Thursday, July 22, 2021

BALOZI MULAMULA AMUAGA BALOZI WA INDIA

 Na mwandishi wetu, Dar

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) amemuaga Balozi wa India hapa nchini, Mhe. Sanjiv Kohli ambaye amemaliza muda wake wa uwakilishi nchini.

Akiongea katika hafla ya kumuaga balozi wa India iliyofanyika leo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam, Waziri Mulamula amempongeza Balozi Kohli kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kudumisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya India na Tanzania.

Pamoja na mambo mengine, Balozi Mulamula amemuahidi Balozi Kohli kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na India katika sekta za elimu, afya, maji, kilimo, tehama na utalii kwa maslahi mapana ya nchi zote mbili.

"Kwa niaba ya Serikali ya Tanzania nakuahidi ushirikiano kutoka kwetu, nakutakia kila la kheri katika maisha yako nje ya Tanzania na ni imani yangu kuwa utakuwa balozi mzuri wa Tanzania duniani," Amesema Balozi Mulamula

Kwa upande wake Balozi Kohli ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kumpa ushirikiano wa kutosha wakati wa kipindi chake cha uwakilishi hapa nchini.

Balozi Kohli ameelezea kufurahishwa na uhusiano mzuri uliopo baina ya India na Tanzania na amepongeza hatua mbalimbali ambazo Serikali ya Tanzania imeendelea kuzichukua katika kuimarisha diplomasia ya uchumi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimkaribisha Balozi wa India aliyemaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini, Mhe. Sanjiv Kohli katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Balozi wa India aliyemaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini, Mhe. Sanjiv Kohli akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Libarata Mulamula akimueleza jambo Balozi wa India aliyemaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini, Mhe. Sanjiv Kohli


Maongezi baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Libarata Mulamula na Balozi wa India aliyemaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini, Mhe. Sanjiv Kohli yakiendelea


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Libarata Mulamula akimkabidhi zawadi ya picha ya Mlima Kilimanjaro Balozi wa India anayemaliza muda wa uwakilishi nchini, Mhe. Sanjiv Kohli



No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.