Dodoma, 04
Juni 2019
TAARIFA KUHUSU UTHIBITISHAJI WA NYARAKA
Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuufahamisha Umma kwamba, kuanzia
tarehe 20 Mei, 2019 malipo yoyote Kwa Wizara yanafanyika kwa njia ya
Kielektroniki kupitia mfumo wa GOVERNMENT ELECTRONIC PAYMENT GATEWAY (GePG).
Hivyo, wateja wote
watakao hitaji kufanya malipo ya uthibitisho wa nyaraka mbalimbali zikiwemo;
vyeti vya talaka, ndoa, kuzaliwa, Kifo n.k wanapaswa kabla ya kufanya malipo
yoyote kuwasiliana na ofisi za Wizara kupitia vituo vyake vilivyopo Dodoma, Dar
es salaam na Zanzibar ili kupatiwa ‘Control
Number’ ili kufanikisha malipo husika kupitia Akaunti ya Benki ya CRDB.
Wateja
wanaoleta nyaraka hizo kwa uthibitisho, wanaendelea kukumbushwa pia kukamilisha
hatua muhimu kabla ya kupatiwa ‘Control
Number’ ikiwemo kupelekwa kwanza
katika Mamlaka na Taasisi husika zilizotoa vyeti/nyaraka hizo ili vihakikiwe na
kuthibitishwa.
UMMA WOTE UNAOMBWA KUZINGATIA RAI KWAMBA, MALIPO
YOYOTE YATAKAYOFANYIKA KINYUME NA MAELEKEZO BAADA YA TANGAZO HILI,
HAYATOPOKELEWA
Imetolewa
na:
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki,
|
Tuesday, June 4, 2019
TAARIFA KUHUSU UTHIBITISHAJI WA NYARAKA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.