Monday, July 19, 2021

TANZANIA NA UMOJA WA ULAYA ZAAHIDI KUIMARISHA USHIRIKIANO

 Na Mwandishi wetu, Dar

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Umoja wa Ulaya (EU) zimeahidi kuimarisha ushirikiano kwa maslahi ya pande zote mbili.

Hayo yamesemwa kwenye mkutano kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) hapa nchini, Mhe. Manfredo Fanti, uliofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Balozi Sokoine ameeleza kuwa Serikali ya Tanzania inaridhishwa na uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya ambao umepelekea kuzaa matunda yenye manufaa kwa pande zote mbili. Aidha, ameahidi kuendelea kuimarisha uhusiano huo kwa maslahi ya pande zote.

Kwa upande wake, Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) hapa Nchini, Mhe. Manfredo Fanti amesema Umoja huo utaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Napenda kukuhakikishia kuwa Umoja wa Ulaya utaendelea kushirikiana kwa ukaribu na Tanzania kwa ajili ya kuleta maendeleo ya wananchi wake,” amesema Balozi Fanti.

Katika tukio jingine, Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine pia amekutana kwa mazungumzo na Kaimu Balozi wa China hapa Nchini Mhe. Xu Chen katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wawili walijadili masuala mbalimbali ya kuendeleza na kuimarisha ushirikiano wa uwili (Bilateral Cooperation).

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akiongea na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) hapa nchini, Mhe. Manfredo Fanti wakati walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) hapa nchini, Mhe. Manfredo Fanti akimuelezea jambo Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine wakati walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Mazungumzo baina ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) hapa nchini, Mhe. Manfredo Fanti yakiendelea 

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akimueleza jambo Kaimu Balozi wa China hapa nchini, Mhe. Xu Chen wakati walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Kaimu Balozi wa China hapa nchini, Mhe. Xu Chen akiongea na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine wakati walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Mazungumzo baina ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine na Kaimu Balozi wa China hapa nchini, Mhe. Xu Chen yakiendelea 



Thursday, July 15, 2021

WAZIRI MKUU MSTAAFU WA ETHIOPIA AHAMASISHA KILIMO KAMA NJIA YA KUONDOKANA NA UMASIKINI NCHINI

Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa katika mazungumzo na Mwenyekiti wa Taasisi ya Mapinduzi ya kijani Afrika yaani Allience for a Green Revolution in Afrika (AGRA) ambaye pia ni Waziri Mkuu Mstaafu wa Ethiopia Mhe Hailemariam Dessalegn,Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa katika mazungumzo na Mwenyekiti wa Taasisi ya Mapinduzi ya kijani Afrika yaani Allience for a Green Revolution in Afrika (AGRA) ambaye pia ni Waziri Mkuu Mstaafu wa Ethiopia Mhe Hailemariam Dessalegn pamoja na ujumbe walioambatana nao Jijini Dar es Salaam

Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na  Mwenyekiti wa Taasisi ya Mapinduzi ya kijani Afrika yaani Allience for a Green Revolution in Afrika (AGRA) ambaye pia ni Waziri Mkuu Mstaafu wa Ethiopia Mhe Hailemariam Dessalegn mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika Dar es Salaam
Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) wakiwa katika picha ya pamoja na  Mwenyekiti wa Taasisi ya Mapinduzi ya kijani Afrika yaani Allience for a Green Revolution in Afrika (AGRA) ambaye pia ni Waziri Mkuu Mstaafu wa Ethiopia Mhe Hailemariam Dessalegn pamoja na baadhi ya Wajumbe walioambatana nao mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika Dar es Salaam,Julai 15,2021.(Mwisho kushoto aliyevaa kilemba cheusi ni Balozi Naimi Azizi,Mkurugenzi wa Idara ya Afrika,Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki)


WAZIRI MKUU MSTAAFU WA ETHIOPIA AHAMASISHA KILIMO KAMA NJIA YA KUONDOKANA NA UMASIKINI NCHINI


Tanzania imetakiwa kuwekeza zaidi katika sekta ya kilimo ili kuifanya nguvu ya Tanzania kuingia katika uchumi wa kati ionekane kwa wananchi walio wengi kutokana na uwepo wa fursa ya eneo kubwa la ardhi yenye rutuba.

 

Mwenyekiti wa Taasisi ya Mapinduzi ya kijani Afrika yaani Allience for a Green Revolution in Afrika (AGRA) ambaye pia ni Waziri Mkuu Mstaafu wa Ethiopia Mhe Hailemariam Dessalegn ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula Jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa Tanzania ina eneo kubwa lenye rutuba kwa kilimo cha zao lolote na hivyo endapo sekta hiyo itapewa kipaumbele njia muafaka ya kuwaondoa katika umasikini wananchi wake.


Ameongeza kuwa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete ni mjumbe katika Taasisi hiyo ambayo imekuwa ikihamasisha kilimo kwa ajili ya usalama wa chakula lakini pia kilimo cha biashara kwa kuangalia miradi na mpango wa kitaifa wa uendelezaji wa kilimo na kwa hapa Tanzania Taasisi hiyo imesaidia katika upatikanaji wa mbegu bora,mafunzo,umwagiliaji pamoja na utoaji wa mitaji kwa ajili ya kuwajengea uwezo wanawake katika sekta hiyo.

 

Katika tukio jingine Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Nchi wa Umoja wa Falme za Kiarabu Mhe. Sheikh Shakhboot Bin Nahyan ambaye ni Mjumbe Maalum wa Mrithi wa Ufalme wa Abu Dhabi na Naibu Kamanda Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Umoja wa Abu Dhabi Mhe. Mohamed Bin Zayed Al Nahyan ambapo katika mazungumzo hayo wamegusia suala la ushirikiano katika usafiri wa anga,biashara na uwekezaji.

 

Balozi Mulamula ameongeza kuwa fursa za ushirikiano katika Nyanja za biashara na uwekezaji kati ya Nchi hizo mbili ni kubwa ambapo kwa sasa kikwazo ni ugonjwa wa UVIKO 19 na kwamba baada ya maradhi hayo kumalizika pande zote mbili zitakutana ili kuibua maeneo ya kuchochea ukuaji wa uchumi kwa haraka.

 


 

BALOZI MULAMULA AKUTANA NA UJUMBE MAALUM WA FALME ZA KIARABU UKIONGOZWA NA WAZIRI WA NCHI WA UMOJA WA FALME ZA KIARABU MHE. SHEIKH SHAKHBOOT BIN NAHYAN

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akisalimiana na kumkaribisha Waziri wa Nchi wa Umoja wa Falme za Kiarabu Mhe. Sheikh Shakhboot Bin Nahyan.

 

Mhe. Nahayan yuko Nchini kuwasilisha  Ujumbe Maalum wa Mrithi wa Ufalme wa Abu Dhabi na Naibu Kamanda Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Umoja wa Abu Dhabi Mhe. Mohamed Bin Zayed Al Nayhan kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Nchi wa Umoja wa Falme za Kiarabu Mhe. Sheikh Shakhboot Bin Nahyan.

 

Mhe. Nahayan yuko Nchini kuwasilisha  Ujumbe Maalum wa Mrithi wa Ufalme wa Abu Dhabi na Naibu Kamanda Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Umoja wa Abu Dhabi Mhe. Mohamed Bin Zayed Al Nayhan kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Nchi wa Umoja wa Falme za Kiarabu Mhe. Sheikh Shakhboot Bin Nahyan pamoja na ujumbe alioambatana nao.

 

Mhe. Nahayan yuko Nchini kuwasilisha  Ujumbe Maalum wa Mrithi wa Ufalme wa Abu Dhabi na Naibu Kamanda Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Umoja wa Abu Dhabi Mhe. Mohamed Bin Zayed Al Nayhan kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan.


Waziri wa Nchi wa Umoja wa Falme za Kiarabu Mhe. Sheikh Shakhboot Bin Nahyan akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula(Mb) (hayupo pichani)  walipokutana kwa mazungumzo

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akimkabidhi zawadi Waziri wa Nchi wa Umoja wa Falme za Kiarabu Mhe. Sheikh Shakhboot Bin Nahyan.

 

Mhe. Nahayan yuko Nchini kuwasilisha  Ujumbe Maalum wa Mrithi wa Ufalme wa Abu Dhabi na Naibu Kamanda Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Umoja wa Abu Dhabi Mhe. Mohamed Bin Zayed Al Nayhan kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan.

 

Tuesday, July 13, 2021

BALOZI MULAMULA AKUTANA NA BALOZI WA MSUMBIJI HAPA NCHINI BALOZI RICARDO MTUMBUIDA

 



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Msumbiji hapa Nchini Balozi Ricardo Mtumbuida. Balozi Ricardo amekutana na Balozi Mulamula kwa lengo la kujitambulisha kwake na kuzungumzia maeneo ya kipaumbele ya kushirikiana ili kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na Msumbiji
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Msumbiji hapa Nchini Balozi Ricardo Mtumbuida
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa anafafanua jambo kwa Balozi wa Msumbiji hapa Nchini Balozi Ricardo Mtumbuida
Balozi wa Msumbiji hapa Nchini Balozi Ricardo Mtumbuida akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) hayupo pichani walipokutana kwa mazungumzo

BALOZI WA SOMALIA NCHINI TANZANIA, BALOZI ABDI MOHAMED HUSSEIN AAGA BAADA YA KUMALIZA MUDA WAKE WA UWAKILISHI HAPA NCHINI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akizungumza na Balozi wa Somalia hapa Nchini Balozi Abdi Mohamed Hussein. Balozi Abdi Mohamed Hussein amefika kuagana na Balozi Mulamula baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi hapa Nchini

Balozi wa Somalia hapa Nchini Balozi Abdi Mohamed Hussein akisisitiza jambo wakati alipokutana na kuzungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) (hayupo pichani


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akizungumza na Balozi wa Somalia hapa Nchini Balozi Abdi Mohamed Hussein.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akimkabidhi zawadi  Balozi wa Somalia hapa Nchini Balozi Abdi Mohamed Hussein.Balozi Abdi Mohamed Hussein amefika kuagana na Balozi Mulamula baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi hapa Nchini


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiagana na  Balozi wa Somalia hapa Nchini Balozi Abdi Mohamed Hussein. Balozi Abdi Mohamed Hussein ameaga baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi hapa Nchini
 

Monday, July 12, 2021

SERIKALI YAKUTANA NA TAASISI,MASHIRIKA NA MABALOZI KUJADILI MAPATO NA MATUMIZI YA BAJETI

Na Mwandishi wetu

Katika kukuza Diplomasia ya Uchumi, kuimarisha na kushirikisha Jumuiya za Kimataifa Serikali imekutana na Mabalozi, Wakuu na Wawakilishi wa Mashirika na Taasisi za Kimataifa zilizopo hapa nchini kujadili Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/22 pamoja na mbinu za pamoja za kupambana na ugonjwa wa UVIKO 19.

Mkutano huo umefanyika Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Wizara za Kisekta zikiwemo Fedha na Mipango, Viwanda na Biashara, Afya, Maliasili na Utalii, Uwekezaji na Wizara ya Fedha na Mipango – Zanzibar pamoja na Mabalozi na Wawakilishi wa mashirika ya Kimataifa 54 kutoka nchi na taasisi mbalimbali.

Lengo la Mkutano huo pamoja na mambo mengine, ni kuwapitisha Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa kwenye Bajeti ya Serikali ya 2021/22, Mipango ya Utekelezaji wake na Maeneo ya Ushirikiano.

Akiongoza Mkutano huo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) ametaja sababu za Serikali kukutana na Mabalozi pamoja na Wawakilishi wa Mashirika na Taasisi za Kimataifa ambao pia ni wadau wa maendeleo ili kuwajengea uelewa katika mipango na utekelezaji wa Bajeti ya Serikali ya 2021/22 pamoja na maeneo ya Ushirikiano.

“tumeona tuweke utaratibu wa kukutana na wadau hawa wa maendeleo ili kujenga uelewa wa pamoja katika maeneo muhimu yaliyoainishwa katika bajeti ya Serikali ili waweze kupata picha halisi ya mipango na mikakati ya Serikali katika utekelezaji wa Bajeti,” amesema Balozi Mulamula

Kwa Upande wake Balozi wa nchi za Umoja wa Ulaya (EU) hapa Nchini, Mhe. Manfredo Fanti amesema uamuzi wa Serikali wa kukutana na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika na Taasisi za Kimataifa umekuwa mzuri sana umesaidia kufahamu mipango na mikakati mbalimbali ya Serikali katika utekelezaji wa bajeti yake ya 2021/22.

“Kupitia mkutano wa leo tumeweza kupata picha halisi ya ushirikiano wetu na Tanzania na umezidi kuimarika lakini pia tumeweza kuona na kujadili baadhi ya vipaumbele vya bajeti ya Serikali ya Tanzania, mipango ya maendeleo jambo ambalo sisi kama wadau wa maendeleo limetuhamasisha kuendelea kushirikiana kwa ukaribu n a uwazi zaidi,” amesema Balozi Fanti   

Mkutano huo umehudhuriwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigula Nchema (Mb), Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo (Mb), Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb), Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima (Mb), Waziri wa Fedha na Mipango kutoka Serikalini ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali, Pamoja na Naibu Waziri Wizara ya Uwekezaji Mhe. William Tate Olenasha (Mb).  

Pamoja na Mambo mengine, Mawaziri hao wamepata fursa ya kutoa ufafanuzi katika maeneo yanayohusu wizara zao ikiwa ni pamoja na mipango ya Serikali katika kukuza uchumi, kukusanya mapato, kukuza Viwanda, kuboresha mazingira ya Biashara na Uwekezaji, kukuza utalii na jinsi Serikali inavyojipanga kuboresha sekta ya afya nchini hasa katika kupambana na janga la UVIKO 19. 

Baadhi ya Mawaziri walioshiriki katika Mkutano wa Mabalozi, Wakuu na Wawakilishi wa Mashirika na Taasisi za Kimataifa zilizopo hapa nchini kujadili Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/22 pamoja na mbinu za pamoja za kupambana na ugonjwa wa UVIKO 19. Aliyevaa kitenge katikati ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiongoza Mkutano huo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) akichangia jambo wakati wa Mkutano wa Mabalozi, Wakuu na Wawakilishi wa Mashirika na Taasisi za Kimataifa zilizopo hapa nchini kujadili Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/22 

Sehemu ya Mabalozi, Wakuu na Wawakilishi wa Mashirika na Taasisi za Kimataifa zilizopo hapa nchini wakifuatilia Mkutano 


Balozi wa Canada hapa nchini, Mhe. Pamela O'Donnell akichangia jambo katika Mkutano wa Mabalozi, Wakuu na Wawakilishi wa Mashirika na Taasisi za Kimataifa zilizopo hapa nchini kujadili Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/22  

Balozi wa Kenya hapa nchini, Mhe. Dan Kazungu akichangia jambo katika Mkutano wa Mabalozi, Wakuu na Wawakilishi wa Mashirika na Taasisi za Kimataifa zilizopo hapa nchini kujadili Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/22

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Mhe. Christine Musisi akichangia jambo katika Mkutano wa Mabalozi, Wakuu na Wawakilishi wa Mashirika na Taasisi za Kimataifa zilizopo hapa nchini  

 

Balozi wa Ufaransa hapa nchini, Mhe. Frederic Clavier akichangia jambo katika Mkutano wa Mabalozi, Wakuu na Wawakilishi wa Mashirika na Taasisi za Kimataifa zilizopo hapa nchini  

Balozi wa Rwanda hapa nchini, Meja Jenerali Charles Karamba akichangia jambo katika Mkutano wa Mabalozi, Wakuu na Wawakilishi wa Mashirika na Taasisi za Kimataifa zilizopo hapa nchini  

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiongea na waandishi wa habari leo Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Mabalozi, Wakuu na Wawakilishi wa Mashirika na Taasisi za Kimataifa zilizopo hapa nchini  


Balozi wa nchi za Umoja wa Ulaya (EU) hapa Nchini, Mhe. Manfredo Fanti akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Mabalozi, Wakuu na Wawakilishi wa Mashirika na Taasisi za Kimataifa zilizopo hapa nchini  





Saturday, July 10, 2021

CHODOTA; MIRADI YA MIUNDOMBINU INAYOTEKELEZWA NCHINI ITACHAGIZA KASI YA USTAWI WA EAC


Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ameleza kuwa, utekelezaji wa miradi ya nishati ya umeme na barabara inayoendelea katika maeneo mbalimbali nchini itachagiza ustawi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuwa itarahishisha shughuli za usafirishaji na upatikanaji wa huduma. 

Bw. Chodota ameeleza haya alipokuwa akihitimisha ziara yake ya kutembelea miradi ya Kikanda ya Miundombinu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyopitishwa na Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki inayohusisha Ujenzi wa Bwawa la Umeme la Julius Nyerere (Julius Nyerere Hydropower Project), Utekelezaji wa Mradi wa Barabara ya Afrika Mashariki (Tanga-Bagamoyo/Malindi –Lungalunga), Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa-SGR, na Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) cha Holili, jijini Tanga. Bw. Chodota amefanya ziara hiyo kwa lengo la kujionea hali ya utendaji na hatua ya maendeleo iliyofikiwa katika utekelezaji wa miradi hiyo.

Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Afrika Mashariki katika kiwango cha lami unahusisha barabara yenye urefu wa Kilomita 245 kwa upande wa Tanzania, ambayo itaanzia Bagamoyo hadi Makurunge, Tanga. Utekelezaji wa mradi ambao umegawanyika katika sehemu nne tayari umeshaanza. Mfano, ujenzi unaoendelea sasa wa sehemu ya kwanza ya barabara hii kutoka Pangani (Tanga) hadi Mkange (Pwani) yenye jumla ya kilomita 50. Barabara hii inatarajiwa kuwa kiungo muhimu kati ya Tanzania na Nchi zingine za Afrika Mashariki.

Bw. Chodota ameeleza kuwa miradi hii pindi itakapo kamilika inatarajiwa kuleta mapinduzi makubwa katika upatikanaji wa nishati ya umeme wa kutosha, kurahisisha usafiri na usafirishaji nchini na katika Jumuiya kwa kuwa itarahisisha zaidi usafirishaji wa bidhaa hususani baina ya Tanzania na Kenya na upatikanaji wa huduma za jamii kwa urahisi na haraka. Sambamba na hayo, Bw. Chodota ameeleza kuridhishwa kwake na ushiriki wa Watanzania katika ujenzi wa miradi mikubwa nchini hususani katika Ujenzi wa Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere, ambapo asilimia 89% ya wataalam ni Watanzania.

Katika ziara hiyo Bw. Chodota ambaye ameambatana na baadhi ya Watalaam kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wamevutiwa na kasi na ubora wa kazi katika utekelezaji wa miradi yote iliyotembelewa.
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota (wa kwanza kulia) na baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia maelezo kuhusu mradi wa Bwawa la Kuzalisha umeme la Julius Nyerere.
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota (wa kwanza kulia) na baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia maelezo kuhusu mradi wa Bwawa la Kuzalisha umeme la Julius Nyerere. 
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota na Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia maelezo kuhusu mradi wa Bwawa la Kuzalisha umeme la Julius Nyerere.
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki walipotembelea mradi wa ujezi wa Bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere.
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota (mwenye tai) na baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na Wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na TANROADS wakiwa kwenye ziara ya kutembelea mradi wa ujenzi wa Barabara ya Afrika Mashariki (Tanga-Bagamoyo/Malindi – Lungalunga)
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota (mwenye tai) na baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na Wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na TANROADS wakiwa katika ziara ya kutembelea mradi wa ujenzi wa Barabara ya Afrika Mashariki (Tanga-Bagamoyo/Malindi–Lungalunga)
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota na baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na Wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na TANROADS wakiwa kwenye eneo la ujenzi wa kipande cha barabara ya Tanga miji hadi Pangani.
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota (wa kwanza kulia) na baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na Wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wakiwa kwenye ziara ya kutembelea Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) Holili, Tanga.
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota na baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na Wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wakiwa wakiangalia ukarabati wa jengo la Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) Holili, Tanga.
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota na baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na Wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wakiwa katika picha ya pamoja walipotembelea Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) Holili, Tanga.