Friday, September 9, 2022

TANZANIA, DENMARK KUSHIRIKIANA SEKTA ZA UCHUMI WA BULUU, KILIMO

Katika jitihada za kukuza na kuendeleza diplomasia ya uchumi, Serikali za Tanzania na Denmark zimeahidi kuendelea kushirikiana katika sekta za uchumi wa Buluu pamoja na Kilimo.

Makubaliano hayo yamefikiwa wakati Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb.) alipokutana na Balozi wa Denmark nchini, Mhe. Mette Norgaard Spandet katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.  

Waziri Mulamula ameeleza kuwa Ushirikiano wa Tanzania na Denmark ni wa muda mrefu na wa kihistoria hivyo Tanzania itaendeleza  ushirikiano huo kwa maendeleo ya  kichumi na kijamii kwa maslahi ya mataifa yote mawili. 

Pamoja na mambo mengine, Waziri Mulamula amemuelezea Mhe. Mette Spandet juu ya fursa mbalimbali ambazo ziko Tanzania katika kukuza sekta za uchumi wa buluu na kilimo.

“Tanzania inazo fursa nyingi katika sekta ya Uchumi wa Buluu ikiwemo uvuvi, idadi kubwa ya Samaki na wa aina mbalimbali ambapo ni fursa ya kibiashara, tunazikaribisha kampuni za Denmark kuwekeza kupitia sekta hiyo,” amesema Balozi Mulamula.

Viongozi hao pia wamejadili njia za kuboresha sekta ya kilimo nchini Tanzania ili kuwawezesha Watanzania wengi kunufaika na sekta hiyo hasa ikizingatiwa kuwa asilimia kubwa ya watanzania hutegemea kilimo.

Kwa upande wake Balozi wa Denmark nchini, Mhe. Spandent ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano wake na Denmark na kuahidi kuendelea kuudumisha ushirikiano huo katika sekta za kilimo, biashara na uwekezaji, tehama, utalii, demokrasia na uwezeshaji wa wanawake kiuchumi.

Katika tukio jingine, Waziri Mulamula amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa China nchini, Mhe. Chen Mingjian katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam na kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya mataifa hayo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimueleza jambo Balozi wa Denmark nchini, Mhe. Mette Norgaard Spandet wakati wa mazungumzo yao katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam 

Kikao cha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Balozi wa Denmark nchini, Mhe. Mette Norgaard Spandet kikiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na Balozi wa Denmark nchini, Mhe. Mette Norgaard Spandet katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na Balozi wa China nchini, Mhe. Chen Mingjian katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Balozi wa China nchini, Mhe. Chen Mingjian katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam 



















VACANCY ANNOUNCEMENT



 

Thursday, September 8, 2022

RAIS SAMIA AIELEKEZANDC KUTOA KIPAOMBELE KWA WANAWAKE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama,Wizara na taasisi mbalimbali kuwateuwa washiriki wenye sifa hususan vijana na kuwapa kipaumbele wanawake kushiriki mafunzo yanayotolewa na Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC).

Mhe. Rais Samia ametoa maelekezo hayo Septemba 8, 2022 wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Chuo cha Taifa cha Ulinzi mwaka 2012.

Mhe. Samia alisema kuna umuhimu wa kuwapa kipaumbele wanawake ili waweze kupata mafunzo hali itakayosaidia kuongeza tija na ufanisi katika maeneo yao ya kazi na Taifa kwa ujumla kwani ukimuelimisha mwanamke umeelimisha jamii.

Alisema pamoja na mafanikio yaliyopatikana kwenye kipindi cha miaka kumi anapenda kuona masuala muhimu yanatimia katika muda mfupi ikiwemo kwenda kuwafundisha watu wa ngazi za chini kwenye Serikali za Mikoa na  Wilaya kwani huko ndio kuna kundi kubwa la watu.

"Mafunzo yanayotolewa kwenye ngazi za juu ni lazima yashuke chini ili wafundishwe na kupata uelewa wa masuala ya msingi ya usalama na kuitumikia nchi kizalendo.

Kwa upande wake Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Tax alisema kuwepo kwa chuo hicho nchini kimeliwezesha Jeshi la Tanzania kutoa mafunzo kwa maafisa wakuu wengi zaidi tofauti na awali ambapo Jeshi lililazimika kuwapeleka maafisa wake kupata mafunzo hayo nje ya nchi.

Aliongeza kuwa NDC imewezesha kutoa mafunzo kwa idara nyingine za Serikali na viongozi mbalimbali kwa kuwajengea uelewa wa pamoja juu ya usalama.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ni mdau muhimu kwa maendeleo ya Chuo Cha Taifa Cha Ulinzi ambapo hadi sasa Wizara imeendelea kupeleka washiriki kwenye kozi ndefu na fupi ambapo miongoni mwao Wanawake wawili walioshiriki kozi ndefu walitunikiwa tuzo za uongozi kwa nyakati tofauti.

Wanawake hao ni Mkurugenzi wa Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini, Balozi Mindi Kasiga mwaka 2019 pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Itifaki, Bi. Naomi Zegezege mwaka 2022 wote kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Kadhalika, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula katika mahojiano binafsi alisema kuwa Chuo Cha NDC kimekuwa msaada mkubwa katika kuwanoa viongozi mbalimbali na baadhi ya watumishi wizarani kujengewa uwezo jambo ambalo limeongeza ufanisi kazini.

"Kila mwaka tumekuwa tukipeleka watumishi wawili katika Mafunzo ya muda mrefu NDC na matunda ya mafunzo hayo yamekuwa chanya kwa Wizara ninayoisimamia, natumaini kuwa tutaendelea kuwapeleka watumishi wengi zaidi baadae hususan Wanawake ili kuwajengea uwezo zaidi wa kujiamini wakati wanapotekeleza majukumu Yao," alisema Balozi Mulamula
Hafla ya Maadhimisho ya miaka 10 ya NDC ilihudhuriwa na Viongozi mbalimbali waandamizi wa Serikali.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Chuo cha Taifa cha Ulinzi mwaka 2012 
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Mambio ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Midni Kasiga (wa kwanza kushoto) akiwa na baadhi ya viongozi waliopata fursa ya kusoma kozi za muda mrefu  katika Chuo cha NDC

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb.) (katikati) pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Mchemba (Mb.) wakizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Vita Kawawa (Mb.) waliposhiriki katika hafla ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Chuo cha Taifa cha Ulinzi mwaka 2012

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akiteta jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Vita Kawawa (Mb.) wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Chuo cha Taifa cha Ulinzi mwaka 2012

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na Viongozi waandamizi wa Serikali na Wahitimu wa NDC

 

BALOZI MULAMULA AIFARIJI FAMILIA YA RAIS MSTAAFU ALI HASSAN MWINYI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb.) ametoa pole kwa Familia ya Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Alhaj Ali Hassan Mwinyi kufuatia kifo cha mtoto wake Hassan Ali Hassan  kilichotokea tarehe 31 Agosti, 2022 katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja, Zanzibar.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akitoa mkono wa pole kwa Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Alhaj Ali Hassan Mwinyi alipomtembelea nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akitoa mkono wa pole kwa familia ya Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Alhaj Ali Hassan Mwinyi alipomtembelea nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akitoa mkono wa pole kwa familia ya Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Alhaj Ali Hassan Mwinyi alipomtembelea nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam

Wednesday, September 7, 2022

NORWAY KUONGEZA BAJETI YA KUTEKELEZA MIRADI MBALIMBALI NCHINI


Waziri wa Norway anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa na nchi za Nordic Mhe. Anne Beathe Tvinnereim amesema Serikali ya Norway imeongeza bajeti ya kufadhili miradi mbalimbali ya kijamii na maendeleo nchini. 

Waziri Tvinnereim aliyeambatana na ujumbe wake amesema hayo alipozungumza na wakazi wa kijiji cha Chihembe kilichopo Mvumi-Chamwino jijini Dodoma. 

Akizungumza (Jumatano, Septemba 7, 20220) na Wananchi ambao ni wanufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Waziri Tvinnereim ametaja baadhi ya maeneo ambayo bajeti hiyo itaelekezwa kuwa ni kukabiliana na madiliko ya Tabia Nchi, kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na mpango wa kunusuru kaya maskini nchini kupitia TASAF.

“Natambua na kupongeza kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Tanzania katika kuboresha maisha ya wananchi wake, hata hivyo Serikali ya Norway inatambua changamoto zinazoikabili dununi kwa sasa, kama vile vita vinaovyoendelea kati ya Urusi-Ukraine na COVID19 ambazo zimepelekea ongezeko la bei ya bidhaa muhimu ikiwemo chakula, mafuta na gesi kwa nchi nyingi duniani ikiwemo Tanzania, hivyo tumeona ni vyema tukaongeza bajeti ya kusaidia miradi na programu mbalimbali za kiuchumi na kijamii zinazotekelezwa Tanzania ili kuwawezesha wananchi huhimili gharama za maisha”

Kuhusu kusaidia kubabiliana na mabadiliko ya Tabia Nchi Waziri Tvinnereim, amesema Norway imesukumwa kusaidia eneo hilo kwa kutambua kuwa asilimia kubwa ya pato la Tanzania linachangiwa na sekta ya kilimo na wananchi wake wengi wamejiajiri katika sekta hiyo huku wakitegemea mvua kuendesha shughuli hizo. 

Ameongeza kuwa ni vyema kuhakikisha uzalishaji katika sekta ya kilimo hauathiriwi na hali ya hewa kwa kukabiliana na Mabadiko ya Tabia Nchi. 

Akiwa ziarani jijini Dodoma Waziri Tvinnereim amefanya shughuli mbalimbali ikiwemo kutembelea miradi inayotelezwa na TASAF katika eneo la Mvumi, wilayani Chamwino, sambamba na kutembelea wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya maskini na kuzungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Dkt. Selemani Jafo na Uongozi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI). 

Waziri Tvinnereim na ujumbe wake ambaye pia ameambatana Balozi wa Tanzania nchini Sweden Mhe. Grace Martini yuko nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
Waziri wa Norway anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa na nchi za Nordic Mhe. Anne Beathe Tvinnereim akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa Serikali walipotembelea mradi wa bwawa uliotekelezwa na TASAF katika eneo la Mvumi jijini Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Dkt. Selemani Jafo na Waziri wa Norway anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa na nchi za Nordic Mhe. Anne Beathe Tvinnereim na ujumbe wake wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa Serikali alipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule na Waziri wa Norway anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa na nchi za Nordic Mhe. Anne Beathe Tvinnereim na ujumbe wake wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa Serikali alipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akiwa na Waziri wa Norway anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa na nchi za Nordic Mhe. Anne Beathe Tvinnereim alipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma.
Waziri wa Norway anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa na nchi za Nordic Mhe. Anne Beathe Tvinnereim akifurahia jambo na Bi. Agness Mkunya mkazi wa Mvumi jijini Dodoma alipomtembelea nyumbani kwake.
Waziri wa Norway anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa na nchi za Nordic Mhe. Anne Beathe Tvinnereim akiwa katika mitaa ya Mvumi jijini Dodoma alipotembelea miradi inayo tekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)
Waziri wa Norway anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa na nchi za Nordic Mhe. Anne Beathe Tvinnereim akizungumza na wananchi wa kijiji cha Chihembe-Mvumi jijini Dodoma.
Waziri wa Norway anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa na nchi za Nordic Mhe. Anne Beathe Tvinnereim akisalimiana na Bi. Agness Mkunya mkazi wa Mvumi jijini Dodoma alipomtembelea nyumbani kwake.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Dkt. Selemani Jafo akisalimiana na Waziri wa Norway anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa na nchi za Nordic Mhe. Anne Beathe Tvinnereim alipowasili ofisini kwake jijini Dodoma

WAZIRI MULAMULA AKUTANA NA MABALOZI WA UTURUKI, ETHIOPIA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) kwa nyakati tofauti amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Uturuki nchini, Mhe. Dkt. Mehment Gulluoglu na Balozi wa Ethiopia nchini, Mhe. Shibru Mamo Kedida tarehe 7 Septemba 2022 katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. 

Akiongea na Dkt. Gulluoglu Waziri Mulamula amesema  Tanzania itaendelea kushirikiana na Uturuki katika masuala ya biashara, masoko, kilimo, uwekezaji, utalii, madini na uchumi wa bluu.

Naye Balozi wa Uturuki nchini, Mhe. Dkt. Mehment Gulluoglu ameeleza kuwa katika kipindi chake cha uwakilishi anafanya jitihada za makusudi kuhakikisha Mkutano wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Uturuki unafanyika ili kuongeza nguvu ya utekelezaji katika maeneo ya ushirikiano yaliyokubaliwa.

Katika tukio jingine, Waziri Mulamula amemhakikishia Balozi wa Ethiopia nchini, Mhe. Kedida kuwa Tanzania itaendeleza ushirikiano wa muda mrefu na wa kihistoria ulioasisiwa na waasisi wa mataifa yao ili kufikia malengo ya utekelezaji wa diplomasia ya uchumi.

Ameongeza kuwa Tanzania itaendelea kuzingatia utekelezaji wa makubaliano mbalimbali yanayofikiwa katika Umoja wa Afrika hususan umuhimu wa mto Nile na manufaa yake katika sekta za kilimo na huduma nyingine za kijamii.

Naye Mhe. Kedida amemueleza Waziri Mulamula kuwa Ethiopia itaendeleza jitihada za kukuza ushirikiano katika maeneo mbalimbali ikiwemo kusimamia makubaliano yaliyoanzishwa kati ya Tanzania na Ethiopia hususan ushirikiano kati ya Shirika la Utangazaji la Tanzania na Shirika la Utangazaji la Ethiopia pamoja na ushirikiano kati ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Ethiopia.

=======================================

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Balozi wa Uturuki nchini, Mhe. Dkt. Mehment Gulluoglu tarehe 07 Septemba 2022 katika ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam.

Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Swahiba Mndeme na maafisa kutoka Wizara hiyo wakifuatilia mazungumzo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na Balozi wa Uturuki nchini, Mhe. Dkt. Mehment Gulluoglu katika ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam.

Picha ya pamoja
==================================

Wakati huohuo Waziri Mulamula alikutana kwa mazungumzo na Balozi wa Ethiopia nchini, Mhe. Shibru Mamo Kedida.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Balozi wa Ethiopia nchini, Mhe.Shibru Mamo Kedida katika ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam.

Watumishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mazungumzo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiteta jambo na Mhe. Kedida katika ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam.





BALOZI SOKOINE AKUTANA NA MKUU WA IDARA YA UHAMIAJI WA SAUDI ARABIA

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine amekutana kwa mazungumzo na Mkuu wa Idara ya Uhamiaji wa Ufalme wa Saudi Arabia Luteni Generali Suliman Al-Yahya katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Pamoja na Mambo mengine, viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali ya kukuza ushirikiano baina ya pande hizo mbili ambapo Saudi Arabia imeonyesha utayari wa kujadiliana na Serikali ya Tanzania kuhusu masuala ya upatikanaji wa viza za kuingia nchini Saudi Arabia.

Kwa upande wake, Balozi Sokoine ameishukuru Serikali ya Saudi Arabia kwa ushirikiano wake kwa Tanzania katika nyanja mbalimbali.

Balozi Sokoine ametumia mazungumzo hayo kuelezea utayari wa Tanzania kuingia makubaliano ya kuanzishwa Tume ya Kudumu ya Pamoja (JPC) kati ya nchi hizi mbili katika kusimamia utekelezaji wa masuala mbalimbali ya ushirikiano.

Ujumbe wa Saudi Arabia ukiongozwa na Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Luteni Generali Suliman Al-Yahya ukijitambulisha wakati wa kikao baina yake na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Kikao baina ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine na Mkuu wa Idara ya Uhamiaji wa Ufalme wa Saudi Arabia Luteni Generali Suliman Al-Yahya kikiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine amekutana kwa mazungumzo na Mkuu wa Idara ya Uhamiaji wa Ufalme wa Saudi Arabia Luteni Generali Suliman Al-Yahya kikiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Mkuu wa Idara ya Uhamiaji wa Ufalme wa Saudi Arabia Luteni Generali Suliman Al-Yahya akieleza jambo wakati wa kikao chake na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Mkuu wa Idara ya Uhamiaji wa Ufalme wa Saudi Arabia Luteni Generali Suliman Al-Yahya akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine  

Ujumbe wa Tanzania ukiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Saudi Arabia


BAKITA YATOA VITABU 1,650 VYA KISWAHILI KWA UBALOZI WA TANZANIA UJERUMANI

Katika jitihada za kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili Duniani Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) limetoa vitabu 1,650 vya Kiswahili  vitakavyotumiwa na vyuo, vituo na taasisi zinazojishughulisha na ufundishaji wa lugha ya Kiswahili nchini  Ujerumani.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya vitabu hivyo, iliyofanyika jijini Dar es Salaam,  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine ameipongeza BAKITA kwa kuunga mkono jitihada za Serikali ya katika kubidhaisha lugha ya Kiswahili katika ukanda wa Kimataifa.

“Naamini kuwa BAKITA itaendelea kufungua mlango kwa ajili ya maombi ya vitabu vya kufundishia lugha ya Kiswahili katika nchi rafiki na nchi nyingine zote duniani ambazo zitaonesha nia ya kufundisha raia wake lugha adhimu ya Kiswahili, alisema Balozi Sokoine

Alisema kuwa juhudi hizo ni muhimu sana wakati huu kwa kuwa Shirika la UNESCO liliipitisha tarehe 7 Julai ya kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili duniani, huku SADC, EAC na AU pia zilipitisha lugha ya Kiswahili kuwa miongoni mwa lugha rasmi zinazotumika katika utendaji kazi wa mitangamano hii na kuongeza kuwa kwa sasa ni dhahiri kuwa lugha ya kiswahili itakuwa kwa kasi na mahitaji ya vitabu na zana nyingine za kufundishia yataongezeka pia

"Kitendo hiki ni muhimu sana hasa ikizingatiwa kuwa  UNESCO iliipitisha tarehe 7 Julai ya kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili duniani, SADC, EAC na AU nazo zilipitisha lugha ya Kiswahili kuwa miongoni mwa lugha rasmi za kazi, ni dhahiri kuwa lugha hii sasa itakuwa kwa kasi na hivyo, mahitaji ya vitabu na zana nyingine za kufundishia yataongezeka,” amesema Balozi Sokoine.

Naye Naibu katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amesema uchapishwaji wa vitabu hivyo utasaidia kukuza lugha ya kiswahili nchini Ujeremani pamoja na mataifa mengine ya jirani.

Akizungumza katika hafla hiyo Katibu Mtendaji wa BAKITA Bi. Consolata Mushi ameahidi kuwa wataendelea kushirikiana na Serikali katika kuendelea kubidhaisha lugha ya Kiswahili kimataifa zaidi.

“BAKITA katika kutekeleza majukumu yake ya kisheria na mkakati wa taifa wa kubidhaisha Kiswahili itaendelea kusambaza vitabu katika balozi mbalimbali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zikiwemo Urusi, Uholanzi, Afrika Kusini, Burundi, Namibia, Korea Kusini, Nigeria na Mauritius,” amesema Bi. Mushi

Ameongeza kuwa BAKITA imetoa vitabu hivyo ikishirikiana na wachapishaji wa vitabu kutoka kampuni mbalimbali kwa lengo la kubidhaisha lugha ya Kiswahili na kutangaza soko jipya la vitabu katika nchi za Ulaya ikilenga kuwasaidia walimu wanaofundisha Kiswahili ambao ni Wadachi wenye nasaba na Waswahili pamoja na Diaspora wa Tanzania ambao wameanza kufundisha Kiswahili.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine pamoja na Naibu katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu wakimsikiliza Katibu Mtendaji wa (BAKITA), Bi. Consolata Mushi alipokuwa akitoa maelezo kuhusu ukumbi unaotumika kwa tafsiri za lugha mbalimbali katika taasisi hiyo

Katibu Mtendaji wa (BAKITA), Bi. Consolata Mushi akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya makabidhiano ya nakala 1,650 za vitabu vitakavyotumiwa na vyuo, vituo na taasisi zinazojishughulisha na lugha ya Kiswahili Ujerumani 

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine (katikati) akiwasilisha hotuba yake wakati wa hafla ya makabidhiano ya nakala 1,650 za vitabu vitakavyotumiwa na vyuo, vituo na taasisi zinazojishughulisha na lugha ya Kiswahili Ujerumani 

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akiangalia moja kati ya Vitabu vilivyotolewa na BAKITA kwa Ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani. Wengine ni Naibu katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu (kulia) pamoja na Katibu Mtendaji wa (BAKITA), Bi. Consolata Mushi (kushoto)

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akipokea boksi la Vitabu vilivyotolewa na BAKITA kwa Ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani kutoka kwa Naibu katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu pamoja na Katibu Mtendaji wa (BAKITA), Bi. Consolata Mushi

Meza Kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa BAKITA


TANZANIA, NORWAY KUSHIRIKIANA KUIMARISHA UCHUMI

Serikali za Tanzania na Norway zimesisitiza kuendelea kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo ili kukuza uchumi.

Msisitizo huo umetolewa wakati wa mazungumzo ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb.) na Waziri wa Norway anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa na nchi za Nordic, Mhe. Anne Beathe Tvinnereim walipokutana tarehe 06 Septemba 2022 katika ofisi ndogo za wizara Jijini Dar es Salaam.

Nchi hizo zinashirikiana katika masuala ya elimu, afya, kilimo, uwekezaji, miundombinu, nishati, madini, tehama, utafiti, maboresho kwenye mifumo ya ukusanyaji wa kodi, uchangiaji wa bajeti kuu ya Serikali, misitu, demokrasia, haki za binadamu, usawa wa jinsia, utunzaji wa mazingira na ukuzaji wa sekta ya biashara.

Balozi Mulamula alieleza kuwa Tanzania inathamini ushirikiano uliopo baina yake na Norway kwa kusimamia miradi ya maendeleo iliyo kwenye makubaliano na kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano kwa lengo la kujenga uchumi wa Wananchi.

“Norway ni mshirika wa maendeleo wa Tanzania wa muda mrefu na imesaidia kujenga uwezo katika maeneo mbalimbali ya kiutendaji ikiwemo uboreshaji wa mazingira wezeshi ya uwekezaji na biashara, usimamizi wa mfumo wa ulipaji kodi,” alisema Balozi Mulamuala.

Kadhalika, Serikali ya Norway imeongeza muda wa miaka mitano ya utekelezaji wa makubaliano ya majadiliano ya kisiasa yaliyoingiwa kati yake na Tanzania yanaendelea ili kuimarisha ushirikiano katika maeneo ya kipaumbele ya Serikali ya awamu ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wake Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Doroth Gwajima alieleza kuwa Tanzania ipo tayari kushirikiana na Norway katika utekelezaji wa pendekezo la mpango wa miaka mitano wa kujenga usawa na uwezo kwa wanawake, vijana na makundi maalum unaotegemewa kuinua uchumi na kuwawezesha kuajiriwa na kujiajiri katika kazi rasmi. 

Mpango huo pia umezingatia umuhimu wa  afya ya uzazi kuwa agenda muhimu ili kuyafikia Malengo ya Mpango wa Maendeleo Endelevu.

Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Antony Mavunde alieleza kuwa kupitia sekta ya kilimo Tanzania inayo nia ya kushirikiana na Norway katika masuala ya kujenga uwezo katika vyuo vya kilimo na taasisi zake ili kuwezesha tafiti za sekta hiyo kwa lengo la kuinua uwezo binafsi wa kuzalisha mbegu za mazao, kusimamia usalama wa chakula nchini, kujenga mabwawa na kuimarisha miradi ya umwagiliaji.

Maeneo mengine ya ushirikiano ni pamoja na upatikanaji wa mbolea kwa gharama nafuu, uimarishaji na ujenzi wa miundominu ya kilimo ili kujenga uwezo wa kuzalisha kwa mwaka mzima badala ya kusubiri msimu wa mvua kama ilivyosasa.

Vilevile Wizara ya Kilimo imeandaa mpango wa miradi ya kilimo kwa Wanawake na Vijana itakayotekelezwa katika mikoa ya Mbeya na Dodoma ambapo mradi huo utatumia jumla ya ekari 69 hivyo, kupitia ushirikiano uliopo Tanzania ina dhamira ya dhati ya kushirikiana na Norway ili kuyafikia malengo ya uzalishaji yaliyowekwa katika kufanya kilimo cha biashara na kulifikia soko la kimataifa.

Naye Mhe. Tvinnereim ameeleza kuwa Norway imejenga uwezo mkubwa katika masuala ya uzalishaji wa mbegu hivyo itaendelea kushirikiana na Tazania katika eneo hilo na maeneo mengine yaliyoelezwa na mawaziri walioshiriki mazungumzo hayo kwa lengo la kuondoa umasikini, kuongeza nafasi za ajira na kujenga uwezo wa kiuchumi kwa wananchi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Kushoto) akizungumza na ujumbe wa Norway ulioongozwa na Waziri wa Norway anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa na nchi za Nordic, Mhe. Anne Beathe Tvinnereim katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Doroth Gwajima (Kushoto) akizungumza na ujumbe wa Norway ulioongozwa na Waziri wa Norway anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa na nchi za Nordic, Mhe. Anne Beathe Tvinnereim katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Norway anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa na nchi za Nordic, Mhe. Anne Beathe Tvinnereim (Kulia) akizungumza na ujumbe wa Tanzania  ulioongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Antony Mavunde akieleza jambo wakati wa mkutano baina ya  Balozi Mulamula na Waziri wa Norway anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa na nchi za Nordic, Mhe. Anne Beathe Tvinnereim katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Waziri wa Norway anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa na nchi za Nordic, Mhe. Anne Beathe Tvinnereim akipokea zawadi ya picha ya Mlima Kilimanjaro kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Ujumbe wa Tanzania ukiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Norway