katika kukuza mahusiano kati ya Tanzania na Marekani katika Sekta mbalimbali.


Picha na Reginald Philip.