Tuesday, June 4, 2019

Prof. Kabudi afanya mazungumzo na Mwakilishi wa UNESCO nchini Tanzania.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi(Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi,na Utamaduni (UNESCO) nchini Bw. Tirso Dos Santos. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje zilizopo jijini Dar es Salaam tarehe 04, Juni 2019
Bw. Santos akimweleza jambo Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akiwa katika picha ya pamoja Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi,na Utamaduni (UNESCO) nchini.



No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.