Dodoma, 14 Juni 2019
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kampuni 11 za Uturuki zatafuta fursa za Uwekezaji
Ujumbe wa kampuni 11
kutoka Uturuki upo nchini kwa ajili ya
kuangalia fursa mbalimbali za uwekezaji, hususan kwenye sekta ya viwanda vya
dawa za binadamu, vifaa vya maabara, vyombo vya ndani, vifaa vya umeme, ujenzi pamoja na ununuzi wa
korosho.
Ziara hiyo imetokana
na uratibu wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uturuki kwa kushirikiana na Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na Taasisi ya Sekta
Binafsi Tanzania (TPSF).
Ujumbe huo ambao
uliwasili nchini tarehe 10 Juni 2019 ulishiriki mkutano (B2B) uliondaliwa na
TPSF tarehe 11 Juni 2019. Katika mkutano huo pamoja na mambo mengine, wawakilishi kutoka Kituo cha Uwekezaji
Tanzania (TIC), Mamlaka ya Ukanda wa Uwekezaji (EPZA) na Mamlaka ya Maendeleo ya
Biashara Tanzania (Tantrade) walitoa maelezo kuhusu kanuni, taratibu na
mazingira ya kufanya biashara hapa nchini.
Ujumbe huo
utatembelea Zanzibar tarehe 13 Juni 2019 na baadaye Dodoma kwa ajili ya
kuangalia maonyesho ya masuala ya ujenzi. Ujumbe huo utaondoka nchini tarehe 16 Juni 2019 kurejea
Uturuki.
Imetolewa
na:
Kitengo
cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.