Rais wa Zimbabwe Mhe. Emmerson Mnangagwa akizungumza na wafanyakazi pamoja na wanafunzi wanaosoma katika Chuo cha Kilimo na Mifugo cha Kaole (hawapo pichani). |
Friday, June 29, 2018
Ziara ya Rais Mnangagwa katika picha
Thursday, June 28, 2018
Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe Mh. Emmerson Mnangagwa afanya ziara nchini.
Ndege iliyombeba Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe Mhe. Emmerson Dambudzo Mnangagwa ikiwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es salaam, tarehe 28 Juni 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akimkaribisha mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe Mhe. Emmerson Dambudzo Mnangagwa mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Mhe. Rais Mnangagwa akiwapungia mkono wananchi waliofurika kumlaki katika uwanja wa ndege Dar es salaam.
Mhe. Rais Magufuli akiwa na mgeni wake Mhe. Rais Mnangagwa mara baada ya kukagua vikundi vya ngoma vilivyokuwa vikitumbuiza uwanjani hapo.
Wednesday, June 27, 2018
Katika picha; Taswira ya jengo la Kituo cha Kutoa Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) cha Tunduma
Mwonekano wa jengo la Tunduma OSBP kwa upande mbele (upande wa kuingilia) |
Mwonekano wa jengo la Tunduma OSBP kwa upande wa kuingilia |
Mwonekano wa jengo la Tunduma OSBP kwa upande wa kutokea (kuelekea Nakonde, Zambia) |
Mwonekano wa jengo la Tunduma OSBP kwa ndani |
Baadhi ya vifaa vya ujenzi vikiwa kazini. |
Kamati ya ujenzi wa Tunduma OSBP ikiwa kwenye kikao cha kutathimini maendeleo ya ujenzi kilichofanyika katika moja ya ukumbi wa mikutano uliopo kwenye jengo hilo hivi karibuni. |
Kamati ya ujenzi ikitembelea sehemu ya eneo la kuegesha magari ambalo ujenzi wake bado unaendelea |
Kamati ya ujenzi ikiangalia maendeleo ya ujenzi wa ghala la kuhifadhia bidhaa katika kituo hicho. |
Mradi wa ujenzi wa Kituo cha Kutoa Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) cha Tunduma, mpaka kati ya Tanzania na Zambia umekamilika kwa takribani 95%.
Ujenzi wa Kituo hiki unatarajiwa kuboresha mazingira ya biashara baina ya nchi hizi mbili (Tanzania/Zambia).
Ujenzi wa mradi huu ulioanza mwaka 2016 umechukua ukubwa wa eneo linalokadiriwa kuwa na takriban kilomita za mraba 43,000.
Ujenzi wa mradi huu unafadhiliwa na shirika la TradeMark East Afrika.
Mkutano wa 16 wa Majadiliano ya Kisiasa kati ya Tanzania na Korea Kusini wafanyika jijini Dar
Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Astralasia Bibi Yusta Nyange (wa pili kutoka kushoto) akifurahia jambo kwenye majadiliano ya 16 ya Kisiasa kati ya Tanzania na Jamhuri ya Korea, yaliyofanyika tarehe 27 Juni 2018 , katika ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere(JNICC), Dar es salaam.
Wengine katika picha ni Maafisa kutoka Wizarani Emmanuel Luangisa(wa mwisho kulia), Ramla Hamisi(wa kwanza kulia) na anayefuata ni Bi Blandina Kasagama wakifuatilia majadiliano hayo.
Pamoja na mambo mengine majadiliano hayo yalijikita katika kuzungumzia namna ya kuimarisha mahusiano yaliyopo kati ya Tanzania na Korea katika maeneo mbalimbali.
Mkutano ukiendelea
Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika na Mashariki ya Kati, Bw. KOH Kyung-sok(wa pili kushoto), akiwa na ujumbe wake kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea na Ubalozi wa Korea nchini wakiwa katika majadiliano hayo.
Bibi Yusta Nyange(kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Bw.
KOH Kyung-sok baada ya Mkutano.
KOH Kyung-sok baada ya Mkutano.
Bibi Yusta Nyange(kulia) akimkabidhi zawadi Bw. KOH Kyung-sok baada ya Mkutano.
Picha ya Pamoja baada ya Mkutano
RAIS WA ZIMBABWE ZIARANI NCHINI
Taarifa kuhusu ziara ya Rais wa Zimbabwe nchini
Mheshimiwa Emmerson Dambudzo Mnangagwa, Rais wa
Jamhuri ya Zimbabwe atafanya ziara ya kitaifa nchini Tanzania tarehe 28 hadi 29
Juni, 2018. Hii itakuwa ziara ya kwanza ya Mheshimiwa Rais Mnangagwa nchini
Tanzania tangu aingie madarakani mwezi Novemba, 2017.
Lengo la ziara hii ya Rais wa Zimbabwe ni
kujitambulisha kwa Rais na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tangu
aingie madarakani, Mheshimiwa Rais Mnangagwa ameshafanya ziara katika nchi za
Namibia, Zambia, Msumbiji, Angola, Afrika Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo na Botswana.
Ziara hii ni muhimu kwa Tanzania kwani itatoa fursa
ya kuimarisha na kukuza zaidi mahusiano mazuri yaliyopo ya kidiplomasia,
kihistoria, kiuchumi na kijamii kati ya nchi hizi mbili. Ziara hii pia itatoa
fursa kwa viongozi wetu kujadili masuala mbalimbali yanayohusu nchi hizi mbili
ya kikanda na kimataifa.
Wakati wa ziara hiyo, Mhe. Rais Mnangagwa atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais Mnangagwa anatarajiwa
pia kutembelea Chuo cha Kilimo cha Wazazi Kaole Bagamoyo ambacho awali kilitumika
kutoa mafunzo kwa wapigania uhuru kutoka nchi za Kusini mwa Bara la Afrika na
Mhe. Rais Mnangagwa ni miongoni mwa waliopata mafunzo katika chuo hicho.
Mhe.
Rais Mnangagwa anatarajiwa kuondoka tarehe 29 Juni 2018 kurejea chini Zimbabwe.
-Mwisho-
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam, 27 Juni, 2018
Tuesday, June 26, 2018
Balozi Migiro azindua rasmi Jumuiya ya Watanzania waishio Uingereza-ATUK
Mhe. Balozi Migiro akifurahia jambo na sehemu ya Watanzania walioshiriki uzinduzi huo |
Sehemu ya Watanzania na wageni waalikwa waliohudhuria tukio hilo la kihistoria |
===================================================
UZINDUZI WA ASSOCIATION OF TANZANIANS IN
THE UK – ATUK
Mhe. Dkt.
Asha-Rose Migiro, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, alikuwa mgeni rasmi
kwenye sherehe za uzinduzi wa Jumuiya Mwamvuli ya Watanzania waishio nchini
Uingereza na Ireland ya Kaskazini iitwayo ATUK –Association
of Tanzanians in the UK zilizofanyika mjini Reading tarehe 23
Juni, 2018. Jumuiya hii inatokana na muungano wa jumuiya za diaspora kutoka
mikoa mbalimbali ya hapa Uingereza na wanachama wa kujitegemea.
Wajumbe
wa Kamati ya Muda iliyoratibu kuanzishwa kwa ATUK walipongeza
na kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli za
kupambana na ufisadi, kusimamia uwazi na uwajibikaji katika utumishi wa umma na
kuongeza kasi ya kujenga uchumi wa viwanda. Kauli mbiu ya hafla hii ilikuwa
“UMOJA NI NGUVU, TANZANIA YA VIWANDA INAWEZEKANA”. Hivyo mojawapo ya malengo ya
kuanzishwa kwa ATUK ni kujenga umoja na kukusanya nguvu za kuchangia jitihada
za kujenga uchumi wa viwanda nchini mwetu.
Akihutubia
hadhara hiyo Balozi Migiro aliwapongeza ATUK na
alihimiza umoja na kukumbusha kwamba wakati wote Mhe. Rais amekuwa akisisitiza
umoja wa Watanzania bila kujali tofauti zao kwani umoja ni nyenzo muhimu ya
kujiteletea maendeleo. Hivyo Balozi Migiro aliwashukuru kwa Muungano huo na
kueleza kwamba wakiendeleza mshikamano wataweza kuchangia kwa
ufanisi jitihada kubwa za Mhe. Rais Magufuli na Serikali ya Awamu ya
Tano katika kuwaletea maendeleo Watanzania wote.
Katibu Mkuu akutana na wadau mbalimbali kutoka Serikalini na Taasisi za Umoja wa Mataifa kujadili SDGs.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Aldof Mkenda akisistiza jambo wakati wa ufunguzi wa Mkutano kati ya Serikali na Umoja wa Mataifa na Taasisi zake kujadili utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu. Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC), Dar es Salaam, Tarehe 26 Juni2018.
Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Dunia(SDGs) yako 17 yenye shabaha 169 na Viashiria 232, malengo hayo yanatekelezwa kwa pamoja na Jumuiya ya Kimataifa kwa kushirikisha kila sekta na utekelezaji wake unahimiza ushiriki wa kila kundi kwenye jamii.
Katibu Mkuu Prof. Mkenda( wa pili kushoto), Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Prof. Faustine Kamuzora, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (mwisho kulia) na wa mwisho kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Bw. Alvaro Rodriguez, wakifuatilia majadiliano ya Mkutano huo.
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akielezea malengo ya Mkutano huo.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Bw. Alvaro Rodriguez, akitoa taarifa ya ufunguzi kwa upande wa Umoja wa Mataifa.
Sehemu ya washiriki wakifuatilia mkutano huo.
Wa pili kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar na washiriki wengine kutoka Serikalini walioshiriki katika mkutano huo.
Sehemu ya Maafisa kutoka Wizarani wakifuatilia mkutano huo.
Katibu Mkuu Prof. Mkenda akiwaelezea wanahabari kuhusu mpira uliondikwa Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ya Dunia, aliokabidhiwa na Bw. Rodriguez kuashiria utekelezaji wa malengo hayo kwa kasi na kuzingatia Muktadha wa mazingira ya Tanzania.
Picha ya pamoja baada ya mkutano.
Waziri Mahiga akutana kwa pamoja na Balozi wa Uingereza na Kaimu Balozi wa Marekani nchini
Dkt. Mahiga akisalimiana na Mhe. Balozi Cooke. |
Dkt. Mahiga akimsikiliza Mhe. Balozi Cooke alipokuwa akimweleza jambo wakati wa mazungumzo yao |
Mkutano ukiendelea. |
Monday, June 25, 2018
Washindi wa TBL watembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi
Balozi Mumwi akifanya mazungumzo na washindi hao. |
Subscribe to:
Posts (Atom)