Wednesday, November 21, 2018

Wawekezaji kutoka Uturuki wajionea fursa za uwekezaji jijini Dodoma



Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Bw. Godwin Kunambi akitoa taarifa ya fursa za uwekezaji zinazopatikana jijini Ddodma kwa wafanyabiashara wakubwa kutoka Uturuki ambao wameonesha dhamira ya kuwekeza katika jiji hilo. Fursa zilizoelezwa ni pamoja na ujenzi wa mahoteli yenye hadhi ya nyota tano, ujenzi wa maduka makubwa (shopping malls), masoko makubwa, shule za kimataifa na nyumba za kuishi. Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Mamlaka ya Maji safi na Maji Taka Dodoma (DOWASA walikuwepo kuwahakikishia wawekezaji hao kuwa nishati ya umeme na maji sio tatizo jijini Dodoma. wawekezaji hao wamekuja kufuatia jitihada zinazofanywa na Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo.  


Awali Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Bw. Maduka Kessy alifungua mkutano kikao hicho kwa kuwahahakishia wawekezaji hao ushirikiano unaohitajika ili dhamira yao iweze kutimia.
Sehemu ya wawekezaji hao wakimsikiliza kwa makini Bw. Kunambi.
Wawekezaji wakimsikiliza kwa makini Bw.  Kunambi aliyekuwa akielezea maeneo mbalimbali ya uwekezaji katika jiji la dodoma.
Juu na Chini ni Sehemu ya watumishi wa Serikali na Ofisi ya Mkurugenzi wa jiji wakimsikiliza Bw. Kunambi.

Wawekezaji kutoka Uturuki walipata fursa ya kuuliza maswali mbali mbali mara baada ya kupata maelezo juu ya maeneo mbalimbali ya uwekezaji katika Mkoa wa Dodoma.


Majadiliano yakiendelea wakati wa mkutano.
Wawekezaji walipata fursa ya kutembelea kwenye maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji katika jiji la Dodoma.
Wawekezaji kutoka Uturuki wakipata maelezo ya ramani ya eneo la uwekezaji kutoka kwa Mchumi na Mratibu wa Maswala ya Uwekezaji katika Halmashauri ya jiji, Bw. Abel Msangi.
Hili ndio eneo la uwekezaji lililotembelewa na wawekezaji hao kutoka uturuki.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Bw. Maduka Kessy akiwaelezea jambo Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya, Bw. Jestas Nyamanga pamoja na Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Bw. Godwin Kunambi
Wawekezaji kutoka Uturuki wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wao.













Monday, November 19, 2018

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje akutana na Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania, Perth pamoja na Balozi wa Kenya nchini

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza na Konseli wa Heshima wa Tanzania kwenye Jimbo la Perth nchini Australia, Bw. Didier Murcia alipofika kwenye Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam tarehe 19 Novemba, 2018 kwa lengo la kujitambulisha kwa Mhe. Naibu Waziri  pamoja na kumweleza utekelezaji wa majukumu yake katika kuiwakilisha Tanzania, Perth. 

Ujumbe uliofuatana na Bw. Murcia. Kutoka kushoto ni Bw. James Chialo na Bw. Thierry Murcia kutoka Kampuni ya Ndovu Resources ya jijini Dar es Salaam

Bw. Murcia akimweleza jambo Mhe. Dkt. Ndumbaro wakati wa mazungumzo yao

Mazungumzo yakiendelea. Kulia ni Katibu wa Mhe. Naibu Waziri, Bw. Charles Faini.



..........................Mkutano kati ya Naibu Waziri na Balozi wa Kenya nchini


Wakati huohuo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro alikutana kwa mazungumzo na Balozi wa Kenya nchini, Mhe. Dan Kazungu. Mazungumzo hayo yalifanyika kwenye Ofisi ndogo za Wizara zilizopo jijini Dar es Salaam tarehe 19 Novemba 2018. Pamoja na mambo mengine walizungumzia namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizi mbili hususan kupitia Jumuiya ya Afrika Mashariki. Pia Balozi Kazungu alitumia fursa hiyo kumweleza Mhe. Naibu Waziri kuhusu Mkutano wa Kimataifa kuhusu  Rasilimali Endelevu za Majini utakalofanyika nchini Kenya kuanzia tarehe 26 hadi 28 Novemba 2018

Katibu wa Naibu Waziri, Bw. Charles Faini (kushoto) akiwa na Bw. Medard Ngaiza, Afisa Mambo ya Nje wakifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Dkt. Ndumbaro na Mhe. Balozi Kazungu ambao hawapo pichani

Mhe. Balozi Kazungu akimweleza jambo Mhe. Dkt. Ndumbaro wakati wa mazungumzo yao

Mhe. Balozi Kazungu akimkabidhi Mhe. Dkt. Ndumbaro moja ya nyaraka kuhusu Mkutano wa Kimataifa wa Rasilimali Endelevu za Majini utakaofanyika nchini Kenya.

Mhe. Dkt. Ndumbaro akiagana na Balozi Kazungu mara baada ya mazungumzo kati yao

Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje akutana na Balozi wa Namibia nchini



Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi akisalimiana na Balozi wa Namibia nchini, Mhe. Theresa Samaria alipofika Wizarani kwa ajili ya kumsalimia na  kuzungumzia kuhusu kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Namibia kwenye sekta mbalimbali ikiwemo biashara, kilimo, uvuvi na mifugo. Mazungumzo hayo yamefanyika tarehe 19 Novemba, 2018.
Mhe. Balozi Samaria akimweleza Dkt. Kasidi kuhusu fursa mbalimbali za biashara ambazo Tanzania inaweza kuzichangamkia kwenye nchi yake ambayo ina ukame uliokithiri kutokana na kuzungukwa na Majangwa ya Kalahari na Namib. Fursa hizo ni pamoja na biashara ya nyama, matunda, nafaka mbalimbali na korosho.
Mazungumzo yakiendelea huku Afisa aliefuatana na Balozi Samaria akinukuu
Katibu Mkuu, Dkt. Kasidi akisoma nyaraka aliyopatiwa na Balozi Samaria ambayo ni mkataba ulioanzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Namibia miaka 20 iliyopita. 

Dkt. Kasidi akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi Samaria mara baada ya kumaliza mazungumzo yao


Piacha ya pamoja kati ya Dkt. Kasidi na Balozi Samaria pamoja na  Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Ubalozi wa Namibia nchini walioshiriki mazungumzo kati ya viongozi hao 


Wawekezaji kutoka Uturuki wajipanga kuja kuwekeza nchini mwakani


Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo akifungua mkutano kati ya ujumbe kutoka Makampuni 7 makubwa ya Uturuki na  wadau muhimu wa masuala ya uwekezaji  jijini Dar es Salaam ambao  ni Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Chama cha Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Wakulima (TCCIA), Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji Tanzania (EPZA), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). Katika mkutano huo ambao ulifanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) tarehe 19 Novemba 2018, Prof. Kiondo alieleza kuwa wawekezaji hao kutoka Uturuki wana nia ya dhati ya kuwekeza hapa nchini kwa kuanzia na mikoa ya Dodoma na Simiyu katika sekta za viwanda vya nguo, uongezaji thamani bidhaa za kilimo, ujenzi wa maduka makubwa ya biashara na ujenzi wa hoteli za kimataifa.
Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mhe. Ali Davutoglu nae alitumia fursa hiyo kuwahakikishia wawekezaji hao mazingira rafiki ya uwekezaji yaliyopo hapa nchini kutokana na uzoefu wake wa kuwepo nchini.
Sehemu ya ujumbe kutoka Makampuni hayo ya Uturuki wakifuatilia mkutano. Kulia ni kiongozi wa msafara wa wawekezaji hao Bw.Cengiz Ertas
Sehemu nyingine ya wawekezaji hao kutoka Uturuki


Mkutano ukiendelea

Sehemu ya wadau kutoka sekta muhimu za Tanzania nao wakifuatilia mkutano huo

Afisa kutoka TIC, Bi. Diana Ladislaus akiwasilisha mada kuhusu Uwekezaji nchini Tanzania kwa wawekezaji hao kutoka Uturuki

Wadau wakifuatilia kwa makini mada ya uwekezaji iliyokuwa ikiwasilishwa

Wadau kutoka sekta mbalimbali za Tanzania ikiwemo EPZA, TCCIA, TANESCO nao wakifuatilia mkutano

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bw. Jestas Nyamanga (katikati) nae akiwa kwenye mkutano huo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa TIC, Bw. John Mnali

Bw. Nyamanga nae akichangia jambo wakati wa mkutano huo ambapo aliwakaribisha wawekezaji hao nchini

Kiongozi wa Msafara wa Wawekezaji hao, Bw. Cengiz Ertas nae akizungumza na kueleza nia yao ya kuja kuwekeza nchini ambapo alisema kwa ujumla wametenga kiasi cha Dola za Kimarekani milioni 100 kwa ajili ya uwekezaji huo ambao wanatarajia kuuanza mwaka 2019. Pia alieleza kufurahishwa na taarifa kuhusu mazingira mazuri ya uwekezaji hapa nchini.


Mwakilishi kutoka TPSF akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kwa wawekezaji hao
Mhe. Prof. Kiondo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mkutano na wawekezaji hao. Kulia ni Balozi wa Uturuki nchini, Mhe. Davutoglu.
Bw. Nyamanga (katikati) na Bw. Mnali (kulia) wakimsikiliza Mhe. Prof. Kiondo (hayupo pichani) akizungumza na waandishi wa habari


Picha ya pamoja
Mhe. Balozi Ali Davutoglu akisalimiana na Bw. Hassani Mwamweta, Afisa Mambo ya Nje mara baada ya mkutano kati ya wadau muhimu wa uwekezaji wa hapa nchini na ujumbe wa Makampuni ya uwekezaji kutoka Uturuki


Wakati huohuo wawekezaji hao wakiongozwa na Balozi Ali Davutoglu walihudhuria maadhimisho ya miaka 30 ya TCCIA yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam

Wadau kutoka Uturuki na Tanzania kwenye maadhimisho ya miaka 30 ya TCCIA

Kina mama ambao walikuwepo kwenye maadhimisho hayo

Dkt. Mahiga amwakilisha Mhe. Rais Magufuli katika Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa AU

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Dkt. Mahiga amwakilisha Mhe. Rais Magufuli katika Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa AU

Mhe. Augustine P. Mahiga (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alimwakilisha Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Mkutano Maalum wa 11 wa Wakuu Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika uliyofanyika tarehe 17-18 Novemba, 2018 mjini Addis Ababa, Ethiopia. Mkutano huo, uliitishwa kufuatia maamuzi ya Mkutano wa 31 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika uliofanyika mwezi Julai 2018 mjini Nouakchott, Mauritania ambapo Wakuu hao walielekeza uitishwe Mkutano Maalum kujadili kwa kina mabadiliko ya kitaasisi ndani ya Umoja huo.

Mkutano huo ulijadili na kutolea maamuzi mapendekezo kuhusu Muundo wa Uongozi (Portfolios) za Kamisheni za Umoja wa Afrika; chaguzi za Uongozi wa Kamisheni; Kusitisha ajira za viongozi wa Kamisheni; na Mabadiliko ya kiutawala na fedha ikijumuisha utendaji.
Mkutano ulikubaliana kupunguza idadi ya wajumbe wa Kamisheni klutoka 10 hadi 8 ambao ni Mwenyekiti wa Kamisheni, Makama Mwenyekiti na Makamishna 6. Maamuzi hayo yataanza kutekelezwa mwaka 2021 baada ya uongozi wa Kamisheni uliopo sasa kumaliza muda wake. Maamuzi yote yaliyotolewa yalilenga kuboresha utendaji wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika.

Mhe. Waziri aliungana na viongozi wengine waliochangia katika mjadala wa kuboresha utendaji wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika kwa kuunga mkono mabadiliko ya kitaasisi katika Umoja huo. Mhe. Waziri alieleza kwamba maamuzi hayo yanalenga kuleta ufanisi kwenye kutekeleza majukumu ya Kamisheni na kuhakikisha Afrika inapata maendeleo inayostahili haswa kwa kuzingatia Agenda 2063 ya Umoja wa Afrika.

Katika Mkutano huo Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Mhe. Paul Kagame alitoa salamu za rambirambi kwa Serikali za Tanzania, DRC na Malawi kufuatia vifo vya walinda amani wa nchi hizo nchini DRC.
Mhe. Waziri alimshukuru Mhe. Kagame kwa salamu hizo za rambirambi na kuahidi kwamba Tanzania itaendelea kuwa mstari wa mbele kupigania amani ya kudumu barani Afrika.

Mkutano pia ulijadili Mamlaka ya Wakala wa Maendeleo ya Umoja wa Afrika (African Union Development Agency - AUDA). Mkutano ulifahamishwa kuwa mchakato wa kubadilisha Taasisi ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Uchumi (New Economic Partnership for Africa’s Development – NEPAD) kuwa AUDA utakamilika Februari 2019 kama inavyoelekezwa katika Maaumuzi ya Umoja wa Afrika Na. 691. Mkutano ulikubaliana na mapendekezo yote kuhusu Mamlaka ya AUDA na kwamba programu na miradi ya AUDA itafadhiliwa kupitia bajeti ya Umoja wa Afrika na misaada ya washirika wa maendeleo.

Agenda nyingine iliyojadiliwa wakati wa mkutano huo ni mabadiliko katika Taasisi ya Mchakato wa Kujitathimini kiutawala Bora Africa (African Peer Review Mechanism - APRM), ambapo mapendekezo yalitolewa ya kuiunganisha APRM kuwa moja ya taasisi za Umoja wa Afrika na kugharamia shughuli zake kwa kutumia bajeti ya Umoja huo. Aidha, iliamuliwa kuwa Wanachama wote wa Umoja wa Afrika wawe Wanachama wa APRM na APRM iwe huru katika kutekeleza majukumu yake.

Agenda nyingine kuu iliyojadiliwa na kutolewa maamuzi ni mapendekezo ya makadirio mapya ya viwango vya kuchangia Umoja wa Afrika na mapendekezo ya adhabu kwa Nchi ambazo zitachelewa kulipa michango yake. Mkutano uliazimia kuitishwa kwa Mkutano kati ya Kamati ya Kudumu ya Mabalozi, Wataalam wa masuala ya Fedha kutoka nchi wanachama na Kamati ya Mawaziri wa Fedha kupitia makabrasha yote yanayohusu Viwango vya kuchangia na adhabu kwa nchi ambazo hazitoa michango yao kwa wakati. Mkutano huo, unatarajiwa kufanyika tarehe 28-29 Novemba, 2018, Addis Ababa, Ethiopia na mapendekezo ya wataalam yatawasilishwa kwenye Kikao kijacho cha Baraza la Mawaziri mwezi Februari 2019.

Mkutano pia ulipokea mapendekeo ya mgawanyiko wa majukumu kati ya AU, Jumuiya za Kikanda na Nchi Wanachama. Mgawanyo wa majukumu unapendekezwa kuwezesha Jumuiya za Kikanda, Umoja wa Afrika na Nchi Wanachama kila moja kutekeleza majukumu yake na yale ambayo watachangia kwa pamoja.

Pembezoni mwa Mkutano huho wa Dharura Wakuu wa Nchi na Serikali walizindua Mfuko wa Amani wa Umoja wa Afrika (AU Peace Fund) ambao utashughulikia masuala yote ya Amani na Usalama katika Nchi Wanachama  ikiwemo viashiria vya uvunjifu wa Amani ili kuzuia kuibuka kwa migogoro. Mhe. Waziri alishiriki katika uzinduzi huo.
                                                      -Mwisho-
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma, 19 Novemba 2018
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa, Ethiopia. Nyuma yake ni Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Mhe. Bi. Naimi Aziz.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Rais Mpya wa Ethiopia, Mhe. Sahle Work Zewdu katika Ikulu ya nchi hiyo tarehe 18 Novemba 2018. Dkt. Mahiga alikwenda kumpongeza Mhe. Rais kwa kuteuliwa na wote wawili walisisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Ethiopia.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga. (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia, Mhe. Dkt Workneh Gebeyehu alipokwenda kumtembelea kwa ajili ya kufahamiana jijini Addis Ababa.