Tuesday, July 6, 2021

BALOZI MULAMULA AAPA KUWA MJUMBE WA BARAZA LA MAAMUZI LA EALA

Na Mwandishi wetu, Dar

Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) limemuapisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula kuwa Mjumbe wa Baraza la Maamuzi wa Bunge hilo.

Akizungumza mara baada ya kuapishwa na Spika wa Bunge hilo Mhe. Martin Ngoga leo tarehe 6 Juni 2021 katika mkutano uliofanyika kwa njia ya Mtandao jijini Dar es Salaam Balozi Mulamula amesisitiza umuhimu wa bunge hilo kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano kutokana na umuhimu  na matarajio ya Wananchi kwa Bunge hilo.

Aidha Balozi Mulamula amepongeza jitihada zinazofanywa na Bunge hilo kuendelea na vikao vyake kwa njia ya mseto ikiwa ni pamoja na kukutana ana kwa ana ama kwa njia ya mtandao licha ya changamoto ya uwepo wa ugonjwa wa UVIKO – 19 hali inayoonesha dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi.

“Wananchi wamekuwa na matarajio makubwa sana kupitia Bunge hili la Afrika Mashariki kiuweza kuona faida na mambo mazuri yanayofanyika kupitia jumuiya hii ya Afrika Mashariki,” Amesema Balozi Mulamula

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akiapa kuwa Mjumbe wa Baraza la Maamuzi wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) leo tarehe 6 Juni 2021 katika mkutano uliofanyika kwa njia ya Mtandao jijini Dar es Salaam 



No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.