Wednesday, June 12, 2019

Prof. Kabudi aviomba vyombo ya habari kuelimisha umma kuhusu SADC




Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akizungumza na Wamiliki na  Wakuu wa Vyombo vya Habari nchini katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere leo. Prof. Kabudi aliwaeleza Wamiliki na Wakuu wa Vyombo vya Habari kuhusu Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika nchini mwezi Agosti 2019. Prof. Kabudi aliwasihi Wakuu hao kushirikiana na Serikali hususan katika kueleimisha umma kuhusu SADC pamoja na kutoa elimu kwa wafanaybiashara na wananchi kwa ujumla kuhusu fursa za mkutano huo za zile zinazopatikana katika nchi wanachama wa SADC. 

Msemaji wa Serikali na Mkurugenzi wa Habari katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbas akitoa neno katika mkutano huo kabla ya kumkaribisha Prof. Kabudi azungumze na Wamiliki na Wakuu wa Vyombo vya Habari nchini. Dkt. Abbas alimuhakikishia Mhe. Waziri kuwa namna anavyovijua vyombo vya habari vya hapa nchini vinavyofanya kazi hana shaka yoyote kuhusu kutoa ushirikiano wao.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akisisitiza jambo kwa Wamiliki na Wakuu wa Vyombo vya Habari.
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Mhe. Paul Makonda akiongea na Wamiliki na Wakuu wa Vyombo vya Habari nchini. Mhe. Makonda alisema kuwa mkoa wa Dar Es Salam umejipanga kupokea ugeni mkubwa wa mkutano wa SADC ambao unakadiriwa utahudhuriwa na watu zaidi ya 1000 kutoka nchi 16 wanachama wa SADC.
Meza Kuu kutoka kulia ni Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini, Bw. Henry Mwanika, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Bi. Agnes Kayola, Waziri Prof. Kabudi, na Dkt. Abbas.
Baadhi ya Wamiliki na Wakuu wa Vyombo vya Habari nchini walioshiriki katika kikao cha Waziri. Mwenye tai nyekundu ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania, Dkt. Ayoub Rioba.
Mkutano wa Wamiliki na Wakuu wa Vyombo vya habari na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ukiendelea
Wakongwe wa tasnia ya Habari nchini ambao walikuwa walimu wa Mhe. Waziri katika fani hiyo.
Picha ya Pamoja kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wamiliki na Wakuu wa Vyombo vya Habari nchini.



VACANCY ANNOUNCEMENT AT THE COMMONWEALTH SECRETARIAT


PRESS RELEASE


VACANCY ANNOUNCEMENT AT THE COMMONWEALTH SECRETARIAT

The Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation has received vacancy notification from the Commonwealth Secretariat inviting qualified Tanzanians to apply for the post of Adviser, Service Delivery and Reporting.

Application details can be found through the Secretariat’s website, http://thecommonwealth.org/jobs. Closing date for application is Tuesday 18th June 2019.

“The Ministry encourages qualified Tanzanians to apply”.

Issued by;
Government Communication Unit,
Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation,
Dodoma.
12th June 2019.


Tuesday, June 11, 2019

ZOEZI LA KUPIMA UTAYARI KUKABILI MAGONJWA YA MLIPUKO MIPAKANI LA ZINDULIWA

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalim (katikati), Waziri wa Viwanda wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Adan Abdulla Mohammed pamoja na Mhe. Cristophe Bazivambo kwa pamoja wakionyesha vitabu vinavyoelezea Umuhimu wa kufungua zoezi la Kupima Utayari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kukabiliana na magonjwa ya mlipuko mipakani. Uzinduzi huo umefanyika Namanga Mpakani mwa Tanzania na Kenya tarehe 11 Juni, 2019  
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalim akihutubia kwenye ufunguzi wa zoezi la Kupima Utayari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kukabiliana na magonjwa ya mlipuko mipakani, ambapo amesisitiza umuhimu wa Sekta za Afya kutumia Dhana ya Afya moja, wakati  akifungua zoezi hilo.  

 

Sehemu ya Viongozi kutoka Upande wa Kenya wakimsikili kwa makini Mhe. Mwalim
Waziri wa Viwanda wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Adan Abdulla Mohammed naye akihutubia kwenye ufunguzi huo. 


 Juu na chini ni wageni walio hudhuria ufunguzi wa zoezi hilo

Mhe. Mwalim, Mhe. Mohammed pamoja na Mhe. Ulega wakitiza na kupama maelezo kutoka kwa mtaalamu wa kukabiliana na Magonjwa ya Mlipuko


 Juu na Chini Mawaziri hao walitembelea vituo vya Kutolea Huduma kwa pamoja (OSBP) vilivyopo Namanga mpakani mwa Tanzania na Kenya.

Prof. Kabudi afanya mazungumzo na Waziri wa Viwanda na masuala ya Afrika Mashariki wa Sudan Kusini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba John Kabudi akisalimiana na Waziri wa Viwanda, Biashara na masuala ya Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Sudan Kusini, Mhe. Paul Mayom Akech kabla ya kuanza mazungumzo yao. Mazungumzo hayo yamefanyika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam tarehe 11 Juni 2019.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba John Kabudi akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mazungumzo kati yake na Waziri wa Viwanda, Biashara na masuala ya Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Sudan Kusini, Mhe. Paul Mayom Akech (kushoto). Mazungumzo hayo yamefanyika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam  tarehe 11 Juni 2019.
Waziri wa Viwanda, Biashara na masuala ya Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Sudan Kusini Mhe. Paul Mayom Akech, akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) baada ya mazungumzo kati yake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.  Profesa Palamagamba John Kabudi. Mazungumzo hayo yamefanyika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam tarehe 11 Juni 2019.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Profesa Palamagamba John Kabudi (katikati) akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mazungumzo kati yake na  Waziri wa Viwanda, Biashara na Masuala ya Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Sudan Kusini Mhe. Paul Mayom Akech (kushoto). Kulia Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaack Kamwelwe. Mkutano huo ulifanyika katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam tarehe 11 Juni  2019.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.  Profesa Palamagamba John Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Mhe. Paul Mayom Akech,Waziri wa Viwanda,Biashara na Masuala ya Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Sudan Kusini. Kushoto kwa Profesa Kabudi ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaack Kamwelwe akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe. Mazungumzo ya viongozi hao yalifanyika katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam tarehe 11 Juni 2019.

Washiriki wa Mafunzo kutoka NDC wafanya ziara ya mafunzo nchini India

Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda (kushoto) akimkaribisha Ubalozini Brig. Jenerali Chestino Msola, Kiongozi wa Ujumbe wa Washiriki wa Mafunzo kutoka Chuo cha Ulinzi cha Taifa (NDC) walipotembelea ubalozini hapo wakati wa ziara yao ya mafunzo ya siku tano nchini humo iliyoanza tarehe 10 Juni 2019.
Mhe. Balozi Luvanda (kushoto) akizungumza na Brid. Jenerali Msola (mwenye sare za jeshi za rangi ya kijani) pamoja  na viongozi wengine wa ujumbe wa washiriki wa mafunzo kutoka Chuo cha Ulinzi cha Taifa (NDC) walipotembelea Ubalozi wa Tanzania nchini India wakati wa ziara yao ya mafunzo nchini humo. Kulia ni Comodore Michael Mumanga na Dkt. Lucy Shule, Mkurugenzi wa  Mafunzo wa NDC.
Mhe. Balozi Luvanda akizungumza na ujumbe wa washiriki wa mafunzo (hawapo pichani) kutoka Chuo cha Ulinzi cha Taifa (NDC) walipotembelea Ubalozi wa Tanzania nchini India wakati wa ziara yao ya mafunzo nchini humo. 
Mhe. Balozi Luvanda akiendelea na mazungumzo na ujumbe huo kutoka NDC
Mhe. Balozi Luvanda akipokea zawadi ya ukumbusho (memento) kutoka kwa Brig. Jenerali Msola
Mhe. Balozi Luvanda akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa ujumbe wa washiriki wa mafunzo kutoka Chuo cha Ulinzi cha Taifa (NDC) walipotembelea Ubalozi wa Tanzania nchini India wakati wa ziara yao ya mafunzo nchini humo. 
Mhe. Balozi Luvanda akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wote.

Wednesday, June 5, 2019

Maandalizi Ya Mkutano Wa Jumuiya Ya Maendeleo Ya Nchi Za Kusini Mwa Afrika (SADC) Yaanza

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akisalimiana na Katibu Mtendaji wa wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC, Dkt Stagomena Tax kabla ya kuanza kikao cha awali cha mashauriano kuhusu mkutano wa SADC unaotarajiwa kufanyika Nchini Tanzania August,2019. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar Es Salaam, June 05,2019
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) (katikati) akishauriana jambo na Katibu Mtendaji wa wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC Dkt. Stagomena Tax (kulia) wakati wa kikao cha awali cha mashauriano kuhusu mkutano wa SADC unaotarajiwa kufanyika Nchini Tanzania August,2019,kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Mnyepe.Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar Es Salaam, June 05,2019
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) (katikati) akimsikiliza Katibu Mtendaji wa wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC Dkt. Stagomena Tax (kulia) wakati wa kikao cha awali cha mashauriano kuhusu mkutano wa SADC unaotarajiwa kufanyika Nchini Tanzania August,2019,kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Mnyepe.Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar Es Salaam, June 05,2019
Maafisa wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC walioambatana na Dkt. Stagomena Tax wakisikiliza kwa makini mkutano huo.
Sehemu ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo nao wakifuatilia kwa makini, katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Grace Martine, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Stephen Mbundi na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje Bi. Agness Kayola. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi (Mb) (katikati) akiongoza  kikao cha awali cha mashauriano kuhusu mkutano wa SADC unaotarajiwa kufanyika Nchini Tanzania August,2019.Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar Es Salaam, June 05,2019


Prof. Kabudi azungumza na Idara ya Itifaki ya Wizara yake.

Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akizungumza na Watumishi wa Idara ya Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (hawapo pichani) alipokutana nao kwa mara ya kwanza baada ya kuteuliwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye nafasi hiyo tarehe 3 Machi 2019. Pamoja na mambo mengine, Mhe. Prof. Kabudi aliwataka Watumishi wa Wizara kubadilika na kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu miongozo na maelekezo mbalimbali pamoja na kuwa wazalendo na kufanya kazi zao kwa kushirikiana na  kwa weledi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa. Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Mkurugenzi wa Idara ya Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje Mhe. Balozi Grace Martin na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Katika Wizara ya Mambo ya Nje. Aidha, mazungumzo hayo ni mwendelezo wa Vikao vya Prof. Palamagamba John Kabudi na Watumishi wa Wizara yake, ambapo yamefanyika katika Ofisi ndogo jijini Dar es Salaam tarehe 04 Juni, 2019 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akutana kwa mara ya kwanza na kiting cha Itifaki cha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Mkurugenzi wa Idara ya Itifaki ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Grace Martini akitoa maelezo ya majukumu ya kitengo hicho kwa Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi alipokutana na Kitengo hicho kwa mara ya kwanza katika ofisi ndogo za Wizara hiyo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Idara ya Itifaki wakimsikiliza Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi ambaye hayupo pichani alipozungumza nao
Sehemu nyingine ya Watumishi wakifurahia jambo wakati wakimsikiliza Mhe. Prof. Kabudi (hayupo pichani)
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa kwenye mkutano wao na Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (hayupo pichani).
Mhe. Prof. Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Idara ya Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.








Dkt. Mnyepe afanya mazungumzo na Balozi wa Msumbiji hapa nchini.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Msumbiji hapa nchini Mhe. Monica Patricio Clemente. Mazungumzo yao yamefanyika katika Ofisi Ndogo zilizopo jijini Dar es Salaam tarehe 04 June, 2019
Mazungumzo kati ya Dkt. Mnyepe (wa pili kutoka kulia) na Balozi Clemente (wa pili kutoka kushoto) yakiendelea, wa kwanza Julia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Wilbroad Kayombo akifuatilia kwa making mazungumzo hayo. 

Tuesday, June 4, 2019

Prof. Kabudi afanya mazungumzo na Mwakilishi wa UNESCO nchini Tanzania.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi(Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi,na Utamaduni (UNESCO) nchini Bw. Tirso Dos Santos. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje zilizopo jijini Dar es Salaam tarehe 04, Juni 2019
Bw. Santos akimweleza jambo Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akiwa katika picha ya pamoja Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi,na Utamaduni (UNESCO) nchini.



TAARIFA KUHUSU UTHIBITISHAJI WA NYARAKA

Dodoma, 04 Juni 2019

TANGAZO KWA UMMA

TAARIFA KUHUSU UTHIBITISHAJI WA NYARAKA

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuufahamisha Umma kwamba, kuanzia tarehe 20 Mei, 2019 malipo yoyote Kwa Wizara yanafanyika kwa njia ya Kielektroniki kupitia mfumo wa GOVERNMENT ELECTRONIC PAYMENT GATEWAY (GePG).

Hivyo, wateja wote watakao hitaji kufanya malipo ya uthibitisho wa nyaraka mbalimbali zikiwemo; vyeti vya talaka, ndoa, kuzaliwa, Kifo n.k wanapaswa kabla ya kufanya malipo yoyote kuwasiliana na ofisi za Wizara kupitia vituo vyake vilivyopo Dodoma, Dar es salaam na Zanzibar ili kupatiwa ‘Control Number’ ili kufanikisha malipo husika kupitia Akaunti ya Benki ya CRDB.

Wateja wanaoleta nyaraka hizo kwa uthibitisho, wanaendelea kukumbushwa pia kukamilisha hatua muhimu kabla ya kupatiwa ‘Control Number’ ikiwemo kupelekwa kwanza katika Mamlaka na Taasisi husika zilizotoa vyeti/nyaraka hizo ili vihakikiwe na kuthibitishwa.

UMMA WOTE UNAOMBWA KUZINGATIA RAI KWAMBA, MALIPO YOYOTE YATAKAYOFANYIKA KINYUME NA MAELEKEZO BAADA YA TANGAZO HILI, HAYATOPOKELEWA


Imetolewa na:
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,