Friday, August 16, 2019

MABALOZI WA TANZANIA WATEMEBELEA MRADI WA RELI NA UPANUZI WA BANDARI YA DAR ES SALAAM



Mhe. Nahim Azizi Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia na Umoja wa Afrika  akisalimiana na mfanyakazi wa Bandari ya Dar es Salaam akiwa na ujumbe wa mabalozi wengine walipowasili bandarini hapo kwa ziara ya kikazi.


Wakiwa katika Bandari ya Dar es Salaam mabalozi walipata nafasi ya kutembelea mradi wa ujenzi wa upanuzi wa bandari sambamba na kuongeza kina cha bahari ili kuweza kuhudumia meli zinazobeba mzigo mkubwa. 

Mara baada ya kukamilika kwa mradi huo, Bandari ya Dar es Salaam itakuwa na uwezo wa kuhudumia mizigo ya kiasi cha tani milioni 28 kwa mwaka, ikiwa ni mara mbili ya kiwango cha sasa ambapo inauwezo wa kuhudumia mizigo kiasi cha tani milioni 13 pekee. 

Aidha, sambamba na kuongezeka kwa uwezo wa kuhudumia mizigo mingi, pia mradi huo utapunguza muda wa kuhudumia meli kutoka masaa 80 kwa meli moja kama ilivyo sasa hadi masaa 30 mara mradi huo utakapo kamilika.

Wakati huo huo  mabalozi walitembelea mradi wa ujenzi wa wa reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) ambapo walipata fursa ya kuona maendeleo ya ujenzi wa mradi huo kuanzia Stesheni jijini Dar Salaam hadi Soga mkaoni Pwani.

Mabalozi wamefurahishwa na jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi madhubuti wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kuendelea kutekeleza miradi ya  maendeleo kwa kasi  na ufanisi wa hali ya juu kwa manufaa ya Wananchi.  Mabalozi kwa nyakati tofauti wamesema licha ya miradi hii kuliongezea pato Taifa, mara baada ya kukamilika miradi hii itaiweka Tanzania katika nafasi nzuri zaidi ya ushindani wa kibiashara katika soko la Afrika Mashariki na katika ukanda wa Kusini mwa Afrika

Balozi Ramadhani Mwinyi Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akisaini kitabu cha wageni alipoambatana na mabalozi katika ziara ya kikazi Bandari ya Dar es Salaam.
Mhe. Dkt. Asha Rose Migiro Balozi wa Tanzania nchini Uingereza akizungumza wakati wa ziara ya kikazi Bandari ya Dar es Salaam
Mabalozi wakifuatilia wasilisho kuhusu mradi wa upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam

Mabalozi wakisiliza ufafanuzi kutoka kwa mtaalamu wa Shirika la Reli kuhusu mchoro wa mradi mpya wa SGR
Mabalozi wakipanda Treni tayari kwa safari ya kuelekea Soga mkoani pwani, ambapo pamoja na mambo mengine walijionea kiwanda cha kuunda baadhi ya vifaa vya kujengea mradi
Sehemu ya mabalozi wakiangalia mandhari yanayozunguka eneo la mradi wa SGR wakiwa njiani kuelekea kambi ya mradi ya Soga
Sehemu nyingine ya mabalozi wakifurahia jambo wakati wa ziara ya kikazi kutoka stesheni, Dar es Salaam kuelekea  Soga, Pwani. 
Sehemu ya Watendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki walioambatana na ujumbe wa mabalozi wakati wa kutembelea mradi wa ujenzi wa SGR


Mabalozi wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa Wizara, Shirika la Reli na wafanyakazi wa ujenzi wa mradi wa SGR
Baadhi ya Wafanyakazi wakiendelea na majuku ya kutengeneza zana za kujengea mradi wa SGR kwenye kiwanda kidogo kilichopo kambi ya Soga, Pwani.


Thursday, August 15, 2019

Mabalozi wa Tanzania watembelea mradi wa bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere







TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MABALOZI WA TANZANIA WATEMBELEA MRADI MKUBWA UMEME WA JULIUS

NYERERE

Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi wameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kubuni, kutekeleza na kukamilisha miradi mikubwa ya maendeleo yenye manufaa kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Mabalozi hao kutoka nchi 42 za uwakilishi duniani kote wametoa pongezi hizo tarehe 14 Agosti 2019 walipoutembelea mradi mkubwa wa kufua umeme wa Julius Nyerere uliopo Wilayani Rufiji, mkoani Pwani.

Akizungumza na Vyombo vya Habari kwa niaba ya Mabalozi wengine, Kiongozi wa Mabalozi hao, Mhe. Naimi Aziz, Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia na Umoja wa Afrika amesema kuwa Serikali ya Awamu ya tano chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni ya kupigiwa mfano kwa hatua kubwa iliyofikiawa katika maendeleo ndani ya kipindi kifupi cha uongozi wake.

"Kwa dhati na kwa heshima kubwa tunaipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa hatua hizi kubwa za maendeleo ikiwemo kubuni na kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo yenye manufaa mengi kwa nchi yetu. Sisi mabalozi tunaoiwakilisha Tanzania nje tunaona fahari na tunajivunia kuwa na Rais mchapakazi na tunatembea kifua mbele tunapoiona miradi mikubwa kama hii ikitekelezwa ndani ya nchi yetu”, amesema Balozi Aziz.

Naye Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Mhe. Abdallah Possi alieleza kuwa Mabalozi wanaunga mkono jitihada hizi za Serikali na wapo tayari kuendelea kusaidia jitihada hizo ikiwa ni pamoja na kuwaleta nchini wawekezaji na wataalam wenye tija kwa taifa.

Akiwasilisha mada kuhusu mradi huo wa Julius Nyerere utakaozalisha umeme wa Megawatt 2115 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Rufiji, Meneja wa Mradi huo, Mhandisi Stephen Manda amesema kuwa mradi huo ambao ni wa nne kwa ukubwa barani Afrika na wa kwanza Afrika Mashariki utakamilika ifikapo mwaka 2022.

Aliongeza kusema kwamba, mradi huo unasimamiwa na watanzania kwa asilimia mia moja na kugharamiwa na Serikali ambapo kiasi cha shilingi trilioni 6.5 zimetengwa kukamilisha mradi huo. Kati ya fedha hizo tayari Serikali imewalipa wakandarasi wa mradi huo ambao ni Kampuni za Arab Contractors na Elsewedy Electric za nchini Misri kiasi cha shilingi trilioni 1.7 ambayo ni asilimia 15 ya fedha zote za mradi huo.

Akielezea faida za mradi huo Mhandisi Manda alisema zipo za kiuchumi, kijamii na  kimazingira.
Kiuchumi mradi huo utaongeza uzaishaji viwandqni kutokana na kuwepo kwa umeme wa uhakika na hivyo kuzalisha ajira kwa vijana. Pia mradi huo utakuza utalii kutokana na maeneo pembezoni mwa bwawa hilo kuwa na nafasi ya kujengwa hoteli na fukwe za kupumzikia. Kijamii Mhandisi Manda amesema kuwa, mradi huo hadi sasa umewawezesha wananchi wa Rufiji kupata huduma mbalimbali za kijamii kwa uhakika kama vile maji, umeme kutokana na mradi huo kupita kwenye eneo lao.

Kuhusu utunzaji mazingira, Mhandisi Manda alieleza kuwa, tahmini ya kina kuhusu mazingira yanayozunguka mradi huo imefanywa na kuwaomba Mabalozi kusaidia kutoa elimu zaidi ili kufuta dhana inayoenezwa kuwa mradi huo utaharibu mazingira. Alifafanua kuwa, Mradi huu pamoja na mambo mengine utachangia utunzaji mazingira kwa kiasi kikubwa kwenye eneo lotelinalouzunguka kwani kutokana na umeme utakaozalishwa wananchi hawataendelea kukata miti kwa ajili ya nishati ya kuni. Pia mradi huo utasaidia kutunza mazingira ya eneo hilo kwa kudhibiti mafuriko yaliyokuwa yanatokea kwenye ukanda wa eneo hilo.

Mradi huo mkubwa wa umeme ulibadilishwa jina na kuitwa Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere wakati wa uwekwaji wa jiwe la msingi uliofanywa na Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli mwezi Julai 2019 ili kuenzi maono ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere ambaye alikuwa na ndoto ya kujenga bwawa hilo wakati wa utawala wake.

Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi wapo nchini kuanzia tarehe 14 hadi 22 Agosti 2019 kwa ajili ya kushiriki Kikao Kazi chao Maalum pamoja na Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serial,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar es Salaam.
15 Agosti 2019

Balozi Ramadhani Mwinyi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, (wakwanza kushoto) akifuatilia uwasilishwaji wa taarifa ya hatua za maendeleo ya ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme wa bwawa la Julius Nyerere (2115MW) unaotekelezwa na Serikali wilayani Rufiji.


Mabalozi wa Tanzania wanaoiwakilisha nchi katika mataifa mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Wizara na Wafanyakazi wa Mradi ,katika moja ya njia ya chini (tunnel) katika mradi wa ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere lililopo katika hifadhi ya Selous wilayani Rufiji. Mabalozi walitembelea maradi huo kujionea hatua mbalimbali za maendeleo ya utekelezaji. Mradi huu unaotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano unatarajia kuzalisha Megawati 2115 baada ya kukamilika kwake mwaka 2022.
Mhe. Nahim Azizi Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia akizungumza mara baada ya kuwasili eneo la ujenzi wa mradi
Mabalozi wakisikliza maelezo kuhusu ujenzi wa mradi kutoka kwa Mhandisi Stevene Manda


Mabalozi wakisikiliza hotuba fupi ya ukaribisho kutoka Mhe. Juma Abdallah Njwayo Mkuu wa Wilaya ya Rufiji mara baada ya kuwasili katika eneo la mradi


RAIS CYRIL RAMAPHOSA AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA SIKU MBILI.

Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa akiwa na mkewe Dkt. Tshepo Motsepe wakiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Rais Ramaphosa amewasili Nchini kwa Zara ya kikazi ya siku mbili na bade atashiriki Mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo kwa Nchi za Kusini mua Afrika (SADC)

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akimlaki Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar Es Salaam. 

Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kisare Makori.
Wengine judoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo,Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sarah Msafiri,Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa ameongozana na Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa.
 

Monday, August 12, 2019

BALOZI MTEULE WA DENMARK AKABIDHI NAKALA ZA HATI YA UTAMBULISHO KWA PROF. PALAMAGAMBA JOHN KABUDI


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akisalimiana na Balozi Mteule wa Denmark hapa Nchini,Mhe. Mette Norgaard Dissing-Spandet alipofika katika ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kukabidhi nakala za hati za utambulisho.August 12,2019

Balozi Mteule wa Denmark hapa Nchini,Mhe. Mette Norgaard Dissing-Spandet akimkabidhi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi nakala za hati za utambulisho. Tukio hilo limefanyika katika ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam.August 12,2019

Balozi Mteule wa Denmark hapa Nchini,Mhe. Mette Norgaard Dissing-Spandet akiwatambulisha kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi baadhi ya maafisa aliongozana nao,wakati alipofika katika ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kukabidhi nakala za hati za utambulisho. August 12,2019.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule wa Denmark hapa Nchini,Mhe. Mette Norgaard Dissing-Spandet. Walioko pembeni ni baadhi ya wakurugenzi na maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na Ubalozi wa Denmark nchini Tanzania. August 12,2019.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mteule wa Denmark hapa Nchini,Mhe. Mette Norgaard Dissing-Spandet. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika Bw Jestas Nyamanga na Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na Ubalozi wa Denmark nchini Tanzania. August 12,2019.

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika Bw. Jestas Nyamanga wakipunga mkono kuagana na Balozi Mteule wa Denmark hapa Nchini,Mhe. Mette Norgaard Dissing-Spandet. August 12,2019.






PROF. PALAMAGAMBA JOHN KABUDI AKAGUA PIKIPIKI MPYA KWA AJILI YA SADC

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa anashuhudia namna mojawapo ya pikipiki mpya zinazoandaliwa kwa ajili ya mapokezi na kuongoza misafara ya viongozi,Wakuu wa Nchi na Serikali watakaohudhuria mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaoendelea Jijini Dar es Salaam,Tanzania ikiunganishwa. Anayeshuhudia ni Afisa Usafirishaji – IKULU Bw. Zuberi Kachingwa.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa anafurahia mojawapo ya pikipiki mpya zinazoandaliwa kwa ajili ya mapokezi na kuongoza misafara ya viongozi,Wakuu wa Nchi na Serikali watakaohudhuria mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaoendelea Jijini Dar es Salaam,Tanzania. Anayeshuhudia ni Afisa Usafirishaji – IKULU Bw. Zuberi Kachingwa.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa anajaribu moja ya pikipiki mpya zinazoandaliwa kwa ajili ya mapokezi na kuongoza misafara ya viongozi,Wakuu wa Nchi na Serikali watakaohudhuria mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaoendelea Jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni Afisa Usafirishaji – IKULU Bw. Zuberi Kachingwa.

Baadhi ya pikipiki mpya zitakazotumika katika mapokezi na kuongoza misafara ya viongozi,Wakuu wa Nchi na Serikali watakaohudhuria mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaoendelea Jijini Dar es Salaam zikiwa tayari kwa mapokezi.

Thursday, August 8, 2019

TANZANIA IKO TAYARI KUWAPOKEA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI KWA AJILI YA MKUTANO WA 39 WA SADC

Bw. Zuberi Kachingwe Afisa Usafirisahaji, IKULU,(katikati) akitoa maelezo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akikagua magari yatakayotumiwa na viongozi na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kujiridhisha juu ya matayarisho ya mapokezi kwa ajili ya mkutano huo utakaofanyika Dar es Salaam,Tanzania. Kulia ni Afisa Usafirishaji Msaidizi Bw. Athumani Natepe. August 8, 2019.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akipewa maelezo na Bw. Zuberi Kachingwe Afisa Usafirisahaji, IKULU,wakati Prof Palamagamba John Kabudi akikagua magari yatakayotumiwa na viongozi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kujiridhisha juu ya matayarisho ya mapokezi ya wakuu wa Serikali na Nchi watakaohudhuria mkutano huo Dar es Salaam,Tanzania. August 8, 2019.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Bw. Zuberi Kachingwe Afisa Usafirisahaji, IKULU pamoja na Bw. Athumani Natepe Afisa Usafirishaji Msaidizi mara baada ya kumaliza kukagua magari yatakayotumiwa na viongozi na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) mkutano utakaofanyika Dar es Salaam,Tanzania. August 8, 2019.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa amesimama mbele ya magari yanayotarajiwa kutumiwa na viongozi na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kujiridhisha juu ya matayarisho ya mapokezi kwa ajili ya mkutano huo utakaofanyika Dar es Salaam,Tanzania. August 8, 2019.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa ndani ya mojawapo ya magari yanayotarajiwa kutumiwa na viongozi na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kujiridhisha juu ya matayarisho ya mapokezi kwa ajili ya mkutano huo utakaofanyika Dar es Salaam,Tanzania. August 8, 2019.

Baadhi ya magari yanayotarajiwa kutumiwa na viongozi,wakuu wa Nchi na Serikali wakati wa mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) mkutano utafanyika Dar es Salaam,Tanzania. August 8, 2019.

Baadhi ya magari yanayotarajiwa kutumiwa na viongozi,wakuu wa Nchi na Serikali wakati wa Mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) mkutano utafanyika Dar es Salaam,Tanzania. August 8, 2019.

CHINA YATOA MSAADA WA VIFAA VYA OFISINI KWA AJILI YA SADC

Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akisaini pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Wang Ke nyaraka za makabidhiano ya Masada wa vifaa vya ofisini vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mia mbili kumi na saba vitakavyotumika wakati wa Mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC),August 08,2019

Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akisaini pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Wang Ke nyaraka za makabidhiano ya Msaada wa vifaa vya ofisini vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mia mbili kumi na saba vitakavyotumika wakati wa Mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Wanaoshuhudia ni maafisa kutoka Ubalozi wa China na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. August 08,2019. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akikabidiana nyaraka za Msaada wa vifaa vya ofisini vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mia mbili kumi na saba vitakavyotumika wakati wa Mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Wanaoshuhudia ni maafisa kutoka Ubalozi wa China na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. August 08,2019. na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China hapa Nchini Mhe. Wang Ke 



Saturday, August 3, 2019

WATUMISHI WA UMMA NA MAAFISA ITIFAKI WAPATA MAFUNZO KUHUSU UTOAJI WA HUDUMA SADC

Wakufunzi wa mafunzo kwa watumishi wa umma na Maafisa Itifaki watakaotoa huduma kwa wageni watakaoshiriki Mkutano wa 39 wa SADC wakimsikiliza mtoa mada (hayupo pichani) wakati wa mafunzo hayo. Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa mkutano wa kimataifa wa Julius Nyerere,Dar es Salaam. 03 August,2019.

Baadhi ya watumishi wa umma na Maafisa Itifaki waliohudhuria mafunzo maalum ya namna yakuwahudumia wageni wa mkutano wa SADC wa 39 yaliyoratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere,Dar es Salaam. 03 August 2019.

Baadhi ya watumishi wa umma na Maafisa Itifaki waliohudhuria mafunzo maalum kuhusu namna yakuwahudumia wageni wa mkutano wa SADC wa 39 wakifuatilia mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere,Dar es Salaam. 03 August 2019.

Add caption