Tuesday, June 11, 2019

Prof. Kabudi afanya mazungumzo na Waziri wa Viwanda na masuala ya Afrika Mashariki wa Sudan Kusini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba John Kabudi akisalimiana na Waziri wa Viwanda, Biashara na masuala ya Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Sudan Kusini, Mhe. Paul Mayom Akech kabla ya kuanza mazungumzo yao. Mazungumzo hayo yamefanyika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam tarehe 11 Juni 2019.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba John Kabudi akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mazungumzo kati yake na Waziri wa Viwanda, Biashara na masuala ya Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Sudan Kusini, Mhe. Paul Mayom Akech (kushoto). Mazungumzo hayo yamefanyika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam  tarehe 11 Juni 2019.
Waziri wa Viwanda, Biashara na masuala ya Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Sudan Kusini Mhe. Paul Mayom Akech, akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) baada ya mazungumzo kati yake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.  Profesa Palamagamba John Kabudi. Mazungumzo hayo yamefanyika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam tarehe 11 Juni 2019.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Profesa Palamagamba John Kabudi (katikati) akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mazungumzo kati yake na  Waziri wa Viwanda, Biashara na Masuala ya Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Sudan Kusini Mhe. Paul Mayom Akech (kushoto). Kulia Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaack Kamwelwe. Mkutano huo ulifanyika katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam tarehe 11 Juni  2019.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.  Profesa Palamagamba John Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Mhe. Paul Mayom Akech,Waziri wa Viwanda,Biashara na Masuala ya Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Sudan Kusini. Kushoto kwa Profesa Kabudi ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaack Kamwelwe akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe. Mazungumzo ya viongozi hao yalifanyika katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam tarehe 11 Juni 2019.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.