Saturday, July 10, 2021

CHODOTA; MIRADI YA MIUNDOMBINU INAYOTEKELEZWA NCHINI ITACHAGIZA KASI YA USTAWI WA EAC


Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ameleza kuwa, utekelezaji wa miradi ya nishati ya umeme na barabara inayoendelea katika maeneo mbalimbali nchini itachagiza ustawi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuwa itarahishisha shughuli za usafirishaji na upatikanaji wa huduma. 

Bw. Chodota ameeleza haya alipokuwa akihitimisha ziara yake ya kutembelea miradi ya Kikanda ya Miundombinu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyopitishwa na Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki inayohusisha Ujenzi wa Bwawa la Umeme la Julius Nyerere (Julius Nyerere Hydropower Project), Utekelezaji wa Mradi wa Barabara ya Afrika Mashariki (Tanga-Bagamoyo/Malindi –Lungalunga), Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa-SGR, na Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) cha Holili, jijini Tanga. Bw. Chodota amefanya ziara hiyo kwa lengo la kujionea hali ya utendaji na hatua ya maendeleo iliyofikiwa katika utekelezaji wa miradi hiyo.

Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Afrika Mashariki katika kiwango cha lami unahusisha barabara yenye urefu wa Kilomita 245 kwa upande wa Tanzania, ambayo itaanzia Bagamoyo hadi Makurunge, Tanga. Utekelezaji wa mradi ambao umegawanyika katika sehemu nne tayari umeshaanza. Mfano, ujenzi unaoendelea sasa wa sehemu ya kwanza ya barabara hii kutoka Pangani (Tanga) hadi Mkange (Pwani) yenye jumla ya kilomita 50. Barabara hii inatarajiwa kuwa kiungo muhimu kati ya Tanzania na Nchi zingine za Afrika Mashariki.

Bw. Chodota ameeleza kuwa miradi hii pindi itakapo kamilika inatarajiwa kuleta mapinduzi makubwa katika upatikanaji wa nishati ya umeme wa kutosha, kurahisisha usafiri na usafirishaji nchini na katika Jumuiya kwa kuwa itarahisisha zaidi usafirishaji wa bidhaa hususani baina ya Tanzania na Kenya na upatikanaji wa huduma za jamii kwa urahisi na haraka. Sambamba na hayo, Bw. Chodota ameeleza kuridhishwa kwake na ushiriki wa Watanzania katika ujenzi wa miradi mikubwa nchini hususani katika Ujenzi wa Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere, ambapo asilimia 89% ya wataalam ni Watanzania.

Katika ziara hiyo Bw. Chodota ambaye ameambatana na baadhi ya Watalaam kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wamevutiwa na kasi na ubora wa kazi katika utekelezaji wa miradi yote iliyotembelewa.
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota (wa kwanza kulia) na baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia maelezo kuhusu mradi wa Bwawa la Kuzalisha umeme la Julius Nyerere.
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota (wa kwanza kulia) na baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia maelezo kuhusu mradi wa Bwawa la Kuzalisha umeme la Julius Nyerere. 
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota na Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia maelezo kuhusu mradi wa Bwawa la Kuzalisha umeme la Julius Nyerere.
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki walipotembelea mradi wa ujezi wa Bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere.
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota (mwenye tai) na baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na Wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na TANROADS wakiwa kwenye ziara ya kutembelea mradi wa ujenzi wa Barabara ya Afrika Mashariki (Tanga-Bagamoyo/Malindi – Lungalunga)
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota (mwenye tai) na baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na Wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na TANROADS wakiwa katika ziara ya kutembelea mradi wa ujenzi wa Barabara ya Afrika Mashariki (Tanga-Bagamoyo/Malindi–Lungalunga)
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota na baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na Wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na TANROADS wakiwa kwenye eneo la ujenzi wa kipande cha barabara ya Tanga miji hadi Pangani.
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota (wa kwanza kulia) na baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na Wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wakiwa kwenye ziara ya kutembelea Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) Holili, Tanga.
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota na baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na Wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wakiwa wakiangalia ukarabati wa jengo la Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) Holili, Tanga.
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota na baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na Wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wakiwa katika picha ya pamoja walipotembelea Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) Holili, Tanga.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.