Wednesday, March 17, 2021

TANZANIA–CHINA KUENDELEA KUDUMISHA USHIRIKIANO


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge mapema leo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa China nchini Mhe. Wang Ke katika ofisi za Wizara jijini Dodoma. 

Wawili hao wamejadili masuala mbalimbali yanayolenga kudumisha zaidi ushirikiano na uhusiano wa kidiplomasia na biashara. Vilevile wamejadili kuhusu ufuatiliaji wa maendeleo ya miradi na programu mbalimbali zinazotekelezwa kwa ushirikiano wa Tanzania na China ili kuhakikisha zinaleta tija kwa manufaa ya pande zote mbili.

Balozi Ibuge kwa upande wake ameeleza kuwa kuwepo kwa uhusiano mzuri wa Kidiplomasia baina ya Tanzania na China kumechagiza kwa kiasi kikubwa kukuwa kwa biashara, utali na uwekezaji baina ya nchi hizi mbilia hivyo urafiki na undugu kati ya Mataifa haya mawili unapaswa kulindwa, kudumisha na kuendelezwa siku zote na katika hali yoyote. “China kwa muda mrefu imekuwa ikichangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo ya Taifa letu kupitia sekta mbalimbali kama vile ujenzi wa mundombinu ya usafirishaji na mawasiliano kama vile reli na barabara, hivyo Wizara na Serikali kwa ujumla inadhamini na kulinda undugu huu wa kihistoria” Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge

Mheshimiwa Balozi Wang Ke kwa upande wake ameshukuru kwa ushirikiano ambao amekuwa akiendelea kuupata kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Serikali kwa ujumla katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku. Ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano ili kuhakikisha serikali za nchi hizi mbili na watu wake wananufaika kotokana na uhusiano mzuri wa kidiplomasia uliopo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge afafanua jambo kwa Balozi wa China nchini Mhe. Wang Ke walipokutana kwa mazungumzo jijini Dodoma.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge akimsikiliza Balozi wa China nchini Mhe. Wang Ke wakati wa mazungumzo yaliyofanyika katika ofisi za Wizara jijini Dodoma.

  Mazungumzo yakiendelea



Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge akisisitiza jambo kwa Balozi wa China nchini Mhe. Wang Ke walipokutana kwa mazungumzo jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge na Balozi wa China nchini Mhe. Wang Ke wakiwa katika picha ya pamoja  mara baada ya kuhitimisha mazungumzo yao yaliyofanyika jijini Dodoma

Monday, March 15, 2021

TANZANIA, VATICAN KUHIMIZA AMANI

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Tanzania na Vatican zimeahidi kuendelea kuhimiza amani na utulivu katika masuala yenye changamoto mbalimbali ili kuwezesha uwepo wa amani na kutambua mchango mkubwa unaotolewa na Baba Mtakatifu katika kuhimiza amani, utulivu na usalama duniani.

Ahadi hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi, (Mb) wakati alipokutana kwa mazungumzo na Balozi wa Vatican nchini Mhe. Askofu Mkuu Marek Solczynski leo jijini Dar es Salaam.

Prof. kabudi amesema kuwa Tanzania na Vatican kwa kutambua umuhimu wa amani, zimeahidi kuendelea kushirikiana katika mikutano ya Umoja wa Mataifa kuhimiza amani, utulivu na mshikamano katika masuala mbalimbali yenye changamoto kwa binadamu duniani.

 “Tumeongelea umuhimu wa kulinda amani, utulivu na usalama duniani kote hasa katika maeneo yanayokumbwa na matatizo ya vita…….. katika hilo pia tuliongela suala la amani na usalama katika ukanda wa nchi za maziwa makuu, Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika tukijua kuwa kuna maeneo yanayohitaji amani ikiwemo eneo la kaskazini mwa Masumbiji, na mashariki ya Demokrasia ya Kongo,” Amesema Pro. Kabudi

Prof. Kabudi ameongeza kuwa katika miaka ya hivi karibuni na hata sasa dunia inakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinahitaji mshikamano wa mataifa yote duniani ili kuweza kuyakabili hii ikiwa ni pamoja na masuala yanayohusu amani, utulivu, majanga, na magonjwa ya mlipuko kama vile Covid 19, na yale yanayohusu umasikini na hali yamaisha ya watu kubaguliwa na kuonewa.

“Mfano katika mapambano dhidi ya Uviko 19, Vatican na Baba Mtakatifu wanayo nafasi kubwa ya kutoa mchango wao katika eneo hilo katika kuhakikisha kuwa mapambano dhidi ya Covid 19 hayageuzwi kuwa katika masuala ya kibiashara na kisiasa na badala yake mapambano hayo yazingatie utu, undugu na imani, Ameongeza Pro. Kabudi

Kwa upande wake Balozi wa Vatican hapa Nchini Mhe. Askofu Mkuu Marek Solczynski amesema kuwa Vatican itaendelea kuimarisha mahusiano yake ya kidiplomasia na Tanzania kwa masuala yenye maslahi ya haki, utu, amani na utulivu.

“Maongezi yangu na Mhe. Waziri yalikuwa mazuri kwani tuliongelea masuala mbalimbali yenye maslahi kwa binadamu yakiwemo masuala ya kukuza diplomasia yetu pamoja na masuala ya amani na usalama duniani,” Amesema Askofu Mkuu Solczynski.

Baba Mtakatifu Papa Francisko alimteua, Askofu Mkuu Marek Solczyński kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Tanzania mwezi Aprili, 2017. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Solczyński alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Georgia, Armenia na Azerbaijan.

Katika tukio jingine, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Tate Olenasha amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Algeria hapa nchini Mhe. Ahmed Djellal ambapo pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali yanayohusu kuimarisha diplomasia baina ya Tanzania na Algeria.  

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi, (Mb) akisalimiana na Balozi wa Vatican nchini Mhe. Askofu Mkuu Marek Solczynski wakati walipokutana kwa mazungumzo leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam 


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi, (Mb) akiongea na Balozi wa Vatican nchini Mhe. Askofu Mkuu Marek Solczynski wakati walipokutana kwa mazungumzo leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam 




Balozi wa Vatican nchini Mhe. Askofu Mkuu Marek Solczynski akimuelezea jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi, (Mb) wakati walipokutana kwa mazungumzo leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam 


Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na UShirikiano wa Afrika MAshariki, Mhe. William Tate Ole Nasha akiongea na Balozi wa Algeria nchini Mhe. Ahmed Djellal wakati walipokutana kwa mazungumzo leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam 


Balozi wa Algeria nchini Mhe. Ahmed Djellal akiongea na Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na UShirikiano wa Afrika MAshariki, Mhe. William Tate Ole Nasha wakati walipokutana kwa mazungumzo leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam 



WATUMISHI WA WIZARA WAHIMIZWA KUFANYA KAZI KWA UWELEDI NA NIDHAMU.


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amewahimiza Watumishi wa Wizara kufanya kazi kwa kujituma, weledi na nidhamu. Amesema haya alipokuwa akifungua mafunzo maalumu ya siku tano kwa Watumishi wa Wizara yanayoendelea jijini Dodoma.

Katibu Mkuu amewakumbusha na kusisitiza kuwa, Watumishi wa Wizara wakati wote wakiwa katika utekelezaji wa majumu yao iwe ndani au nje ya mipaka ya nchi, wanapaswa kuielewa na kuzingatia miongozo mbalimbali inayotumiwa na Wizara. Ameitaja baadhi ya miongozo hiyo kuwa ni pamoja na Sera ya Mambo ya Nje, Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, Ilani ya CCM ya Mwaka 2020-2025, Hotuba ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati anafungua Bunge la 12, Mpango Mkakati wa Wizara ambao huhuishwa kila mwaka wa fedha, na sheria na kanuni zinazoongoza utumishi nje. Aliongeza kuwa Mkataba wa Vienna (Vienna Convention) wa Mwaka 1961 na ule wa mwaka 1963 unaohusu mahusiano ya kidiplomasia na mahusiano ya kikonseli mtawalia pamoja na Kanuni za Utumishi Nje za Mwaka 2016 pia ni muhimu zizingatiwe. 

“Natambua ni ndoto ya kila Afisa Mambo ya Nje (Foreign Service Officer) ni kwenda posting siku moja, kwa mtakaobahatika kupata fursa ya kwenda kwenye Balozi zetu, mjue kwamba mna deni kubwa kwa nchi yenu. Mnawiwa kutekeleza majukumu yenu kwa kujituma, uzalendo, na kuhakikisha ulinzi na usalama wa maslahi ya nchi yetu.” Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge. 

Licha ya mafunzo hayo kulenga kuwasaidia watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuelewa misingi bora ya maadili ndani ya Utumishi wa Umma, Balozi Brigedia Jenerali Ibuge ameeleza mataumani yake kuwa mafunzo hayo yatawasaidia watumishi kupata uelewa wa jumla kuhusu Maslahi ya Taifa, Diplomasia ya Uchumi, Itifaki, Usalama wa kimtandao na utendaji wa kazi katika mazingira ya kimataifa. 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge akizungumza na Watumishi wa Wizara (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo maalumu kwa watumishi hao yatakayofanyika katika ukumbi wa Veta, jijini Dodoma.

Sehemu ya Watumishi wa Wizara wakifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge kwenye ufunguzi wa mafunzo maalumu kwa watumishi wa Wizara yanayofanyika katika ukumbi wa Veta, jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge (katikati walioketi), Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu Bw. Alex Mfungo (kulia walioketi) na Mhe. Balozi Abdulrahman Kaniki wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo.

Shemu nyingine ya Watumishi wa Wizara wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa Mafunzo

Shemu nyingine ya Watumishi wa Wizara wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa Mafunzo

Friday, March 12, 2021

TANZANIA YAJIVUNIA MIAKA 40 YA MAFANIKO SADC

 Na Mwandishi wetu,

Tanzania imejivunia mafanikio iliyoyapata katika kipindi cha  miaka 40 ya uanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) ameyataja mafanikio hayo kuwa ni pamoja na miaka 40 ya uanachama wa SADC tangu 1979, lugha ya kiswahili kutumika katika mikutano yote ya kisekta ya SADC pamoja na kutengenzwa sanamu maalumu ya Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.  

“Pamoja na mambo mengine, mkutano wetu wa leo wa Baraza la Mawaziri wa SADC tunategemea kujadili masuala mbalimbali anayohusu jumuiya hiyo likiwemo suala la matumizi ya lugha ya Kiswahili katika mikutano yote ya kisekta,” Amesema Prof. Kabudi.

Mambo mengine yatakayojadiliwa ni pamoja na suala la kutengeneza sanamu maalumu ya Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambapo sanamu hiyo itawekwa katika jengo la Amani Addis Ababa nchini Ethiopia, pamoja na maadhimisho ya miaka 40 ya SADC.

“Hivyo kupitia mkutano huu tutakamilisha mchakato wa kumpata mtu atakae ifua sanamu hiyo ya Mwl. Nyerere ambapo itawekwa katika jingo la Amani Ethiopia,” Amesema Prof. Kabudi

Prof. Kabudi ameendelea kueleza kuwa katika mkutano huo suala la maadhimisho ya miaka 40 ya SADC pia limejadiliwa ikiashiria umoja wa SADC kudumu kwa miaka 40.

“Miaka 40 ya SADC ina umuhimu mkubwa sana kwa Tanzania kwa sababu miongoni mwa viongozi nane walioasisi sadc ni Mwl. Julius Nyerere katika mkutano uliofanyika mwaka 1979 mkoani Arusha ambapo Tanzania iliamua kuingia rasmi katika jumuiya hiyo,” Ameongeza Prof. Kabudi 

Tanzania itakuwa inasherekea miaka 40 ya SADC ikiwa tayari Kiswahili ni moja ya lugha rasmi za jumuiya hiyo, lakini pia ikiwa na sanamu maalumu ya kumuenzi na kumheshimu baba wa Taifa na Muasisi wa SADC Mwl. Julius Nyerere.

Hivyo Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo unaongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb), Waziri wa Afya wa Zanzibar, Mhe. Nassor Ahmed Mazrui, Waziri wa Fedha na Mipango – Zanzibar Mhe. Jamal Kassim Ali, Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Mhe. Omar Said Shaaba, Naibu Waziri Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Godwin Mollel, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na UShirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaban.

Februari 27, 2021 katika mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ulifanyika kwa njia ya Mtandao, wakuu wan chi waliridhia lugha ya Kiswahili iwe lugha ya tatu katika shughuli za jumuiya hiyo sambamba na lugha ya kifaransa kuwa lugha ya nne.

Kadhalika, Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC katika mkutano wao wa 39 uliofanyika jijini Dar es Salaam mwezi Augusti, 2019 waliridhia na kuipitisha kiswahili nne ya mawasiliano, ikiungana na lugha za Kifaransa, Kiingereza na Kireno zinazotumika katika jumuiya hiyo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akifuatilia Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb), katikati pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge na Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Agnes Kayola wakifuatilia mkutano


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge wakati wa mkutano wa baraza la mawaziri  


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (anaesoma taarifa) na Waziri wa Afya wa Zanzibar, Mhe. Nassor Ahmed Mazrui (kulia) pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge (kushoto) wakifuatilia mkutano  


Ujumbe wa Tanzania ukiendelea kufuatilia mkutano wa Baraza la Mawaziri SADC


Ujumbe wa Tanzania ukiendelea kufuatilia mkutano wa Baraza la Mawaziri SADC

Mkutano ukiendelea  


Wednesday, March 10, 2021

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

 


MAKATIBU WAKUU SADC WAENDELEA NA KIKAO

 Na Mwandishi wetu,

Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wameendelea na kikao chao kwa siku ya pili ikiwa ni maandalizi ya mkutano wa baraza la mawaziri wa SADC unaotarajiwa kufanyika tarehe 12 – 13 Machi, 2021 kwa njia ya mtandao jijini Dar es Salaam.  

Ujumbe wa Tanzania katika kikao hicho unaongozwa na Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge pamoja na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaban.   

Mkutano wa Baraza la Mawaziri ujumbe wa Tanzania utaongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Africa Masahariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) ataongoza ujumbe wa Tanzania.

Mwenyekiti wa Sasa katika Jumuiya ya SADC ni msumbiji na ndiye atakayeongoza majadiliano ya Mkutano huu.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akiwasilisha mada katika kikao cha Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kinachoendelea jijini Dar es Salaam kwa njia ya mtandao. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaban. Kikao hicho ni maandalizi ya Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC utakafanyika tarehe 12 - 13, Machi 2021 kwa njia ya mtandao jijini Dar es Salaam. 


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akiwasilisha mada katika kikao cha Makatibu Wakuu wa SADC kinachoendelea jijini Dar es Salaam kwa njia ya mtandao. Kikao hicho ni maandalizi ya Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC utakafanyika tarehe 12, Machi kwa njia ya mtandao jijini Dar es Salaam. 


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, akiongoza ujumbe wa Tanzania katika kikao cha makatibu wakuu wa SADC, kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaban pamoja na Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Agnes Kayola


Washiriki wa kikao cha makatibu wakuu wakifuatilia kikao kinachoendelea kwa njia ya mtandao jijini Dar es Salaam


Washiriki wa kikao cha makatibu wakuu wakifuatilia kikao kinachoendelea kwa njia ya mtandao jijini Dar es Salaam


Kikao kikiendelea  



Monday, March 8, 2021

KISWAHILI CHAPENDEKEZWA KUTUMIKA RASMI SADC

 Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

Lugha ya Kiswahili imependekezwa kuanza kutumika rasmi katika majadiliano kwenye vikao vya ngazi ya baraza la mawaziri na katika utendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Pendekezo hilo limewasilishwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge katika kikao cha Makatibu Wakuu wa SADC kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam kwa njia ya mtandao.

“Sisi kama Tanzania tumependekeza suala la lugha ya Kiswahili kutoka kwenye lugha ya kazi kwenye ngazi ya baraza la mawaziri hadi wakuu wa nchi na serikali wa SADC linabadilika na kuiwezesha lugha ya Kiswahili kuwa lugha rasmi kwenye utendaji wa SADC,” Amesema Balozi Ibuge.

Balozi Ibuge ameongeza kuwa, SADC wamekuwa wakitumia lugha za kikoloni kwa muda mrefu na kwa busara za wakuu wa nchi na Serikali wameamua kuanza kwa mpangilio ambapo lugha ya Kiswahili itaanza kutumika katika ngazi ya baraza la mawaziri pamoja na  vikao vya wakuu wa nchi, na kuishusha lugha hiyo kwenye sekta na kuingia rasmi katika matumizi ya SADC.

Kikao hicho ni maandalizi ya Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC unaotegemewa kufanyika tarehe 12, Machi jijini Dar es Salaam kwa njia ya mtandao.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akiwasilisha mada katika kikao cha Makatibu Wakuu wa SADC kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam kwa njia ya mtandao


Mkutano ukiendelea 


Mkutano ukiendelea