Friday, July 12, 2019

Maabara ya kisasa ya kupima afya ya udongo kwa kutumia gari maalum yazinduliwa

Makamu Waziri wa Uholanzi Bi. Marjolijn Sonnema (watatu kushoto) na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi wa Tanzania Bw.Abdallah Ulega(watatu kulia) akikata utepe kuashilia uzinduzi wa Teknolojia ya Maaabara ya kupima afya udongo kwa kutumia gari maalum uliofanyika Jijini Arusha hivi karibuni. kushoo ni Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Joroen Verheul, wapili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa SAGCOT centre ltd Bw.Geoffrey Kirenga, wa pili kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe na kulia ni Mkurugeni Mkuu wa Kampuni ya Life Support System Tanzania (LSSL) Dkt.Edmond Matafu ambaye ndie mwekezaji wa teknolojia hiyo nchini.
Mkurugeni Mkuu wa Kampuni ya Life Support System Tanzania (LSSL) Dk. Edmond Matafu (kulia) akitoa maelekezo ya namna Maabara ya kupima afya ya udongo inavyofanya kazi kwa Makamu Waziri wa Uholanzi Bi.Marjolijn Sonnema(wapili kulia) mara baada ya kuzindua maabara hiyo inayotumia gari maalum hivi
karibuni jiijini Arusha. Wapili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa SAGCOT Centre Ltd, Geoffrey Kirenga.
Gari Maalum yenye maabara ya kupima afya ya udongo limezinduliwa hvi karibuni jijini Arusha. Kampuni ya Life Support System Tanzania (LSSL) ndiyo itakayoendesha zoezi la kupima afya ya udongo katika mashamba ya wakulima kote nchini kwa gharama ya shilingi 25,000 mpaka 30,000.
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akipeana mkono na Dk. Edmond Matafu, ambaye ni moja wa wawekezaji walioleta maabara hiyo ambayo itaidia sana wakulima kwani watakuwa wanapima udongo huo kabla ya kulima. 
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, akizungumza jambo mara baada ya kuzindua maabara hiyo ya upimaji wa udongo. 
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega, Naibu Waziri wa Kilimo Maliasili na Usalama wa Chakula Bi. Marjolyn kutoka nchini Uholanzi, pamoja na Dk. Edmond Matafu, wakikata utepe ikiwa ni ishara ya maabara hiyo ya kutembea imezinduliwa rasmi. 
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akizungumza jambo mara baada ya kuzindua maabara hiyo ya upimaji wa udongo.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo maliasili na Usalama wa Chakula Bi Marjolyn kutoka nchini Uholanzi wakikata utepe ishara ya kufungua rasmi maabara za utupimaji wa udongo. (Picha zote na Ahmed Mahmoud, Arusha).


Na Mwandsihi Wetu, Arusha

TEKNOLOJIA ya maabara ya kupima afya ya udongo kwa kutumia gari maalumu lenye uwezo kupima zaidi ya sampuli 100 za udongo kwa siku moja limezinduliwa hapa nchini ili kupima udongo na kumhakikishia mkulima uzalishaji wa mazao kwa wingi na yenye tija sokoni.



Uzinduzi wa Teknolojia hiyo kutoka nchini Uholanzi ulifanyika jijini Arusha kati ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi wa Tanzania Bw.Abdallah Ulega kwa niaba ya Tanzania na Makamu Waziri wa Kilimo na Ubora wa Chakula wa Uholanzi, Bi.Marjolijn Sonnema kwa niaba ya nchi yake ili kufanikisha mageuzi katika sekta ya kilimo.

Akizungumza mara baada ya kufanya uzinduzi wa teknolojia hiyo, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Bw Ulega aliishukuru Serikali ya Uholanzi kwa kutoa teknolojia yake kwa Tanzania na kusema kuwa itasaidia kuleta mapinduzi katika uzalishaji mazao.

“Kupima afya ya udongo inatoa majibu juu ya ubora wa ardhi husika, mazao yanayofaa kulimwa katika eneo hilo, kiwango cha mbolea kinachotakiwa na kutoa makadirio ya kiwango cha mavuno katika eneo husika,” alisema Naibu Waziri Ulega.

Aliongezea kuwa gharama ya kupima shamba iliyowekwa ya shilingi 25,000 mpaka 30,000 wakulima wanaweza kumudu na kuwataka wapema mashamba yao kabla ya kufanya kilimo ili kujua matatizo yaliyopo kwenye ardhi yake na nini afanye ili tija ya uzalishaji iongezeke.

“Teknolojia hii imeletwa kwetu hivyo tunakila sababu ya kuhamasisha wakulima nchini kupima mashamba yao ili wajipatie uhakika wa zao lilalofaa katika ardhi yake na nini afanye katika kuboresha ili aweze kuongeza tija ya uzalishaji,” alisema.

Naibu Waziri Ulega aliesema kuwa mageuzi katika sekta ya kilimo yatapatikana kupitia teknolojia hii ya kupima afya ya udongo na kupelekea kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao ya kilimo hali itakayochochea ujenzi wa viwanda vya kuchakata na kuongezea thamani ya mazao.

“Ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi kunachochea kasi ya maendeleo kwa kuibua teknolojia na ujuzi mbalimbali katika kuiletea nchi maendeleo, naipongeza kampuni ya Life Support System Tanzania (LSSL) kwa kuwekeza kwenye ketnolojia hii,” alisema Ulega Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa LSSL, Dkt.Edmond Matafu alisema magari manne yapo tayari pamoja na handheld soil scanner 100 ambazo zitatumiwa na maafisa ugani kwa ajili ya kuchukua sampuli za udongo katika maeneo ya vijiji kote nchini.

“Hii itasaidia kufanya zoezi la kupima afya ya udongo kwa wakati pasipo kuchelewa kipindi cha kulima ambapo itampa unafuu mkulima kujua mahitaji katika shamba lake ili aweze kupata tija katika uzalishaji mazao,” alisema Dkt. Matafu.

Aliongezea kuwa juhudi za Serikali za kujenga uchumi wa kati na viwanda zitatekelezeka kwa ushirikiano kati ya sekta binafsi na Serikali kufanya kazi kwa pamoja kuhakikisha vikwazo vyote vinavyokwamisha maendeleo vinatatuliwa ili maendeleo tunayoyatarajia yaweze kufikiwa kwa vitendo.

“Zoezi la kupima afya ya udongo litafanyika kote nchini kwani tumejipanga vizuri katika kutoa huduma hii kwa wakulima hivyo ushirikiano ndio kitu muhimu katika kufanikisha zoezi hili ambalo litakwenda kuinua hali ya uzalishaji zao nchini,” alisema Dkt. Matafu.

Uzinduzi wa Maabara ya kupima udongo kwa kutumia gari maalum ulishuhudiwa na Makamu Waziri wa Kilimo na Ubora wa Chakula kutoka Uholanzi, Bi. Marjolijn Sonnema, Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania

Joroen Verheul, Katibu Mkuu Wizara ya Mifungo na Uvuvi Profesa Elisante Ole Gabriel na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Kuendeleza Kilimo Nyanda za Juu Kusini, Bw. Geoffrey Kirenga.






Watanzania wachangamkia soko la biashara Komoro


Balozi wa Tanzania nchini Komoro, Mhe. Balozi Sylvester Mabumba akitoa hotuba yake kwenye ufunguzi wa  mkutano wa wafanyabiashara (hawapo pichani) wa Tanzania na Komoro, katika hotuba yake aliwahakikishia wafanyabiashara kutoka Tanzania kuwa Ubalozi unaendelea kufanya kazi kwa bidii katika kuratibu shughuli za biashara baina ya Tanzania na Komoro, pamoja na kuwashauri wafanyabiashara hao kufika Ubalozini pindi watakapo kabiliwa na changamoto za aina yoyote ile.

Katika Mkutano huo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Biashara wa Komoro Mhe. Mohamed M'saidie, ambapo aliambata na 
Rais wa Chamber of Commerce ya Comoro, Ndg. Ahmed Bazi, Rais wa Chamber of Commerce wa Anjouan, Ndg. Soyad Mohamed, Rais wa Chamber of Commerce ya Ngazidja, Ndg. Soibroi Eddine Mohamed Balozi wa Sudan, Mhe. Issam Muhi El Dine Khalili na Kaimu Balozi kutoka Ubalozi wa Afrika Kusini Bi. Chwane Nomcebo Valentia Mthethwa.

Aidha, 
washiriki kutoka Tanzania walipata fursa ya kuonesha, kuuza na kutangaza bidhaa zao. Sambamba na hilo washiriki waliweza pia kufanya majadiliano ya kibishara (B2B) na kuweza kuingia makubaliano ya kufanya biashara na Wakomoro.

 Sekta ambazo zimeonekana kuchangamkiwa zaidi ni sekta ya ufugaji wa kuku, mayai, bidhaa za mboga mboga na biashara ya nyama ya Ng’ombe.


Mkutano huo umefanyika katika Hoteli ya Retaj nje kigodo ya mji wa Moroni. 
Mhe Ahmed Bazi Rais wa Chamber of Commerce ya Komoro naye akitoa hotuba yake kwenye ufunguzi wa Mkutano uliowakutanisha wafanyabiashara kutoka Tanzania na Komoro
Mwakilishi wa Waziri wa Uchumi na Uwekezaji wa Komoro naye akitoa hotuba yake kwenye ufunguzi wa mkutano wa wafanyabiashara.
Add caption
Wadau wa Biashara kutoka Tanzania na Komoro wakisikiliza Hotuba zilizokuwa zikiendelea 
Maonyesho ya Bidhaa za Tanzania yakiendelea nje ya Hotel Retaj Moroni
Wajumbe wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza ufunguiz wa Mkutano ulio wakutanisha wafanyabiashara kutoka Tanzania na Komoro.








Thursday, July 11, 2019

Mhe. Balozi Seif Ali Idd atembelea maonesho ya 43 ya biashara ya kimataifa (Sabasaba)


Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akisaini kitabu cha wageni, alipotembelea banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwenye maonesho ya 43 ya biashara ya kimataifa yanayoendea katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akisikiliza maelezo kutoka kwa Bi. Tagie Daisy Mwakawago Afisa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akisoma moja ya Kitabu cha Wizara hiyo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akipokea Vitabu vilichapishwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kutoka kwa Bi, Tagie Daisy Mwakawago.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Wizara alipotembelea banda la Wizara kwenye maonesho ya sabasaba





Wednesday, July 10, 2019

KATIBU MKUU JUMUIYA YA MADOLA AFANYA MAZUNGUMZO NA PROF. KABUDI

Katibu Mkuu wa jumuiya ya Madola Bi. Patricia Scotland akisalimiana na waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) katika ofisi za Sekretarieti za jumuiya hiyo zilizopo London,Uingereza. July 9, 2019.
Katibu Mkuu wa jumuiya ya Madola Bi. Patricia Scotland akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) katika ofisi za Sekretarieti za jumuiya hiyo zilizopo London,Uingereza. July 9, 2019.
Katibu Mkuu wa jumuiya ya Madola Bi. Patricia Scotland akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) katika ofisi za Sekretarieti za jumuiya hiyo zilizopo London,Uingereza. July 9, 2019.
 Katibu Mkuu wa jumuiya ya Madola Bi. Patricia Scotland (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) alipomtembelea katika ofisi za Sekretarieti za jumuiya hiyo zilizopo London,Uingereza. Kulia ni Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza Dkt. Asha-Rose Migiro. July 9, 2019.




Saturday, July 6, 2019

Prof. Palamagamba John Kabudi atembelea maonesho ya 43 ya biashara ya kimataifa (Sabasaba)

Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akisaini kitabu cha wageni, alipotembelea banda la Wizara hiyo kwenye maonesho ya 43 ya biashara ya kimataifa yanayoendea katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (wa kwanza kutoka kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Bi. Tagie Daisy Mwakawago Afisa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Bw. Hassan Mnondwa akielezea picha za Mawaziri waliowahi kuiongoza Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa wanafunzi waliojitokeza kwenye banda hilo. 

Bw. Joseph Mwasoto akifanunua jambo kwa wateja waliyotembelea banda la Wizara kwenye maonesho ya sabasaba
Bi. Praxida Gasper akifanunua jambo kwa wateja waliyotembelea banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kwenye maonesho ya sabasaba

Huduma zikiendelea kutolewa kwa Wananchi mbalimbali wanaoendelea kutembelea banda la Wizara kwenye maonesho ya Sabasaba
Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akisaini kitabu cha wageni, alipotembelea banda la Chuo cha Diplomasia kwenye maonesho ya 43 ya biashara ya kimataifa yanayoendea katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akitizama Ramani ya Majengo mapya ya Chuo hicho yanayoyengwa sasa hivi, Kurasini jijini Dar Es Salaam 
Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akisaini kitabu cha wageni, alipotembelea banda la Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa (AICC) kwenye maonesho ya 43 ya biashara ya kimataifa yanayoendea katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akijionea ufanisi wa utengezaji wa bidhaa mbalimbali za Nyumbani zilizotengenezwa na Jeshi la Magereza, alipotembelea banda la Jeshi la Magereza kwenye maonesho ya 43 ya biashara ya kimataifa yanayoendea katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.

Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Wizara alipotembelea banda la Wizara kwenye maonesho ya sabasaba
Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika mahojiano na wanahabari kwenye maonesho ya biashara kimataifa maarufa sabasaba yanayofanyika jijini Dar  es Salaam