Tuesday, June 18, 2019

TANZANIA YAWAHAKIKISHIA MAZINGIRA BORA WAWEKEZAJI WA KIMAREKANI NCHINI


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akihutubia wakati wakufunga Mjadala wa kwanza wa Kibiashara kati ya Tanzania na Marekani, ulioandaliwa kwa ushirikiano kati ya Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji, Ubalozi wa Marekani, Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa wa afrika mashariki na Wizara ya Viwanda na Biashara  pamoja na Chemba ya wafanyabiashara wa kimarekani nchini Tanzania ikiwa ni juhudi za serikali ya Tanzania kupitia Wizara na taasisi za Serikali kusikiliza na kutatua changamoto za wawekezaji na wafanyabiashara wa Ndani na Nje. Ambapo Prof. Palamagamba alieleza kuwa Tanzania kwa sasa kuna mazingira mazuri ya kuvutia uwekezaji. 

Aidha, aliezea kuwa Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, imeweka usawa kwa kuwasikiliza wawekezaji wa Ndani na wawekezaji kutoka Nje. 

Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wa Kimarekani nchini Tanzania (AMCHAM) Bw. Garry Friend akipokea nakala za vitabu vya bajeti ya serikali kutoka kwa Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) ili kujionea mabadiliko ya uwekezaji nchini yalivyoboreshwa.
Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wa Kimarekani nchini Tanzania (AMCHAM) Bw. Garry Friend akimsikiliza kwa makini Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani) alipokuwa akihutubia.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe (wa kwanza kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda wakifuatilia kwa makini mambo yaliyokuwa yakielezwa na Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani)
Kaimu Balozi wa Marekani Dkt. Inmi K. Patterson naye akizungumza kwenye Mjadala wa kwanza wa Kibiashara kati ya Tanzania na Marekani
Sehemu ya wageni waliohudhuria kwenye mjadala huo, wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Marekani na Ulaya Bw. Jestas Nyamanga.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Mhe. Angela Kairuki (Mb.) naye akihutubia kwenye Mjadala wa kwanza wa Kibiashara kati ya Tanzania na Marekani
Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Mhe. Godfrey Mwambe naye akielezea namna kituo hichi kilivyoboresha na kinavyoshirikiana na taasisi nyingine katika kuhakikisha mwekezaji anapokuja nchini hapati shida. 
Juu na Chini ni Sehemu ya wageni waalikwa wakimsikiliza Bw. Godfrey Mwambe (hayupo pichani).


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi akisalimiana na Kaimu Balozi wa Marekani Dkt. Inmi K. Patterson 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi akijadiliana jambo na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa (wa kwanza kilia)
Prof. Palamagamba John Kabudi, Mhe. Angela Kairuki pamoja na Dkt. Faraji Mnyepe wakijadiliana jambo kabla ya kuanza kwa Mjadala wa kwanza wa kibiashara kati ya Tanzania na Marekani
Meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa kutoka Ubalozi wa Marekani hapa nchini pamoja na wageni waalikwa waliohudhuria kwenye mjadala huo















No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.