Friday, March 24, 2023

TANZANIA – KOREA KUENDELEA KUWEKEZA KATIKA KUKUZA BIASHARA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) ameeleza kuwa Serikali na wadau inaendelea kuweka jitihada katika kuboresha mazingira ya biashara baina ya Tanzania na Jamhuri ya Korea ili kuendelea kuinua kiwango cha biashara na uwekezaji baina ya nchi hizi mbili. 

Waziri Dkt. Tax ameeleza hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Mhe. Kim, Sun Pyo mapema leo tarehe 24 Machi 2023 jijini Dodoma. 

Dkt. Tax amemuhakikishia Balozi Kim kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kushirikiana na kufanya kazi kwa karibu na Jamhuri ya Korea ili kuwezesha biashara baina ya pande hizo mbili inaendelea kushamiri zaidi tofauti na ilivyo sasa. Dkt. Tax ameeleza baadhi ya hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Tanzania ni pamoja na kuendelea kutekeleza na kubuni programu zinazolenga kuongeza mwingiliano wa watu (people to people exchange) kati ya Tanzania na Jamhuri ya Korea. 

Kwa mujibu wa takwimu za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) za mwaka 2020, Korea iliagiza bidhaa zenye thamani ya shilingi za Tanzania bilioni 340.3 kutoka Tanzania, huku Tanzania ikiagiza bidhaa zenye thamani ya shilingi bilioni 290.3 kutoka Jamhuri ya Korea.

Kwa upande wake Balozi Kim, Sun Pyo ameeleza kuwa Jamhuri ya Korea inaendelea kuwahamasisha watu wake kuchangamkia fursa mbalimbali za biashara zinazopatikana nchini ikiwemo katika sekta ya kilimo, viwanda, ujenzi wa miundombinu, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na Utalii. 

Takwimu kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) zinaonyesha kuwa katika kipindi cha miaka saba (2015-2022), Korea imewekeza nchini dola za Kimarekani milioni 18.01 katika sekta mbalimbali zikiwemo za kilimo, ujenzi na usafirishaji na uchukuzi. Uwekezaji huo unakadiriwa kuzalisha fursa za ajira zipatazo 531. 

Mbali na hayo Waziri Tax ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Korea kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania katika utekelezaji wa miradi na programu mbalimbali zinazolenga kuboresha hali ya maisha ya watu ikiwemo elimu, afya, kuendeleza uchumi wa buluu, kilimo, Teknolojia ya Habari na ujenzi wa miundombinu. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Mhe. Kim, Sun Pyo wakiwa katika picha ya pamoja walipokutana kwa mazungumzo jijini Dodoma
 Mazungumzo yakiendelea.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Mhe. Kim, Sun Pyo yaliyofanyika jijini Dodoma
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akimsikiliza Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Mhe. Kim, Sun Pyo walipokuwa kwenye mazungumzo jijini Dodoma
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Mhe. Kim, Sun Pyo wakiwa katika picha ya pamoja walipokutana kwa mazungumzo jijini Dodoma

Thursday, March 23, 2023

DKT. TAX AKUTANA NA BALOZI WA SWEDEN NA MWAKILISHI MKAZI WA ICRC

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) amekutana na Balozi wa Ufalme wa Sweden nchini, Mhe. Charlotta Ozaki Macias na Mwakilishi Mkazi wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu Duniani (ICRC) Bw. Bart Vermeiren  ofisini kwake jijini Dodoma.

Akizungumza na Balozi wa Sweden nchini, Dkt. Tax amemuhakikishia Balozi huyo kuwa Tanzania itaendelea kudumisha uhusiano wa kihistoria na kidiplomasia baina ya nchi hizo mbili na kusimamia miradi ya ushirikiano kwa maendeleo na ustawi wa watu wake.

Pia ameishukuru Serikali ya Sweden kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta za elimu; afya; Uwekezaji na biashara; Teknolojia ya Habari, Usafirishaji na  Miundombinu; Nishati; Madini; Utafiti; maboresho kwenye mifumo ya ukusanyaji wa kodi; uchangiaji wa bajeti kuu ya Serikali; Misuti; Demokrasia, Haki za binadamu, Usawa wa jinsia; Utunzaji wa mazingira; na Mabadiliko ya Tabia Nchi.

Naye Balozi Charlotta Macias ameeleza kuwa wakati huu ambapo Tanzania na Sweden inaadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa rasmi kwa ushirikiano wa kidiplomasia ingependa kushirikiana na Tanzania katika shughuli mbalimbali zilizoandaliwa katika kuadhimisha kumbukumbu hiyo.

Aidha, amefafanua kuwa miongoni mwa shughuli za maadhimisho hayo ni; Kukutana na Wahitimu wa kitanzania waliosoma nchini Sweden katika ngazi mbalimbali ambapo watajadili shughuli wanazozifanya na malengo yao ya baadae.

Vilevile akafafanua kuwa shughuli kama hizo za maadhimisho zitakuwa zikifanyika na ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden ambapo hivi karibuni kuliitishwa mkutano mkubwa wa Watanzania wanaoishi nchini Sweden ambao kwa upande wa Serikali ya Tanzania uliwakilishwa na uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na kwamba hiyo ni moja ya jitihada zinazofanywa na serikali zetu katika kuimarisha ushirikiano.

Pia, akaeleza kuwa Sweden itaungana na nchi nyingine za Nordic kuadhimisha wiki ya Nordic itakayofanyika tarehe 29 Mei 2023 hadi tarehe 1 Juni 2023 katika maadhimisho yanayotarajiwa kuwakutanisha Mabalozi wanaowakilisha nchi za Nordic nchini, nchi marafiki wa Nordic na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Tanzania.

Pamoja na ushirikiano uliopo kati ya Sweden na Tanzania katika miradi ya maendeleo, kampuni za kutoka nchini Sweden zimewekeza nchini katika sekta mbalimbali ambazo ni pamoja na kampuni ya Ericsson, Tigo, Scania na kampuni za uchimbaji wa madini.

Katika hatua nyingine, Dkt. Tax amekutana na Mwakilishi Mkazi wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) Bw. Bart Vermeiren aliyefika ofisini kwake kujitambulisha. 

Katika mazungumzo yao Dkt. Tax amemuhakikishia Bw. Vermeiren kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na ICRC katika kuhakikisha kuwa Tanzania wanakuwa na uelewa wa pamoja kuhusu kuanzishwa kwa kamati ya kitaifa ya ICRC.

“Karibu sana Tanzania, nikuhakikishie kuwa Tanzania itaendelea kufanya kazi na ICRC Tanzania, ili wadau wapate uelewa wa pamoja na hivyo kurahisisha kuanzishwa kwa kamati ya Kitaifa,” alisema Dkt. Tax.

Naye Bw. Bart Vermeiren amemhakikishia Mhe. Wazirii kuwa ICRC Tanzania itaendelea kufanya kazi na Tanzania na kumuahidi kuwa Kamati hiyo iko tayari kushirikiana na Tanzania ili kufanikisha azma ya Tanzania kuanzisha kamati ya kitaifa katika eneo la kujenga uwezo katika Sheria za Kimatifa za msaada wa kibinadamu.

Ameipongeza Tanzania kwa kuendelea kuwa nchi ya amani katika ukanda wake. Pia amewapongeza wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma kwa kushinda mashindano ya Sheria za Kimataifa za Msaada wa Kibinadamu kwa bara la Afrika.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) akisalimiana na Mwakilishi Mkazi wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu Duniani (ICRC) Bw. Bart Vermeiren walipokutana kwa mazungumzo jijini Dodoma
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) akisalimiana na Balozi wa Ufalme wa Sweden nchini Mhe. Charlotta Ozaki Macias walipokutana kwa mazungumzo jijini Dodoma.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akiwa katika mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu Duniani (ICRC) Bw. Bart Vermeiren yaliyofanyika jijini Dodoma
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akielezea jambo wakati wa mazungumzo na Balozi wa Ufalme wa Sweden nchini Mhe. Charlotta Ozaki Macias yaliyofanyika jijini Dodoma
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Mwakilishi Mkazi wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu Duniani (ICRC) Bw. Bart Vermeiren wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa Wizara na ICRC.
Mazungumzo baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Balozi wa Ufalme wa Sweden nchini Mhe. Charlotta Ozaki Macias yakiendelea. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Balozi wa Ufalme wa Sweden nchini Mhe. Charlotta Ozaki Macias wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa Wizara na Ubalozi. 

NORWAY YAIHAKIKISHIA TANZANIA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA YA KILIMO

Serikali ya Norway imeihakikishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ushirikiano katika sekta za kilimo, usalama wa chakula, nishati, biashara na uwekezaji na mabadiliko ya tabianchi.

Ahadi hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Norway anayeshughulikia Maendeleo ya Kimataifa Mhe. Bjørg Sandkjær alipokutana kwa mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Balozi Mbarouk alisema kuwa Norway imekuwa mdau mkubwa wa Tanzania katika sekta ya afya na imekuwa ikisaidia katika masuala mbalimbali katika sekta hiyo.

“Katika hii ziara Mhe. Naibu Waziri anatagemea kufanya ziara ya kutembelea hospitali ya Kiluteri ya Hydom ambayo imekuwa ikifadhiliwa na Serikali ya Norway……… madhumuni ya zaira hiyo ni kuangalia ni kwa namna gani Norway inaweza kuongeza ushirikiano na kuisaidia hospitali hiyo,” alisema Balozi Mbarouk.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Norway anayeshughulikia Maendeleo ya Kimataifa Mhe. Bjørg Sandkjær amesema kuwa ameitembela Tanzania kutokana na ushirikiano imara uliopo baina yake na Serikali ya Norway uliodumu kwa muda mrefu na ulianza kama ushirikiano wa maendeleo. 

“Lengo la ziara yangu hapa Tanzania ni kuangalia ushirikiano katika sekta ya afya kwa sababu Norway imekuwa ikifadhili sekta, Mashirika ya Umoja wa Mataifa, mifuko ya kimataifa, wadau wengine wanaohusika katika sekta ya afya pamoja na asasi za kiraia zinazofanya kazi na Serikali ya Tanzania katika kuboresha huduma za afya,” alisema Mhe. Sandkjær. 

Hivyo nitaitembelea Hospitali ya Kilutheri ya Haydom ili kujionea shughuli zinavyofanyika na kuangalia zaidi maeneo ya ushirikiano katika sekta hiyo.

Tanzania na Norway zimekuwa zikishirikiana katika sekta za afya, elimu, uvuvi, nishati jadidifu, kilimo, ushafirishaji na utalii pamoja na masuala ya bahari. 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akimsikiliza Naibu Waziri wa Norway anayeshughulikia Maendeleo ya Kimataifa Mhe. Bjørg Sandkjær walipokutana kwa mazungumzo na katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Balozi wa Norway nchini, Mhe. Elisabeth Jacobsen (kushoto) akieleza jambo wakati wa kikao cha Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk na Naibu Waziri wa Norway anayeshughulikia Maendeleo ya Kimataifa Mhe. Bjørg Sandkjær katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Kikao cha Balozi wa Norway nchini, Mhe. Elisabeth Jacobsen akieleza jambo wakati wa kikao cha Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk na Naibu Waziri wa Norway anayeshughulikia Maendeleo ya Kimataifa Mhe. Bjørg Sandkjær kikiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Kikao cha Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk na Naibu Waziri wa Norway anayeshughulikia Maendeleo ya Kimataifa Mhe. Bjørg Sandkjær kikiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, Naibu Waziri wa Norway anayeshughulikia Maendeleo ya Kimataifa Mhe. Bjørg Sandkjær katika picha ya pamoja na Balozi wa Norway nchini, Mhe. Elisabeth Jacobsen 



Wednesday, March 22, 2023

DKT. TAX AKUTANA NA BALOZI WA MAREKANI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) amekutana na kuzungumza na Balozi wa Marekani nchini, Mhe. Michael Battle katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili kuhusu maandalizi ya ziara ya Makamu wa Rais wa Marekani nchini, Mhe. Kamala Harris, masuala ya ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani na jinsi ya kufanya kazi kwa pamoja katika kuendeleza uhusiano wa kidiplomasia uliopo baina ya mataifa hayo mawili.

Dkt. Tax ameishukuru Serikali ya Marekani kwa kushirikiano na Serikali ya Tanzania wakati wote tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya mataifa hayo na umekuwa na maslahi mapana kwa wananchi wa pande zote mbili.

Naye Balozi wa Marekani Nchini, Mhe. Battle ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kudumisha uhusiano wake na Serikali ya Marekani.

Katika tukio jingine, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb.) amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Urusi nchini Mhe. Mhe. Andrey Avetisyan katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Balozi Mbarouk ameipongeza Urusi kwa fursa za masomo zinazotolewa na nchi hiyo kwa watanzania na kuomba fursa zaidi za ushirikiano katika sekta za kilimo, madini, afya na uhandisi.

Naye Balozi wa Urusi Mhe. Andrey Avetisyan amesema Serikali ya Urusi inategemea kuongeza idadi ya ufadhili wa nafasi za masomo kutoka idadi ya nafasi 90 hadi 120 ili kutoa nafadi zaidi kwa watanzania kunufaika na fursa za elimu zinazopatikana nchini Urusi.

Urusi imekuwa ikishirikiana na Tanzania katika nyanja mbalimbali hususan sekta za elimu, afya, utalii na utamaduni, mafuta na gesi, ulinzi na usalama, madini, kilimo na uhandisi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisalimiana na Balozi wa Marekani nchini, Mhe. Michael Battle katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Balozi wa Marekani nchini, Mhe. Michael Battle katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga (kushoto) pamoja na Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje wakifuatilia majadiliano ya Mhe. Waziri Dkt. Tax na Balozi wa Marekani nchini 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akimkaribisha Balozi wa Urusi nchini Mhe.  Andrey Avetisyan katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Balozi wa Urusi nchini, Mhe. Andrey Avetisyan akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akimueleza jambo Balozi wa Urusi nchini, Mhe. Andrey Avetisyan katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam



Monday, March 20, 2023

TANZANIA YAKABIDHI RASMI MSAADA NCHINI MALAWI



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi, Mhe. Nancy Tembo mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kamuzu Jijini Lilongwe. Dkt. Tax alikuwa nchini Malawi kukabidhi msaada wa kibinadamu kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kufuatia kimbunga Freddy kilichoikumba Nchi hiyo tarehe 13 Machi 2023.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akimsikiliza Balozi wa Tanzania Nchini Malawi, Mhe. Humphrey Polepole wakati wa hafla fupi ya kukabidhi msaada wa kibinadamu kwa Serikali ya Malawi iliyofanyika Ikulu Jijini Lilongwe, Malawi leo tarehe 20 Machi 2023

Rais wa Malawi Mhe. Dkt. Lazarus Chakwera akipokea ujumbe maalum kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax. Dkt. Tax alikuwa nchini Malawi kukabidhi msaada wa kibinadamu kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan

Rais wa Malawi Mhe. Dkt. Lazarus Chakwera akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax baada ya kuwasilisha msaada wa kibinadamu kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa Serikali ya Malawi

Rais wa Malawi Mhe. Dkt. Lazarus Chakwera katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi, Mhe. Nancy Tembo pamoja na viongozi waandamizi wa Serikali ya Malawina na ujumbe wa Tanzania


 


NCHI ZA SADC ZAWEKA MIKAKATI YA KUJIKWAMUA KIUCHUMI




Waziri wa Mtangamano wa Kikanda wa DRC na Mwenyekiti wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC, Mhe. Didier Mazenga Mukanzu akisoma hotuba yake wakati wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (kushoto) pamoja na Mawaziri wenzake wakiwa wamesimama kwa ajili ya kuimba nyimbo za Taifa wakati wa hafla ya ufunguzi ya Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Anthony Mavunde akichangia jambo wakati wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC

Waheshimiwa Mawaziri na wajumbe wengine wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wakifuatilia hotuba wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akitenda jambo na Msaidizi wake, Bw. Seif Kamtunda.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya je na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga akifuatilia hotuba za viongozi wakati wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akitenda jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushurikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Talha Waziri.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akimsikiliza Waziri wa Zambia wakati waliposhiriki hafla ya ufunguzi ya Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)


Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Anthony Mavunde akiongea na mmoja wa Mawaziri walioshiriki Mkutano wa Baraza la Mawaziri
Kikundi cha Utamaduni kikiwaburudisha wageni wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)
uliofanyika Kinshasa, DRC

Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Anthony Mavunde akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Tanzaia ulioshiriki Mkutano wa Baraza la Mawaziri

Waheshimiwa Mawaziri wakiwa katika picha ya pamoja nje ya Ukumbi uliofanyika Mkutano wa Baraza la Mawaziri 


 


Saturday, March 18, 2023

KAMPUNI YA MABASI YA CLASSIC COACH KUTANGAZA FILAMU YA THE ROYAL TOUR NCHINI DRC

 




Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) akibofya batani ili kucheza filamu ya The Royal Tour kwenye Basi la abiria la Kampuni ya Classic Coach ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa kampuni hiyo kuonesha filamu hiyo kwa abiria wanaotumia mabasi yake. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) akitoa maelezo mafupi kwa wageni walioshiriki hafla ya uzinduzi wa kuonesha filamu ya the Royal Tour katika mabasi ya kampuni ya Classic Coach.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) akitoa maelezo mafupi kwa wageni walioshiriki hafla ya uzinduzi wa kuonesha filamu ya the Royal Tour katika mabasi ya kampuni ya Classic Coach

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) akitoa maelezo mafupi kwa wageni (hawapo pchani) walioshiriki hafla ya uzinduzi wa kuonesha filamu ya the Royal Tour katika mabasi ya kampuni ya Classic Coach. Wengine katika picha, watatu kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini DRC, Mhe. Said Mshana na watatu kulia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) akielezea kuhusu faida za kuitangaza Filamu ya the Royal Tour, huku akipigiwa makofi na ujumbe aliongozana nao kwenye hafla ya uzinduzi.

Wageni waalikwa walioshiriki hafla ya uzinduzi wa uoneshaji wa filamu ya The Royal Tour katika mabasi ya kampuni ya Classic Coach.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) akimshukuru Mwakilishi wa kampuni ya Classic, Bw. Jonathan kwa uamuzi wao wa kukubali kuonesha filamu ya the Royal Tour kwa abiria wanaotumia mabasi ya kampuni hiyo.

Baadhi ya wageni walioshiriki hafla ya uzinduzi wakiwa kwenye moja ya basi litakalotumika kuoneha filamu ya the Royal Tour

Moja ya basi linalomilikiwa na Kampuni ya Classic litakalotumika kuonesha filamu ya The Royal Tour kwa ajili ya kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania kwa abiria wanaotumia mabasi ya kampuni hiyo.